KAKA MICHUZI,


NACHUKUA FURSA HII KUWAWAKILISHA WATU WA UBUNGO WENZANGU KUELEZA KILIO CHETU JUU YA HILI BONDE UNALOLIONA.


HILO BONDE KABLA HALIJAFIKIA HALI HIYO LIMESHAWEKEWA VIKAO SI CHINI YA KUMI KUWACHANGISHA WANA UBUNGO WOTE, NA SISI RAIA KWA KUPENDA MAENDELEO TUKAITIKIA WITO WA SERIKALI YETU YA KIJIJI TUKACHANGA'TENA NA TENA. 'LAKINI KAKA MICHUZI, AMINI USIAMINI, TANGU TUCHANGE ZAIDI YA MARA 7 HAKUNA HATA KIPANDE CHA KOKOTO KILICHOWEKWA KWA BONDE HILO MPAKA LIMEFIKA HATUA HIYO.


SASA WATU WA KUKAMATA MAFISADI WASIKAMATE HUKO JUU TU WAJE NA HUKU VICHOCHORONI. WAPO' MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA UBUNGO KIBANGU NA DIWANI WAKE WAHOJIWE KUHUSU FEDHA ZA MICHANGO ZA HAPA.


MDAU
UBUNGO KIBANGU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Poleni sana Wabungo Kibangu. Lakini naomba kuuliza, Hivi Diwani wa Kata yenu anapeperusha bendera ya Chama gani?

    ReplyDelete
  2. Tatizo bongo ni wachache wanao take advantage kutokana na tatizo. vilevile tatizo jingine ni kwa wachangiaji kuungia mkenge bila ya kujua udhibiti wa michango yao. Cha Muhimu ni jambo zuri na lenye manufaa kuchangia maendeleo lakini ni bora zaidi kudhibiti wachache wenye malengo mabaya.
    Fungueni Escrow account ambayo watu hawawezi kutia mikono mpaka wahusika wote watie saini kukubali kufanya hivyo na yeyote atakaegushi saini basi kajitafutia kesi kuliko kutojua kabisa hiyo michango imeenda wapi.

    ReplyDelete
  3. NYIE WAPENI KULA YAO TU TENA SIKU IKIFIKA.

    ReplyDelete
  4. Wee wacha tu! umeutonesha moyo wangu kuhusu hao wa serikali za mitaa, wamewekwa kutunyonya tu wananchi na si kingine! kuna siku huku mitaani kwetu (jina kapuni) wamenila 50,000/= kwa ajili ya kunipatia karatasi tu ambayo mpaka leo mwaka wa tatu sijaiona nimefuatilia mpaka naona aibu mwenyewe hata kupita njia tu hapo ofisini kwao na nimewaachia maana hata aibu wao hawana. Ushauri wangu msiwaachie umoja ni nguvu kutateni mfuatilie kumbukeni mmejinyima vingapi kwa kutaka bonde hilo liondoke na ndo kwanza linazidi, litawameza na nyumba zenu! hata kuwashitaki ikibidi maana ndo mafisadi wenyewe hao, haijalishi bendera gani inapepea ikibidi itashushwa tu tumechoka!

    ReplyDelete
  5. Bongo tambarrrarrrrreeeee

    Ha ha ha.........

    ReplyDelete
  6. Kibangu ni kwetu jamani, miaka zaidi ya 15 tangu nilipo yoyoma. Chakusikitisha ni bado maaendeleo kuwatembelea.

    Nadhani swala hili haliwezi kufanywa na serikali ya mitaa wala diwani. Hili ni swala la central government. Tatizo hapo ni mmomonyoko wa wa udongo, na ili kuzuia swala hilo wataalamu wa construction ndio wanatakiwa. Mimi sio mtaalamu wa mambo hayo, lakini nimeona huku ng'ambo wanavyodeal na mambo kama hayo.

    JK na serikali yake kwa kupitia wizara ya ujenzi wanaweza kutafuta permanent strategy ya swala hilo.

