Michuzi,
Mtanzania mwenzangu, nakutahadharisha kama hujui lugha ya kiingereza ni bora uandike kila kitu kwa lugha ya kiswahili fasaha, hata siku moja usigeuze kiingereza kuwa kiswahili, haviendani na havieleweki na tena unajiaibisha sana ndugu yangu. Kwa mfano kwenye picha zako kwenye mtandao umeandika Ndugu fulani na mai waifu wake(my wife -maana yake mke wangu kwa kiingereza).
Sasa unaposema jamaa..... na maiwafu wake una maana -jamaa na mke wako na wake. uoni hiyo haileti aana yoyote??? au umesema bi......na maihazbandi wake( my husband- maana yake mume wangu)kwa maana hiyo unasema mume wako na mume wake- havina maana hata kidogo. tumia lugha ya kiswahili peke yake tutakuelewa vizuri sana, sio lazima kutumia kiingereza na haujui maana yake au hata jinsi ya kubadilisha sentensi kuiweka kiswahili ni aibu sana kwa mwandishi wa habari kama wewe.
Kuna ugumu gani wa kusema ndugu fulani na mkewe au mumewe!!!!!!!!!!!Huu ni ushauri tu usichukulie vibaya kabisa, naona utaendelea kujidhalilisha ndio maana nimechukua muda kidogo kukukosoa. Kaa salama na unafanya kazi nzuri, Wasalimie watanzania wote.

Maggie
f rom London.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 60 mpaka sasa

  1. Weee Maggie jinga kabisa,kwa akili zako nusu nusu unafikiri michuzi akisema english not reachable ni kweli???sana sana huwa anajoke tu na wanablog,michuzi anakielewa sana kienglish ukiona anafanya hivyo ujue ni "ngoma inogile"anasanifu tuu.sasa kwa sababu ni kichwa maji unafikiri kachemsha.Mwenzako kasoma enzi hizo na english inapanda sana tuu ila hapa huwa anafanya jokes tuu,na sisi tunaomwelewa tunafurahi kwa vitu vyake.Muulize anavijinondoozz vingapi na kavichukulia wapi halafu utajua ni mtu wa aina gani.

    ReplyDelete
  2. Maggie ur missing the point hapa,michuzi anatumia lugha hiyo kuongeza radha ya maneno ni si kwamba hicho kiingereza unachozungumzia weye hakifaahamu.kwa mfano nimeona akitumia neno GLOBU badala ya BLOG na maneno mengi tu.hiyo ndio style yake na sidhani kuna tatizo hata chembe.Tunashukuru sana kwa somo lako kwa namna moja ama nyingine na chellenge kwa kaka michuzi vilevile.

    ReplyDelete
  3. wewe Maggie Mai Waifu kweli... ze ubongo izi noti richabo... Unajisanifu mwenyewe hapa ki-ingilishi chako...! I think you should just follow the blog for a little while before starting to diss Michuzi.. you shall save yourself some embarrasment!

    ReplyDelete
  4. Maggie wala usihofu, Michuzi anakifaamu Kiingereza vizuri sana, cha kuandika na kuongea bila wasiwasi wowote. Ila hapa kwenye blog huwa anafanya masikhara hayo kufurahisha wadau. Hebu bwana Michuzi mwonjeshe Maggie "ungéngé" kidogo tu wakati wa kumalizia haka kamjadala, umfurahishe roho yake.

    ReplyDelete
  5. Huyu maggie kanitia Hasira sana za kujifanya mjuaji eti maggie London kwanza anajitafutia eti sifa hivi english unajua weweee kweli au sasa ndio unajifanya kufundisha watu kwanza kabisa nikwambie wewe utakuwa mgeni wa mambo ya blogs ndio maana uelewi kwa taarifa yako hii sisi hapa tunatumia KISWANGLISH ndio maana ngoma ina noga hapa kama alivyosema ANON Sunday, November 25, 2007 10:06:00 lala mbele maggie kama uelewi ungejua kaka michuzi amesoma na nondoz anazo ambazo nyie mkusanye ukoo mzima zinaweza kufika level ya A LEVEL nimemaliza

    ReplyDelete
  6. Dada yetu Maggie,
    Inaelekea mgeni hapa globuni. Nadhani inabidi tumuelewe tu na kumkaribisha. Hata mimi ni mbongo ninaeishi London lakini naelewa lugha ya globu vizuri tu. Karibu globuni Maggie. Ukitembelea mara mbili tatu utajikuta umezoea na haitapita siku bila kutembelea.

