Nini wa Mars!!Sisi wa pluto muda mreeefu tulifika!!!Tengenez mazingira mazuri kaka ya akupata mshindi wa uhakika!!!
Spoiler!!

------------------------------------------------------------------------------------------------

hahaha! wadau msikonde na wala msirushwe roho na hawa wadau wa mars na pluto ambao naawahakikishia kwamba kwenye dola 500 hata wafanye ufisadi vipi hawataona ndani. jopo la ufundi la globu yenu hii ya jamii liko makini kwa wadau hao toka sayari ingine. vile vile nawaambia wadau hao wa sayari zingine kwamba hii dola 500 ni ya mdau wa hapa hapa duniani.

-------------------------------------------------------------------------------------------------

kuna wadau ambao wameuliza swali la msingi kwamba endapo hawatokuwa ama hawana kamera wafenyeje kuweza kuunasa ukurasa pindi hesabu ifikikiapo milioni 3. ni rahisi sana na kama utafuata maelekezo (fanya tizi kwanza) utaweza tu hata kama huna kamera.

1. fungua ukurasa wa globu kama kawaida

2. angalia vitufe vya kompyuta yako upande wa juu kulia utakuta kimoja kimeandikwa 'print screen/sysr9' ama kama ni laptop imeandikwa PRT Sc/ Sys Rq. kibonyeze hicho ambapo utakuwa umekopi ukurasa wote

3. Nenda chini shoto kwenye All Programs, bofya na elekeza mshale kwenye 'accessories' ambapo itakupeleka kwenye orodha ndefu ambapochagua 'paint' na bofya.

4. ukishabofya 'paint' litakuja dirisha. angalia juu shoto nenda kwenye neno 'edit' ambako ukibofya utatafuta neno 'paste' ukibofya tu, ule ukuruasa wa glob utakuja wote hapo.

5. kwa kuwa ukurasa ni mkubwa itabidi uupunguze. bofya 'image' ambapo utakutana na neno 'resize/skew' na ndani ya hiyo kuna tarakimu 100 ziko mbili. badili tarakimu weka 50 kwenye kila hizo 100. sema 'ok'. na saizi itapungua.

6. nenda juu shoto kwenye neno 'file' ambapo ukibofya litakupa orodha ndefu. nenda kwenye 'save as' na kisha utabofya hapo na box litakuonesha kwa chini 'save type as' ambapo utabofya na kupelekwa kwenye orodha. chagua 'jpeg' na pia kwenye 'file name' weka jina kama ni 'blog' ama jina lako. hapo usisahau sehemu ya kulihifadhi faili hilo. nakushauri chagua 'desktop' juu shoto. kisha bofya na ukurasa utakuwa umehifadhi ukurasa.

7. fungua internet explorer kama unavyotaka kutuma email. bofya 'attach file' panapotakiwa kufanya hivyo.

8. nitumie faili hilo kupitia issamichuzi@gmail.com

9. penye ujumbe weka anuani yako ili iwe rahisi kukufikia.

10. subiri maelekezo ya namna utavyopata dola zako 500

*Tafuta ushauri kwa mwenye kuifahamu kompyuta akusaidie endapo maelekezo yatakushinda.

*wanaotaka kufanya ufisadi wasijisumbue kwani nina njia zangu za kung'amua posti kanyaboya kama za hao wadau wa mars na pluto


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Je mie nayetumia Macintosh na sina kamera nifanyeje?

    ReplyDelete
  2. michu wlaa usijisumbue kufundisha as mie mshindi nitakua na camera na kila kitu siku ikifika...kwa hiyo hizo dola mia tano we niandalie tuu
    na vipi zile dola mia 5 zangu zingine???za arsenal na man utd??

    dola 1000 mtaji tosha wa kuanzisha bnez la nguvu

    ReplyDelete
  3. Kawaida simba mwenda pole ndie mla nyama..bro michu umesomeka vyema maelezo yako kwa sie tuliokuwa kwenye mapori natumai hiyo Usd 500 itabaki kwenye nchi yetu ya mafisadi....

    ReplyDelete
  4. Michuzi!, thats why you are MICHUZI and I pray for you to get michuzi as your name is, yaani mapene au fweza,

    I don't know what you are getting for doing all these stuffs for us, but what I can say now is 'BLESS YOU' you have done alot, u just don't know, hebu fikiria, stress mashift kwa mpigo, kukumbuka home, box kwa sana ukirudi home hoi, huna hata mtu wa kucheka nae, wachikaji mnaonana mara moja kwa wiki, so unaishia chumbani wewe na pc, then ukiingia bloguni basiii weeeeee yani huna mbavu, nakuheshimu kwa hilo michuzi,

    the main point here, ilonifanya niandike huu ujumbe nikuhusu maelekezo yako hapo juu, u know what, you can even make a good teacher or instructor, mi ni mwalimu wa computer, yani umeeleza vizuri sana kwa malena wakifuatilia hayo maelezo basi mambo tambarare, what impressed me is, you dedicate your time and write that long paragraph, you know I found myself reading the whole thing, and I was like wow!

    good day michu!

    ReplyDelete
  5. Bro michu vipi, najiandaa pat adola zangu vipi kuhusu zile dola zangu za Man U vs Arsenal. Nasubiri Kaka. Sijui na huo utaita ufisadi?

    ReplyDelete
  6. hivi kwa nini neno FISADI linatumika ndivyo sivyo?maana mimi ninavyojua FISADI ni mtu anayechjukua wake za watu na hapa linatumika kama mwizi,inakuwaje?naomba kutolewa tongo wadau


    mzushi.com

    ReplyDelete
  7. namuunga mkono mdau wa January 23, 2008 3:07:00 AM EAT, mimi ni bonge la kishoka mambo ya computer lakini maelekezo yake nimeyafuatilia na nimefaulu, and quess what, itanisaidia kwenye kazi zangu nyingine pia, nakumbuka kuna wakati nilikuwa napata error kwenye mambo yangu ya kazi, nareport wananiambia ni print screen waone tatizo lakini wapi, sasa nipo fit zije tu errors
    Ubarikiwe sana michuzi na uongeewe zaidi na zaidi

    ReplyDelete
  8. Wa mars inabidi wabadilishe saa zao ziendane sawa na za duniani.

    Gwangju, Korea ya Kusini, tumefanya hivyo.

    omarfh@gmail.com

    ReplyDelete
  9. Mdau wa milioni tatu anakaribia sasa kweli omarfh@gmail.com kutoka Koreaaaaa!!!

    ReplyDelete
  10. Vipi mbona ilipokaribia kufika milion 3 comp yangu inaandika error # 10, kuna ufisadi hapa?

    ReplyDelete
  11. Naona wajanja wamepata pesa, I missed for a second, toa hiyo pesa kaka michuzi, kwa huyo mshindi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...