machinga akilia baada ya kudhalilishwa hadharani
wasamaria wakiwa na machinga wa watu aliye mtupu
bidhaa zilizomponza machinga huyu, na chini ni wadau wenye hasira wakisubiri askari wa jiji waliofanya unyama huu watolewe walimojificha...
juzi michuzijr alishuhudia tukio hilo la kikatili na la kudhalilisha likimtokea huyu machinga ambaye baada ya kukamatwa na askari wa jiji alipigwa na kuvuliwa nguo hadharani kwa kosa la kufanya biashara katikati ya jiji kinyume cha sheria. wadau wenye hasira hawakukubali. waliwatoa mkuku askari hao wa jiji na migwanda yao ya kijani ambao walijihifadhi kwa usalama wao kwenye jengo la jirani hadi polisi walipofika. mbaya zaidi inasemekana hata tujisenti twake twa mauzo ya pipi na fegi walibeba kabla ya kukimbia.
hii wadau imekaaje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 59 mpaka sasa

  1. Naomba mnieleweshe

    Askari wa jiji ni nani hao?
    Tofauti yao na Polisi ni nini?

    Wanavaa kijani ehh?

    shukurani

    ReplyDelete
  2. Muhidin,

    Nimeitazama picha hii mara kadhaa. Nimeitafakari picha hii mara kadhaa. Kwa dhati yangu na mbele ya Mwenyezi Mungu nasema picha hii imenitia uchungu na huzuni isiyo mithili.

    Picha hizi za tafrani za Wamachinga na wanamgambo wa city tumeziona mara nyingi mno humu kwenye magazeti tando(blogs). Kadhalika nimekuwa nikiuliza maswali mengi kuhusiana na matukio haya yakiwemo: Wanamgambo wa city wanawajibika kufuatana na sheria gani? Wanapata mafunzo kiasi gani? Nafasi yao katika kulinda usalama, amani na utii wa sheria za Taifa(Tanzania) ni ipi?

    Kwa namna wanavyofanyakazi wanamgambo wa city badala ya kuwa walinzi wa usalama, wasimamizi wa amani na utii wa sheria wanakuwa ndiyo chachu ya uasi na pengine kitalu cha kuotesha waasi kama wale wa Sierra Leone, Liberia, Kongo, Ivory Coast, na "makadogoo" wengine wowote waliopata kuibuka popote duniani hutokana na chuki ya uonevu, kunyanyaswa na kukandamizwa kwa sababu ya nafasi yao katika jamii kuwa ya kimasikini.

    Kinyongo, mgogoro, chuki, na kisasi cha wanaokandamizwa huwa kinaoteshwa na kuneemeshwa na hali kama hizi za mgambo wa city (wakala wa wakandamizaji) na Wamachinga na ndugu, jamaa, na marafiki wa wanaokandamizwa, kuonewa, na kunyanyaswa.

    Nina hakika kuna waliomo serikalini ambao wanapita kwenye magazeti tando na kuyaona haya. Ninachowasihi na kuwaasa ni kuchukulia hatua kali suala hili. Pia kuangalia upya suala zima la mahusiano kati ya raia na askari. Vinginevyo tutakuja kujutia hali ya wananchi kutokuwa na imani na serikali na matokeo ya kutokuwa na imani ambayo huwa ni uasi wa sheria ambazo kwa maneno mengine ni vurugu, machafuko na hatimaye vita.

    Tusipoziba ufa tutaja jenge ukuta.

    Ni mimi Mtanzania mwenzenu.

    ReplyDelete
  3. UKATILI UKOMESHWE MARA MOJA.SISI WATANZANIA SIO KWAMBA TULIUMBWA SIKU NYINGINE NA BINADAMU WA MATAIFA MENGINE.AMANI NI FIKRA.UKATILI HUU HAUPIMIKI.

    ReplyDelete
  4. michuzi, sina la kusema. HUU NI UONEVU ULIOVUKA MIPAKA.........

    ReplyDelete
  5. Bongo TAMBARARE.

    ReplyDelete
  6. Inatia huruma kweli kweli. Kijana inakuwa kama mkimbizi, hapati uhuru nchi kwake.
    Sasa government ina panga nini kusaidia vijana???? Kijana anauza pata pesa yake bado ni shida kubwa jamani. Je ikiwa mwizi si shida kwa wote?? Government should assist small projects to provide income to guys like that one above. It's sad indeed.

    Thank you.

    Inge Maria Sorensen
    Denmark

    ReplyDelete
  7. Kusema kweli vyombo vingi vya usalama tanzania huwa wanatumia majukumu yao vibaya kuanzia wagambo mpaka wanajeshi.hii sio haki kabisa kupora vijisenti vyake pamoja na kumvua nguo na sio kwamba kachukua nafasi yoyote manake huo ungo wake na bidhaa zake hinaonesha anatembea sehemu tofauti kuuza kujariobu kupata vijisenti vyovyote aweze kukizi maisha magumu tuliyokuwa nayo.wanajeshi nao waache kupiga raia.

