mama mzazi wa mtoto salome yohana aliyechinjwa majuzi akiwa amepagawa kwa uchungu wakati akisaidiwa kuweka udongo kwenye kaburi la binti yake wakati wa mazishi tabata segerea jioni hii. globu hii inatoa rambirambi kwa wafiwa na kuomba haki itendeke ili kila aliyehusika na kitendo hiki cha kinyama ahukumiwe ipaswavyo.
Mola Ilaze pema Roho ya Salome Peponi - Amin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Cha kusikitisha ni kuwa huyo muusika wa mauaji haya naye anaonekana kuwa ana matatizo ya akili....anahitaji psychiatric evaluation kwani kwa kweli ni mgonjea kama anasema huwa anaishi kwa kunywa damu za watu na alipokamatwa na kichwa cha huyo marehemu alianza kukinyonya damu mbele ya walinzi!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. we are speechless and gutted,may the heavens accept the innocent soul of salome

    ReplyDelete
  3. dah aisee R.I.P

    ReplyDelete
  4. Rest In Peace Babygirl. Your gone but you will never be forgotten. May Allah keep you warm and safe up there and here inshallah justice will be saved upon your death. Gone so young and naive, but continue to look after your fam and give mommy strength to go on.

    P.S, Parents becareful with ur kids, this world has turned into some cruel place. People are just redeculous.

    R.I.P SALOME.

    ReplyDelete
  5. Mungu ailaze roho ya mtoto/malaika Salome Yohana mahali pema peponi, Amen. Na wahusika waadhibiwe kwanza hapa duniani, then Mungu atajuana nao tena watakapofika mbele yake!

    ReplyDelete
  6. What!!! yaani alianza kukinyonya damu kichwa mbele ya kadamnasi??????????......Mh, basi huyo atakuwa VEMPIRE. Na Ma-vempire wakikamatwa huwa wanauliwa so na yeye auliwe tu ili hicho kichaa chake kisiendelee kuumiza watu wengine.
    R.I P baby Salome.

    ReplyDelete
  7. Nikiwa kama mzazi na uchungu wa mwana, pole nyingi zimfikie wazazi, ndugu na jamaa za Salome. Na msiache kuwa mstari wa mbele kuhakikisha haki ya Salome inapatikana kwa maana ya mchawi, bibi yake na jamaa zake wote wanafilia jela. Hii itasaidia kwani hakuna mtoto au mtu mzima mwingine ambaye ataumia. Poleni na Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kizito

    ReplyDelete
  8. inasikitisha sana, nawaomba wazazi wasiwe wanawaacha watoto kucheza usiku nje ya nyumba zao, ni hatari sio tu kwa wauaji bali pia wabakaji. May God grant her eternal peace, amen.

    ReplyDelete
  9. Salome pumzika Yohana Pumzika kwa Amani. Umenipa uchungu kama mama pia yaani siwezi sema zaidi. wazazi wengine lindeni wanenu hii hali inatisha msiwaache waneno peke yao hata kama jua linawaka wakombatieni malaika wenu.
    Nikiwaza hii habari nakosa raha basi tu Mungu ametwaa.
    R.I.P Salome

    ReplyDelete
  10. Rest In Peace our lovely Baby Girl Salome!!

    ReplyDelete
  11. mungu ailaze roho ya salome mahali pema peponi, mungu awape nguvu wazazi wake pia waweze kutetea haki ya mtoto salome, wazazi tulinde watoto wetu sasa dunia ya sasa si ile ya zamani tena ya kumuacha mtoto akacheze kwa jirani.
    R.I.P BABY SALOME.

    ReplyDelete
  12. Kama mama ni jambo la kuhuzunisha mno kuona mzazi anapitia mambo kama haya..Mungu awafariji na awatie nguvu wazazi wa marehemu Salome.Yeye peke yake ndiye atakayefuta machozi yenu kwa kuwatendea haki ktk msiba huu mkubwa.
    R.I.P Baby Girl Salome.

    ReplyDelete
  13. Inalillah wainaIlahi rajiun. May Allah rest her soul in peace. Nawapa pole wazazi na familia ya baby Salome - May Allah give you patience and strength to go on. I hope justice will prevail the cruelty that happened to this very young, innocent child. Wazazi kuweni waangalifu na watoto wenu wanaume kwa wanawake dunia imebadilika, kuna alot of perverts out there. Take care of your babies please..

    ReplyDelete
  14. Huku UK kuna ma paedophile wazazi tumeweka roho juu huko nyumbani kumezuka ma dracula looo! dunia imekwisha hakuna hata pakujificha wala usalama, ukisikia karne za mwisho mwisho ndio hizi.Poleni sana wazazi wa Salome picha inaonyesha uchungu mno ambao utachukua muda mrefu kuondoka.
    M'Mungu ilaze roho ya salome wetu peponi.Amin

    ReplyDelete
  15. Rest in peace my dear angel!!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. Pole Mama Salome, wafiwa wengine na wote walioshtushwa na kuhuzunika na msiba huu kama mimi.

    Sisi waislamu kwa mujibu wa imani na itikadi zetu tunaamini mtoto hana dhambi na kwa kuwa Salome hakuwa na dhambi basi yeye atakwenda kupumzika milele peponi-Amen.

    ReplyDelete
  17. Salome pumzika kwa amani, malaika wa bwana wakulinde. Sina mtoto ila machungu ninayoyasikia juu yako ni makubwa sana.

