Mdau John Kitime leo anatuamsha na 'Fimbo lugoda' Orchestra Tancut Almasi: Toka kushoto Buhero Bakari (Trumpet),Kyanga Songa, Kasaloo Kyanga, Kabeya Badu, Kalala Mbwebwe,Abdul Mngatwa,Akuliake Salehe (King Maluu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Doh! hicho kikosi kilikua ni moto wa kuotea mbali,lakini cha kusikitisha ktk hiyo picha nadhani labda walio hai ni watatu tu kama sikosei,kwa uhakika kalala mbwembwe hayupo duniani,kasaloo kyanga pia hayupo duniani,hao wengine sijawasikia muda mrefu,sijui wapo wapi.

    ReplyDelete
  2. Chonde chonde usimuue Kasaloo yuko hai na yuko Mwanza anaimba.Marehemu hapo ni Kyanga Songa,na Kalala Mbwebwe wengine wote wako hai

    ReplyDelete
  3. Bwana wee!
    Mie hawa wananikumbusha ule wimbo wao "Masafa Marefu".

    "Ninakwendaa Safarii, safari yenyewe ya masafa marefu,
    Ninajuaa mama utabakii watasema mengi, pia wabaya wetu mamaa watafurahii....

    ..Lakini usisikie yao mama watoto oo,
    Nakwenda kutafuta maisha ya watoto wetu mamaa...
    Chunga watoto wetu mama nitarudii,
    Tutaonanaa kwa Mapenzi ya Mungu..."

    Mwana wane. We acha tu!
    Kuna mdau mwenye huo wimbo original anitumie jamani?
    Sio wa 'Remix'.

    ReplyDelete
  4. Jamani nisaidieni nimesikia bendi moja katika wimbo wake unaokwenda kwa jina la HESHIMA KWA WANAWAKE (kama sijakosea) wakisema "AMENIIBIA KOMPYUTA AKIDHANI NI TV". Nimechanganyikiwa!

    Hivi ni nani kapoteza hapo?? Nimechoka kabisa .....

    ReplyDelete
  5. ....... keba, keba, keba, keba kebaaaa.... fimbo, fimbo, lugoda, mangalaaaaa!

    Those were the old good days mwanawane.

    ReplyDelete
  6. eeeeh! keba! keba! keba! keba! keba! kebaaaaaaa! fimbo!fimbo!logoda!logoda!Mangalaaaa!
    Duu,sio mchezo maanake.Hawa jama jamaa walikuwa wanatisha enzi hizo.Maana nakumbuka walikuwa wakivamia jiji walikuwa maarufu kama "mabush stars".Walikuwa wakisha moto kweli kweli.Hapo sijawaona Abdul Salvadoo"father kidevu"(ndani ya keyboard)Kawelee Mutimwana( ndani ya solo)na wakali wengine.Aaaah! enzi hizo bwana!

    ReplyDelete
  7. Kitime hawezi kutusaidia zile nyimbo zote za Tancut original zikwekwa katika CD kisha zikauzwa nchi nzima na nje?Siyo Remixes au Replays nasema zile zilizomo katika Audio Tape kama zilivyo rekodiwa na Radio Tanzania?Najua kuna suala la Hakimiliki hapo,lakini suala hilo liko ndani ya uwezo wako Kitime!Wapenzi wengi sana wa Tancut wamekuwa wakihangaika kupata zile original recordings za Tancut Orchestre.Matumaini yangu kwamba utanijibu kupitia blogu hii kama itawezekana au haitawezekana na sababu zake!You will be paid for the reply dont worry,si kasoda tu kwanza bia yenyewe hunywi au vipi Kitime?

    ReplyDelete
  8. Perez tutafutane.Karibuni tulijikusanya wanamuziki wa Tancut wote tuliobaki, kwanza ilikuwa uchungu na furaha kwa wakati moja.Kuna mpango wa kujaribu kuona kama tutaweza kuzitoa original recordings.Be bia naonja Jumatano na Alhamisi ya mwisho wa mwezi

    ReplyDelete
  9. jamani kabeya badu yupo wapi kwa sasa Papa Ngongi Amaon Ngongi Mtoni kwa Azizi Ally unakiona hicho kikosi wakati ule Iringa ilikuwa moto

    ReplyDelete
  10. Kwa mpenzi yeyote wa Tancut Almasi,mimi ninazo nyimbo karibia zote zilizo tamba kama masafa marefu,butinini,tucheze ngoma za africa,Helena,Matatizo,Pili Wangu,Samahani ya uongo,Uzuri wangu Na kadhalika,sasa kama kuna mtu anae zihitaji,tuwasiliane ili tuongee dili,maana hizo hata ukimuuliza Kitime mwenyewe hana.

    ReplyDelete
  11. Kuna mdau kauliza Kabeya Badu yuko wapi? Hivi sasa Kabeya Badu yuko na King King na Bendi ijulikanayo kama Ya Capital Africa Bara Motto (Wazee Sugu Waliokubuhu).

    Wanapigia Maeneo mbalimbali mjini Dar es Salaam

    ReplyDelete
  12. "Kinye kinye kisonzo tisa kumi mangala kinye kinye kisonzo tisa kuma mangala" hapo kwenye gitaa ya bess yupo marehemu Amani ngenzi pia namkumbuka baunsa wa bendi short man Tafu nae ni marehemu mambo yalikuwa poa sana ndani ya ukumbi wa olofea pale Iringa Mjini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...