Majina ya Utani ya Wachezaji wa Bongo!Brother Michu, hebu tufanye kama tumesahau kidogo wakina John Arne Riise, bwawa la maini n.k!:-)


Katika vitu vilivyokuwa vinaleta raha ya mpira wa kibongo ni majina ya utani ya wachezaji wetu na majina mengine yasiyo ya kawaida sana. Je wadau mnaelewa asili na maana ya baadhi ya majina haya ya utani?Baadhi ya majina niliyofanikiwa kuyakumbuka na kuyapata ni haya yafuatayo:

Celestine “Sikinde” Mbunga, Abdallah “King” Kibadeni Mputa, Mohamed Kajole “Machela”, Makumbi Juma “Homa ya Jiji, Mohamed Yahaya “tostao”, Abas Dilunga “Sungura”, Kitwana Manara “Popat” Rashid Idd “Chama”, Athumani Juma Chama “Jogoo”, na Boi Idd “Wikens”.


Wengine ni Leodgar Tenga “Engineer” Edgar ‘Fongo’ Mwafongo, Juma Pondamali “Mensah”, John Makelele “ Zig Zag”, Salum Kabunda “Ninja”, Maulidi Dilunga “Mexico” Zamoyoni Mogella “Golden boy”, Michael Paul “Nylon”, Saidi Swedi “Scud”, Frank Kassanga “Bwalya”, na Malota Soma “Ball Juggler”.


Wengine ni Mohamed Hussein “Mmachinga”, Madaraka Selemani "Mzee wa Kiminyio”, Iddi Selemani “Nyigu”, Fumo Felician “Mwalimu”, Jimmy Mored “Moro”, Abubakar Salum ‘Sure Boy’, Saidi Mwamba “Kizota” Hamis Gaga “Gagarino”, Mohamed Mwameja “Tanzania One”, Hussein Masha “Smart boy”, Method Mogella “Fundi”, Sanifu Lazzaro “Tingisha”, Samli Ayubu “Beki Mstaarabu”, Godwin Aswile “Scania”, Twaha Hamidu “ Noriega”, Abeid Mziba “Tekero”, Jobe Ayubu “Kwasa Kwasa”

Watani wa jadi : Peter Otieno “Basanga”, Sammy Onyango “Jogoo”, Charles Omondi “Korea”


Na hapa ni Ze riali majinaz :
Ikupilika Nkoba , Kalimangonga Ongala , Quresh Ufunguo, Kichochi Lemba, Jumanne Masimenti, Hamza Maneno, Bahatisha Ndulute,Wastara Baribari, Duncan Butinini, Mohamed Kampira, Pondamali, Mkandawile, Athumani Mambosasa, Sekilojo Chambua , Abdallah Mbuzi, Abdallah Boli, Selemani Mkati, Mohamed Mkweche, Jangalu, Hussein Mwakuluzo, Deo Mkuki, Damian Kimti, , Moshi Majungu, Abdul Mashine etc.

Patamu hapo! Kuna timu ilikuwa kutoka Mbeya inaitwa Zimanimoto. Maana yake????

N.B Mvua ikinyesha tu ujue Simba analowa siku hiyo!Mambo ya kuchimbia vitu golini, kurusha njiwa n.k.Tehe tehe tehe!

Mdau,
Denmark.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 78 mpaka sasa

  1. jumanne hassan "masmenti"

    ReplyDelete
  2. haHAHAHHAHA

    Sasa naomba kuuliza kama walikuwa hawana jezi ,timu ya nyumba ndio ilikuwa inavaa tshirt je ya ugenini kifua wazi au inakuwaje wadau nisaidieni maana nimecheke mwenyewe

    ReplyDelete
  3. Loh unatukumbusha mbali mdau,namkumbuka sana Hussein Mwakuluzo.Kichochi nilimwona mara ya Mwisho Kaitaba 1986 akiwa anadakia RTC Kagera nikiwa Form I Bukoba 'seko'!!!