    Mdau wa US

    ReplyDelete
  7. Hey u bway na wewe kwa akili zako kabisa unaenda kuishi huko Kibangu, r u ok? njoo uishi huku masaki

    ReplyDelete
  8. Hii ndio Tanzania yetu. Mafisadi wanakula na kusevu hela kibao huku sisi wa hali ya chini tunanyong'onyea kila kukicha. Tazama hiyo nyumba hapo pembeni,Huyo ndugu hapo atakuwa hapati usingizi hasa mvua ikinyesha. Na ikibomoka ndio basi tena hata mchango japo wa kupata kibanda hautakuwepo. Sintasahau ile siku gari ya Pepsi ilipodondoka hapo. Huwezi amini miaka mitano tulikuwa tunapita na daladala na magari binafsi hapo lakini sasa ivi hata kwa baiskeli ni taaabu kama unavyomwona huyo jamaa hapo. Jamani Wadanganyika sasa tuamke usingizini. Tukatae kwa nguvu zote mambo kama haya ya uzembe uzembe. Yani mpaka afe mtu hapo ndio patashugulikiwa. Cha!!!!! Shie!!!!!!! Nagira

    ReplyDelete
  9. Kuna wizara inaitwa ya miuno mbinu, nasikia kuna wataalamu waliopopea. Hawa wanasubiri karibu na 2010, watafika tu usiwe na wasiwasi.
    Bwana michuzi , kero kama hizi zipo nyingi, na tunapozituma kwako tunaomba uziweke wazi, kwani kwa kufanya hivi, wao watashtuka, na huenda wakawajibika. Nasema hivi kwasababu gani, nilikutumia kero ya Usafiri wa Gongolamboto,lakini hukuiweka hewani. Sio mbaya, huenda umeidedisha kimakosa.
    m3

    ReplyDelete
  10. Hameni haraka hapo eneo kama hilo ni eneo lijulikanalo kama "Condemed area" hameni wenyewe haraka.

    Mtu utaishije eneo kama hilo? Hapo ni Dar es salaam au Ngorongoro Crater. Hapo hakuna chama tawala wala cha upinzani kinachoweza kuwatetea mkifa.

    Kama hamtaki kuhama shauri yenu mimi nawaapia sitakuwepo huko bondeni kuwadaka kama golikipa nyumba zenu zikianza kuporomoka na nyie mkianza kuanguka kwa staili ya kenge kuelekea huko bondeni kwa sababu ya maporomoko ya udongo.

    ReplyDelete
  11. Kabla ya kuwalaumu wengine kwanza tuangalie makosa tuliyofanya sisi wenyewe...

    Chanzo cha tatizo hili la kibangu ni tabia ya wakazi wake ya miaka mingi.Walikuwa wanatumia ukingo wa mto kama sehemu ya kutupa takataka.

    Jitihada za kuwafanya waache tabia hizo kwa njia ya matanazo hazikufanikiwa.Matokeo yake ardhi imekuwa laini na mmomonyoko ndio kama unavyoonekana.

    Hii itumike kama fundisho kwa wakazi wa maeneo mengine ambao hawayatunzi maeneo yao.

    Nini kifanyike sasa Kibangu?: tatizo limeshakuwa kubwa kuliko uwezo wa serikali ya mitaa.Serikali ya jiji inabidi iingilie kati.Kuna wakati mjadala wa bonde hili ulikuwa bungeni ila uliishia kwenye porojo tu. Sasa basi inabidi mmuwashike viongozi wenu shati mpaka swala hilo litatuliwe kutoka kwenye kodi ambazo serikali ya jiji inakusanya kila siku.

    In the mean time hapo inabidi pafungwe kabisa,na pafungwe kikwelikweli(physical barrier) sio kama walivyofanya wao kuweka kibao cha "usipite hapa"...

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 01, 2008

    Mi nasikitika tu kwa vile kuna demu wangu anaishi mitaa hiyo, siwezi kufika kwake na usafiri wangu. Inabidi niishie River side.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 01, 2008

    HAA HAAA HAAA! ATI MBUNGE WAO ANAITWA KEENJA LAKINI YEYE ANAISHI TAMBARAREEEE PALE VICTORIA...ANALALA USINGIZI MNONO KWAKE NYIE MSUBIRINI TU 2010 ATAWATEMBELEA TENA KUOMBA KULA YAKE! TEH TEH TEH! SI MLIMCHAGUA WENYEWE, TENA KWA KISHINDO!
    HIYO WIZARA YA MIUNDOMBINU WALA MSITHUBUTU KWENDA IMEOZAAA!! BOSI WAO SI NDIO MZEE WA VIJISENTI!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 02, 2008

    Anony May 01, 2008 12:57 PM. Sio Mzee wa Vijisenti, Ni MZEE VICENT!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...