May 2007
no image
BARUA YA WAZI KWA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WATANZANIA UINGEREZA

31.05.2007

Abubakar Faraji
Mwenyekiti
Jumuiya ya Watanzania Uingereza


Ndugu Mwenyekiti

YAH: USIMAMIZI WAKO WA KADHIA YA UKAGUZI WA MAGARI YAENDAYO TANZANIA

Nadhani barua hii itakukuta katikati ya shughuli za kawaida za kimaisha pamoja na kushughulikia masuala ya jumuiya.

Kama mmoja wa Watanzania waishio Uingereza napenda kukuandikia waraka huu kukuelezea masikitiko yangu juu ya namna unavyolishughulikia suala hili.

Nimelazimika kuchukua hatua hii licha ya ukweli kuwa na mimi ni mmoja wa wajumbe wa kamati mojawapo mpya zilizoundwa, hii ni kwa vile Mwenyekiti umeamua kulitolea kauli suala hili bila kufanya tafakuri na mtu yeyote ndani ya Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza.

Jitihada zangu za kukushawishi ujizuie kutoa tamko hadharani mpaka hapo utakapo kutana na wajumbe wenzako japo wa kamati ndogo ya Utendaji zimeshindikana, nimelazimika kuandika waraka huu kuelezea maoni yangu hadharani ili ieleweke wazi kwamba katika hili Mwenyekiti unaiongoza vibaya jumuiya.

Taarifa zako kuhusu kadhia ya WTM Utility Services na TBS zinaonyesha Mwenyekiti haupo katika upande WA Watanzania walio wengi, zinajikanganya na hazitoi picha halisi ya maumivu na dhulma ya dhahiri inayoonekana kufanywa kwa Watanzania:

Taarifa hii kuhusu mkataba huu usio na maslahi kwa Watanzania ilianza kujulikana kupitia tovuti yako binafsi
www.tzuk.com tarehe 26.05.2007 ambapo uliitoa kama habari tu. Kama Mwenyekiti wa Watanzania mwenye jukumu la kusimamia maslahi yetu tulitarajia kwamba ungetoa maelekezo haya hata katika tovuti ya Jumuiya www.tzcommunity.co.uk ili watanzania wajue kuwa kuna utaratibu mpya wa ukaguzi. Ni taarifa ambayo inawagusa watanzania walio wengi kama sio wote waishio nchini hapa, hukuona umuhimu wa kuweka taarifa hii katika tovuti ya Jumuiya badala yake ukaweka katika tovuti yako binafsi ambayo kama mmoja wa waandishi wa tovuti hiyo siku za nyuma,nafahamu kwamba inaendeshwa kibiashara…


Kuna maswali mengi hoja namba moja hapo juu:

- Je ulipokea malipo yoyote katika kutoa taarifa hii kwa Watanzania waishio Uingereza?
- Kama Mwenyekiti wa Watanzania hukuona umuhimu wa kutaka kujua zaidi na kuwasilisha maslahi ya watanzania ikiwa ni pamoja na kutaka kuhoji baadhi ya matatizo ya dhahiri ambayo yamejionyesha katika taarifa yenyewe?

Baada kufanya mawasiliano binafsi nawe, tarehe 28.05.07 ulikiri kuwa umepokea malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania, lakini hukuona umuhimu wa kuitisha mkutano wa wajumbe wenzako kujadili hili? Badala yake tarehe 30.05.07 ulitoa tamko kuwajulisha watanzania kuwa umepokea malalamiko yao na kama Mwenyekiti unafanya jitihada za kutoa tamko, ndani ya siku tano baada ya kukusanya ushahidi toka pande zote. Siku ya pili 31.05.07 umekurupuka na kutoa tamko kuelezea yaliyojiri katika mazungumzo yako na TBS, pekee!

Ukweli ni kuwa katika mazungumzo yetu baada ya tamko la kwanza, ulisema kikubwa ulichoongea na wadau husika [TBS] waliotoa zabuni kwa kampuni moja tu kufanya ukaguzi huu wa magari ni kutaka kujua vigezo wanavyoangalia katika ukaguzi. Licha ya kuwa hukushariana [kwa mara ya pili na kiongozi yeyote mwenzio ndani ya jumuiya na licha ya kukusihi sana usiendelee kutolea tamko hili suala mpaka hapo umekutana na wenzako wote] na yeyote, kwenye maelezo yako marefu ya tarehe 31.05.07, Mwenyekiti kipengele hiki kikubwa kilichotawala mazungumzo yako na TBS hukukiweka kwenye taarifa!