    Mama na baba Salome, mungu awatie nguvu katika hiki kipindi kigumu, na mjue ya kwamba taifa lote linalia pamoja na nyie. Mungu awalinde na awape nguvu ya kufuatilia haki ya Salome. Sote tuko pamoja na nanyi.

    ReplyDelete
  18. Little Angel REST IN PEACE, Mungu aliyekuleta duniani atakupigania, haijulikani ni wangapi waliotendewa unyama huu kama wewe ila kwa uwezo wa MUNGU aliye hai watafichuliwa wote, shetani sasa hana pa kujificha. Poleni sana wazazi wa Salome na pia wote mlioguswa na msiba huu Mungu awatangulie sana AMEN

    ReplyDelete
  19. Yaani nasikia tumbo linavurugika, ukizingatia nina baby girl same age, sitaki kufikiria wazazi wake wanajisikiaje...all in all, May God give them extra strength to carry this, and may his love shield and comfort them. Mtoto yeye ni angel, ameshapumzika kifuani mwa bwana, na machungu ameyasahau. Halafu bwana mimi nakerwa (samahanini) na wanaosisitiza mtoto ana psychological probs,afanyiwe uchunguzi kiakili etc...kwa taarifa yenu alishapimwaga mhimbili akaoneka ni mzima kabisa.Sasa aliyewaambia wachawi akili zao mbovu ni nani? These are supernastural issues and have to be dealt with supernaturally!Sio kwa mganga, shetani hafukuzi shetani mwenzie, that child with his evil gang need deliverance, maombezi ya nguvu otherwise mwezi wa tatu utafika akiwa bado jela atatafuta mtu mwingine wa kunywa damu,mapolisi beware!Na ameshasema kuna ajali ameplant manzese darajani...jamani watumishi wa Mungu something needs to be done immediately to protect innocent souls! Na iwe fundisho kwetu sote, tunahitaji ulinzi wa damu ya yesu, seriously, kwa kuwa shetani na kundi lake pia hawalali usingizi. RIP baby girl!

    ReplyDelete
  20. inauma jamani,mimi bado sina mtoto lkn nimeumia na nimelia sana nilipoona kwenye TV mazishi ya cute baby salome,Mungu awape nguvu wazazi na ndugu wakati huu mgumu wa majonzi.

    ReplyDelete
  21. RIP Salome,mimi nadhani haya ndo mambo ya kuandamana haswa kwa wale wapenda maandamano,kupinga mauaji ya kikatili ya mtoto salome hususani uchawi na ushirikina ili kuishinikiza serikali itoe/iseme uamuzi wa maana juu ya hili na sio bla bla.

    ReplyDelete
  22. Pole sana mama, yaani sijui ni hukumu gani itakayomrudishia faraja huyu mama! Sioni hata moja.

    Hasara ya kupoteza mtoto ni kubwa mno mno, kuliko hata viwango vya adhabu zote duniani. Sisi wazazi tunaelewa thamani ya mtoto, lakini nahisi mfiwa ndio pekee anayejua uchungu wa kupotelewa mtoto.

    Mungu akufariji.

    Mdau- Amsterdam

    ReplyDelete
  23. ngugu wafiwa kwanza kabisa napenda kutoa pole na hakika ni msiba wote kwa hakika inasikitisha kuona unyama kama huu unafanyika wanaosisitiza mtoto ana psychological probs,afanyiwe uchunguzi kiakili etc...kwa taarifa yenu alishapimwaga mhimbili akaoneka ni mzima.

    mimi kitu nacho kilaumu sana tanzania yetu imekuwa haina utu hasa serikali imejaa rushwa ya hali ya juu kiasi unaruhusu unyama kufanyika kama huu na kuzudi.

    uchawi hamna ni baishara ya wajanja kuwala waliozubaa kama uchawi uko basi wakafanye haya saudi maana saudi waganga wa kienyeji ijumaa huwa ni panga. sasa kama mtu mchawi basi alizuie hilo panga ikiwa anweza kupindua basi watu wakafa kwanini asizuie panga.

    tatizo afrika kwa ujumla na hasa tanzania inasikitisha watu kuamini sana uchawi kupita kiasi.

    yote ni uongo mtupu tatizo hata viongozi wa serikali tena wenye nyadhifa za hali ya juu wanaamini.

    mimi nilipokuwa tanzania wakati wa uchaguzi kuna rafiki yangu ambaye amejifanya mganga alikuwa akila pesa mbaya yake akaniambia ingalikuwepo dawa nayowafanyia ningalijifanyia mwenyewe na familia yangu lakini wajinga ndio waliwao.
    haki muhimu ikamilishwe mimi ningalipenda napate namba ya mama wa marehemu ili niweze kumsaidi kadri MUNGU atakavyonijalia kwa hali na mali ili haki ipatikane. MUNGU IBARIKI HAKI

    ReplyDelete
  24. Kwa kweli inatia uchungu, sijapata ona, yaani... ahaa. Jamani hakuna mtoto hakuna nini hiyo kijana anyongwe tu.

    ReplyDelete
  25. Hivi hamnalaws. I hope umefika wakati wa kucreate laws.. Tunahitaji alome laws. Watu wa aina hii hamna hata kupeleka kwa judge kupoteza hela. Ni kutia kitanzi tu.

    ReplyDelete
  26. Rest in PEACE, Salome. May God give your parents a strength to carry on.

    By Mchagiaji

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 01, 2008

    its better to carry on your pocket a rosary or tasbii - i dont now how to spell it but its like rosary i guess it gonna help with this devils

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...