    ReplyDelete
  8. NILISOMA KWA MICHUZIJR NIMESIKITISHWA SANA NA UNYANYASAJI HUU INAMAANA NDIO SERIKALI INAWATUMA WAFANYE HIVI KUDHALILISHA JAMII NA UNYANG'ANYI WA FEDHA ZA WATU

    ReplyDelete
  9. michu usinibanie lakini nachotaka kuuliza ni kwamba kandoro ashitakiwe kwa sababu yeye ndio jiji!!!!!! pia ikiwezekana kina lowasa ndo wangefanywa hivi!!!! ni kwa ajili yao wao kuchukua hela ambazo zingeweza kuwafikia walengwa ndio maana walala hoi wanafanya hivi!!!! mgambo hao wafukuzwe kazi!!!!!!WAFUKUZWE KAZI!!!!!

    ReplyDelete
  10. Tatizo bongo kuna AMANI lakini hakuna HAKI.Kitu cha kusikitisha ni kwamba watu wanapenda sana AMANI
    ambayo haina HAKI wakati kama wataamua kupenda HAKI then watainjoi Amani.WAANDISHI WA HABARI BONGO WANATAKIWA WAKAWAINTERVIEW VIONGOZI WA HAO ASKARI WALIOMFANYIA UKATILI JAMAA.WASIISHIE HAPO TU,WAFUATILIE MPAKA MWISHO WAKE.
    WAKIDHARAU,SERIKALI ITADHARAU NA MATOKEO YAKE WANANCHI WATAENDELEA KUKOSA HAKI ZAO MPAKA MWISHO WA DUNIA.

    ReplyDelete
  11. Katika watu huwa nawachukia ni hawa Mgambo wananikera sana na operation yao wallah kwani huyu mjasiariamali ana maisha sawa na wao anaburuzwa kama mbwa... Ningefuahi siku moja Mafisadi wakafanzwa hivi na wao!!
    Katika nchi zetu usifanye dhambi nogo, kama ni dhambi fanya kubwa uone kila mtu atakuwa attention na wewe!!!

    ReplyDelete
  12. Kitendo kimenisikitisha sana nimesjisikia vibaya kuona mtanzania mwenzetu akidhalilishwa katika hali hii.

    Imeniuma sana.Vipi mustakbari wa hao manyang'au wanaojiita wanalinda haki za kiraia?

    ReplyDelete
  13. HUU UKIUKAJI WA HAKI ZA BINADAMU SIJAWAHI KUONA. INGEFANYWA NA KIKUNDI CHA WAHUNI NINGEJIULIZA NIKAPATA JIBU. LAKINI KWA CHOMBO KILICHOWEKWA KWA RIDHAA NA SERIKALI, HAINIJII AKILINI KABISA.

    NDIYO MAANA MIMI HATA UNIAMBIE NIENDE NYUMBANI KUISHI SIENDI HATA KWA WINJI. UMEME GHALI, MAFISADI WADHULUMU NDUGU ZETU, MAJI YA SHIDA, AMBAYO HAYACHIMBWI KAMA MADINI, BADO ADHA YA USAFIRI JAPO UWE NA NAULI YAKO KAMILI.

    JAMANI WENZANGU MNIPE MAELEKEZO LABDA NIMECHANGANYIKIWA. KUNA TUMAINI GANI LA MAISHA HAPA? HIVI HADI WAONE WATU WANABEBA SILAHA KUYAPINGA HAYA NDIO WAJUE HALI NI MBAYA?

    HUU SI UTAWALA BORA HATA KIDOGO. WATANZANIA TUNAPIMA AMANI KWA KUTOUANA NDIO SHIDA YETU.

    I AM REALLY SORRY FOR ALL THIS. I AM SO MAD!

    ReplyDelete
  14. Jamani.. sasa vijana wajisaidie vipi kama serikali inawafanya hivi..?? nini kazi ya hao wanjiita polisi sijui askari!!!? kumdhalilisha mtu kwa kosa la kujitafutia ridhiki yake jamani..Afanye nini basi huyu kijana akaibe????

    Binafsi imenisikitisha sana....hivi viongozi wa serikali huwa wanaviona hivi vitu kweli...???
    Dah mbaya sana

    ReplyDelete
  15. Kitendo cha askari wa jiji kujichukulia sheria mkononi kiasi hiki siyo sahihi. Wanatakiwa wafikishwe mahakamani kwa kumdhalilisha machinga huyu.

    Msimamo wangu kuhusu hizi biashara za mkononi wanazofanya hawa 'machinga' si kweli kwamba zitawaondolea umasikini. Biashara hizi mimi nazitazama kama ndizo zinazochangia kuongezeka kwa umasikini kwa watu wengi ambao wameacha shughuli zenye tija na kuja kubanana mjini wakidai wanatafuta maisha. KAZI AMBAYO MMACHINgA HAO WANGEIFANYA NA KUWALETEA MAISHA BORA NI KILIMO. Wengi wa hawa machinga wametokea sehemu ambazo ardhi yake inarutuba nyingi. Kilimo siyo kazi ngumu kama ilivyo kuuza vitu mkononi. Machinga wanatembea, nadhani, si chini ya kilomita 20 kila siku. Ukizidisha umbali huo kwa mwezi utakuta ni kama km 600 kwa mwezi...siyo utani! Nguvu hii wanayotumia kutembea wangeitumia kwenye kilimo wangekuwa mamilionea. Kilimo sana sana ni miezi 3 au 4 pamoja na kuvuna na kuandaa shamba ni kama miezi 6. Maana yake nusu nzima ya mwaka hakuna kazi ngumu bali ni kula matunda.
    Mimi nafikiri imefika wakati jamii ibadili mtazamo au ibadilishiwe maana watu wanazeeka wakiwa masikini kwa sababu tu hawakujuwa shughuli sahihi ya kuwapatia kipato na kuwaondolea umasikini.
    Matatizo ya soko na upungufu au ukosefu kabisa wa pembejeo yanaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kushirikiana kwa jamii na Wizara husika.
    NILITOA DARASA KIDOGO KWA VIJANA 3 BIHARAMULO NA 2 MBEYA wakanielewa kabisa kwamba umachinga hauwezi kumuondolea mtu umasikini bali unamwingiza kwenye umasikini na tamaa isiyo na mwisho maana hawezi akapata anachohitaji. Mada hii ikienezwa kwa wadau walioko vijijini naamini wanaweza kuyaona maisha kwamba yapo kila mahali na si mijini tu.
    HEBU JAMII IZINDUKE BASI NA KUWAOKOA VIJANA HAWA KUTOKANA NA MAGEREZA YA NJE WALIOJIFUNGA WENYEWE!

