Amini usiamini majadiliano tunayofanya kwenye makundi pepe na kupitia blogu mbalimbali, maoni endelevu yanayoandikwa humu yanawafikia watu kadhaa na pale inapowezekana hatua mahsusi zimechukuliwa.

Picha inayoonekana hapo amenitumia rafiki yangu mmoja aliyoipiga jana eneo la Mwananyamala baada ya mvua kunyesha. Nomba kuifikisha kwa wadau, tafadhali tunaomba mchango katika hili.

Tushirikishane mawazo na suluhisho la matatizo madogo madogo kama haya ambayo tukiyazuia ni rahisi sana kuepuka magonjwa ya mlipuko na kwa hivyo angalao kupunguza idadi ya wagonjwa wa mara kwa mara ambapo kukosekana nguvu kazi yao huchangia pia kupungua kwa uzalishaji na ujenzi wa nchi.

Tujadiliane tafadhali. Hii ndiyo faida ya elimu kwa njia ya mtandao wa intaneti hata ikiwa inawafikia wachache, hao hao wachache ndiyo wanaohusika na kutoa chachu na maelezo ya kimaendeleo.

Elimu muafaka ni kito cha thamani!

Mdau Subi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. kwa kweli hapo hakuna mchango wakutolewa kwa wakati huu hasa kwa kuzingatia kuwa nchi yetu bado changa na wakati utakapofika wahusika wataliangalia hilo na wala sio hilo tu na mengi mengineo ya muhimu katika jamii tuwapeni muda mambo mazuri hayataki hara pole pole ndio mwendo

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi pole kwa kazi,mimi kama mkereketwa hiyo picha hapo juu imenitisha sana,maoni yangu ni kuwa serekali za mitaa zifanye kazi yake, kama hawana pesa basi wende juu zaidi ili wananchi wasipate hizo shida za kuzungukwa na uchafu namna hiyo.Hatutaweza kuondokana na malaria kama hivyo ndivyo itakuwa.Sio hapo tuu bali sehemu nyingi sana hapo nchini.

    ReplyDelete
  3. wewe ndungu yangu unayesema mambo mazuri hayataki haraka unatoka wapi?huo kama hilo ni jambo la muhimu sana?unajua kuna watu wangapi wanakufa kilasiku kwasababu ya uchafu unaowazunguka?naomba ujue serekali ikiamua kulivalia hilo jambo njunga ianawezekana kufanyika mapema iwezekanavyo!mitaro inahitajika kuodoa maji yaliyosimama,sioni kuwa ni jambo jema kuionea huruma serekali.

    ReplyDelete
  4. jamani nini hii nasikia harufu kabisa ya haya maji machafu. mnaishije huko? jamani hakuna DIWANI? na kama yuko anafanya nini! mmmmmmmmm poleni sana

    ReplyDelete
  5. Tatizo kubwa ni wakazi wenyewe pia wanachangia kuziba njia za maji kwa kujenga kuta au nyumba kwenye njia za asili za kupita maji ya mvua ukizingatia maeneo ya Mwananyamala na Msasani yako karibu na pwani, mvua ikinyesha yanakumbwa na matatizo kama hayo.

    Pili unaweza kukuta maji yote hayo si ya mvua bali ule mtindo wa kusubiri mvua inyeshe basi watu wanatapisha vyoo vyao ili uchafu uchukuliwe na maji ya mvua, sasa ukizingatia kufungwa kwa njia za asili, hayo maji machafu yanayotapishwa kutoka vyooni yanakosa pa kwenda. Cha msingi ni kwa mamlaka husika kutumia by laws zilizopo na kuhakikisha kuna miundombinu inayosaidoa watu kuachana na tabia ya kutapisha vyoo kama vile kuunganishwa kwenye seawge system (hili ni long term solution. Kwa short term solutions ni kuwa na magari ya kunyonya maji machafu kwa bei nafuu ili kuwawezesha wananchi kulipia huduma hiyo na kuacha kutapisha.

    Kuhusu maeneo ya asili ya kupitisha maji, hili ni gumu kama mtu amejenga nyumba juu ya hiyo nji lakini kama ni ukuta ni bora uvunjwe ili maji yafate mkondo wake na kwenda moja kwa moja baharini.

    ReplyDelete
  6. Kaka Michuzi,
    Picha hii inasikitisha na kuogopesha.pamoja nakuwa ni wajibu wa serikali lakini pia hata wakazi wa eneo hilo pia waweza fanya kitu,mfano kuchimba shimo la taka,mifereji na kuweka eneo lao safi.CHARITY SHOULD START AT HOME jamani sio kila kitu tufanyiwe

    ReplyDelete
  7. Bongo tambarale kama vile mamtoni tu!Kazi kwenu wazalendo mnaolinganisha Bongo na Mtoni.Bora kuishi Porini na siyo katika mazingira kama hayo ilimradi tu eti nipo Mjini.Ikawa jioni ikawa asubuhi siku ya kumi na moja.

    ReplyDelete
  8. Hakuna maoni ila hiyo ndio certificate yetu kwanini waafrika tunadharaurika sana huku ughaibuni..ukipita customs weupe wapita nawe mzigo kwenye scanner..ukipita Health check weupe wapita wewe mbantu wanadai chanjo..mambo yote haya yameletwa na mafisadi na viongozi wengi wa bara la afrika walio wabinafsi na wasio jali watu wao..wana support mafisadi na vita...Picah kama hizo zinauma sana kuziona kama umeona maendeleo ya wenzetu..