Badala ya kutuelezea vigezo vinavyotumika kwenye ubora wa magari, Mwenyekiti taarifa yako imeelezea kwa kirefu historian na umuhimu wa ukaguzi huu bila kugusa maswali muhimu ya watanzania.
Ndugu Mwenyekiti kukusaidia katika kujua ubaya na uonevu wa dhahiri unaofanywa na TBS ikishirikiana na Kampuni hii changa isiyo na nyenzo za kufanya zoezi zito na kubwa kama hii nakuomba uzingatie maelezo niliyoyatoa katika blog yangu hapo jana: http://saidiyakubu.blogspot.com/2007/05/utaratibu-wa-mpya-wa-kukagua-magari.html

Natambua wazi kwa kueleza msimamo wangu hadharani, nitakuwa sitendei haki nadharia ya uwajibikaji wa pamoja [collective responsibility] lakini kabla hujanisuta kwa hili nakuomba urejee vitendo vyako binafsi kuhusu kadhia hii ambavyo bila shaka kabisa si tu vinakiuka nadharia hii bali pia kuna wasi wasi miongoni mwa watanzania kuwa huenda ni mgongano wa maslahi [conflict of interest] ambayo ni dhambi kubwa zaidi.

Lakini pia nadhani kwa kukaa kimya dhamira yangu ya kukubali kuwa mjumbe wa kuteuliwa kwenye kamati hii kwa maslahi ya watanzania wote itakuwa inanisuta, mimi nawe tumejuana kwa miaka takriban mitano sasa na tumetokea kuwa marafiki wa karibu lakini katika hili Mwenyekiti nimejikuta sina budi kuuweka urafiki wetu kando kuangalia maslahi ya wengi. Ni matumaini yangu Mwenyekiti utakuwa na nguvu na uelewa wa kutambua kuwa ni tofauti katika hili ndio zimetutetanganisha na iwapo tukijirekebisha na kufanya kazi kwa maslahi ya wengi hakuna kitakachoharibika

Tunakuomba Mwenyekiti ili kuendeleza Jumuiya hii changa utoe maelezo binafsi kujiweka kando na mkataba huu vinginevyo utakuwa unapoteza sifa ya kuwa msimamizi mzuri wa haki na maslahi ya watanzania wote kwani msimamo wako katika hili unaonekana kuyumba sana hususan ukionekana kuvutia upande mmoja ambao ni dhahiri sio unaopendelewa na watanzania walio wengi.

Ahsante Sana.

Saidi Yakubu
Mtanzania aishie Uingereza.


Nakala kwa:

BI MWANAIDI SINARE MAAJAR
BALOZI WA TANZANIA UINGEREZA NA MLEZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA.

WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA JUMUIYA YA WATANZANIA.

WATANZANIA WOTE WAISHIO UINGEREZA.


flaviana matata, binti yetu ambaye ni mmoja wa warembo 10 babu kubwa duniani, katua dar masaa machache yalopita na dege la qatar airways na kupokewa kwa shangwe na wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na maria sarungi-tsehai (nyuma yake, picha ya juu) pamoja na bosi wa masoko wa qatar airways tawi la dar teddy mapunda (anaenyoosha kidole picha ya chini) na wengineo. maria kanambia kwamba flaviana imebidi arudi leo na sio jumamosi kama alivyosema awali kwani viza ya binti yetu huyu ilikuwa imeisha...


jaji mkuu mh. barnabas samatta akwia ofisini mwake. mh. samatta anatarajiwa kustaafu mwezi ujao baada ya kuitumikia idara ya mahakama kwa ustadi na uaminifu kwa miaka yote hii, akiwa mrithi wa hayati jaji mkuu francis nyalali. hivi sasa mh. samatta yuko katika ziara ya kuaga mikoa mbalimbali....

mkurugenzi wa twanga pepeta asha baraka akiwa na waimbaji khalidi chokoraa (shoto) na charles baba wakijadili safari yao ya kenya ambayo imeelezwa hapo chini. wanaojua umombo tusaidieni...

