katika kuadhimisha boxing dei leo na tumpongeze bingwa wa dunia wa kickboxing mmbongo japhet kaseba (kulia) kwa kuchaguliwa kuwa mwanamichezo bora wa mwezi Novemba mwaka huu.
kaseba alichaguliwa na chama cha waandishi wa habari za michezo tanzania (taswa) kwa kura 160 mbele ya grace daudi, mfungaji bora wa mpira wa kikapu katika mashindano ya Kombe la Nje ambaye aliyepata kura 132 na catherine mapuwa wa ngome, pia mpira wa kikapu, ambaye alipata kura 104.

wachezaji waliopata kuwa wanamichezo bora wa mwezi kwa kufanya vizuri toka januari mwaka huu ni haruna moshi (soka) masoud Amour (judo), banuelia mrashani ( riadha), ali mustapha ' Barthez; (soka), joseph dimei (riadha), erasto nyoni ( soka), martin sule (riadha), kudra omar ( soka) , osward Morris ( soka) na Mary Meshack (kikapu).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. naomba umnisaidie huyo japhet kaseba ni bingwa wa dunia mbona hapatikani kwenye mtandao? je ni bingwa wa dunia kweli au? nashindwa kuelewa au naomba mnisaidie nitapata wapi habari zake kwenye mtandao?

    ReplyDelete
  2. duh...huyo Mbulushi wa al-qaida au nini?...mbona kanuna!!!

    ReplyDelete
  3. MICHUZI NA WEWE PAMOJA NA KUSOMA NA KUSAFIRI NG`AMBO MBALI MBALI BADO HUJUI NINI MAANA YA BOXING DAY? HII NI SIKUKUU YA KUFUNGUA ZAWADI HAIHUSIANI KABISA NA NGUMI!! AMA KWELI JAMBO USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA GIZA..! HII NDIYO TABIA YA KUKURUPUKIA UTAMADUNI WA NCHI ZINGINE UNACHEMSHA SANA MICHUZI SIKU HIZI!!

    ReplyDelete
  4. Boxing Day is a public holiday celebrated only in the United Kingdom, Canada, New Zealand and Australia and many other members of the Commonwealth of Nations on December 26, the day after Christmas Day; or alternatively on the next weekday after Christmas.
    Boxing Day, contrary to common belief, is not about the sport of boxing. The celebration is traditional, dating back to the middle ages, and consisted of the practice of giving out gifts to employees, the poor, or to people in a lower social class. The name has numerous folk etymologies[3]; the Oxford English Dictionary attributes it to the Christmas box; the verb box meaning: "To give a Christmas-box (colloq.); whence boxing-day."
    AIBU TUPU MICHUZI....HUU UTAMADUNI TUACHIE WENYEWE WABEBA BOX HUKU NG`AMBO.

    ReplyDelete
  5. Mr.Michuzi, Boxing Day is a traditional celebration, consisted of the practice of giving out gifts to employees, the poor, or to people in a lower social class.In short it's a holiday after Christmas, and has no relation to the sport of fighting(Boxing). Thank you ver much.

    ReplyDelete
  6. MICHUZI MIMI MDAU NIKO MAJUU NABEBA MABOX.
    KUULIZA SI UJINGA HIVYO MWENZENU... HIVI BOXING DAY NI SIKU KUU YA WABEBA MABOX DUNIANI AU SIKU KUU YA WATU KUTWANGANA MANGUMI MPAKA MSHINDI AJULIKANEEE.
    AH JAMENI NISAIDIANI MAANA NATESEKA(GA)NA HAKA NENO KILA MWAKA LAKINI NILIONA(GA) NOMA KUULIZA.EEE HAYA TU.

    ReplyDelete
  7. Kaka michuzi labda unieleweshe unakusudia boxing day ipi? Kama ni hii ya tarehe 26/12 siku moja baada ya xmass, huwa haimaanishi boxing (ngumi)-mchezo wa ngumi, nnavyoelewa mimi ni "boxing day" yaani siku ya kufunguwa yale ma box ya zawadi mtu uliyopewa siku ya xmass, wenyewe wazungu huifanya tarehe 26/12 kuwa ndio siku ya kufunguwa hayo mabox yao. Au nakosea waungwana??? Au kama kaka michú ni sehemu ya kuinogesha blog basi sina ubaya na wewe lakini kama ulikuwa hujui ( ingawa sizani kama ni hivyo hujui)basi hem tu "shee" haka ka knowlegde.
    Bablii

    ReplyDelete
  8. Misupu,I hope unaelewa vizuri maana ya Boxing Day. Haiusiani kabisa na Boxing sport. Kwani utakua unatuangusha wadau wako.

    ReplyDelete
  9. NYINYI WABEBA MABOKSI ACHENI USHAMBA HUO. MICHUZI ANAJUA VIZURI MAANA YA BOXUNG DAY AMEWEKA HIYO POST KAMA UTANI TU ILI KUICHANGAMSHA BLOG YA JAMII. HIYO HAINA MAANA KUWA MICHUZI ANACHANGANYA BAINA YA NGUMI NA SIKU YA KUPEANA ZAWADI.