    ReplyDelete
  7. WE MAGGIE (SIJUI NDIO YULE WA KOFFI OLOMIDE) KWA FAIDA YAKO HII NDIO CULTURE YA HUMU KIJIJINI
    "...culture is defined as the shared patterns of behaviors and interactions, cognitive constructs, and affective understanding that are learned through a process of socialization. These shared patterns identify the members of a culture group while also distinguishing those of another group..."

    ACHA KUDANDIA GARI KWA MBELE.

    HIVI VIKOROMBWEZO NDIO STYLE YAKE ALIYOTOKA NAYO.

    KARIBU BWANA NDIO LUGHA YETU HUMU

    ReplyDelete
  8. we Maggie naona u are missing the point that was a joke ngoja nikueleweshe unajua watu wengi wanadhania neno "my wife" ni sawa na "wife" so thats utakuta linatumika kama michu anavyolitumia ili tu ucheke kwa kuona mtumiaji kachanganya madawa..unakumbuka joke ya eid Amini ya hotuba kwa malkia? wadau kama mnayo muimuvuzishe kwake...tehe tehe tehe...unajua ungekuwa na hela ungekuwa unarudi bongo na kuelewa nini Michu ana represent tehe tehe tehe uku bongo kuna kipindi ndo gumzo la jiji kinaitwa "ze komedi" muulize shangazi au mjomba wako ndo utamwelewa Michuzi and ushauri wa bure next time usikurupuke kama mawaziri wa kikwete kabla ya kusoma alama za nyakati....nawakilisha tu.

    ReplyDelete
  9. nyie wanablog wenzangu, Maggie namie nimemshangaa, kanichefua, ila nashangaa kwanini tunamshangaa huyu dada bure tu,,huyu yuko London, tayari HALI INAJIELEZA, beba boksi CHOKA MBAYA, HELLO MAGGIE, kama huelewi blogu hii nenda nyingine ziko nyingi tu, kama unaona hapa lugha inachanganywa na mkubwa wetu kaka muchuzi lugha haipandi, basi we nenda katafute blogu zingine ,kajiunge na wenzako wa EMPTYHEAD.BLOGSPOT.UTAJAZA sisi tuachie hii, ndo inayotukosha roho zetu, kwenda kabebe boksi au nenda kwenu likizo kapumzishe akili, ANTISOCIAL WEWE.

    ReplyDelete
  10. wadau tusiwe wakali sana ila napenda kumwambia dadetu,Maggie kwamba Michuzi amekuja na njia ya kujieza ambayo kwa kweli hata mimi imenikuna(moyoni!!) na kunifanya kuifuatilia sana GLOBU hii. karibu sana, utaipenda,utaifurahia,just let ur brain and heart opened,it is eventually going to sooth you!!!

    Evan wa Mwanza

    ReplyDelete
  11. Hey dada Maggie, kwa siye manyakanga wa hii globu hicho kiinglish tumekiita MICHUZI STYLE. Inaonekana ndiyo kwanza unaiingia humu kijijini, hivyo dada angalia "Donti jampu ini e muvingi treni"

    Mzee wa TBS

    ReplyDelete
  12. Maggie mambo vip MY FRIEND wangu?

    Hii ndio MY BLOG ya misoup utakutana na mengi tu.

    Ukitaka kujua watu wanajua lugha ya MALKIA ...jaribu siku moja tuma picha yako jaribu kumtafuta MY FRIENDS wako ndio utaona ze lugha inavyoFLOO...

    Ene wei nafikiri umeelewa swahiba.

    Msalimie Malkia wenu huo Landani...
    Ukerewe..utanistua ikiwa ufahamu kama upo Ukerewe..hiyo sio ya mwanza bali ya kwa mkoloni.

    karibu..haka ndio kadunia ka blog...mboya hiyo ya

    ReplyDelete
  13. adha pipo wengine, sasa dada tulia siku nyingine kabla ya kukurupuka! pesonali, sioni taabu ya kuelewa mai sensi of hyuma ya mithupu.

    big up, mithupu!