TOPS FROM DAR-TWANGA PEPETA

DT 72 Olympianhero International NGO is set to hold massive fundraising events in Mombasa and Nairobi to feature African stars Band- Twanga Pepeta from Dar es salaam Tanzania.


The premier events to be dubbed TOPS FROM DAR set for Friday 1st June 2007 at the Safari Park Hotel and Saturday 2nd June at LeVans Park in Nairobi West. On Sunday 3rd June 2007 the action moves to Mombasa’s Black Havana from 2pm to dawn.


The events are to help raise funds for the construction of a healthcare facility centre for paraplegic disabilities to cater for rehabilitation, relaxation and research, to be constructed in Kikambala Mombasa.


The debut concert, to be held on Friday 1st June at Safari Park Hotel, will be attended by ODM-Kenya Presidential candidate Hon. Raila Odinga as Guest Star. Other ODM- Kenya luminaries are also expected to attend.


East Africa’s Star artistes, African Stars Band popularly know as Twanga Pepeta, is expected to hit the stage with bang. Their latest style of ‘Mugongomugongo’ is a must-see-to-be-believed spectacle. The band comprising of more than 20 artists is in high spirits, being the biggest orchestra in the region and all that. Comprising of Hamisi Amigolass band leader, and super vocalists Khalidi Chokoraa , Charles Baba and Ali Choki, Salehe Kupaza among others on the men side. The Ladies include Lady Lwiza Mbutu Nyoni (asst. band leader), plus best belly dancers in East Africa - Aisha Madinda, Lilian Internet and Janet Isimike are among the ladies.


Meanwhile the African Stars Group Chairman and CEO, Mr. Baraka Msiilwa who is crrently in Hong kong doing shopping for the band in readiness for the Kenya tour, said “last time I was in Nairobi with MK (muzki wa Kiafrika) group band in 1992 it was big. This tour, the band will come with pure African magic of Kutwanga and Kupepeta that by the end of the tour the Kenyan audience will no longer be interested any more in Congolese stuff like Koffi, Kanda Bongoman, Werrason etc. Our music is great since it is in Swahili, the fans will understand and interpret easily” said Mr. Baraka.


Dick Tiger Murunga the Chairman/CEO of DT 72 Olympianhero NGO is kindly requesting all Kenyans to turn up in big numbers to support these good cause events in Nairobi and Mombasa. “Every shilling contributed will be spent to help build the Paraplegic centre in Mombasa” said Mr. Murunga who won bronze in Olympics in 1972 and Gold in WBA. Tiger became paraplegic disabled in 2004 after leg muscles became stiff. He is yet to raise 3.5m to attend aquapunture treatment in China.


All roads in Nairobi lead to Safari Park on Friday 1st June to celebrate Madaraka Day in style with Twanga Pepeta band from Dar es salaam and Raila Odinga. On Saturday 1st June the party moves to LeVans Park Westlands. Sunday 3rd June from 2pm till dawn catch the action at the Mombasa Black Havana.

The program is being supported by Space Concepts and Starlight Marketing of Mombasa among many others.hiyo ndio meza kuu ilosimamia uchaguzi mkuu wa yanga leo ukumbi wa dayamondi jubilei na matokeo yametoka muda si mrefu ulopita na washindi ni kama ifuatavyo:


1. mwenyekiti - imani madega
2. makamu mwenyekiti - rashidi ngozoma matunda


3. katibu mkuu - lucas kisasa


4. katibu mkuu msaidizi - ahmed mamba


5. mhazini - abeid mohamed abeid


6. mhazini msaidizi - godfrey mwenje


7. katibu mipango - patrick fataa


8. katibu mwenezi - francis lucas
waliogombea walikuwa 51 na wapiga kura walikuwa 1025 kati ya wanachama zaidi ya elfu 5 ambao ni pamoja na wa makundi ya yanga asili, kampuni, bomba na academia.
vigogo walioshindwa ni pamoja na baraka igangula na kibo merinyo, mohamed bindha na ismaili idrisa katika nafasi ya uenyekiti.
vigogo wengine walioshindwa ni pamoja na saidi motisha ambao walianguka katika nafasi ya makamu mwenyekiti, shabani dilunga na patrick fataa aliyejitoa.
vigogo walioanguka nafasi ya katibu mkuu ni constantine maligo na emmanuel mpangala.
mchezaji wa zamani wa yanga bakari malima 'jembe ulaya' alianguka katika nafasi ya katibu mwenezi.
katika nafasi ya uhazini baadhi ya vigogo walioanguka ni castro mketto, jeremiah michael, paschal kiyomba na evarist mwang'onda aliyejitoa.
vioja: pale rais aliyemaliza muda wake francis kifukwe alipogoma kwenda kusimamia uhesabuji kura za mgombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti saidi motisha kwa kile alichodai 'mgombea hana kura za kusimamia', hivyo mgombea akaomba meza kuu imsimamie. pia wanachama waliinuka kucheza 'mugongomugongo' ya twanga pepeta wakati kura zinahesabiwa...
umbea: wanachama waliokataliwa kuingia ukumbini kupiga kura walisikika wakiapa kuwa wataenda mahakamani kupinga uchaguzi baada ya kunyimwa haki yao; madai ni kwamba kwa vile ilikuwa ni siku ya kazi pamoja na kuweko na mvua kubwa na foleni ya magari wengi wao walidai kuwa walichelewa kufika kwa sababu hizo...memba wa yanga wakikaguliwa uhalali wa kadi kabla ya kuruhusiwa ukumbini kwa ajili ya uchaguzi mkuu dakika chache zilizopita. tayari wagombea wote wameshanadi sera na kujieleza na matokeo yatatoka wakati wowote kuanzia sasa. nitawafahamisha. cha kufurahisha ni kwamba hadi naingia mitamboni hakuna bakora hata moja iliyorushwa kuonesha kwamba sasa jangwani ni shwari...

lucas kisasa (shoto) na emmanuel mpangala (kati) wakiwa na mmoja wa wadau wakuu wa yanga suleiman wakiteta jambo. kisasa na mpangala wanagombea nafasi ya katibu mkuu. hapo wanasubiri kwenda kunadi sera na kujieleza mbele ya wanachama

wadau ujumbe huu mwanana umeingia sasa hivi toka newala...
Michu! Mambo vipi mshkaji?
Natumaini mzima sana. Angalia hiyo picha nimekutumia niliyopiga Starbucks. Mwezi huu wana-showcase kahawa ya Tanzania katika starbucks zote hapa New York.

Starbucks ni very popular cafe sio nyc tu bali marekani nzima na hata duniani. Wanauza kahawa na chai bei ghali sana, around $5 kwa kikombe lakini wengi bado wananunua. Sasa kila msimu fulani huwa wanauza coffee beans kwenye paketi kama ya kwenye picha kutoka nchi mbalimbali kama kenya, ethiopia, rwanda, columbia nk.

Sasa ndio wanauza ya TZ katika maduka niliyoona hapa ny. Naamini pengine wanauza katika miji mingine katika msimu huu. Kuna maduka kama 500 ny state, kama 7000 marekani nzima na kama 6000 nchi za nje. Tazama www.starbucks.com/ourcoffees utaiona kama moja ya "featured coffees". Nimeona kwamba huo mfuko unauzwa $13 hivi.naam, kama wadau wengi walivyoshauri, mambo ya flaviana yameisha sasa tuhamie taifa staaz inayocheza na senego jumamosi hii uwanja wa ccm kirumba, mwanza. hapo unamwona kocha wetu mbrazil marcio maximo akiingia uwanja wa karume ambapo amepageuza kuwa kituo kikuu cha mafunzo kwa timu ya taifa. kila siku asubuhi na jioni anawafua kisawasawa tayari tayari kwa mtanange ambao hata jk atahudhuria. bahati mbaya hii haina kupiga kura kama kwa flaviana. dakika 90 ndio zitaamua. hivyo tuelekezeni dua zetu kwa staaz...

jide akiwa na wadau wakati wa ziara yake ughaibuni

Lady Jaydee & Machozi band live gig - every friday
Lady JayDee is so far the most decorated musician in Tanzania, winning an award almost every year from 2001 when she burst into the music scene with her jit 'Machozi'. Complete with her own band the songbird presents to you Lady Jaydee & Machozi Band Live Gig, Every Friday at Ruaha Bar & Restaurant at Kinondoni next to JJ Blue from 2000hrs - Midnite.
This is where beautiful people, friends, celebrities and music fans will connect to start off their weekend.
The Gig will give an outstanding showcase from Lady Jaydee giving you a cocktail of hit songs from all over the world, including songs from all time international greats the likes of Whitney Houston, Tina Turner, Bob Marley, Sade, Aretha Franklin, Marvin Gay...you name them - plus exclusive appearances from local chart toppers.
Come join Bongo's most talented local musician and enjoy your evening...
for more information call +255 784 884 007 or visit www.ladyjaydee.com