    MSIFIKIRI KUWEPO KWENU ULAYA NDIO MANAJUA SANA NA WATU WENGINE HAWAJUI KITU. MNAFANANA NA YULE DADA ALIYEMTAKA MICHUZI AKAJIFUNZE KIINGEREZA KWA KUWA ANACHANGANYA LUGHA.

    HII NI KUIFANYA BLOG IONEKANE SIO TU SEHEMU YA KUELIMIKA BALI PIA SEHEMU YA KUBURUDISHA. HIVYO ONDOWENI HUO MTAZAMO KUWA MICHUZI HAPO KACHEMSHA NI NYINYI NDIO MLIOCHEMSHA KWA KUTOELEWA MAANA YA BLOG YA JAMII.

    INAONEKANA NYINYI MLIOWEKA COMMENTS HAPO JUU NI WAGENI KATIKA BLOG HII YA MICHUZI. HUKO UK MLIPO MICHUZI AMESHAFIKA KWA SANA NA ANA VINONDO KADHAA KACHUKULIA HUKO HIVYO HUO UTAMADUNI WA BOXING DAY ANAUJUA VILIVYO.

    NAKUOMBENI KABLA YA KUKURUPUKA KUANDIKA COMMENTS MUFIKIRIE MARA MBILI MBILI AINA YA COMMENTS ZENU.

    MICHUZI ENDELEZA LIBENEKE.

    ReplyDelete
  10. Michuzi bwana kwa kupenda watu waonyeshe vinywa haujambo. Umenikumbusha enzi zile najifunza kizungu. Ndio kusema kweli hujui Kweli au ulipenda wachangiaji wapya tuwe wengi? Tupe jibu tafadhali. Happy boxing day to you.

    ReplyDelete
  11. Teh teh teh teh,

    Michuzi kweli leo imetoa mpya ya kufungia mwaka 97, Ooops, 2007! Hivi kweli ulikuwa resious kufikiri Boxing day ni siku ya "MANGUMI"? au ulikuwa unatuchemsha wadau??????

    Mbavu sina hapa nilipo. Kama wewe mwandishi wa habari mashuhuri, mwenye exposure ya kutosha bado ukafikiri boxing day ni siku ya mangumi, basi "TUNA" haki sisi tunaokwenda sehemu imeandikwa "Internet cafe" na kuuliza/kuagiza Chai ama kahawa!

    Kaazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  12. Ireland inaitwa St. Stephen's Day, nafikiri michuzi utuletee habari za Stephen wote hapo bongo, halafu wawe watakatifu.


    Teh Teh Teh...

    Misupu acha ushamba....

    ReplyDelete
  13. Nami naungana na mdau wa 26, 2007 2:00:00 AM EAT kwa kuuliza kuwa huyu Kaseba ni bingwa wa dunia wa kupitia chama gani cha masumbwi duniani? Mbona hakuna chama kinachomtangaza kuwa ni bingwa wake wa Dunia? Au Watanzania kutokana na ukosefu wa mabingwa wa Dunia tumiamua kumpa ubingwa wa dunia ili tupate cha kujisifia?

    ReplyDelete
  14. Hii ndio tabia ya Watanzania kudandia mila za watu bila kujua undani wake....

    Boxing Day Tanzania ???? Wapi na wapi...haya ni mambo ya Waingereza na katu si ya Mtanzania...

    Mambo ya gift kwetu wapi na wapi... sisi upendo wetu ndani ya familia ndio gift kubwa.. wao kutoa mabox ya gift ni kama vile kwao upendo wa familia uko siku moja/ au mbili kwa mwaka, siku nyingine zote busy mtu....no time for family au
    jirani upo..kwa hiyo kwao it is nice to be normal just for one day...

    Akili nyembamba za mbongo..