    ReplyDelete
  14. duh nami nilitaka nimsilibie huyu meggie ila dh haya mashambulizi 13 ya juu yangu yamesafais....

    KAMA HUELEWI SIO LAZIMA USOME,EBO!!

    ReplyDelete
  15. Jamani msimshambulie mwelezeni vizuri tu ataelewa.
    Lakini mhu dada kweli umetupa jongoo na mti wake, hivi inaelekea una miaka kibao hujarudi Bongo basi hata ukifika Bongo utashemsha na kugombana na wengi.
    Wataalamu wa lugha wanaita hiyo ndiyo kukua kwa lugha dada, kuna misemo kibao hata tukianza kukuelezea hapa tutajaza blogu. Hata mtoto mdogo Bongo anaujua huo msemo wa my wife wake au my husband wake.

    Jamani muwe munarudi nyumbani hata kila baada ya miaka 2 (Mhu nayo ni mingi utakuta kuna style nyingine tena ya lugha) Siku hizi kuna Qatar airways nauli kutoka London mpaka Bongo wakati mwingine inashuka mpaka dola 500. Hima jamani Bongo rahaa.

    Hata hivyo kama walivyosema wengine tread carefully soma humu utafurahia na hutaacha kuingia kwenye hii blogu kufuata hiyo hiyo my wife wake ya michuzi na vikorombwezo kibao unless kama huna bandama (la kukuwezesha kucheka)!!!

    ReplyDelete
  16. maskini magge,
    unasikitisha, lakini sio kosa lako, nadhani hujaangalia ZE COMEDY, coz thats the language they use,its a fun language, to make us blog users more happy. inaeleweka, sasa tatizo ni nini!! kama ni uzunguni hata michuzi kafika, tena kwa taarifa yako katoroshwa na kukataa kuvihudumia vibibi vizee, upo hapo!!

    ReplyDelete
  17. Teh teh teh watu wengine bwana hivi huwa mnafikiria nini...we Pope unawazaga nini? nahisi na we chizi eti anadandia gari kwa mbele. hehehe hii kali ya mwaka
    Wajameni Maggie amesikia msameheni ndio kwanza katoka kujifunza introduction tu kompyuta sasa anaingia onlaini.
    Karibu mwaya tukandamize kimichuzi- kidhungu

    ReplyDelete
  18. Mi sijawahi ku post comment kabla, na leo ni mara yangu ya kwanza.

    Nadhani huyu Dada hajaenda Tanzania muda mrefu, ama ni mtu ambaye hana 'humour' kabisa. Mai waifu ama Mai hasband ni misemo ya kitani tunayoitumia Tanzania kila siku. Michuzi kama mwandishi kwa miaka mingi, tangu mi nakua namjua. We kwa mtazamo wako unadhani ye ni bwege kiasi hicho. Kuwa London sio issue, na ujue hii blog ni kwa WATANZANIA. Mi mbona niko London na nimeuchuna tu, wala sisemi.
    Nakuonea huruma (sana, sana)

    Daniel, LONDON (msisitizo)

    ReplyDelete
  19. Maggie ni BIG BROTHER LONDON, kutoka hawezi, akitoka kurudi hawezi, ndo maana hata likizo kwao haendi, kadata ama kachanganyikiwa, kwa ufupi watu weupe wanaiita DEPRESSION.......tena mi ingekua wewe Magidalena(wachana na uzushi wa kujiita Maggie), mi kama wewe, ningemuomba radhi Michuzi kwa kumkosea heshima.