mtangazaji wa radio uhuru fm na mjumbe wa baraza la vijana wa ccm mkoa wa Dar violet mzindakaya mpogolo (sister v) akirejesha fomu ya kugombea ujumbe wa halmashauri kuu taifa (nec) kwa kaimu katibu msaidizi wa mkoa wa rukwa ndugu hamis kibonde jana. waandishi na hata wanamichezo kibao wanawania ujumbe wa nec ambapo leo mwanariadha nyota wa zamani filbert bayi na katibu mkuu mstaafu wa simba michael wambura wamefanaya hivyo pia


Wadau wapendwa duniani kote mnaosoma blogu hii!

Samahani kwa kuchelewa kuleta taarifa, kwa kweli jana mara baada ya mashindano kulikuwa na hafla ndogo lakini tulishindwa kuondoka mapema kwani Flavia alikuwa ni gumzo kila kona. Kila mtu alitaka kupiga picha naye na kila mtu alitupongeza.

Kama mnavyofahamu Flavia kaingia 10 bora! Nationalo director wengi wamenifuata na kuniopngeza wakisema kuwa Tanzania imekuw mfano bora kwani ni mara yetu ya kwanza na tumepenya 15 bor, na baada ya raundi ya kwanza tumeingia 10 bora! Nchi pekee iliyofika htua moja mbele kwa njia hii ni Botswana ambayo ilitoa mrembo Mpule kama Miss Universe.

Kwa kweli inbidi Tanzania tujipongeze sana, kwani mrembo wetu ameipeperusha vyema bendera. Ingawa nilikuwa mtanzania pekee kwenye ukumbi lakini baada ya kutangazwa 15 bora, waafrika na watu weusi kam vile Curacao na Bahamas walihamisha ushabiki wao Tanzania na walinisaidia kupeperusha bendera.
Lakini muhimu zaidi Flavia alishangiliwa sana na wenyeji wake watu wa Mexico! Mashabiki hawa waliposikia matokeo ya 5 bora na walipoona kuwa Mexico na Tanzania hawajaingia walianza kumzomea mrembo wa Marekani Rachel Smith.
Rachel alidondoka kwenye steji wakati wa mashindano ya vazi la jioni. MAshabiki wa Mexico waliendelea kumzomea mrembo huyu wa Marekani mpaka wakati wa kujibu swali. Ushabiki baadaye ulihama kwenda kwa Brazil na alipotangazwa mshindi kuwa Japan, watazamaji wengi walionekana kutofurahia sana matokeo.

watalaam wa masuala ya urembo wanaendelea kuchambua matokeo ya mwaka huu na wengi wamesema wazi kuwa mwaka huu bara la Asia lilikuwa lishinde. Hata hivyo kulikuwa na ushindi mkali sana kwani mrembo wa Korea alionekana kuwa na vigezo zaidi ya mrembo wa Japan.

Baada ya ushabiki na uzalendo kumalizika, watu wengi wamekubali kwamba moja wa warembo waliotia fora katika mashindano haya ni Flaviana Matata wa Tanzania. Mrembo huyu ana matumaini makubwa sana ya kuendelea kufanya vyema kimataifa hususan katika dunia ya ulimbwende (modeling).

Zawadi la Miss Photogenic limeenda kwa mrembo wa Ufilipno kwa mara ya 3 sasa, jmbo ambalo halijapokelewa vyema na mashabiki na watazamaji kwani wanadai kuwa ameshinda kwa wingi wa kura za uzalendo na si kwa kustahili
Zawadi la Miss Congeniality yaani mrembo wenye ucheshi na laiyepigiwa kura na warembo wenzake ni Miss China.
Maelezo zaidi nitakaporudi, Alhamisi. Flavia anategemea kutua tarehe 2 mijini Dar-es-Salaam. Asanateni sana Watanzania wote kwa ushirikiano na support mliyompatia mrembo wetu. Tanzania juu!!!

Zawadi la Miss Congeniality yaani mrembo wenye ucheshi na laiyepigiwa kura na warembo wenzake ni Miss China.

