waziri wa fedha mh. zakhia hamdan meghji akiwa na viongozi wapya wa benki kuu profesa beno ndulu (karibu na kamera) na naibu gavana dk enos bukuku (kulia) na katibu mkuu hazina mh. gray mngonja (tai buluu) baada ya kuzindua bodi mpya ya benki hiyo ambayo kaiagiza ifanye kazi kwa ufanisi na kusafisha jina la bot kwa kuhakikisha kwamba kashfa ya epa inashughulikiwa ipaswavyo. bahati nzuri ama mbaya mh. waziri meghji alikuwa bize sana kiasi akakosa nafasi ya kuteta na waandishi baada ya uzinduzi huo kwani alikuwa anawahi shughuli sehemu ingine

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. NADHANI WAKATI UMEFIKA BoT IWE NA BODI SIYO KOFIA MBILI YA UGAVANA NA MWENYEKITI WA BODI HIYO NDIYO ILIYOZAA MATUNDA YA WIZI TUNAOUJADILI WAKATI HUU.

    ReplyDelete
  2. Michu counter ya idadi ya wageni kwenye blog haionekani hapa kwenye kompu yangu umefanya makusudi ama ni wahuni wameiteka ili wajizolee dola 500. lete ufafanuzi!
    mdau finland

    ReplyDelete
  3. Huyu Meghji lazima na yeye yumo kundini! Huwezi kusema ulisiani documeny ambayo baada ya siku nne uka-withdraw! Inaonyesha kuna mtu alimstua kuwa achana na huo ulaji, muda si mrefu watu watatapika! Maana haiingii akilini kwa Waziri kusaini kitu eti kwa kigezo cha kuwa alishauriwa?!?! Ina maana yeye amekaa ofisini muda wote anasubiri kushauriwa badala ya kutumia akili zake mwenyewe?

    Hiyo itakuwa ni experimentation ya office ya serikali! Haiingii kichwani kabisa excuses zake, mpaka amefikia sehemu anadai eti kwa sababu yeye ni mwanamke ndo maana wanamwandama?!! Kama weakness iko kwa uanamke wake, basi aachane na kazi zinahitaji speed kubwa na nguvu za wanaume kama hiyo! Maana kusingizia eti kwa kuwa yeye ni mwanamke ndo maana wanamwandama, mimi sikumwelewa kabisa kabisa. Binafsi.

    Lakini issues ni kwamba amehusika moja kwa moja na kosa. Kwa mfano, mimi siwezi kuiba kitu nikakamatwa na POLICE then niwaambie POLICE kuwa ati ngoja nirudishe hiki kitu ili mniachie maana sitakuwa na kosa!

    Najua anazungukazunguka tu, lakini atalipuka tu. Ngoja Balali arudi.

    ReplyDelete
  4. Na wee michuzi pia umo kwenye timu ya mafisadi mshenzi wee. Kikwete kashirikiana na Balale kuiba mamilioni, tukielezea "conspiracy" yao, unakataa kutundika humu kwenye blog yako ya serikali. Lakini poa tuu, kitakapowaka Kikwete, Balale, Lowasa, wewe na wevi wengine wote tutawaweka kundi moja. Kama unadhania sisi mafala kwamba kikwete anang'ata halafu wewe unapuliza, basi wee subiti tuu.

    ReplyDelete
  5. Mwongo huyo! Hkuwa bize wala nini, alikuwa anaogopa maswali.

    ReplyDelete
  6. Hiyo bodi itasafishaje BOT wakati mikono ya Mngonja ni michafu? Au tunataniana hapa?

    ReplyDelete
  7. hongera meghji kwa kazi yako, all the best

    ReplyDelete
  8. Sio meghji tu aliye kwenye huo ulaji bali kuna vigogo wengi tu waliohusika. Kuna taarifa kwamba serikali imemficha balali kusikojulikana ili asije kutoa ushahidi kwa kuwa anayo hasira kwa kutajwa yeye mwenyewe huku wachunguzi waliochunguza huo ufisadi wakijaribu kuwaficha baadhi ya vigogo ambao hawataki wajulikane hadharani ili kufunika kombe mwanaharamu apite.

    Balali ametolewa kama kafara tu ili kuficha ukweli wa sakata lenyewe. Pia kuna habari kwamba wachunguzi walichezea hesabu. Kiasi halisi cha pesa zilizoibwa ni zaaidi ya billion 300. Hiyo hesabu tunayoambiwa kwamba ni billion 133 ni ya kupikwa. Hili limefanywa kwa makusudi ili kuwapoza wananchi wasiwe wakali sana. Hii hasa nikwa sababu kiasi kikubwa cha pesa zilizochotwa zilielekezwa kwenye kampeni za uchaguzi wa kishindo. Sasa kwa ville wananchi walio wengi ni walio wengi ni mazezeta tukiambiwa kwamba pesa zote zimeibwa na balali tunakubali.

    Kwanza haiingii akilini kwa nini huyo naibu gavana alibakizwa na mbaya zaidi akapandishwa cheo. Nim kwa jinsi gani hakuhusika kwenye huo ufisadi wakati yeye ndiye aliyekuwa mshauri mkuu wa balali au kwa kuwa ni mwanamtandao yupo hapo kulinda maslahi ya wakubwa?

