Bwana Michu,
naomba ufungue ukurasa wa habari hii, naona wadau wamebinya kimyaaa, vilevile cheki link hapo chini ya TED talks [Andrew Mwenda anavyochambua wazungu:Tatizo ni Lugha
Ukiangalia AY yeye kwenda kwa wifi zetu Kenya na Uganda ndo amefika, ni kweli sio mkali lakini namheshimu kwa kujenga jina lake East Africa.
MwanaFa huyu bwana ninaheshimu mashairi yake, ni mkali ktk lyrics, namshauri sasa atunge albamu moja tuu ya kiingereza. Kisha aendelee na nyimbo zake za kiswahili.
Haya sasa nakuja kwa Mr Misifa, hapa ni talent iliyokosa manager wa nguvu na sio wa kutoka bongo. Kwanza kabsa atafute manager nje ya Africa halafu aingie full shangwe katika reggae dancehall riddims, achukue beats zinazotoka kila siku Jamaica, awe anatunga nyimbo hata akiweza aimbe kwa English.
Kila siku kina Sizzla, Jah Cure, Morgan Heritage na kadhalika wanafanya vitu vya uhakika.Sababu moja Bongo Flava haisikiki kimataifa ni lugha, kina 2Face wamefika mbali ni kwa sababu ya English.
Sasa muda umefika kwa hawa wana bongo flava kuanza kuimba kwa kiingereza angalau albamu moja wapige kwa kiiengereza kwa ajili ya INTERNATIONAL MARKET.
Andrew Mwenda:
http://tedtalks.blip.tv/ , cheki video ya Andrew Mwenda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ehe kazi ipo basi ikiwa kuutangaza muziki wako na utamaduni wako basi mpaka uimbe kwa kizungu itakuwa sheshe. Mbona kuna mataifa mengi tu hayaongei kiingereza basi itabidi waimbe kwa kichina, maana wachina wengi duniani soko litakuwa kubwa, kihindi, kiarabu, kilatini.SHUGHULI PEVU!!!

    Tatizo sio lugha, tatizo ni muziki wenje vionjo vya kitamaduni ambao utakuwa tofauti na muziki wa kizungu.

    Jamaa unajua muziki wa kusoma au wa kupromoti, maana muziki ni kiashiria cha utamuduni wa mtu.

    Ulishawahi kumsikia Marehemu HUGWE ZAWOSE! Na wasanii wengine kutoka Chuo cha sanaa Bagamoyo? Ulishawahi kusikia kundi la Tatu Nane?
    Unamjua Fresh Jumbe? Anafanya shughuli zake za muziki Japan lakini anaimba kiswahili.

    Muziki wetu pia utasaidia watu watake kujifunza lugha yetu na lugha ni uchumi unapokazania lugha ya mwenzio unakuza uchumi wake.

    Muziki ni hisia pia naimagine hisia za kiswahili ambazo mtu anazifikiria kichwani kwake kwa kiswahili uziimbe kwa kizungu Mhu hehhe heee Sijui! Labuda mie na ushamba wangu wa kung'ang'ania kiswahili.

    Kuna kina Papa Wemba, na wanamuziki kibao wa kikongo watu wanapenda nyimbo hao bila hata ya kujua maana yake nini. Kuna wanamuziki wa kiarabu pia wakiimba hapo Habibi ya Nurulyaini watu wanachanganyikiwa hata hatujui kimeimbwa nini kwa sababu Music is Universal Language to your ears.Its all about feelings and being touched by what you hear. Ama sivyo watu wasingeomba redioni nyimbo za wazungu na wakongo wakati inglish is not richabo like me.

    Mswahili.

    ReplyDelete
  2. Hapana, sababu siyo lugha ya kiswahili.kitu kitakacho zuia kwa bongo flava kupanda sana chart ni hiki; Bongo flava ni copycat ya western music, hakuna chochote pale kipya hata kidogo cha kuwafanya watu wasisimke na kununua miziki yao.wataimba nini kipya kuwashinda wamarekani ambao ndiyo waanzilishi wa hip hop duniani? bongo flava hawataiona world market katika miziki yao.Ok kama wataimba kizungu waimbe kuzungu sawa ,ila hapo sasa watakuwa wanapambana na akina P Diddy, na akina fifty cents hayo ni mataifa makubwa. wewe ukisikiliza nyimbo za bongo flava huwezi hata ukajua hii ni tyuni ya nani? wote wanafanana na compilation yao yote ni sawa. Miziki yao hina ID maker yaani identification. Mfano, Lionel richie bila hata kuambiwa ukisikia tyuni yake utajua tu huyu ni Lionel Richie,au beyonce utajua tu. Nyimbo ya Linel Richie ya mwaka 80 leo unaweza ukaiimba na kuicheza tofauti sana na bongo flava ambapo wimbo tu wa last week ni vigumu kuukumbuka na kuucheza mbali ya kujua huyu ni nani. Huku ulaya ni kwammba wanamuziki hutengeneza sana pesa wanapo staafu na kutengeneza nyimbo zao kama classics na kuziuza kwa wanamuziki wapya ili wazichanganye au remixing na kuendeleza utajiri kwa wanamuzki wa zamani, sijui muziki wa bongo flava utakuwa na Classic compilations yoyote katika kizazi kijacho. kupona na kuendelea kwa bongo flavani ni kupiga muziki wao kwa tyuni yao ili dunia iweze kutofautisha na muziki wa kimarekani wala si kuimba kwa kizungu.