    ReplyDelete
  4. Michuzi hapo unanikumbusha mwaka wa aibu kwa timu yetu ya taifa ambapo wakati huo chama cha soka FAT kilishindwa kupeleka jezi za timu yetu wakati ilipocheza na timu ya taifa ya Sudan na hapo mgeni rasmi wakati huo Marehemu Nimery aliyekuwa rauis wa Sudan akiikagua timu ya taifa stars akiongozwa na nahodha wake marehemu kwa sasa Abdulrahman Juma aliyekuwa maarufu sana kwa kupiga kona za uhakika.Mwanzo anaonekana Marehemu Chuma beki ya nguvu na alikuwa akiitwa CHUMA CHA MTWARA pia kwa jina la utani,anayefuatia ni Omar Zimbwe huyu kaka alikuwa akipiga free kick ama penalti basi hesabu bao na kipa akijaribu kudaka anaweza kuchanika mikono,anyefuata ni Kitwana Manara ama Popat,alikuwa bingwa kufunga magoli ya vichwa hasa ikipigwa kona na Abdulrahman Juma hesabu bao,anyechungulia ni Abdallah Kibaden unaweza kumita King Mputa,kwa kuchenga walinzi akiwa anacheza nafasi ya kiungo cha ushambuliaji alikuwa kinyanyasa sana ngome za walinzi,hao wengine siwezi kuwataja kwa vile hawaonekani vyema ni nywele tu.
    Michuzi pole kwa jana nisalimie Riise bingwa wa kujifunga wa Bwawa na Maini.

    ReplyDelete
  5. Michuzi leo globu yetu imesheheni na FLASH backs za maana! umeanza na za kifungilo na sasa umetumwagia za Sposiss....

    Pongezi kwa mdau wa Denmark, ana kumbukumbu nzuri na ahsante kwa ku-shea nasi 'vijisenti' vyako.

    Jambo moja naomba niliweke sawa ni kwamba ZIMANIMOTO haikuwa inatoka MBEYA. ZIMANIMOTO ni timu inatoka kule Bombiii nyumbiii nadhani mmenisoma... ukipenda unaweza kukuita Songea

    ReplyDelete
  6. Timu ya Zimanimoto ilikuwa Songea na sio Mbeya mkuu wangu. hiyo timu ulipewa jina la mmoja wa mashujaa wa vita ya Maji maji (Babu yake babangu), huyo chifu aliitwa Zimanimoto Fussi Gama, hiyo timu awali ilijulikana kama Tanesco lakini kufuatia ufisadi na urasimu wa Tanesco makao makuu timu ikakosa pesa, na mara Tanesco walikuwa wanawakatalia wachezaji kucheza mpira kwa vile walitaka timu ihamie makao makuu ili wachote vizuri pesa, wazee wa Songea walipopinga basi Tanesco wakaisusa timu ndo ikachukuliwa na wadau na kuipa jina hilo. Abdallah Kibaden Mputa hilo jina alilipata alipokuwa anafundisha majimaji, Mputa ni jina la mmoja wa machifu huko Songea, kwa hiyo jamaa alipewa jina hilo kufuatia kuwafurahisha wazee wa Songea wakati huo.
    Beki mstaarabu alikuwa mstaarabu kweli, jamaa anapotoka uwanjani ni kama anaingia vile, ilikuwa huwezi kumkuta amechafuka jezi yake, ndo maana akapewa jina hilo, na pia jamaa alikuwa hapendi kucheza faulo wala kujiangusha angusha, ndo maana aliitwa hivyo

    ReplyDelete
  7. Majina haya yana asili mbali mbali. Mengine ni kutokana na kiwango cha ubora cha uchezaji (kama Golden Boy - Kijana wa Dhahabu). Mengine ni majina ya wachezaji maarufu wa nchi zingine ambao walifananishwa uchewaji wao na wachezaji wetu wa Simba, Yanga, PAN etc (kama Tostao). Mengine yalitokana na jinsi mchezaji alivyocheza (kama ninja), mengine yaliibukia tu kutokana na umaarufu wa kitu fulani wakati huo. Mengine yalitokana na imani fulani (kwa mfano watu wengie walijua/waliamini kuwa Tenga alikuwa ameenda shule/msomi). Mengine yanaweza tu kutokana na mtu mmoja kuropoka kitu uwanjani, basi likanata. Na mengine hayana maana yoyote kabisaaaa.

    ReplyDelete
  8. Niongezee majina mengine....MOHAMED MSUBA,OMARI CHOGO`CHOGO CHEMBA`,OMARI KAPERA...PIA SIKU MVUA IKINYESHA KISHA LIKAWAKA JUA IMANI ILIKUWA MNYAMA LAZIMA ACHANE KANDAMBILI...PATAMU HAPOOOO

    ReplyDelete
  9. Umemsahahu Sunday Manara "Computer"

    ReplyDelete
  10. Hii list imeandaliwa na watu naoweza kuwaita 'novices' kwa sababu imewasahau watu kama Mohamed Bakari "Tall", Sunday Manara "Computer".

    MTIHANI: JE MNAKUMBUKA WAFUATAO NA MAJINA YAO YA UTANI???

