Ingawa vyombo vya habari mbalimbali,katika nyakati tofauti tofauti,vimekuwa vikiandika habari zake na yeye kualikwa katika mihadhara mbalimbali kuzungumzia masuala ya kujitolea, umasikini,maradhi na mambo mbalimbali yahusuyo ubinaadamu,yawezekana kabisa ukawa hujawahi kulisikia jina lake wala kuiona sura yake.

Anaitwa John Mashaka (pichani),kijana mdogo wa miaka 30 ambaye kama walivyo watanzania wengine wengi, anakerwa na hali za umasikini,ujinga na maradhi zinazowakabili mamilioni ya watanzania hivi leo. kwa habari zake zaidi nenda www.bongocelebrity.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Neno "illiteracy" kwa miaka mingi limekuwa likitafsiriwa kama "ujinga" naamini hii si sahihi. Ujinga huelezeka kwenye uzembe wa akili na limitations katika fikra na mamuzi na kamwe haiwezi kuwa sawa na kutojua kusoma na kuandika. Marehemu bibi yangu hakuwa akujua kusoma wal kuandika bali alikuwa "clever" au mwerevu katika mambo mengi - ambayo naamini ni kinyume cha mtu mjinga.

    ReplyDelete
  2. Naona hii tabia ya kujionesha na kujitutumua haitatusaida sana watanzania, data shows very disapointing small amount of diaspora investing in tanzania. Help yourself, help your family and help your nation first. Sifa za magazetini kwa faida ya nani? and who is promoting who?
    Mdau makete

    ReplyDelete
  3. Jamaa katushinda, tukubali yaishe. Mambo ya teeee, taaahhhh ya kazi gani, hakuna tulichokifanya afalu tena kwa maelezo yake hajigambi, weneye matatizo ya akili na ajinga ni sisi tuomuonea donge bwana mdogo na jitihada zek. ndo maana wabongo sikuzote ni mambumbumbu, sasa huyu anatikisa ulaya nani kashaweza Tanzania? hakuna Mrs. Migiro na Thabeet wa mpira wa vikapu Tu Go, sis zetu ni ma party za nguvu, na tungu BONGO punguzeni majungu na Tungi. Mashaka, go. Go mashaka go tetetetetetethhhhhh haaaaa...hhaaaaaa walala hoi tupo numa yako

    Kileo - UK

    ReplyDelete
  4. Hongera mdau , mimi namini huyu jamaa sio tajiri ila ni mtu anayeishi maisha mazuri,mpangilio,mwelekeo na anajua anapoelekewa, kwendana na maelezo yake ni mtu anayemwelekeo na anajua anachofanya.Mfano anapata $3000 kwa mwezi ni nyingi sana kama unampangilio na unajuwa unataka ku archive kitu gani, kumbuka ukiweza kujibana kwa mwaka moja au miwili ukaweza ku save kila mwezi $500 au $1000 sioni kwanini ashindwe kufanya vitu vikubwa ,maana najua kunawatu wanasema bills ulaya huwezi ku save lakini inabidi ku sacrifise starehe , kinachotuangusha tanzania ni serikali unaweza ukawapa proposals nzuri na wasizifanyie kazi wanawapa investors toka nje,wakati mwingine unakuta kama muheza tanga kuna machungwa 24/7 unahitaji loan hata million 10 ufunguwe kiwanda cha kutengeneza juice wakati huo huo umesaidia wakazi wa mji huo, basi hata serikali ifunguwe kiwanda kusaidia wakazi wa pale . any way ni mawazo tu wadau

    William Uk

    ReplyDelete
  5. Hivi huyu mtu anajitangaza kwa kazi anazozifanya au anatangazwa? Kama anatangazwa hongera kama otherwise mungu atakulipa duniani na sio akhera.

    ReplyDelete
  6. chuki na majungu ndio zinaturudisha watu nyuma, utakuta hata mtu mzima anamuonea mtoto wa watu wivu anasoma, kweli itakusaidia nini acheni wivu watanzania na muapreciate maisha ya wenzenu.

    ReplyDelete
  7. Jamani naomba kuuliza msilalamike.

    Michuzi, Kama huyo ameooa?? Tafadhali naomba jibu na liwe la kweli. Tunahangaika sana kutafuta wachumba bila mafaniko sasa huyu kaja mwenyewe tena upeo wake upo juuuuuuuuuuu!

    I am serious about that please

    ReplyDelete
  8. Mmh jamanimiaka 30 si mbaba mzimakabisa? Manake hata NBA ukianza 30 tayari jamaa tunakuona utu uzima umetinga

    ReplyDelete
  9. Naona vidole viko wazi.

    Manka Mushi, changamkia tenda hii. CV na mkwanja vimekamilika, sijui size ya kiatu.

    ReplyDelete
  10. Duh, ume-pose vizuri kweli kwa ajili ya hii picha, sasa hapo ni ofisini au nyumbani?