    ReplyDelete
  16. Nimesikitika sana na imeniuma sana. Hao askari wafikishwe mbele ya sheria na huyu kijana alipwe fidia. Kinyume cha hapo, kuna siku Bongo kutakuwa na machafuko.

    ReplyDelete
  17. Bro Michuzi...

    Hizi picha zinasikitisha sana. Hao maaskari wa jiji wawajibishwe.

    Kwa nini hao maaskari wa jiji wasiwafanyie kazi ombaomba na street boyz wanao safaisha vioo za magari kwenye sehemu za trafic lights? Hao wamezidi hata kuliko wamachinga wanao tafuta riziki zao kwa kuuza bidhaa ndogondogo kwa halali. Sehemu nyingine imekuwa hatari kiasi kwamba hata polisi wanabutwaa wakiona dereva akiibia simu au sight mirror akiwa akisamama kwenye trafic lights.

    Je wadau mnasemaje?

    - Mtanzania, MuB.

    ReplyDelete
  18. Kama mlikuwa hamjui hayo ndiyo MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA

    ReplyDelete
  19. Picha ya pili inasikitisha zaidi kuona kuwa wapigapicha wanamsnepu huyo mmachinga badala ya hao maaskari waliofanya kazi hiyo. Maaskari hao wawajibishwe na wapelekwe kwenye chombo cha dola.

    ReplyDelete
  20. Kwa kweli Bro Michu hii imeumiza kuliko matukio yale ya kenya jamani.

    Huyo sio mkimbizi ni Mtanzania halisi na raiya ambae wanategemea Miaka 2 ijayo wamwombe kura yake?

    Je hao Askari waliomfanyia huo unyama leo hii wako wapi?

    Jana nimesoma Hotuba ya Rais wetu akisisitiza Amani, Je amani kwa njia hii bila utu kweli itapatikana?

    Ingewezekana Huyo Rais wetu akapewa Picha ya Mtu kama huyu kijana Mtanzania anayenyanyasika bila huruma kwa kujitafutia angalau riski yake ya siku, Kwanini hawawafwati wale Mateja pale Kinondoni kwa Manyanya wanaonyang'anya watu vitu kwa kuwatolea silaha kama Visu na Bisibisi wakawakamata na kuwazalilisha wanaishia kunyanyasa wale ambao wanajitafutia riski yao bila kugusa kitu cha mtu?

    Huyo kandoro anatakiwa arudi nyuma sasa na ajifikirie vyema kwamba anachokifanya je ni sawa? Na je yeye mwenyewe amezaa na anao watoto tena mmoja alikuwa class meat wangu Collage ila ajue leo na kesho yasiporudi kwake au watoto wake yatarudi kwa wajukuu zake hayo machozi ya machinga wanayo lia.

    Asanteni na samahani kwa Historia ndefu ni uchungu mkubwa hasa kwetu sisi Wakina mama ambao tumeshazaa tunajua watoto watakuja pata shida sana hasa miaka inavyozidi kusogea.

    ReplyDelete
  21. Hivi huyu michuzi JR ni mdogo wake na huyu mheshimiwa baba mmoja na mama mmoja au anajiita tu kwa kuwa ana undugu na misupu?

    Unaweza kukuta ni mdog wake na baba yake na kaka yake.

    ReplyDelete
  22. Nimeumia sana baada ya kuona picha ya huyo kijana aliyeachwa hana nguo. Mimi huwa inanikumbusha kitu kimoja kwamba katika nchi yetu (TANZANIA)hakuna utawala ambao vingozi wetu huwa wanauita 'utawala wa sheria'. Nasema hivi kwa sababu, mtu yeyote ambaye anahisi yeye ana nguvu fulani kisheria katika shughuli zake za kila siku basi ndiye huyo mvunjaji wa kwanza wa hizo sheria na hakuna anayemfokea au ni katika msingi ule ule wa kulindana. Mifano ipo mingi ni pamoja na kuombwa rushwa ili kupata huduma stahiki au ufisadi ambao kwa sasa ndiyo wimbo wetu. Mimi napendekeza hawa mgambo waliohusika na aibu hii wafukuzwe kazi na wapelekwe kwenye vyombo vya sheria kwani wao hawakupaswa kuhukumu. KANDORO WANANCHI TUNAKUSUBIRI KUONA UTAWACHUKULIA HATUA GANI HAWA MGAMBO