    Athumani Mambosasa, Gibson Sembuli, Juma Pondamali, Peter Tino, George Masatu, FUMO FELICIAN, MOHAMED DILUNGA???

    ReplyDelete
  11. Mdau umenikumbusha mbali sana kidogo chozi lintoke, pia unawakumbuka Kaingilila Maufi, Daudi Kufakunoga,Jumanne Ucheche, Mohamedi Mgalike na Said Mrisho "Ziko wa Kilosa" pia unawakumbuka wachezaji wa timu ya Vita ya Zaire kina Mayanga, Kashimuka, Lobilo, Lofombo na Baku, usimsahau mshabiki wa Pan mzee Mbegu na askari Nkama Shapu vilikuwa ni viburudisho vya aina yake.

    ReplyDelete
  12. dah nimekukubali mzee una kumbukumbu si mchezo lakini kuna mchezaji mmoja kwenye majina ya kiukweli umemsahau hilo jina lilikuwa linanivunja mbavu sana mimi naye ni daudi kufakunoga alikuwa akichezea tukuyu stars, unaweza kuongezea abdallah boli pia manake bongo kama huna jina kitendawili huwezi kuwa mchezaji mpira mzuri tehtehte

    ReplyDelete
  13. Si utani babake.Hii ilikuwa inatia raha sana.siku hizi hakuna vitu kama hivi. umenikumbusha mbali sana, ila nadhani kuna majina mengi hayapo kwenye listi

    ReplyDelete
  14. Mi naona nichangie ze riali majinaz.Mchonga (Bakari) inaelekea alikuwa anachonga sana au aliitwa hivyo kutokana na baba wa taifa kuitwa mzee mchonga!

    ReplyDelete
  15. umesahau Juma Limonga "Stop engine"

    ReplyDelete
  16. bila kuwasahau mrage wakabange , joseph machella,sahau kambi ,ebwanae hayo majina yote umenikubusha mbali sana
    mdau uk

    ReplyDelete
  17. Aminia babaake. Usimsahau "Kaingilila Maufi."

    ReplyDelete
  18. Namkumbuka Silvatus Ibrahim "Polisi" wa Yanga "Yosso" miaka ya tisini mwanzoni, akiwa na kina Anwar Awadh, Nonda Shabani "Papii", "Fusso", n.k.

    ReplyDelete
  19. Ahsante sana Ndugu Issa hapa ni mdau mbegu wa Ukerewe napanda kusema umetoa majina mengi lakini sijaliona jina la kaka wa kinyozi wako hapo Migomigo au ni mimi pekee sijaliona? Na si lingine bali "Zembwela" Mwenyewe khalidi Bitebo, Mambo ya kanda za ziwa enzi zake. Ahsante sana mdau Na Vipi kuhusu Obi Mwambungu "mtaalam wa Kona"? Au Original "Nylon" mwenyewe alikuwa Ayoub Shabani Left winger Young Africa? na vipi kuhusu "Bruce Lee" Daud Salum?. Wapo wengi acha niishie hapa ahsanteni wadau.

    ReplyDelete
  20. Zimanimoto mdau najua iko Songea, "pale pale mfaranyaki" karibu na uwanja wa Maji maji. Nakumbuka enzi zetu(July 1992-May 1994) za Box2 waluhila (Songea boys) tukienda pale kuona mazoezi ya Tamsala (Songea Girls) basketball. Kuna kituo cha zima moto labda wenyeji walitoa jina hilo kutokana na kituo hicho. Uwanja wenyewe ulikuwa umechoka ukilinganisha na Maji maji.

    Mdau stori yako imenikumbusha mbali sana

    ReplyDelete
  21. umemsahau mao mkami `ball dance` chibe chibindu, said kolongo, bakari tutu, mchunga bakari, ali kangalu, kuna yule ``zico wa kilosa` said mrisho kama sikosei kipindi kile kulikua na majina mengi na yanavutia kama uchezaji wao.