    ReplyDelete
  20. za jumapili wadau??

    maskini dada Maggie, yani umekurupuka huko ulikotoka kuja kumkosoa michuzi!!, yani unafikiri wadau wote zaidi ya million 2 wanaosoma blogu globo na blog hii wote ni wajinga au hakuna hata mmoja ameona makosa hayo ya michuzi,

    anyway bora tusikuchambe sana tatizo wewe ndo kwanza umeanza kusoma michuzi blog week hii na pia hata hukupata mtu wakukueleza kuwa hivyo ni vijimambo tuu katika kunogesha na kutia chachandu hapa globuni, whether michuzi anajua ki english au hajui hiyo ni lugha yake kajichagulia kuitumia hapa, so tuliza boli, inaelekea wewe ki english chako kinapanda sana, lol, manake yani uko kwenyewe kabisa wanakopika lugha,
    well maggie wasalim hapo kwa brown na sio blair tena.

    ReplyDelete
  21. MEGGIE DADA YANGU!!!

    KABISAA UKAFIKIRI MUCHUZI HAJUI KINGEREZA????

    AU UNAMWONA HE IS A NEW GENEREATION??

    POLE!!!

    ReplyDelete
  22. Masikini Maggie, kujua kwingi kumekutokea puani huko london hata Michuzi alishakaa. siku nyingine usidandie treni subiri kituoni, usijekufa bure mtoto wa london. umeona wanakijiji walivyokuja juu.

    ReplyDelete
  23. Jamani Maggie anatia huruma sana

    ReplyDelete
  24. Watu aina ya Maggie wako wengi. Kwa sababu wako nje ya bongo basi wanaona waliobaki bongo wote washamba na hamna wanachokijua. Mi niko state nakutana na wakinamaggie wengine huku yaani ni shida tupu, wenyewe kila kitu cha Tanzania ni ushamba kwao. mi nafikiri wao ndio wana ushamba wa kusahau walikotoka na kutokujua chochote kuhusu bongoland ya sasa. Tukumbuke kukaa nje ya bongo sio kuwa tunajua zaidi kuliko walioko bongo

    ReplyDelete
  25. Maggie! Nikijifanya nijaribu kukuelewesha lolote NITAKUTUKANA, sasa kuogopa nisivuke mstari, sisemi lolote. Najua aaah acha tu. - OC-Sinza.

    ReplyDelete
  26. Yaani leo nimecheka sana maskini magreti ngoja nikuombie kidogo "kukaa kwako kwenye maboksi faida yake umeiona? shangazi yako naye akisihi sana ujekumuona bongo mgareti ukapuuza" sasa fanya hivi huo waraka uliomuandikia michudhi sasa tukugeuzie wewe maana wewe ndio sio kabisaaaaa kam ulivo udhika ndio nasisi tulivyo udhika nawe lakini kalibu ikenda kwa wenye vyongo ukiweza fumba macho yote mawili ingia" mfungulieni njia kitoto cha anza tambaa"

    ReplyDelete
  27. Dia Maggie, naomba uandike huo waraka wako kwa kimombo maana I kan garantii yu utachemsha....Hovyoo...!!!!Chagua bega mshamba we....unaona kukaa Uingereza ndio kiinglishi unakijua?

    ReplyDelete
  28. Maggie ingekuwa uso kwa uso ni Michuzi tu ndio angekuambia kitu.
    Wote hapo juu wasingekufungulia vyoo vyao uso kukwambia LOLOTE, maandishi tu! Rahisi.

    ReplyDelete
  29. Dada Magge inaonekana ulikua na hasira sana leo...

    Hata kiingereza wana urban tionary. Labda kama umri wako umekatika ndio maana hukutani na watu wanaoongea kiingereza cha mamtoni.....

    http://www.urbandictionary.com/

    Sasa nikikutumia text message kweli utanielewa japo nitaandika kwa kiingereza hebu pitia hapa pia usiachwe na wakati.

    http://www.netlingo.com/emailsh.cfm

    mama yangu kule mndenyi nimeshamfundisha Text messaging shorthand kwa hiyo tuna puchu puchu tu every minute

    Leo tu nimemtumia my mom this text na alijibu in a minute

    Mom HIG? NMHJC. MUSM....."mengine hapa ni NOYB" Nikamalizia na ILU KK...

    sasa wewe si ungenisema kama ulivyomsema Kaka yetu....Nenda na wakati sister ...

    Kila lugha ina funny na ladha yake unafahamu creole...or creolized language? hiyo kuna kiswahili sanifu na english sanifu ...na kiswanglish.