    ReplyDelete
  23. Nadhani ili neno amani amani wengine hawajui amani ni nini? hakuna amani, hamna amani bila haki, kama hakuna haki kwa vyovyote hamna amani, pengine watanzania hatujui lini watu hawa wenye hasira wataamka!!! ni bomu hili 'timed bomb' linasubiri wakati wake, jaani baadhi ya nchi walizopigana wao kwa wao walikuwa na rekodi nzuri ya amani kimataifa,kumbe ndan hamna amani.wameuana sasa wanatafutana usiku na mchana.HAO MGAMBO WANALIPWA SH.NGAPI NAO NI NJAA!! WAMEKUWA KAMA WANAYAMA WATAFUTAO SWALA MBUGANI !! HATA HAO MGAMBO NI BOMU LINGINE..MTU AKISEMA AJE AWAONGE AWACHUKUE WATAKUBALI MAANA TAYARI WAMEKUWA WANYAMA.Baada ya tukio hili walicheka wakajipongeza wakati sisi tunalia.
    Serikali iangalie upya wapi imekosea, kwa nini watu wakimbie vijijini waende mjini?.KUTATUA MATATIZO HAYA KWA NAMNA HII TUNAJIPELEKA PABAYA.KANDORO, WIZARA YA MAMBO YA NDANI HII NINI JAMANI....

    mdau-canada

    ReplyDelete
  24. Dear Michuzi

    This is absolutely pathetic and against human rights, if the government is not going to take any actions against those responsible, I will be ashamed to call myself a Tanzanian, could you please update us with the outcome.

    ReplyDelete
  25. utu wa binadamu tunajua haupo tena.

    LAKINI ;

    serikali, sheria ,haki na hasa haki za binadamu .

    ReplyDelete
  26. Bora sisi wastaarab nusu,kwani ingekuwa Kenya,jamaa angeliwa panga na virungu na wangekuwa wanaokota maiti tuu...AMANI TZ IDUMU KAMWE!!!

    ReplyDelete
  27. Watanzania tuamke!! Haki za binaadamu ziko popote duniani ila tatizo linakuja kwenye elimu. Na kwa watanzania wengi wa kawaida hawajui kama kwa jambo kama hili alilofanyiwa kijana anaweza kuisue (Kuipeleka mahakamani) selikali ta mitaa (jiji) na kuweza kujipatia donge nono ambalo litamwezesha kuihishi maisha yake yote bila kufanya kazi. Hii pia itakuwa fundisho kwa selikali na vyombo vyake kunyanyasa wanachi wa kawaida. Ma Wakili hapo Bongo wanajua hili lakini hawasemi kitu wanasubili kesi za Mameger wanaoishitaki selikali ili ndio wafanye kazi. Kama wakili hii kesi ni open kesi kwani ushahidi upo na mashahidi wapo sasa mnasubiri nini?? Kijana kama moja ya watanzania wengi wasio jua haki zao hajui kama alichotendewa ni kosa na labda ni moja ya "apportunity of his life" lakini hajui. Kuna nini Tanzania ?? Mbona watu tumelala sana. Huku nje mtu unaomba siku ikupate issue kama hiyo ukiwa street ili uepukane na bidaa ya kubeba box. Ushahuri wangu ni huu, Serikali inabaidi iamshwe, kivipi? Kwa Wananchi kufungua kesi nyingi za madai kila siku. Na hii kazi ni ya Mwakaili wa kujitegemea kuelimisha watu, sio mnakaa tu Elimu yenu hamjui kama hiyo elimu mlipata kutokana na Fedha ya hao wavuja jasho?? Sasa wanachohitaji ckutoka kwenu ni "Bring back to the Community" kwa kuwaelimisha na kuwashauri. Ile hali ya Kudhani kuwa Serlikali ni Babayako kwahiyo huwezi kuishitaki ife mara moja. Mwisho: Na kwa majaji wa serikali hakikisheni kesi kama hizo zikiletwa mnazifanyia kazi na sio kuibeba serilkali kwakua ndio muajili wako. Tunaona kesi za Watu wakubwa kila siku wanaidai selikali na wanalipwa mamilioni ya fedha. Tunataka na mwananchi wa kawaida awe na haki ya kufanya hivyo mara moja. Watanzania tusijidanganye kuwa tunaamni na tunapendana kwa hiyo hatuwezi kupigana. Kila siku tunasikia Polisi, JWTZ , JIJI wanawapiga wananchi, hivi chamjui kama hiyo ajira yenu ipo kwa ajili ya kuwalinda wao?? @#$%%%^&* nyie! Au hamjui kama hiyo mishahara yenu inapatikana kutokana na kodi zao. Au hampewi mafunzo mazuri mkiwa huko mafunzoni?? Kumbukeni hizi zahama zikikusanyika kila siku ndio zinajenga chuki. Na malizia kwa kusema " Binadamu akichoka Simba ni cha mtoto"

    ReplyDelete
  28. KAKA MICHUZI MZEE ''TIBAIGANA'' AMEIONA HII THIS IS TOO MUCH JAMANI, MPELEKEE HII HABARI NA PICHA NA UTUSAIDIE KUTUELEZA AMECHUKUA HATUA GANI INATIA MAJONZI nyumbani ni nyumbani lakini duuu sijui tusirudi tujikalie tuuu na wazungu huku kwenye haki za binadamu

    ReplyDelete
  29. mimi ushauri wangu kwa huyo mmachinga ni bora apande ndege aje kuomba ukimbizi tu maana ana kila ushahidi wa kudhalilishwa na serikali maan apolisi ni serikali kwa hiyo serikali mmemzalilisha raia kiasi hicho ?kudadadeki

    ReplyDelete
  30. HUYU BWAMDOGO AKIPATA MTU WA KUMSIMAMIA ANAWASHTAKI NA ANASHINDA KESI NA ANAVUTA MKWANJA!!!