Maelezo zaidi nitakaporudi Alhamisi. Flaviana anategemea kutua tarehe 2 mjini Dar-es-Salaam. Asanteni sana sana Watanzania wote kwa ushirikiano na mliyompatia mrembo wetu. Hii imedhihirisha kweli kwamba kwamba Tanzania tunapendana na tunapenda mafanikio na Mungu akipenda iko siku tutapata makubwa zaidi - amen
Maria Sarungi-Tsehai
ukitaka kumuona flaviana alivyokuwa akijichanganya bofya hapa

hatimaye miss universe ishafanyika na binti yetu flavian matata amemaliza akiwa ndani ya 10 bora. matokeo kamili ni kama ifuatavyo. wanaojua kiinglishi watanisaidia kutransleti kwani kama mjuavyo mie kwangu hicho kin'geng'e iz noti richebo...

Miss Japan, Riyo Mori Crowned MISS UNIVERSE 2007
This evening, during one of the year's most exciting live international television events, a star-studded panel of judges chose Miss Japan, Riyo Mori, as MISS UNIVERSE(R) 2007.

Ms. Mori is 20 years-old and has been dancing since she was 4. She loves traveling the world and enjoys visiting museums and watchingmusicals.

The judging panel for the 2007 Miss Universe Pageant included NBC's"Heroes" James Kyson Lee, NBC's "Deal or No Deal" briefcase model LindsayClubine, Dallas Cowboys quarterback Tony Romo, rocker Dave Navarro, Worldand Olympic figure skating champion Michelle Kwan, fashion designer Marc Bouwer, Novela Star Mauricio Islas, "Project Runway" judge and Ellemagazine fashion director Nina Garcia, and former Miss Universes DayanaraTorres (1993) and Christiane Martel (1953).

Throughout the two-hour event, contestants from 77 countries around theworld competed in three categories: swimsuit; evening gown; and personality interview.
Zuleyka Rivera, Miss Universe 2006, crowned her successor at the conclusion of the two-hour primetime telecast, before an estimated worldwide viewing audience of more than 1 billion in over 170 countries.

Final Results:
First Runner Up: Miss Brazil, Natalia Guimaraes will assume the duties of MISS UNIVERSE 2007 if the title holder forsome reason cannot fulfill her responsibilities.
Second Runner Up: Miss Venezuela, Ly Jonaitis


Rest of Top Five: Miss Korea, Honey Lee; and Miss USA, Rachel Smith.
Rest of Top Ten: Miss India, Puja Gupta; Miss Angola, Micaela Reis;Miss Tanzania, Flaviana Matata; Miss Nicaragua,Xiomara Blandino; and Miss Mexico, Rosa Maria OjedaCuen.

Rest of Top Fifteen: Miss Thailand, Farung Yuthithum; Miss Denmark, Zaklina; Sojic; Miss Slovenia, Tjasa Kokalj; MissUkraine, Lyudmyla Bikmullina; and Miss CzechRepublic, Lucie Hadasova.

Miss Photogenic Award:

Miss Philippines, Anna Theresa Licaros. The general public voted on http://www.nbc.com for the delegate who exemplifies beauty through the lens of a camera. She received a $1,000 cash prize and a trophy from Rogaska Crystal.

Congeniality Award:

Miss China, Ningning Zhang. This award reflects the respect and admiration of the delegate's peers,who voted for her as the most congenial,charismatic and inspirational participant. She also received a $1,000 cash prize and a trophy from Rogaska Crystal.
The MISS UNIVERSE 2007 prize package includes:
Official Miss UNIVERSE
Mikimoto pearl tiara; 2 Year Scholarship from The NY Film Academy in NYC; custom designed wardrobe by Tadashi;
National and International multi-media advertising campaign and a complete denim wardrobe from YMI Jeanswear;
Swimsuit wardrobe from BSC Swimwear Thailand;
Shoe wardrobe from Nina;
A Ritmo Mundo Jumbo Jet Mystery Dial time piece;
Year-long supply of hair care products and tools from Farouk Systems; Membership to Gravity Fitness and papering at John Barrett Salon;
Fashion Portfolio by leading fashion photographer Fadil Berisha;
Consultation with stylist Billie Causieestko;
New York City apartment for the year of her reign including living expenses; professional representation by the Miss Universe Organization and Trump Model Management; and a personal appearance wardrobe.


nawaletea habari njema wote wanaotaka kusafirisha magari toka uk kuja bongo. kazi kwenu kwani jamaa ndo wameshapata baraka zote za tbs. pichani ni bw. mayalla akipokea cheti cha tbs toka kwa bsoi wa taasisi hiyo kinachomuidhinisha kufanya shughuli hiyo...


