unamjua rita paulsen aliyebuni na anayeendeleza mpango wenye fanaka wa kuendeleza vipaji wa bongo star search? basi nenda http://www.bongocelebrity.com/ ukamfahamu mama huyu wa shoka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Atupe inspiration wanawake wenzake kwa kutuelezea alianzia wapi mpaka kupata mtaji na kuweza kufikia hapo pa kuitwa mwana mama wa shoka.
    ILI TUHAMASIKE.

    ReplyDelete
  2. Niliposoma jina la huyu mama kwa mara ya kwanza katika vyombo vya habari nilifikiri ni Mswidi, maana jina hilo la Paulsen, kama ilivyo kwa Iversen, Hansen, Klansen, Madsen, Matthyssen, Olsen nk ni watu kutoka Skandinavia. Kumbe mama wa watu ni mgagagigkoko kama mimi, mweh! Kama nimekosea mnisahihishe wanaglobu.
    Ashukuriwe Michuzi kwa kunifumbua macho!
    Idimu globu hii daima!
    Mdau

    ReplyDelete
  3. Mwambie atupe story zake zote za hapo mjini! Raha ya wabongo lazima tukuchokonoe maisha yako kwanza.

    ReplyDelete
  4. Wanawake wa shoka kwenye TV, RADIO na MTANDAONI. Lakini mmmmhhh mambo yanayoendelea BEHIND THE TEKNOLOGIA ni makubwa kaka yangu.

    Halafu kuna watu wananiudhi kweli kweli, wanajiita wacha mungu, kusali kwa sana lakini libeneke la madhambi liko palepale. Sasa yote ya nini?

    ReplyDelete
  5. Mdada amesimama ile mbaya, Nam"feel" kwa sana. BIG UP MADAME!

    ReplyDelete
  6. Michuzi dont let her lie the public.She's just photocopying American Idol or X-factor in UK.She needs to be creative,imitation is a mother of all cultural problems.Salama is trying to be Simon Cowell. But who is Paula Abdul!!!!

    ReplyDelete
  7. Naunga mkono hoja ya Mdau Sina Makosa kuwa Bibie Paulsen ame- 'copy' na ku-'paste' vipindi vya TV vya 'American Idol' na 'X-Factor'. hapo Bibie hajafanya ubunifu wowote ule. Labda tu ajaribu kutumia mawazo na ubunifu wa 'American Idol' na 'X- Factor' ya Uingereza katika Bongo star search tupate kuwaona wengine walio bora zaidi ya wana muziki wa kizazi kipya walio katika TV za bongo sasa hivi.
    SeniorJunior
    London

    ReplyDelete
  8. Licha ya ku-copy na ku-paste vipindi vya 'American Idol' na 'X- Factor' , hiki cha akina Ritta kinaboa sana sababu wanachokifanya wao ni kuwavuruga na kuwakatisha tamaa vijana. Hawana lugha nzuri ya mwongozo kwa wale wanaoona wamekosea. Wanakosoa vibaya mno. Lakini sishangai sana sababu ukifuatilia background ya Ritta na Salama, utajua mapungufu yao. Maana sijui kama wanajua hata kusoma NOTA za muziki. Matokeo yake wanamharibia heshima hata Kitime. Sasa cha kushangaza utashangaa pale Kitime(mtaalam) anapotoa comments zake, then Salama anamkatisha na kumsahihisha wakati hajui kitu. Ni kichekesho kabisa. So hakuna cha kumsifia Ritta na hicho kipindi. Atupe uzoefu wake huko nyuma kwanza kabla hatujamkubali.

    ReplyDelete
  9. She is beautiful,and i've to come to defend her kwa nyie mnaosema dont let her lie to the public,amewadanganya nini kwani na kumuambia yeye sio creative ni upuuzi wa hali ya juu maana show yake inaangaliwa sana na inapendwa sana,kwenye TV ukiweza kuachieve audience kuna creativity zaidi ya hiyo? mnaonekana hamjui mnaongea nini...hiyo Xfactor na Idol mbona huwaambii wanadanganya wakati show zao zinafanana ila umeishia kumshambulia dada wa watu anadanganya,nafikiri ni wivu tuu unakusumbua na ujue show nyingi dunia nzima zinafanana sana,na ni bora huyu x1000 anaproduce mwenyewe na kutumia watanzania kuliko wanaochukua mikanda ya filamu wanatuwekea kwenye TV...dada endelea kutuletea vitu na show yako ndugu zangu wanapenda sana show yako ingawaje mimi siioni huku,inabidi ufanye mpango episode ya mwaka jana ipatikane kwenye DVD online na sisi tununue
    Mdau kutoka US.