    ReplyDelete
  22. naomba nimrekebishe kidogo mdau toka Denmark zimanimoto ilikuwa inatokea songea sio mbeya ilikuwa tanesco zamani baadae tanesco wakaikataa ndio ikapewa jina la zimanimoto ni jina lammoja kati ya machifu wakingoni aikuendelea sana sababu ya ukata

    ReplyDelete
  23. Katika ze riali majinaz, pia kuna: kaingilila maufi, itutu kigi, moshi majungu, muhidini cheupe, betwel afrika,

    ReplyDelete
  24. Ujinga kweli asilimali ya watanzania!!!...ati tunapeperusha sifa na majina hayo ya kibandia kwa wale ambao hawajafaulu katika fani yeyote ya kuikuza hadhi ya taifa letu kimpira,hebu angalia hali ya kandanda nchini...si aibu tupu tu na huyo mdau wa Denimarki anajionea sifa kwa kutuletea hiyo takataka ambayo kweli badala ya kujivuna tuone aibu na tujifiche mashimoni!!!
    Kuna wachezaji wawili tu waliojulikana kimpira ulimwenguni kutoka TZ...wakiwa Maulid Dilunga na Omar Mahadhi kwa sababu ya kuchaguliwa kuiwakilisha bara la Afrika kule Mexico mnamo mwaka 1970.Wachezaji wengine waliopata sifa kidogo katika sehemu hii ya Afrika Mashariki ni Abdalah Kibaden na Sunday Manara...kwahiyo mdau wa Denimarka hebu acha kupuliza tarumbeta ya kujisifia kwani majina yote hayo ni 'wafukuza hewa,na wapiga mateke gozi lililojaa pumzi tupu!!!

    ReplyDelete
  25. Na mie naongezea wa kina Ali Mchumila,Edward Chumila "Eddo Boy",Yussuf Ismail Bana,Ezekiel Gryson "Jujuman" mnawakumbuka hao???

    ReplyDelete
  26. Kwanza jiulizeni hao wachezaji wamefaidika na nini na mpira wa bongo? sio kutajataja majina tu naweza kutoa mfano ulio hai angalieni kina Peter Tino aliyetupeleka Lagos kwa mara ya kwanza kwenye FAINALI afrika nations amekwisha kwa gongo , kina selemani mkati, John mngazija,Salum Baja,Selemani Bakari, Mohamed Chopa,Emma Peter wote walikuwa MATEJA ya UNGA kina Maulid Dilunga mpaka anakufa alikuwa mlevi wa kutupwa wa gongo kina Abubakar Salum na Marehemu Gaga walikuwa walikuwa wanasifika kwa kupiga mizinga ya bia sasa geuza upande mwengine wa shilingi angalia viongozi wa vilabu na chama cha mpira Taifa wote wana majumba na biashara kwa jasho la wachezaji. kwa Mdau wa Denmark ilikuwa haina haja ya kuwasifia majina ilitakiwa Tuwasikitikie kwa kutupa nguvu zao for nothing.Mdau Zee la Kitaulo.- UK

    ReplyDelete
  27. Anonymous huko juu,
    Gaafar Mohammed El Nimeiry si marehemu, yupo Sudan kwa sasa bado anaishi baada ya kurudi toka uhamishoni Egypt.

    ReplyDelete
  28. Mohammed Kachumbari, Said Jeki, Yanga Bwanga, Kipara (Golikipa wa Lake Star ya Kigoma na Simba ya Dar), Hamisi Askari, Bakari Kidevu

    ReplyDelete
  29. Zimanimoto sio ya Mbeya, ni ya Songea..... umesahau!Badaye ikawa TANESCO Songea. Unaikumbuka MECCO. Mavumbi Omar umemwacha, Ramadhani Leny pia. Zitto Washington DC

    ReplyDelete
  30. yaani mkuu wa wilaya yangu,hapo umenikumbusha mbali..unamkumbuka Lawrence mwalusako(kisomo),James Tungaraza(bolizozo)jamaa alikua sigara ya dar na walimwita hivyo baada yakuifunga simba katika mechi yaligi daraja la kwanza kipindi kile iliitwa,na hilo jiana bolizozo ni lamchezaji wa stela abij`a aliye ifunga simba goli lapili taifa pale na kuchukua ubingwa wa klab bingwa afrika so james alipofunga goli lapili katika mechi na simba maeneo yaleyale so wapenzi wa yanga wakaanza kushangilia wakimwita bolizozo...........sokala bongo lilikua naupinzani na raha kipindi kile

    ReplyDelete
  31. Anony 10:05 na 11:35 wote wa April 23, nawasikitikia sana kwani hamuoni kuwa nyie tu ndio mko tofauti na wengine?? hamjashtuka muwe mnaangalia upepo jamani, mpaka Chenge anawazidi.