Pre-Inspection of all vehicles shipped(exported) to Tanzania from the UK


The Tanzania Bureau of Standards (TBS) has granted WTM Utility Services Company of UK to pre- inspect all vehicles exported to Tanzania as from May 14th, 2007.


Director of WTM Mr Wilson Mutabazi told this blog that they will be a mobile unit for this exercise and upon request they can travel and collect any vehicle/s and be delivered anywhere in UK after inspection. There will be 5 inspection centres for this that are soon to be opened.


For more information please visit our website at wtmutilityservices.com or ring 0788 769 4186 or 0777 168 2378 in the UK. Or you can know more about this venture thru http://www.tzuk.net/index.php?option=com_content&task=view&id=3621&Itemid=39


Tanzania branch contact Mr Niko on +255 754 958 95 or Mr Mayalla on +255 784 929 361,


office Tel-Fax +255 2 221 7034 and their offices can be located at Kawawa Rd and Kiyungi st.opposite roman catholic churh-Magomeni.
CLARIFICATION
1. Pre - shipment from Japan inakuwaga around $200 by JAAI hamna anayelalamimika.
2. Other E. African countries wana requirements kama hii, Kenya wameteuwa Cotecna, fee is around £98 pounds excluding travel for inspection person,
3. Mot inspections is a uk government directive, regulations zao tofauti kidogo, Hiyo price imekuwa set hivyokwa ajili ya several reasons, a) bei ni political if it is too high basi watu watalalamika, b)it is not realistic since average labour cost for a mechanic/inspector is £50 per hour minimum two hours.
4. Penalty fees are upto 40% of the value of the car..assuming vehicle costs £3000 freight 1000, penalty is 40 % of cif works to about £1600 excluding customs, vat import fee storage etc.
5. The company pays a large sum to get the license, it has to pay it back onE way or another.
any more questions?

naona wadau wamepania kunigaragaza na maadobe yao. ah, nifanyeje wakati nawapenda na kuwaheshimu wote zaidi ya kuwaridhia matakwa yao?


naomba anika hii kitu hadharani na uwajulishe wadau espeshali wale wa bwawa la maini kama ulishachukua fomu za uanachama Milan.

Its me MAN U- ORIGINAL
no image
hapa kuna ujumbe mwaridhawa kwa wasomi
Dear Friends,
On Saturday 5th May 2007 Peers Group (Group of Graduates) had an Annual Dinner Attended by more than 70 Peers. Barclays Bank and SimbaNET Limited who were official Sponsors gave a presentation regarding their services.
Barclays Offered $ 500 and SimbaNET $ 1500. Barclays offered Unsecured Loans for all Peers Group Members up to TZS 30 Million as a special package for Graduates.
SimbaNET Offered VSAT Connectivity for Internet as special offer for Peers Group Members with unlimited access on 24 hours basis for $ 1500 (Equipment) instead of $ 3000.
During the Event, Mr Richard Kasesela, Mr. Alloysce Midelo, Dr. Ulomi and Mr. Mtsimbe all made brief presentations on different matters of National Interest. Dr. Milton Makongoro Mahanga, Deputy Minister of Infrastructure Development made a general remark of the occasion. He then Launched Peers Group Website: www.peersgroup.org
Some Peers then made various comments and contributions. There was also a fund raising occasion where more than TZS 5 Million was pledged. Complete report, minutes and pictures of events have all been posted to our website www.peersgroup.org
There is now an initiative of calling the General Assembly of all Graduates and Intellectuals (Peers) so that a formal leadership and initiatives can be formed. The same will be called in June/July and efforts are being made to invite Peers HE Jakaya Kikwete and Hon. Edward Lowassa.
Membership to Peers Group is FREE as long as you are a Graduate, but you must always have POSITIVE ATTITUDE. For Further details visit www.peersgroup.org
or contact:
Sanctus Mtsimbe (B.Sc.; M.Sc.)
Peers Group Coordinator (Group of Graduates and Intellectuals)
Mob. Tel: + 255-754 833 985