    ReplyDelete
  9. anon wa kwanza tangu tupate uhuru tulikuta habari ya kwamba TANU YAJENGA NCHIkilikua chama kimoja itikadi moja mpaka vikaja vyaqma vya upinzani tumeonyesha ukomavu, sasa wewe unapotwambia nchi yeti changa mambo hayataki haraka nusu karne inakatika hiyo hela za kuleta maendeleo zinaishia mikononi mwa wajanja, pangu pakavu wenzangu na mie tunadanganywa kuwa nchi bado changa mpaka tutakufa matunda hatujayaonja? jamani jamani hili neno la uchanga wa nchi wenzetu wanatuacha tunabaki na wimbo wa chama cha jenga nchi chama eeechama cha jenganchi

    ReplyDelete
  10. Acheni umbeya hicho kiwanja kiko kwenye eneo ambalo halijapimwa na serikali.Sasa mnataka serikali ifanyaje?

    Ikienda kuivunja mnasema uvunjaji haki za Binadamu wakiiacha ikae na uchafu wake mnapiga kelele.Acheni umbeya!

    ReplyDelete
  11. Cha muhimu watu wakijenga nyumba kuwe na sheria za drainage systems...hata iwenspector anafanya hivyo na mtu asipojenga kufuata sheria basi apigwe faini ya kuondoa hayo maji...Ni sisi wenyewe tunayaleta haya too many people halafu nyumba zinabanana na nyia za kutoa maji hamna...Hayo maji yatajipeleka wapi?

    Harambee watu kila weekend waanze kuchimba mitaro ya kufanya maji yapite...Kila mtu kwenye mtaa wao wakifanya hivi...mambo yatakua tambarare...kama ni vyandarua au misaada tunasubiri ...basi ni ujinga wetu..

    ReplyDelete
  12. KUSEMA KWELI HUWEZI KUWALAUMU WAKAZI WA HAPO HAYO MAJI YA MVUA KUTOWEZA KWENDA KWENYE MIFEREJI RASMI YA MAJI MACHAFU NA HILI NITATIZO KUBWA DAR ES SALAAM NZIMA NA MIKOA MINGINE.SERIKALI HAIKUWA NA MPANGO MAALUMU WA KUJENGA JIJI NA KUPIMA VIWANJA KIASI CHA KWAMBA UTAKUTA NYUMBA ZIMEJIBANA MNO HAMNA NAFASI YA KUWEZA KUJENGA MIFEREJI YA KUPELEKA MAJI MACHAFU KATIKA ENEO RASMI.MARADHI MENGI MPAKA MALARIA YANATOKANA NA MKUSANYIKO WA MAJI MACHAFU KATIKA ENEO MOJA KWA MDA MREFU KIASI CHA KWAMBA VIJIDUDU VYA MAGONJWA UZALIANA.WATOTO WETU UTAKUTA WANACHEZEA MAJI MACHAFU HAYA HAYA.KWAHIO MISAADA YA MALARIA TUSIWE TUNANUNUA VYANDARUA TU BALI TUJARIBU KUTATUA CHANZO CHA GONJWA LENYEWE KWA KUJENGA MIFEREJI YA MAJI MACHAFU NA BARARA NZURI MAENEO KAMA HAYO.DAR SIO OYSTERBAY PEKE YAKE? TUWAKUMBUKE WATANZANIA WENZETU WALIOKUWA NA MAISHA YA CHINI TUSIWATENGE MPAKA KATIKA MZINGIRA WANAYOISHI.

    ReplyDelete
  13. Tuache kulaumu na kutegemea serikali. Serikali ni nani!!Ni sisi wenyewe. Na nani anaishi hapo? Ni sisi pia so why wait for somebody else to do things for you?
    Kila kitu kikiharibika we blame everybody else but ourselves!!!You live there make your own envinroment comfortable!!!

    ReplyDelete
  14. Tatizo kubwa hapa linasababishwa na wakazi wenyewe na si seikali. Nina imani wengi wenu imejifunza kanuni za usafi lakini wakati mwingine huwa mnazipuzia na haya ndiyo matatizo yake. Mtu ana kiwanya kidogo anataka ajenge vyumba 10 vya kulala na choo 1 (ili apangishe), watu wanatupa hovyo takataka na kuziba mifereji ya maji,n.k na hivi vyote ni vyanzo vya hayo matatizo. kwa mtazamo wangu ni kwambaa inabidi wananchi tuchukie uchafu na tufate kanuni bora za afya. Magonjwa mengi ktk nchi masikini yanatokana na uchafu sasa ni vizuri kwanza tukafanya usafi siyo tu wa mwili na nguo bali pia na wa mazingira yetu. Waelimisheni watu waache uchafu na siyo kulalamikia serikali.

    ReplyDelete
  15. Halafu mjomba Misoup unatwambia bongo tambarare, tambarare yenyewe ndio hii ya kupata magonjwa ya miripuko? hapo lazima uibuke na kipindupindu , kichocho au chronic fungus kulaleeek.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...