    ReplyDelete
  30. Msameheni huyoo! Naona kweli anadandia gari kwa mbele kama Pope alivyosema...

    Maggie, kukaa kote London hujajifunza tu ku-obsevu, au kama usemi wenu huko unavyosema "luuk before you Liip". Siku nyingine mai frendi usitoe kommenti kwenye GLOBU ya mtu kabla ya kuisoma jamii iliyopo... "when in rome do as the romans do". Nenda kapande Victoria Line uende nyumbani mwaya, hapa kwa kaka Michu utaumia kama huna subira!!

    BTW, karibu JamboForums Ujifunze Mengi Kuhusu Nchi Yako!!

    SteveD.

    ReplyDelete
  31. Pole sana dada Mage unadandia daladala kwa mbele?
    Maria
    Brighton

    ReplyDelete
  32. Maggie, hayo ndiyo madhara ya kukaa nje muda mrefu bila kufuatilia mambo ya nyumbani!! Mai waifu wangu ameshauri nikurekeodie kipindi cha ze commedy halafu nikutumie huko huko London uliko (kama ni kweli uko huko..inaweza ikawa changa la macho). Sasa sijui utasemaje ukikiona hicho kipindi...mai waifu wangu anaomba upost address yako ili itusaidie kukumuvuzishia hiyo cd

    ReplyDelete
  33. Hee jamani, huyu Maggie wa wapi? Inawezekana kabisa akawa ni mtu anyeongea kiswahili lakini si mtanzania, labda mkenya, mkongo, mburundi, banyamulenge etc; kwa maana mi sidhani kama kuna mtanzania ambaye haifahamu hiyo misemo ya utani, kama MY wife WANGU / WAKE, BARABARA ya Ali Hassan Mwinyi ROAD, Jumuiya ya EAST Africa MASHARIKI, na mingine kadha wa kadha.

    Bi dada, karibu kwenye lugha ya kijiji. You are so out of this Society !!!

    ReplyDelete
  34. michuzi,
    Ninafurahi kuwa daima umekuwa wajiweka wazi kuwa lugha kwako ni tatizo na hakika hujawahi kutaka kujikuza katika hilo.Sasa huyu Maggie wa london naomba tumueleweshe kuwa hapa katika blog ya michuzi ni sehemu ambayo twaongea lugha ya mtaani na inakwenda na hali halisi ya maisha ya kitanzania kwa ujumla kuanziya msomi na si msomi na moja wapo ya nyenzo za mwandishi wa habari ni kuhakikisha kufikisha ujumbe wake kwa kada zote za watu ndivyo atumuavyo kijana wa zamani michuzi hapa,tazama hata viongozi wako wa nchi mfano Mhe Mkapa alikuwa akisalimiya kwa kusema Mambo....ila si lugha ya mababu but kwa nia ya kufikia kada zote alikuwa akiitumiya.
    maggie karibu bongoland nchi yenye kila kitu achana na kazi za utumwa unazofanya mpaka wasahau maisha.
    Mdau North Carolina.USA

    ReplyDelete
  35. EH huyu mage vipi hivi kama kweli ungekuwa msomaji wa blogu hii ungejua kuwa ndio misemo yake.ingekuwa anachemsha hata cc tuliobongo tungemrekebisha au unafirikiri mlio landani tu ndio englisha imenyooka! kwamba bongo tuliona ni swafi tu NO! NO! NO! mambo ya kibongo hayo wenzio hapo tunamuelewa sana tu mbona!!!!!!!

    ReplyDelete
  36. Dada Maggie unachekesha sana.......!! Siku zote jambo halifanyiki bila mazoea,huwezi kucunga mbuzi kama hujazoea pia. Fuatilia kama kwa wiki moja ukishazoea utacheka mpaka utaagiza mkanda mbavu kila siku baada ya kupitia globu hii......mimi nahudumia wazee huku kwa G.Bush na sijashangaa....!! Ukiona imekushinda hata usishughulike na muda wa kukaa kwenye komput,kumupta,likomupyuta mwanawani we nenda kaongeze tu muda wa kufanya kazi ya KUBEBA MABOKSI huko Ukerewe........Usidhani kuwa London ni sifa,ukirudi home watu wanajua ulikuwa Ukerewe hata hawashangai......!! Mwenzio nilidhani watashangaa eti nimetoka US kumbe wanashangaa nimetoka MTONi.........tena kwa AZIZI ALLY!!