    ndaga fijo
    joune Mwakipesile

    ReplyDelete
  3. Sawa Mdau Mswahili! Hapo nimekubali vionjo vya kiutamaduni [moja ya sababu] lakini ujuavyo bongo flava ime-base sana kwenye hip hop beats [watu wa mamtoni wanapata vionjo hivyo kila siku]. Inakuwa vigumu kwa sisi kukubalika, lazima ukubali pia lugha ni tatizo!

    Sasa hivi naona muziki huo unabadilika pole pole lakini hawa wasanii ambao mimi najua ni wakali sana, wanazeeka na the only strategy ni kusuka angalau albamu moja tuu kwa kiingereza!

    Naamini everything is possible, if you put your mind into it. Kuimba kiingereza sio shida hata akiwa anaziandika kwa kiswahili. Kuna watu wanaoweza kuleta lyrics zako ALIVE kwa kiingereza na kufundisha jinsi ya kuimba nyimbo zilizotafsiriwa na kadhalika!

    Na kitu kingine wenzetu wakiimba wana-accent nzito au ni unique tofauti na sisi ndo maana wanakubalika ukisikiliza nyimbo zao kwa mfano french hip hop na hizo ulizosema ukisikiliza unapata flava fulani ambayo unakosa kwetu. Ni wasanii wachache sana, hata watano hawafiki wa bongoflava wanaoweza kukubalika kwa sababu ya sauti zao!

    Na nimetoa mfano kama Dully, ukisikiliza sauti yake na jinsi anavyoitumia. Unaweza kulinganisha na sauti za kina Sizzla na wa-jamaica wengine wanaopiga slow reggae. Ndo maana nikaona vizuri, ajiachie FULL katika reggae na majaribio kwa kiingereza ni mazuri tuu, hujui litamfikisha wapi kimataifa!

    Kuna vitu vingi vinachangia muziki wa kizazi kipya kutokwenda mbali na mimi nasema tatizo moja kubwa ni Lughaaaa!

    ReplyDelete
  4. Nafikiri jamaa alichokuwa anazungumzia ni huu mziki wa kizazi kipya au bongo flava, ambao ni kopi ya "hip hop culture" na "Rap music" ya hapa Marekani. Sasa hawa wasanii wa Bongo flava kama wanataka soko kubwa zaidi la wapenzi wa "hip hop" ni lazima watoe vile vile albums za lugha asili ya fani ya "hip hop" amabayo ni kiingereza.

    Tunajua kuwa wao sio "originators" wa "hip hop" lakini wanaweza wakawa "innovators" na wakapata wafuasi wengi sana kimataifa. Lakini wakiendelea na hicho Kiswahili wataishia hapo hapo Bongo sanasana Kenya, ambapo kisoko bado ni finyu.


    Kwakifupi kwa vile wanaiga style ya huku juu , wakitaka kuwa next Jay-z, Pac or Biggie Smalls ni lazima watoe vibao kwenye kiingereza, vinginevyo hawatasikika.

    C ya.

    ReplyDelete
  5. Mbona marehemu Brenda Fassie na Wasauz wengi wametoka na kizuru shwanga tu,naona hatua kama ya AY kujitangaza via Utando itasaidia,kina X plastaz pia wamekula showz kibao mbele huko wakichana hadi kimasai. Ila sometime ushauri wake unaweza kuwasaidia pengine,lakini ni lazima wajitangaze ipasavyo kimataifa hata kama wakichana kikoloni.Ila kama mnavyojua,kujitangaza kunahitaji mtaji. Wadau pia tuchangie mawazo ya namna ya hawa jamaa watoke vipi ki intaneshno

    ReplyDelete
  6. Hawa wanamuziki wa kwetu si lazima waimbe kwa kizungu ili wajulikane wanaweza kupiga bongoflava wakichanganya na vionjo vya mnanda ambao una asili ya kitanzania.Kuna mtakaosema mnandani mziki ya wahuni toka uswazi lakini kumbukeni hata walioanzisha RAP walikuwa ni wahuni tu.sijui kama mmenielewa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...