    Aidha walifaidi na mpira au hawakufaidi na mpira, aidha walileta mafanikio nchini au hawakuleta haikuwa busara kwa nyie kutoa maoni kama hayo.
    1.Mpira wa TANZANIA vijana wa na vipaji ilo mueelewe tumekosa uongozi mzuri, umaskini n.k

    2.Tabia ya wachezaji bado pia ni uongozi wa vilabu unachangia, kama unamtumia mchezaji mvuta bangi badala ya kumsaidia aache, unafikiri wa kulaumiwa nimchezaji tu ni wengi,mkiwamo nyie.

    MDAU WA DENMARK AMENIKUMBUSHA MBALI SANA, kuma mmoja hapo juu amesema anataka kutoa machozi,

    nduio pira wetu mbaya, mpira wetu wa kimaskini,lakini kumbukeni kipindi hicho hatukuwa na Luninga ambazo leo hii mna fursa ya kulinganisha mipira,

    kwa sisis maskini ilikuwa ndio rahja yetu , kusikiliza redio Tanzania au kwenda uwanjani, niliPPOKUWA MTOT KILA GAZETI LENYE PICHA YA YA YA MCHEZAJI NILIKUWA NAKATA NA KUTENGENEZA ALBAMU( kubandika picha nilikuwa natumia kama sio uji, basi utomvu wa miti).

    Leo nyie mnajiona mnajua na kuanza kuponda watu kisa eti mnaona Man , Bwawa la maini n.k

    Nyumbani we better be proud for what we are than for what you are not and toy think you are.

    Ndio nyie mnabadilisha uraia na kuukana Tanzania nyakati za kombe la dunia!

    Niko Canada, every one is saying."FOOTBALL IS TOTALLY AN AFRICAN GAME"



    Mdau -Canada

    ReplyDelete
  32. NASHUKURU WADAU KWA KUENDELEZA LEBENEKE LA MAJINA YALIYOSAHAULIKA NAK KUTOA UFAFANUZI!NIMEFURAHI SANA KUONA BAADHI YA MAJINA NILIYOYAACHA KAMA YA KINA KUFAKUNOGA n.k!
    Mdau Denmark.

    ReplyDelete
  33. Ebwana Ndio, mie kwa sababu ni 80s baby acha niwakumbushe early 90s majina ninayoyakumbuka. Mnaikumbuka Reli ya Morogoro, ilikuwa inaitwa kiboko ya vigogo. Simba au Yanga wakija Jamhuri lazima walale, vijana wale kina Said Mtono, Mbuyi Yondani, David Mihambo, Gasper Lupindo, Mohd Msomali alikuwa golikipa. Wadau mnakumbuka timu B ya taifa ilikuwa inaitwa Kakakuona? Kulikuwa na kina Sekilojo Chambua mule ndani walikuwa wanatisha vibay vibaya kulinganisha na timu A Victoria.

    Mmewasahau Coastal Union watoto wa Mkwakwani. Hussein Mwakuruzo, Victor Mkanwa, Reuben Mgaza, Said ngolongo, Razack Yusuf "Careca" Mwameja mwenyewe katokea Cost

    Vijana wa msimbazi na kosi lao la kufa mtu, Kasongo Athumani, Godwin Aswile, George Masatu, Mustafa Hoza, Hussein Aman Marsha, George Lucas Gazza, Tom Kipese, Malota Soma and Edo Chumilla wanakamilisha safu ya ushambuliaji, golini yuko Mwameja, kabla yake alikuwepo Iddi Paza "Father". Aibuuuu palikuwa panachimbika hapo.

    I miss those days man.

    ReplyDelete
  34. Duh kweli mdau ametukumbusha mbali sana sijui amefikiria nini!?Soka la bongo kwa kweli lilikuwa zamani na sio sasa.Mimi nawakumbuka Athuman Abdallah"China",the late Issa Athumani(RIP).Kassongo Athumani,Iddi Cheche,Iddi Pazi"Father",Ally Malilo"Loketo",Abdallah Msamba,Gebo Peter,Fred Felix Isaya Kataraiya "Minziro" Majeshi,hao ni kwa bara,na Zenji ni Innocent Haule,Victor Bambo,Seif Bausi,Mohamed Kachumbari,Duwa Said.

    ReplyDelete
  35. Wadau naomba mniambie kuhusu hili chama, maana Simba alikuwa hatii mguu.
    1.Kinye 1.Sahau Kambi
    2.Yusuph Bana 2.Mwakalebela
    3.Ahmed Amasha 3.ken Mkapa
    4.Chama 4.Aswile
    5.Allan Shomari 5.Kabunda
    6.Isiaka Hassan 6.IssaAthumani
    7.Juma Mkambi 7.Abubakarisalum
    8.Charles bonifas 8. China
    9.Abedi Mziba 9.SanifuLazaro
    10.Makumbi Juma 10. Kizota
    11.Omari Hussein 11.Kipese

    Hapo ndio Jangwani,kumekamilika!