    ReplyDelete
  37. Pooole sana dadetu Magi (Kikombe?), ungeruhusu akili yako kutafakari yasingekukuta haya. Au angalau ungeruhusu super-ego yako kufanya kazi yake ungenusurika na dhoruba iliyokupata, lakini kwakuwa una weak super-ego na strong ego, tunakupa pole tu kwa sasa!! Ukikuta wenzako wametumbua, na wewe tumbua, ndio ustaarabu wa werevu.Wabi'lah tawfiq.

    ReplyDelete
  38. Wajameni naomba tumsamehe bure huyu mdau naona kakurupuka kuingia katika msitu asioujua vizuri au huenda anatania. Tusiumize vichwa bure kumshangaa. Yeye anadhani kuwa anaweza kumfundisha kiinglishi bw. Michuzi. Huyu Michuzi nimepata kumfahamu tangu nikiwa shule ya msingi kupitia kwenye atikos zake na picha alizokuwa na anazoendelea kumwaga kwenye Daily News.Na kwa taarifa yako we Magi hadi sasa michuzi bado anendeleza libeneke kwenye hili gazeti. Hivi wewe hujawahi kusoma atikos zake kwenye hili gazeti uone zilivyokuwa na akili au unataka kutufanya tuamini kwamba wewe umezaliwa ukerewe na hujawahi kukanyaga hapa uswazi? Kama ulikuwa unatania tafadhali tuambie tuelewe tusiendelee kukushangaa!


    Ninachofahamu ni kwamba michuzi ni mwandishi wa habari mwandamizi ambaye huwezi kumfananisha na makanjanja wa siku hizi wanaoandika habari kwa ajili ya kugangia njaa au kwa kumfarahisha mtu fulani na huwezi kumfundisha kiingereza hata kidogo hata kama umekaa ukerewe kwa miaka mingi. Kwanza we magi kiingereza unachokifahamu ni kile kiingereza cha “please give me some water to drink” lakini kile kiingereza makini kwako ni noti richebo.Ini tamus ovu engilishi grama wewe tukikulinganisha na michuzi ni sawa na kumlinganisha mjusi na mamba au sungura na tembo. Hebu pata picha hapo wewe mwenyewe katika huo ulinganisho.

    Wadau najua mna hasira sana lakini naomba tumsamehe huyu mtu bure bilashi.
    Naomba kutoa hoja.

    ReplyDelete
  39. dada maggie... umeongea kwa jazba sana.wadhungu wanasema dont judge a book by its cover..just because michuzne writes swanglish, doesnt mean he cant write kidhungu unachotaka akiandike..anafanya hivi kutufurahisha sisi wasomaji.. na zaidi ya hapo ni lugha ambayo inatumika bongoz, sasa kama wewe bongo NO KURUDI, basi siku nyingine kabla hujakurupuka, ni mara alfu ukamuuliza michuz amemaanisha nini au anamaanisha nini kama huelewi na sio kuRopoka hovyo kama ulivyofanya tena kwa mmakonde mwenzako. aibu sana.. au mwenzetu vikongwe unavyovilea huko vilikufrustrate ukaamua kumalizia MAHASIRA YAKO kwa blaza michuzi? nafikiri utajifunza kutokana na makosa uliyoyafanya.. mimi nina uhakika kabisa kuwa skonga nehi hapo ze brain yako.. na huko ukonga sijui hata ulifikaje... gud dei

    ReplyDelete
  40. Mimi nahisi Maggie ni mwenzetu kabisa...labda alitaka kujua na kuona reaction zetu na kama pia huwa tunasoma comments na kutembelea globu hii maarufu. Mimi kama mkazi wa east afrika mashariki nafarijika sana kuona watu wanavyokienzi kiswaglish.....na kwamba kumbe watu ni wakali na hasa wakitoka weekend!!!