    Teh Teh Teh

    ReplyDelete
  15. WOTE MNAOSEMA MICHUZI KACHESHA, MIMI NAKATAA,NYIE NDIO MMECHEMSHA NA NI WASHAMBA SANA, MICHUZI ALIKUA ANAWATEGA TU NA KAWAPATA, SASA NANI MJANJA? NA MWELEVU, MICHUZI KAWAPIGA BAO LA KISIGINO,
    UKIONDOA KUA NI MWANDISHI WA NA MPIGA PICHA ALIE FUZU, NI MTOTO WA MJINI PIA, YEYE ANAJARIBU KUTUMIA LUGHA YENYE MVUTO KWA WANA BLOG,
    NA UKIINGI MJINI UTAKUTA VIJANA WANGI WAKIZAZI KIPYA UTUMIA LUGHA HII.NYIE WADAU MSIOELEWA, JARIBUNI KUKUMBUKA KUA MICHUZI UONGOZANA NA RAIS KATIKA MISAFARA YA KIMATAITA, KAMA VILE UN, MNATEGEMEA UKO ANAZUNGUMZA LUGHA GANI,ANAELEWA FIKA MAANA YA BOXING DAY, ALIKUA ANATOA CHANGA MOTO KWA WADAU, NA KWELI KAWAPATA WATU WENYE UPEO MDOGO,MICHUZI AMEKWISHA SAFIRI SANA KATIKA DUNIA HII, UPEO WAKE SIO WAKUTWA KUJUA MAANA YA BOXING, DAY.WACHENI MIJUNGU YENU NA MIWIVU YENU.
    kUHUSU BONDIA JAFET KASEBA, MIMI NI RAFIKI YANGU SANA, TUMEKUA PAMOJA, SISI TUNAMWITA MBESE.MIMI PIA NINATAKA KUJUA NI BINGWA WA DUNIA,KWA MPANGO GANI, NIMEMTAFUTA SANA, KATIKA MTANDAO SIMPATI,LAKINI NAKUMBUKA ALIKUJA HAPA HOLLAND KWENYE MPAMBANO NA ALISHINDA VIZURI, ALIPOKUJA HAPA ALINITAFUTA, KWA KUNIPIGIA SIMU, TULIZUNGUMZA NAE KWA KIREFU,LAKINI ALINIELEZA ATAKUA NA ZIARA YA JAPANI NA AMERICA.NAOMBA MICHUZI UNIFAHAMISHE KAMA KWELI, KAMANDA WANGU AMEKWISHA KUA BINGWA WA DUNIA NA KWA VIGEZO GANI. E MAIL YANGU NI butijiwe@yahoo,com
    bu.ti.jiwe@hotmail.com
    michuzi endeleza libeneke,wasikukatishe tamaa, hao wadau wasio elewa maana ya blog ya jamii. nakutakia Mwaka mpya mwema.
    Mdau kutoka NEDERLAND

    ReplyDelete
  16. Mimi hapa wakili wa kujitegemea na najitolea kumtetea michuzi bila ujira. Michuzi is a clever guy - never did he claim it to mean marking the sporting activity. All he said was that we would be congratulating the kick-boxer on that day - he could have opted to congratulate him on New Year's Eve - sasa kosa liko wapi? Further, it could have been a picture of Mapepe and his great song, Kilimanjaro Stars losing to Sudan or some of you bending your backs under the weights of PC World boxes to be delevered for Christmas. I therefore ask the jury to acquit brother michuzi. This issue is now closed.

    ReplyDelete
  17. Boxing Day ni sikukuu ya sisi wabeba maboxi popote tulipo!!!Jamani naomba mawasiliano na huyo kaka hapo kushoto...loo kapendeza sanaaaa!Kama kaoa basi mkewe anisamehe sana.

    ReplyDelete
  18. Uliyeandika, "Akili nyembamba za mbongo..", jihadhali sana ma ku-"generalise"!

    Samaki mmoja akioza kapuni, sio wote ndani ya kapu!

    ReplyDelete
  19. michuzi ana akili zake timamu kuandika hivyo!!! issue ni kwamba huyo kaseba anatambulika na chama gani duniani? ndio ishu hiyo hebu tusaidieni

    ReplyDelete
  20. Kilichowashangaza nini hapo Kaseba kuitwa bingwa wa dunia. Si ni nyie nyie wana blogu mlileta habari hii kwa Michuzi mkasema Michuzi kawabania kwa kuwa Kaseba kapigana na huyo Gabacholi hapo pembeni yake kamshinda na hakuitoa hiyo taarifa kwenye blogu? Au mmesahau ni vipande vya magazeti mkatubandikia? Sasa lilikuwa shindano la Tanzania la kikiboksing, la Africa, la Asia au la Dunia (Hilo alilopigana na huyo jamaa kutoka India) Kwa lugha nyingine lilikuwa kwenye level gani hilo shindano lao?
    Au bingwa wa dunia mnataka mpaka awashinde kickboxers wote duniani?

    Ngoja nikasachi kickboxing nione maana sina kazi ya kufanya iliyobaki ni udaku tu.

    Happy boxing days maboxers wa Ukerewe na Usagara!!

    ReplyDelete
  21. Yaani waandikaji comments wengine humu ndani wanajifanya wanajua saanaaaaa kumbe wajinga wajinga tu. I wish watu wote wangekua wanaandika na kujulikana ni nani...acheni majikuuu.....Mbona wengine wanaita Thanks giving Turkey day nao mtawaita wajinga au washamba????? Acheni hizo....

    ReplyDelete
  22. Anonym 26/12/07 2:54 na wengine wote wanaojaribu kumfanya Michuzi kuwa ni mungu (anajuwa kila kitu) kwa hapa si mtetei nimeiiyangalia habari critically, nna 100% michuzi alikuwa hajui maana ya "BOXING DAY" kwani michuzi ni nani?si binaadamu kama wewe anweza akajuwa mengi lakini pia akawa hajui mengi mfano hili la boxing day,Kutembea sana duniani au kusoma sana sio kigezo cha kujuwa kila kitu!! Acheni kutaka kumgeuza michuzi "Mungu mtu" hata yeye mwenyewe naamini hapendi kufanywa hivyo, na kwa busara yake nnayo ijuwa mimi basi atatowa tamko juu ya hili, yaani atakiri kwamba hapa ameelimishwa juu ya boxing day.MIchuzi haogopi kuelimishwa sababu ni mtaalam alielimika(anajuwa kamba hajui kila kitu)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...