    ReplyDelete
  36. Mdau wa Canada ahsante kwa kuongeza mvuto wa hii stori yaani mambo ya kubandika picha za wachezaji ilikuwa ndio yenyewe. Naongezea ile ya fungulia mbwa yaani dakika kadhaa kabla ya mpira kwisha mnaruhusiwa kuingia uwanjani. Askari wakisahau mnawapigia kelele. Na kuna miaka vijana tulikuwa tunaruhusiwa uingia bure(yoso). Mnajipanga foleni mnazama ndani. Wabongo tulivyokuwa noma unakuta mtu mzima nae anajipinda ili aonekane mdogo, soo pale ndata/mwela(polisi) wanapokustukia panakuwa hapatoshi kwa virungu.

    Mdau Shinyanga

    ReplyDelete
  37. nae rashidi mandanje ,stanley sungura ,ikupilike nkoba,lagu shinje na hezron mauma na felix MINZIRO walikuwapo kwenye ze real majinazi

    ReplyDelete
  38. Bila ya kusahau familia za soka kina Marehemu Mussa Kiwelu,Jamuhuri Kiwelu,Mwanamtwa Kiwelu,Mhehe Kiwelu,Joram Mwakatika 'kipara',Isack Mwakatika,Julius Mwakatika,Said John,Michael John

    ReplyDelete
  39. DUUH NAONA UMEWASAHAU WAKINA ITUTU KIGI,CHACHALA MUYA,KICHOCHI LEMBA,EMANUEL TENENDE,EMANUEL CHTETE.MIKIDADI MAUMBA,JELLA MTAGWA NA JUMANNE SHANGO MTAALAM

    ReplyDelete
  40. Nakumbuka enzi hizo tumesakua sana majalalani kutafuta mgazeti yenye picha za Wachezaji na kubandika kwenye daftari la zamani kwa gundi ya ugali wa muhogo .. michuzi anakumbuka sana . tulikuwa tunaita BOOK.

    ReplyDelete
  41. Kwa kuchangia zaidi nilikuwa napenda kumjibu mdau wa canada anon april 24 12.49am kabla ya kutulaumu angesoma vizuri maada yangu, kwa ufupi maoni yangu sikulaumu majina wala nini. kama mpira mimi mwenyewe nimecheza kiwango cha timu ya taifa vijana iliyokuwa na kina ayoub mzee,zamoyoni,malota,abdu amasha.tobias nkoma ,raha msigala na wengineo kabla ya kuacha soka (kwa ajili ya masomo)milango ya 80 nilichokuwa nazungumzia sio kuponda majina nilikuwa nasikitikia wachezaji wa zamani kukosa msaada(mpaka wengine wakawa walevi na mateja) kutoka vyama vya mpira ,vilabu na serikalini na ndicho kilichosababisha mpira wa bongo kukosa raha kama zamani. leo wachezaji wa zamani kama wangeenziwa ingekuwa changa moto kubwa sana kwa wachezaji wa wakati huu wangekuwa wakicheza ki ari na mapenzi sababu mpira ni moja ya kiburudisho.tungetizama upande mwengine wa picha tukajiuliza hao waliokuwa wakituletea raha na burudani leo wapo wapi ? na mpira ule wa zamani upo wapi ?. sio kuwataja majina tu beki mstaarabu,jembe ulaya,sikinde,mbuzi,kidevu nk. tutakuwa wachoyo wa fadhila kama hatutawasikitikia wale waliokuwa wakitupa burudani kwa jinsi walivyotupwa na mpira huo tunaozungumzia itabaki HISTORY- huo mtazamo wangu. Zee la Kitaulo-

    ReplyDelete
  42. Coastal Union: Salim Omar, Ally Maumba, Hilal Hemed, Said George...na mshabiki namba one, bonge la mtu linalosindikizwa na umati wa mashabiki kwenda mkwakwani: "Bwa Kaka". Hizo zilikuwa enzi.

    ReplyDelete
  43. Shilingi, Shiwa, Mnyepe, hao wa Moro.

    Mengi Matunda,

    Nani, Dunga, Chuma,

    Aloo Mwitu, Isihaka Mwitu.

    ReplyDelete
  44. Wadau hamuwezi kuwataja hao bila kuwasahau Dominic Chilambo, Ahamed Jongo, Omari Jongo, Charles Hillary, Brother Mick, Abisai Steven etc.