    ReplyDelete
  41. DADA MAGGIE (MAGDALENA) POLEE USIWAJALI HAWA WAKAKA WAPO WAKUTOSHA UNATAKIWA U "DATE SAM BADE ELSE"

    ReplyDelete
  42. Hahahahaaaaa.....mwanamke mwenzangu yamekupata, pole weee, sasa wee ulijua Michu anachemsha kweli? maskini weeee...yani kweli ungeonekana wa maana kama hata huo ujumbe ungeuandika kiingereza basi, usijitie kimbelembele kukurupukia vitu usivyojua wewe, yamekushuka shost magdalena!!

    ReplyDelete
  43. Michudhi, umenibania comment yangu ambayo nilimwambia Muggy binti Kikombe bin Bilauri aombe mshamaha ndani ya masaa 6. Huyu mwanamke hayuko serious, kwanza pole misupu kwa karaha uliyoipata na wana blog wote kwa usumbufu huu. Thijui Nnlie!

    ReplyDelete
  44. SASA VEVE CHUZI BANA TUKANWA NA MANAMKE, LAKINI VEVE HABANA KASIRIKA, OOOOH CHUZI VEVE IKO MUTU JULI SANA. CHICHI VANA BLOG KACHIRIKA SANA VILE HII TOTO IKO CHONGA DOMO. MIMI NI MATUMBI ENJIO LAKINI PENDA FIKISHA JUMBE KWA MAGGE, KWANJA RUDI HAPA TANJANIA, MAANA HUKO UNGELEJA YEYE NALEA MIJEE YA KIJUNGU, YEYE TUKANWA, HALAFU KACHIRIKIA VEVE CHUZI!

    ReplyDelete
  45. We Magdalena, nani kwanza mshamba huyo au wewe mwenyewe umechachawa kujiita Maggie, Michuzi ana mke, tafuta mzee wa kizungu tu huko, hata yule unaemlea kama kafiwa na mkewe chukua huyo. Nhiiiiiiiii, nhiiiiiii, nhiiiiiiiii(Nalia kwa uchungu sana)Pole mdogo wangu Michudhi(Misupu)

    Mbona hapa Mwenyewe Michuzi wana blog wanamwita Michudhi, Misupu hakasiriki au unawafanya watu hawajui kuita Michuzi. Jamani Ushamba hauna mwenyewe, kwako umelala, tena tutakumia Interpol wakukamate wakurudishe kwenu, sio Dar kijijini kabisa. Kazi unazozifanya huko Ukerewe zinakutia wazimu. Juzi kulikuwa na mdahalo wa mambo mnayoyafanya hapo Ukerewe, watu hatujasahau unaleta hizo. Kwanza kaone!

    ReplyDelete
  46. maggie, hivi kweli ulipokuwa unaandika comment yako ulikuwa na akili timamu au shemeji kakutibua kidogo? mwanamke mwenye busara asingeweza kuandika upuuzi kama uliouandika wewe.. either umemwagwa na semegi au hao wadhungu huko unaowaogesha wamekukorofisha ukaamua kumalizia hasira zako kwa kaka michuzi..kaka michuzi, hebu mteremshie li-rain la ki-english huyu mag(kikombe) ili atafute dictionary kidogo.. ninauhakika hajui proper QUEENS ENGLISH.. wabongo wakiwa nchi za watu bwana wanajifanya kuwa wao ndio wadhungu kuliko wenye nchi.. dada kuwa na busara..gud dei.. SAYS MISS CHECKS

    ReplyDelete
  47. Duh! wadau mna hasira utafikiri mmemwagiwa tindikali(Acid).Nafikiri inatosha, huyo dada kama ana busara aombe radhi!!!
    Mimi nimemsamehe nimeshafahamu tatizo lake sijui nyinyi wadau?

    ReplyDelete
  48. Kha!! Huyu naye katoka wapi? Ati na yeye kifimbo cheza? Mwee jamani mbona tutaona mambo!!! Mjukuu wangu Michuzi hebu niletee huyu nimpige sopusopu (haya sasa nimeleta balaa jingine!!!) Sasa ndo kaja tufundisha BBC au kutaka kutukoga ati naye wa baga sosi (ahaa kivumbi hapa tena!!) --- (dRU)

    ReplyDelete
  49. jamani taratibu ameshaelewa dadaangu,amesema arudii tena

    ReplyDelete
  50. wewe maggie kama hutaki tumie blog ya michuzi tafuta www. nyingine tumechoshwa na watu kama nyinyi

    mdau
    London

    ReplyDelete
  51. na ninyi wadau mmezidi kujishaua,mbona mnajipendekeza hivyo kwa mithupu?asisemwe?