    ReplyDelete
  31. Lazima huyo "MGAMBO KATILI" (Msiseme askari tafadhali hawajaenda CCP hao wameishia kwata ya mgambo) Wapeni heshima hao askari wetu.

    ReplyDelete
  32. HUYO MGAMBO WA JIJI """AMEZOEA SODOMA NA GOMORA"" ..... NINA HAKIKA ALIVYO MUONA HUYO MMACHINGA ... AKA.. AKA..AKAMTAMANI....
    HIYO SIO BANGI WALA NINI NI TABIA MBAYA TU ALIYOKUWA NAYO. (AFUNGWE MAGEREZA HUYO.

    ReplyDelete
  33. INASIKITISHA SAN!!!
    1. Serikali mpo wapi???
    2. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora..Mhe. Jaji Kisanga na safu nzima mpo wapi???
    3. Legal and Human Rights Center...Mama Hellen Kijo-Bisimba na vijana wako mpo wapi???
    4. TAMWA... Mama Ananilea Nkya, Dada Raziah Mwawanga mpo wapi?????
    5. TGNP--- Mama Rusimbi na Dada Usu Malya --- Mbona hatuwasikii hapa????

    OMBI KWENU WOTE TUNAOMBA MSINGOJE MATUKIO YA VIFO AU MAJERUHI WA DAMU NDIO MVAE VIBWEBWE ANZENI NA HILI HUYU KIJANA AMEPATA JERAHA KUBWA SANA MAISHANI MWAKE...ANAWEZA KUFA KWA MAWAZO YA KUDHALILISHWA. TAFADHALI MICHUZI HAKIKISHA HAWA JAMAA NILIOWATAJA WANAPATA E-MAIL HII KUPITIA KWENYE OFFICE ADDRESS ZAO TUNATAKA ... MOTOMOTO TOKA KWAO

    ReplyDelete
  34. Nikilichambua hili tukio naona kuna mambo makubwa matatu ambayo ni changamoto kubwa kwa serikali yetu na wananchi pia.

    Kwanza huu ni uonevu mkubwa sana kwa mwananchi huru katika nchi yake kudhalilishwa kiasi hiki na kuvunjiwa utu wake na vyombo vya serikli vya kulinda sheria. Ni jambo baya kwani ni uvunjaji wa haki za binadamu na linalootesha chuki kati ya serikali na wananchi.

    Pili hii hali ya wananchi kuamua kuchukua sheria mkononi kupambana na askari wa jiji ni dalili za mwanzo za wananchi kuchoka na kutoviamini nyombo vya dola. Uchovu wa namna hii ukishaingia na kujengeka kwenye akili za watu huleta hali ya kukata tamaa kwa wananchi na kuamua liwalo na liwe tu. hali hii si ya kuombea wala kujaribu kuijenga kwani kurekebisha kwake ni kwa gharama kubwa. mfano wake ni jirani zetu kenya.

    Tatu inaonyesha Uongozi mbovu na sera mbaya za viongozi la jiji katika kutatua tatizo la wamachinga mjini Dar. Hili ni tatizo la muda mrefu, na jiji mara zote imekua ikifanya vita ya zima moto na wamachinga badala la kuandaa sera ya muda mrefu ya kuwasaidia wamachinga kufanya biashara zao. Sekta ya wafanyabiashara ndogondogo inachangia kwa kiasi kikubwa kwa ajira ya wananchi, hivyo basi inawaongezea kipato kwa wananchi na pia inaweza kuwa chanzo kikubwa cha mapato ya kodi ya jiji kama utaratibu mzuri na ushirikiano ungekuwepo baina yao.

    Naitakia kila la heri nchi yangu Tanzania na wananchi wake

    ReplyDelete
  35. haki ya mungu AMANI ya Tazania inavunjwa ana wana usalama wantakiwa kulinda usalama wa watu na kuleta AMANI hata kama ningekuwepeo ningesaidia kuwapiga mawe hao wanamgambo.

    ReplyDelete
  36. Jamani Watanzania Tumekwisha sasa. Hivi nyie Mahakimu wa Serikali Mko wapi? Je Wakuu wa Haki za binadamu nanyi Mko wapi? Huyu kijana Hajatendewa haki kabisa na inawezekana hajui sheria ghani anaweza kufuata ili aweze kupatiwa haki yake kama Mtanzania Halisi, Je hao askari waliojitokeza hapo kutuliza hiyo ghasia wamewafanyia nini hao Mghambo au wanaojiita askari wa Jiji?

    Tanzania hatuna amani bali tunaimani na ndio maana tunaishi.

    Broo Michu msaidie huyu jamaa hata kwa kukutana nae huko stand, Mwongoze ni nini cha kufanya. Mimi ningekuwa hapo bongo ningempeleka mkono kwa Mkono hadi kwa kandoro pamoja na hizo picha ili aweze kutoa uamuzi wake.