    ReplyDelete
  11. Huyu ni mshikaji sana. Namfahamu tangu UN-Arusha, alikuwa mdogo sana kipindi hicho, nadhani ilikuwa ni baada ya kumaliza high school kabla ya kwenda Marekani

    Ila ninachojua, ni kwamba ana akili sana alafu mtaratibu sana. Wazungu walimpenda sana, sana, sana Arusha, kati ya watanzania. alikuwa miaka 16 au 17

    Ni mwanasheria huko Marekani, anafanya kazi Wall-Street na moja ya Investment Banks

    Manka, Hii tenda imekuja kinywani usipomeza shauri yako. Huyu ni Rais mtarajiwa, sis yetu macho tu.

    Hoya mshaka nitafute

    Jairo-Arusha

    ReplyDelete
  12. HUYU MKAKA NI SINGLE, HANA MKE WALA MTOTO.....NILIMUONA NA MARK II ZILE ZA KISASA BONGO AKITANUA. ILA NI MTARATIBU

    ILA SIJUI KUNA NINI KATI YAKE NA JOKATE......

    ReplyDelete
  13. Walai Michuzi, usibanie email ya huyu kaka. Tunatafuta wanaume hadi kwa dawa lakini hatupati, alafu unatuanikia picha ya kaka msomi, mwenye hela na roho nzuri ukidhania nini?
    Haya Basi ukidhania mimi nacheza basi utakoma, lazima unipe email ya huyu kaka.Sasa tukale polisi? Subiri nami niwe Manka mwingine ndo utakoma ubishi.

    Hauwezi kuandika kwamba yuko singo kana kwamba sisi siyo wanawake.

    ReplyDelete
  14. GOMBEA URAISI TAFADHALI

    ReplyDelete
  15. me simtaki awe mpenzi wangu, anisaidie kupata kazi tu tehe tehe tehe!!!.........
    nimesoma pia, nna akili with masters na certifications za kumwaga!!michu...contacts??

    ReplyDelete
  16. jamani habari ya MASHAKA kwangu ina Mashaka Makubwa. Wtz tunannunua story kienyeji sana.sijaona kubwa alilofanya kama kuchimba kisima kijijini sio jambo kubwa.

    Mheshimiwa MKONO anafanya mambo mengi jimboni kwake amejenga shule tano za mfano.

    mashaka naomba evidence zaidi juu ya kazi zako za kujitolea umefanya wapi?makala yako unasema ni siri kubwa lakini mama Thereza alijitolea na tunaona kazi zake wapi alipeleka.

    ukituonesha utatutia moyo zaidi kuliko kutupa mashaka kama haya.

    ReplyDelete
  17. Fisadi Michuzi,

    Nenda bongocelebrity.com uone wenzio wasio mafisadi wanavyomchambua rafiki ako Mashaka kiufanisi bila kubania points za kueleweka.

    Acha ufisadi wa kuzibia points za maana just for selfish reasons Bro.

    ReplyDelete
  18. yoh girls stay away from JOHN hes taken kwanza sidhan kama wanaume wanatafutwa kwa njia hii.....jitahidini na nyie mpate wenu si wawenzenu!nadhani mmeshaelewa mpaka hapo nimemaanisha nini kama bado JOHN is MINE!

    ReplyDelete
  19. HAPA KUNA KITU KINAENDELEA MPAKA MWANAKIJIJI KUAMUA KUJITOKEZA KWA PICHA NA UJUMBE USIOKUWA NA MATERIAL EVIDENCE.
    125TH ST.HARLEM.

    ReplyDelete
  20. hongera kaka umeongea kitu kwa ufasaa unahabari kuna mdada amejiweka wazi kuwa amekuzimia mmmm kazi kwako! utafatwa na wengi mpk utachanganyikiwa

    ReplyDelete
  21. Watanzania, tuacheni mambo ya kipumbavu. Nadhani mgesoma mahojiano yote, mngetuliza mapozi. Sasa huyu kosa lake ni nini?

    Wengine wanajitahidi kuleta mabadiliko, yetu sisi ni matusi.Bwana mdogo endelea na kazi yako, kama ulivyosema, wengine wataomba usiamke usingizini.Jitayarishe, watakuchukia kweli wengine lwa ,maana kasi yako inawatisha

    Michzui usibanie comments yangu. Hawa vijana wetu wajinga sana, inabidi wasome badala ya bla, blah,blah kibao kila ya chochote ya kuonyesha.

    ReplyDelete
  22. Kumbe ni mwanakijiji wa jamboforums ok angalau tumemwuona

    ReplyDelete
  23. Nafikiri BUSARA ni kufurahia anayoyafanya bwana Mashaka.Kuangalia upande unaofaa katika jamii ni muhimu sana katika kuchangia maoni.Hivyo kumpa moyo ili aweze kuokoa ndugu yetu mmoja au wawili ambao hawakupata nafasi ya mchango wa msaada wako wowote ni vizuri.Kuongea lugha itakayomfurahisha Mashaka ni sawa na msaada wako kwake.Tunashukuru bwana Mashaka kwa yote uliyoyafanya kwa jamii husika.
    Waka,
    Mwanakijiji

    ReplyDelete
  24. Mbona huyo kwanza kachoka alafu anasaidia watoto yatima kakomaa mhh kweli balaa hilo.
    Mdau kutoka
    U.K
    Liverpool

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...