    ReplyDelete
  52. hahaaaaaaaaaaa..you guys just made my day with your comments....mpaka nahisi labda ni michu mwenyewe kafanya hivyo ili acheke na reaction zetu...kama ni maggie kweli pole dadaa..hahahaaaaaaaaaa mithupu oyeeeeee

    ReplyDelete
  53. Wewe Michuzi huyu dada MAGIDA, kama tunavyoita kwetu umbulu yuko kweli au mikogo yako tu. Kama kweli yupo tuletee majibu yake tuone kama ameelewa somo, maana hao walimu hapo juu nadhani atapata diploma ya kiswanglish.

    Halafu kama mtu ana CD ya WAKILISHA yenye wimbo wa Kiswanglish naomba mtumieni kwenye graduation yake ya kupata hii diploma, sijui itakuwa lini? Maana kahitimu.

    Tunasubiri majibu Michuzi yu wapi dada Maggie/Magida agraduate, maana ni wiki ya graduation hii!!

    ReplyDelete
  54. naona michu wadau wa jimbolako la uglobu wamekufagilia, huyo dada anahitaji mikonoz atatulia.

    mdau wa newala.

    ReplyDelete
  55. pole dadah mage ndio ukubwa huo.lol dadangu kwanza ungeanza kwa kuuliza ,mambo yanavyokwenda hapa kijiweni,sa ulivyoamua kutoa lekcha la kiinglishi kwetu sie waswahili tumeona mhmh mbayaaaa kama unajishaua vile.Afu mwenyewe unasema landani jamani we saa nyingine miji mingine muone aibu kuitaja,landani nako si kariakoo tu.ah mie nshachoka karaha mara landani mara wichita,ovyooooo.

    ReplyDelete
  56. Wandugu naomba radhi nimekosa mimi kuongelea haya mambo bila uchunguzi wa kitaalamu! au bila ridhaa yenu waungwana.Wakiomba radhii wenye makosa husamehewaaaa....Asanteni saana.
    Wenu awaheshimuye Maggie.

    ReplyDelete
  57. Waungwana

    Inaelekea wanaglobu mna hasira ya kuua mbu! Yaani huo msongamano wa comment umefanya Dada Mage wa Rondon kuona ni bora aombe radhi.

    Kiungwana ni kwamba gasira zishushwe na kutulizwa; dada maggie naye achunguze mambo kabla ya kubwatuka: na akina sisi ambo english not reachable tunaonelea bambo ...,. ohh,, sore very; bomba kutumia Swanglish. Kaka Mi-curry endereza kuvulumisha grobu kwa kuenderea mbere!

    Tenk yu very

    Mwanagrobu mkimya

    ReplyDelete
  58. Hey!!!

    I'm also in London, this is the guy who always give use breaking news....it seemed you are behind your time because this sort of language has nothing to do with any msg...Mzee Ojwang' in Kenya used this language in 1990s when was performing his art and Michuzi is using this today...there is no problem with the language!!

    Just simple advice..p'se before speaking try to engage brain...and don't ever be selfish as you have shown today, everybody understand what Michuzi writes except you...it's a shame!!!

    ReplyDelete
  59. Jamani Maggie nadhani mmeshamshambulia vya kutosha namuombea TIME OUT. Ni kweli amechemsha ila kwa kutokuelewa unajua tena ukiwa mgeni nyumbani kwa mfalme kila unachoona unadhani dhahabu.

    ReplyDelete
  60. Jamani Maggie ameshaomba msamaha 27 Nov saa 12:36:00AM EAT kwa niaba ya wadau na mkubwa michuzi i think umesamehewa ila take care wadau wana hasira hapa bloguni, si umeona mwenyewe ulivyokanyaga nyoka mkiani mambo yalivyokuwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...