    ReplyDelete
  9. Ni kweli kabisa wewe annon unayeongelea ufisadi. Inaelekea hii issue ya ufisadi inawezekana isije julikana daima. Mimi nina wasi wasi kabisa mambo yakaja kupotea kimya kimya baada ya muda!

    Tatizo la bongo misamiati mingi mno mpaka inatuvuruga. Tulianza na mambo ya MAHAFIDHINA kule Zenj, tukazubaa zubaa hata bila ya kuelewe maana yake hasa, ghafla ikaja msamiati wa UTAJIJU! Wakati tukiendelea kutafuta maana yake ghafla tu ikaibuka issue ya MKANDAMIZAJI! Tukingali tunaendelea kutafuta nani anayekandamizwa, imeibuka FISADI! Mwanzoni sisi wengine tulidhani ni tusi kubwa sana, ingawaje mpaka sasa hatuelewi maana yake, bila shaka kuna terminology nyingine itazuka na Balali pamoja na kundi lake tutawasahu. NJII HII BWANA,,, hatuiwezi kabisa msee!

    ReplyDelete
  10. Hizo zote blahblah kibao, hilo kundi lote hapo linajifanya halijui kilichokuwa kinaendelea BoT!

    ReplyDelete
  11. mdau wa finland naomba tuwasiliane kuna mambo napenda unifahamishe, email yangu ni
    kimondo1978@yahoo.co.uk

    naitwa constantin

    ReplyDelete
  12. Ndugu Wadau mie hainiingii akilini,ati Naibu Gavana anapandishwa cheo.hapa wanajaribu kufichiana makosa.Kilichokuwa kinafanya hapo wote wanajua wakiamua chota pesa ata Naibu anamgahao wake.Sasa itawezakana vipi ati Naibu alikuwa ni mtu poa???????? Mie nilidhani kikwete angechagua watu wapya kabisa hapo BOT.sio kupandishana Vyeo. Wote hao walikuwa group moja la ufisadi.

    ReplyDelete
  13. Kuna uwezekano mkubwa huyo Nd. Gray Mgonja naye akawa amehusika na ubadhirifu wa mabilioni hapo benki kuu. Na kuna uwezekano mkubwa kuwa ametajwa kwenye ripoti ya E&Y kuhusiana na ubadhirifu huo. Sasa sielewi itakuwaje ndani ya kikao cha bodi wakati wanajadili ubadhirifu huo wakati mtuhumiwa mmoja wapo naye yuko miongoni mwa wajumbe. Itakuwa vyema iwapo Mh. JK akamweka pembeni huyu bwana kwa muda wakati uchunguzi ukiendelea.

    ReplyDelete
  14. kweli usilolijua ni kama usiku wa giza.... wajameni ngoja niwaambie Naibu Gavana alieteuliwa kuwa Governor aliteuliwa na rais less than 3 months ago... Rais alimteua Prof Ndulu aliekuwa anafanya kazi UN then, na DR Mkilla kuwa manaibu gavana wakimsaidia reli ambae nae aliteuliwa early 2007. wote watatu walikuwa ni msaada kwa Gov Balali who at the time hakuwepo hata nchini. kwa hiyo mjaribu ku-argue in those grounds

    ReplyDelete
  15. Wanatuchezea mchezo wa kuigiza na mazingaombwe na sie tumekaa pembeni tunashangilia 'amechukuaa, amewekaa, waaaaaa!!' Wabongo jamani! Mbona wamekazania EPA, EPA hizi account nyingine vipi? Wafanyakazi huko BoT wamekopeshwa mamilioni, wanaishi kwenye mapalace, wanaendesha magari ya kifahari, watoto wao wanasoma kwenye shule za bei mbayaaa! Hata kama ni mikopo pamoja na kuiba watarejesha vipi wakati mshahara wa mfanyakazi wa serikali unafahamika??? Wataifishiwe majumba yao ya wizi wa kodi za watanzania masikini fedha zirejeshwe kwenye zahanati za kata na ujenzi wa shule za sekondari! Wallah msituchangishe teeena!!

    ReplyDelete
  16. Mgonja hajahusika kabisa,yeye ndie aliwatuma Deloitte kufanya audit,na ex Governor alipodanganya, alimuibua
    wanaosema amehusika ni ma agent wa mafisadi wanaotaka kumuuangamiza kwa sababu ALIWALIBUA.Yeye ni WHISTLE BLOWER na cover yake imekuwa blown up.
    Balali had the full mandate of managing the funds.Ma lawayer, analysts, funds managers,auditors wa BOT waulizwe wali approve vipi.Mgonja's role as Director of Board will be revealed in the investigation.He questioned alot kwenye bodi

    ReplyDelete
  17. Hili Suala la BoT tusubiri wengi wataaibika kama kiliamuliwa kufuatiliwa kikweli kabisa Balali katolewa kachumbari tu kwani aliiba peke yake? Kwanini afukuzwe mmoja hizo kampuni 22 zilizohusika Serikali inachukua hatua ipi? Haka ni kamchezo Watanzania ndio kawaida yetu tutasahau sasa hivi ingekuwa Kenya moto ungesikika remember goldenburg.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...