    ReplyDelete
  37. This is crime against humanity! Hivi haya ndio maisha bora kwa kila Mtanzania???? Nimeiangalia hii picha, nikajiweka katika nafasi ya huyo kijana, kwa kweli imeniuma sana, hata machozi yamenilengalenga! Kwa kweli sisi tunasubiri hatua watakayochukuliwa hao askari wa jiji! kinyume cha hapo, nitaona Bongo tuna viongozi madikteta.

    ReplyDelete
  38. kwa kweli inauma sana kuona mtz mwenzetu ananyanyasika kiasi hiki, Michuzi ukiwa kama mwanahabari tunaomba jambo hili lisiishie hapa ikiwezekana magazeti yote yaweze kuandika habari hiii mpaka wahusika waweze kuona na kuchukua hatua kama ilivyokuwa kwa mafisadi, nyinyi waandishi wa habari mkiamua inawezekana angalia kwa mwandishi mwenzenu kubenea mliandika mpaka yakafika kwa wahusika sasa tunaomba na hili pia mlivalie njuga, tumechoka kuonewa.

    ReplyDelete
  39. Huu ni Unyama. Watawala wakumbuke hii ndio hali iliyokuwepo kwa Watani wetu wa Jadi (Kenya). Wananchi walivumilia sana wakapata mwanya wakati wa matokeo ya uchaguzi ya mwaka jana. Hata wahenga walisema: "Bwawa la Udongo likibomoka huwa na kishido kikuu".

    ReplyDelete
  40. hii sio haki kabisa, nimesoma nimelia saana, imenisikitisha saana..
    Tanzania tunakwenda wapi? hamna utu kabisa... mtu wa watu anaangaikia maisha yake, hata kama anakosa sio kumvua nguo like that... so sad!
    askari wa jiji? ebu tufafanulie..
    huo uaskari walijifunza lini? shule jamani muhimu saana.. mtu mwenye akili zake hawezi kufanya hivyo! anyway...update up plz..
    J

    ReplyDelete
  41. Michuzi..mimi nililia nilipoona hii kitu..mwanzo nilidhani kibaka lkn baada ya kusoma machozi yalinitoka... hasa ukizingatia ugumu wa maisha,halafu hicho kidogo alichopata mtu anamdhulumu..mungu atamlipia..lakini sijui utampata vipi huyu kijana michuzi..mie nataka nimsaidie angalau kamradi kake karudi... lkn sijui utampata wapi?

    ReplyDelete
  42. huu ni ukiukwaji wa haki za binaadamu hata wanyama wana afadhali kuliko ndata wetu,mpenda haki.

    ReplyDelete
  43. machozi yamenitoka. Hii inasikitisha sana. Hivi tukimaliza shule tukiamua kuzamia huku huku tuliko mtatusema kweli!!!! Afadhali nibebe box huku kuliko mateso haya. Huko hata nikirudi nikakosa kazi mtu akitaka kujiajiri kwa mwendo huu itatafutwa sababu biashara iuliwe kuondoa competition kwa viboba.

    ...I am scared. Inasikitisha na this is so inhumaine.

    ReplyDelete
  44. YOU KNOW...TUKIMALIZA MAFISADI TUANZANE NA HAWA WA VYOMBO VYA SHERIA WANAOJICHUKULIA SHERIA NA KUDHALILISHA WATU HIVI.

    ReplyDelete
  45. MIMI NADHANI KUWA HAO ASKARI WA JIJI AU MANISPAA WAMEFANYA KAZI KINYUME NA MAELEKEZO NA TARATIBU ZA KAZI ZAO. NINA HAKIKA SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE NA WALA HAPA HAKUNA SUALA KISIASA.

    NAKUMBUKA HAITAKUWA MARA YA KWANZA KUADHIBIWA KWA MUJIBU WA SHERIA KWA HAO ASKARI WA JIJI/MANISPAA.

    KUMBUKUMBU ZANGU ZINANIKUMBUSHA KITENDO WALICHIKIFANYA WAKATI FULANI HUKO CHA KUMPIGA MKAZI WA JIJI AMBAYE NADHANI ALIKUWA ANAMILIKI MIFUGO. WALE ASKARI WOTE WALIFIKISHWA MAHAKAMANI NA WALIPATIWA ADHABU YA VIFUNGO JELA.

    KWA HIYO KATIKA HILI NADHANI NI SUALA LA MASAA TU HAO ASKARI WATAFIKISHWA PANAPOSTAHILI KWA KITENDO CHAO WALICHOFANYA.

    NINACHOSHAURI KWA SASA JIJI LITOE TAMKO RASMI LA KUELEZEA TUKIO HILI NA HATUA AMBAZO ZIMEKWISHACHUKULIWA.