    ReplyDelete
  10. nafiriki anony uliyekuja kudefend mtu sidhani kama na wewe umeelewa malalamiko ya watu,japo sijui hicho kipindi kinavyoendeshwa ama kitu chochote kuhusu hicho kipindi ila swala ni kwamba hao majaji na mmoja wapo ni Salama Jabir sio? nani asiyemjua huyo dada?mtu mpaka unakuwa unamsahihisha mwenzako yeye kasoma wapi? ndio unaweza ukawaa na uzoefu ila sio kuponda kiasi cha kukatisha tamaa,kwani huku sisi tulio ulaya ama amerika wangapi waangalia hivyo vipindi kama vyenu? mimi huyo dada mwingine simjui na wala siwezi kumponda kwasababu mpaka hatua ya kufungua kipindi na watu wakakipenda hata kama ameiga ila amefanya kitu flani ila swala langu ni huyo dada mfupi. na wala sio kama nina chuki nae hapana ajifunze lugha nzuri.na mimi sielewi kwanini watu hawamchifupa mpaka saa hizi lol! maana kero zimezidi khaaaaaa

    ReplyDelete
  11. Dada yangu Paulsen ili kuendeleza u-celebrity kwako binafsi na washindi bora wa Bongo Star Search, naomba utafute mbinu ili walau waibukao washindi waweze pia kuwa artist ambao hata kwenye mtandao wa www.YOUTUBE.com wawe favourites. Mfano dadetu Rose Muhando sasa hivi ktk www.YOUtube.com watu kibao wasiongea kiswahili na waongeao kiswahili washatembelea video za Rose Muhando ktk www.youtube.com na idadi yao ni zaidi ya 250,000(laki mbili unusu) hayo ni mafanikio makubwa , hivyo BongoStar search muelekee huko huko ktk kujulikana kilimwengu.

    ReplyDelete
  12. Mmmh mambo haya!! Mimi naona kuwa kuiga sio big issue.. haswa ukizingatia mambo ni kuigana tuu siku hizi!! Cha muhimu ukiiga ongeza vibwagizo vyako na viutundu tundu vyako ila walao kuwe na tofauti kidogo.

    ukija kwenye majaji hapo mimi nitaponda haswaaa manake kama alivyosema mdau mmoja hapo juu wanachemsha kwa kuwa sasa wameamua mpaka kuiga mapozi na comment za majaji wa xfactor na american idol. Kwa mfano kumuiga simon cowel kwa kutoa kashfa fulani fulani... na mapose ya sharon osbourne..niliangalia kwa kweli nikapatwa na kichefu chefu... in short rita anapozi kama sharon, salama anamuiga cowel, ila huyo kaka mwingine walao he is more kwenye kazi na ufahamu wake. nimechoka nikianza kuandika hapa itafika asubuhi manake nilikuwa bongo na kuangalia kipindi kimoja tuu kichefu chefu

    ReplyDelete
  13. sina mengi ya kusema na muunga mkono kwa kutafuta vipaji vya kuimba vya wazalendo wenzangu lakini hicho kipindi kaiga, kutoka Marekani na hapa UK, tunajua mwanzilishi wake atafungwa kwa kudai kuanzisha hicho kipind

    ReplyDelete
  14. Madam Rita aache ku-earmark mshindi mapema. Inaonekana anmpigia upatu Kelvin wa Dar - e.g. come and hug me; ninakuchagukia mwenyewe wimbo; you are everything n.k. Salam Jabir naye sijui ana maana gani alipomwambia Kevin "watakuja hapa na mbwembwe, na kurukaruka sana jukwaani, lakini ukubwa wa pua si wingi wa makamasi- wewe ni funika bovu" Hivi comments kama hizo zinatueleza kipaji cho chote cha mshiriki? Nanashauri majaji wa BSS waangalie Tusker Project Fame ili wajue kinachotakiwa kumwambia mshiriki na si kumfananisha au kumtumia kuwaponda washiriki wenzake. Mimi binafsi mshiriki mshindi ni yule mwenye kumudu njanja zote za muziki - kupiga vyombo, kutunga, kuimba, kumiliki jukwaa, kupagawisha watazamaji, mwenye mvuto kimavazi, kihaiba, n.k. Mshiriki aimbe nyimbo tofauti tofauti ili tuweze kumjudge.
    Ushauri wa bure kwa Master J - aache lugha chafu dhidi ya P-Funk. Akumbuke yuko mbele ya camera na sisi wananchi tunamtazama - maneno kama 'kuwa mwanamume bwana, sisi wote tunalipwa mshahara na Bench Mark huna haja ya kuifagilia kila mara, n.k si y amtu mwungwana, la sivyo atuambia tu kuwa ana bifu na Paul (P-Funk). Kwanza P-Funk ndiye judge ninayona yuko serious na comments zake ni za kumjenga mshiriki kimuziki. Big up P-Funk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...