    ReplyDelete
  45. Juma Mgunda an mchango wake dhidi ya watani watu wa jadi - kwa kibaki halafu tusimsahau pia mtaalmu wa kupiga mpira nje, Twaha Hamidu

    ReplyDelete
  46. mwingine ni Razak Yusuf "Careca", Athuman Abdallah "China"

    ReplyDelete
  47. AFC LEOPARD :- Abbas Mahmoud, JJ Masiga (dr wa Meno), John Otieno (Basanga), Wilberforce mulamba(maradona), Josephat Murila (Kenya5), John Arieono, Joe Kadege, Keffa Tasso.
    Nakumbuka mechi ya Simba na Yanga Mwanza mwaka 1774. Kulikuwa na washabiki wa timu zote. Yanga wakiimba "Yanga yanga" na Simba wakiimba " Nani kauwa? Manyota Ndimbwa MS***E." Sijui ilitokana na nini. Siku hiyo nikiwa Kinondoni sikuweza kwenda nyumbani na kulala kwa Shangazi maana kumba kumba ya mashabiki na mioto wakipita unaweza kufa ... Sikonge

    ReplyDelete
  48. Aaah, umenikumbusha la IPP la mwaka 1999-2001; kina Hamza Nzoa, Ally Mkongwe, Imma Zunda, Aidan Mahimbo,James Job, Eliakim Chilale, Kiki De Kiki, Isaack Machibya, Mussa Hassan Mgosi, Nico Nyagawa na Deo Macha. Chama lilikuwa aibu!

    ReplyDelete
  49. jamani pamoja na wachezaji wote hao tusiwasahau waalimu wa miaka hiyo wafuatao
    mzee fideli,peter mandawa,magram,msomali,dan korosso,kilambo,paul gwivaha,joel bendera,nk

    ReplyDelete
  50. Mdau uliyemtaja MAULID DILUNGA kuwa
    marehemu, angalia vizuri data zako.
    UTAFUNGWA...!

    ReplyDelete
  51. Wapi Peter Dao Toka Kwa Watani Wa Jadi?

    Izz Wa

    ReplyDelete
  52. Mnakumbuka kikosi cha Coastal Union katika fainali za Klabu Bingwa Afrika Mashariki kule Mombasa?

    1. Hamisi Makene baadae Mwameja
    2. Saidi Kolongo
    3. Douglas Muhani
    4.
    5. Yasin Abuu Napil
    6. Ali Maumba
    7. Ali mwaliza
    8. Razk Yusf Careca
    9. Juma Mgunda
    10. Kasa Musa
    11. Huseni Mwakuruzo

    Kikosi hiki kiliitoa jasho AFC Leopards nyumbani kwao. Those days, my primary school days...... ngoja nirecall kikosi cha RTC Kigoma. Zitto, Washington DC

    ReplyDelete
  53. Muheshimiwa Zitto RTC Kigoma ilikua na kina Zaid masoud,sanifu lazaro,mavumbi omar

    ReplyDelete
  54. Mdau wa watangazaji hapo juu, ukumbuke bila ya mtu aliyekua anaitwa NOEL NAMALOWE wananchi walikua hawakai barazani kusikiliza mtanange.
    Charles Hilary atataja wote, lakini bila Noel Namalowe basi hewani hakuendeki.
    Hakika tulipotoka ilikuwa burdani ya kutosha.

    ReplyDelete
  55. Haiwezekani Ubao huu ufungwe bila kuwataja hawa maana nao ni muhimu,

    Hassan Afif - Simba
    Amour Aziz- Malindi
    Nkama Ntare- RTC Kagera
    Benny Luoga- Sigara
    Joseph Kapinga- Sigara
    Uganda- George Semogerere
    mtaniongezea wengine toka Uganda enzi hizo

    ReplyDelete
  56. Kulikuwa na Timu inaitwa Ujenzi Rukwa ilikuwa nayo Balaa.

    Kulikuwa na akina

    Atupele Mapugilo,
    Bahati Mwaipopo
    Eddo

    ReplyDelete
  57. Mbona tumemsahau Edbily Lunyamila aliyetutesa sana msimbazi? halafu yule jamaa Rafael Paul yuko wapi siku hizi wadau?