    ReplyDelete
  46. NOOOOO,NOOOOOOOOOO,NOOOOO
    JAMANI, THIS IS PURELY UNFAIR GAME,NOOO, JAMANI, ALIWAHI KUSEMA MWANASHERIA MMOJA MACHACHARI WA CHADEMA, ADVC TUNDU LISSU KATIKA CHANNEL 10 NA KILA MTU ALIMSIKIA, KWAMBA ITABIDI MAPINDUZI YA KIJESHI YATOKEE NDIO HALI ITAKUWA SHWARI,MAANA HUKU SASA TUNAKOELEKEA NI KUDHALILISHANA NA KUCHEZEA HESHMA STAHIKI YA BINADAMU, NA HAPO NI DAR AMBAPO VIONGOZI WOTE WANAISHI WAKIWAMO WANAOFANYA MADUDU KM LOWASSA.....ASALALEEE, SIKU IKIFIKA NA SISI TUTASAIDIA KUTUMA SILAHA ZA KUWAFYEKA MAFISADI NA WASIOJUA KUSIMAMIA SHERIA, ITS SO PAINFUL!!

    ReplyDelete
  47. Hivi yule Mama Bisimba-Kijo yupo? au yeye mpaka aonewe mwandishi wa habari ndiyo hujitokeza?

    Huyu Mama anapenda ujiko na nadhani ni mwanasiasa.

    ReplyDelete
  48. Pole sana rafiki.

    Najua kama alivyosema Prof Jay kwenye BONGO Bsm..wanawaita machinga ingawa si wote kutoka mtwara.....

    Naogopa sana wanaonyanyaswa WATAKPOSEMA ...tumechoka...

    Ene wei..naamini tutafika tu

    ReplyDelete
  49. Inasikitisha, inatia hasira, inaudhi.

    Huu ni unyama kabisa.

    Wananchi, kumbukeni kitu kimoja. Utendaji wa watu wa chini ni tafsiri ya jinsi wanavyowaona viongozi wao.

    Mfanyakazi akiamini anafanyia kazi Serikali ya kunyanyasa watu atajiamini na yeye atanyanyasa na kudhalilisha. Akiamini wakubwa wake hawafumbii macho unyanyasaji hawezi kuthubutu kufanya hivyo.

    Hawa askari wa Jiji wako chini ya nani? Wizara na Mambo ya Ndani ama Mkuu wa Mkoa.

    Naomba munijushe nani kiongozi wao na ikiwezekana munipatie number yake ya simu ili nirikishe malalamiko yetu.

    Kumbukeni, leo kafanyiwa huyu ndugu yetu tukinyamaza basi kesho tunaalika na sisi tuvuliwe nguo hadgarani.

    ReplyDelete
  50. JAMANI WANAKIJIJI,

    HABARI RASMI NILIZOPATA NI KUWA HUYU KIJANA ALIPOKAMATWA MOJA YA MAMBO ALIYOFANYA NI KUGOMA KUKAMATWA NA KUJIVUA NGUO MWENYEWE KATIKA HARAKATI ZA KUKAMATWA.

    NILIPOCHANGIA MARA YA KWANZA NILIANDIKA KWA HASIRA MNO. ILA SASA NAOMBA MJENGWA NA KAKAKO MICHUZI MTUPE HABARI ZA UHAKIKA ZAIDI. ALIVULIWA AU ALIJIVUA KAMA 'MBINU'?? MAANA NIMESIKIA HIVYO TOKA CHANZO NYETI CHA RAIA WEMA.

    NIMEFIKA MAHALI NIKAONA HALI INAFANANA NA MAELEZO. UKIANGALIA KIJANA ALIVYOKAA, ANAONEKANA NI MTU ASIYEONA HAYA KUONYESHA UTUPU WAKE. ALIYEVULIWA LAZIMA ANGEJIKUNYATA KWA SONI (AIBU).

    JAMANI, TUCHAMBUE HABARI KWA MAKINI KABLA YA KUWEKA HUMU NDANI. VINGINEVYO MTASABABISHA TUUANE SISI KWA SISI KAMA WAKENYA. NA IKITHIBITIKA KUWA ALIJIVUA, WALAI MLIOLETA HABARI HIZI NITAWAONA KAMA Mwai Kibaki na ODINGA WALIOGONGANISHA WATU WAUANE KWA MASLAHI YAO YA KISIASA.

    mdau,

    (STATES)

    ReplyDelete
  51. Hii si mara ya kwanza kwa kitendo cha kinyama kama hicho kutendwa na askari wa jiji katika jiji la Dar es salaam.Ninge watahadharisha tu Viongozi wa Jiji la DSM na hiyo Modernisation YAO ya Jiji la DAR!Hao Viongozi wakumbuke walikotoka!Wengi wao,kama siyo wote wakumbuke walipokuwa shule za msingi Mama zao waliuza pombe za kienyeji katika mazingira duni zaidi wakapata pesa za kuwasomesha na hii leo kwa elimu walionayo wamebahatika kuwa viongozi katika sehemu zao za kazi.NAWASIHI WAKUMBUKE SANA WALIKOTOKA!Huu mwelekeo wa kuwabomolea watu vibanda vyao vya biashara bila fidia au staha za kistaarabu,kunyanyasa wamachinga wanaohangaika kujitafutia riziki keo hii wamegeuka wakoma wasiotakiwa katika mitaa ya jiji,kwa kweli ni kichekesho na aibu kubwa kwa Taifa letu!Hiyo haraka ya kuubadilisha Mji wa Dar es salaam imetoka wapi?Ukitaka kuhamisha watu,kwanza tengeneza kule utakako wahamishia.Kisha wahamishe.Hujatengeneza,unawafukuza wakaishi wapi?Basi kwa staili hiyo ya kunyang'anya wafanya biashara ndogondogo hata Maji ya Chupa?Kwa kuwadhalilisha hadharani wakiwa watupu bila ya nguo mwilini?Hiyo ndiyo Modenaizesheni ya Jiji?Mimi nafikiri umefika wakati viongozi wanaohusika na JIJI wawajibishwe kwa kuondolewa kazini wakafanye kazi zingine.Hatuwahitaji hao hapa katika jiji la Dar es salaam.TUWAULIZE,WANAMTUMIKIA BWANA GANI?Sisi wana Dar es salaam wanyonge na masikini ambao tunafikia karibu asilimia 96% ya idadi ya wakazi wote wa hapa jijini Au hao wenye pesa na waliosomeshwa na mama zao kwa hela za pombe za kienyeji ambao hawazidi asilimia 4% ya wakazi wote wa jiji AU hao Makaburu wanaotaka wabakie wao tu katikati ya jiji?Nimesikia Uchungu sana mambo haya ya aibu yanatendeka katika Tanzania yetu huru miaka 47 baada ya Uhuru,huku sera za Uchumi zikinuka Uvundo na Viwanda vyote vikiwa chali havina mnunuzi!TUONE AIBU KIDOGO.

    ReplyDelete
  52. Myie mnaosema haki za bnadamu au kufananisha na kenya, mnatakiwa mtambue kuw sisi watanzania tuko wepesi sana wa kutojua sheria na hivyo kuzivunja. Sheria inasema kutojua sheria siyo sababu ya kukwepa mashtaka! Askali wa jiji wapo kisheria (City By laws) na ni dunia nzima kama hivi. Wale machinga wengi ana wanafanya vit vya ajabu ajabu.

    Hawa Machinga ni sawa sawa na jamaa waliopata visa kwenda Ulaya na hawakurudi au walio-forge document na kutokomea Ulaya. Ni suala la time tu nao washughulikiwe kama huyu Machinga.

    Tumieni muda mwingi kuwaelimisha watu wenu jamani! Elimu ni silaha ya kila kitu duniani. Sisi wabongo tumezidi kuchonga. Elimu shallow!

    ReplyDelete
  53. Hatuwezi kufanana na nchi za ulaya 'reality' yao ni tofauti na ya kwetu. Sisi tuna umaskini uliyokithiri, watu vijijini hawawezi kuishi kule kwasababu hailipi wanakuja mijini kutafuta masihs kama utitiri tupende tusipende. Sasa mambo ya 'kufagia' na 'kusafisha' wa machinga 'in the name of city bye-laws' imepitwa na wakati, inakuwa uonevu mwishowe. Ni lazima tuwe na sera na mikakati inayoendana na hali yetu, utamaduni wetu na 'reality' yetu ya Africa!!!

    Dis-Appointed

    ReplyDelete
  54. Michuzi, nitafutie au kama una contact za huyo kijana nipatie.
    Email yangu unayo, nilikutumia picha za FLOWERS OF MANCHESTER(OLD TRAFFORD)

    ReplyDelete
  55. Michuzi na wadau
    Nilichelewa kuweka comments kwa sababu picha zilikuwa bado na utata. Mtu akivuliwa jeans, purukushani yake si ndogo. Lakini mbona malapa a.k.a yebo yebo ambazo ndizo rahisi kuvuka bado zimo miguuni?
    Pili naona jeans iko na mkanda. je ni rahisi kwa jeans kuvuliwa kwa nguvu na mkanda ukabaki imara?

    Naungana na mdau anony 8:56. Nikweli kuwa picha na maelezo yanatofautiana. Lengo si kuwatetea askari wa jiji, ila ni kuweza kujua ukweli na kutoa shutuma kikamilifu pale inapobidi

    ReplyDelete
  56. BRO MICHUZI,
    MI hawa askari wa jiji wananichefua sana inaonekana kwamba wameamua kufanya wanavyotaka kwa hawa wamachi9nga na swala hili hakuna ambaye analiongelea.
    hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kupiga mtu mwingine ni kinyume cha sheria sasa inakuwaje kwa muda mrefu sasa tunashuhudia hawa jamaa wanavunja sheria kwa kuwanyanyasa hasa wamachinga kisa eti wanfanya biashara haramu.sawa biashara hairuhusiwi katika maeneo ya jiji,hii isiwe chanzo cha unyanyasaji kwa walalahoi ambao wanajitahidi kupa ridhiki yao kwa njia za "uhalali".ufumbuzi ni kuwakamata labda wapigwe faini,zitungwe sheria kushughulikia swala hili.
    nawakilisha....

    ReplyDelete
  57. jami mbona mi sioni chupi ama boxer iko wapi ?? ina maana huyu jamaa alikuwa napeperusha bila ya chupi ?? te he hehehe ......mambo ya jua la bongo hayo nini ??
    Na yeye nae anataka shoo amejaaliwa nini mana angekuwa hajiamini vipi si angevua hiyo T shirt shingoni akajistiri chini ?? ........ladba dili hilo ......!! bongo noma..!!

    ReplyDelete
  58. ALIVUA NGUO/SURUALI MWENYWE..

    ReplyDelete
  59. huu ni uonevu polisi na machinga hawana tofauti kwahiyo polisi wasijidai kuwaone watoto wa watu.Machinga tembea na silaha wakikuletea fyatua tu hamna noma wala nini.Ingekuwa mimi natembea na dozi ya lethal mgambo ukileta za kuleta I put you to sleep very silent.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...