    ReplyDelete
  58. Oya wadau vipi Bakari Malima "JEMBE ULAYA" wa Yanga

    ReplyDelete
  59. lilla shomari,juma shabani"uncle j",charles kilinda,charles alberto,saleh hijja,juma hassan masmenti,medard madalle,mrage wa kabange,nico njohole,deo njohole ocd,selemani pembe,nico bambaga.beya simba,shabani katwila,martin kikwa,michael kidilu.benedicto mwakisalu.saulo jaji,ayubu mzee,yasin abuu napili.denis mdoe,itutu kigi,damian mrisho kimti,mohd mwinyimkuu,naona niishie hapo kwa leo.rp amekufa.

    ReplyDelete
  60. Wale wenzangu na mie wazenji nadhani pia mtaikumbuka Small Simba "Moto Small" iliyokuwa na watu kama Karume Mussa, James Kisaka,Ali Muhsin,Zuberi Wambura,Omar Hassan "King",Kapten Fadhil Ramadhan,Abdul-Wakati Juma,Marehem Kassim Kirara,Lenard William,Rashid Tall,Rashid Khamis,Abouf,Salum Baja,Bausi na wengine wengi chini ya mwenyewe Super Coach Abdul-Ghanny Himid Msoma.

    ReplyDelete
  61. Tusimsahau Sekilojo Chambua wa Yanga and Ally Yusuph "TIGGANA" pamoja na Thomas Kipese "UNCLE TOM" wa Simba.

    ReplyDelete
  62. Masela naomba mniambie wapi Mwameja Tanzania One, maana kimyaaaaaa, ni katika baadhi ya makipa waliosifika sana Bongo, mwenye data zake atudondoshee.


    Mdau wa Spoti

    ReplyDelete
  63. hivi jamani huyo Reporter wa TV inayoitwa BEN ..Ayub Mzee SIO YULE ALIYEKUWA ..Mchezaji wa Nyota Nyekundu..

    ReplyDelete
  64. mmesahau wastara bari bari, natimu ya tukuyu stars ilikuwa na wanyakyusa wameshiba

    ReplyDelete
  65. Willy Martin "Gari Kubwa", Madundo Mtambo, Kipanya Malapa.
    By Festo K.

    ReplyDelete
  66. Lazima niwakumbushe chaam la AFC Arusha,
    James Kisaka
    Ally Pande
    Simon Kishoka
    Juma Mkulila
    Lila Shamari
    Charles Mngodo
    Mwanga Luheya
    Muhidini Cheupe/George Liganga
    Mohamed Bob Chopa
    Feruzi Juma
    Mohamed Mateneke
    AP

    ReplyDelete
  67. Wadau mmewataja woote lakini mmemsahau mtu mmoja alikua anaitwa PETER TINO, huyu jamaa alikua anaujua mpira sio masihara, nakumbuka picha yake moja akiwa na bandage kichwani siku ya mechi nadhani ya taifa stars.

    Kumjibu jamaa alietaka kujua kuhusu Raphael Paul ni kwamba huyu bwana ni marehemu tayari.

    ReplyDelete
  68. Wazalendo acheni mambo mumemsahau mzee wao,ngoma kubwa JELA MTAGWA hakuna kama yeye katika TANO(5) zote zilizopita bongo mpaka sasa hivi BY Mlalahoi.

    ReplyDelete
  69. Na mie nakuja na chama zet za Lake zone.
    Naanza na timu ya home:PAMBA YA SHINYANGA
    1.Hamis Maftah
    2.Khasim Nadhir
    3.Hashim Liseki
    5.Sululu Mrisho
    6.Bakari Kulewa
    7.Nasib Hussein
    8.Abbas Magongo- kabla hajaenda Gor Mahia ya Kenya.
    9.Seif - Mhindi wa kwanza kumuona anacheza boli la uhakika
    10.Issa Mohamed
    11. Dennis Donoa baadae akaitwa Abdul Donoa.
    WANACHEZA hapo KAMBARAGE na MWADUI
    1.Ibrahim Ismail- kabla hajaenda Shabana ya Kisumu
    2.Eliakim Brando
    3.Mwambete
    4.Chia Masonga kabla hajenda AICC
    5.Charles Mwanga kabla hajenda Yanga
    6.Prosper Mboya
    7.Justin Nelson Simfukwe kabla hajenda CDA
    8.Willy Kiango then Simba
    9.Abdallah Shebe then Gor Mahia
    10.Shaaban Katwila then Yanga
    11.Joseph Mbelwa.
    Duuh hapo Kambarage ni sell out na nimeingia uwanjani kwa kubeba viatu vya Nasib Hussein.
    Cha chandu - UK

    ReplyDelete
  70. Bado niko kwetu Kanda ya ziwa chama la PAMBA YA MWANZA enzi hizo limetua Kambarage Stadium kucheza na PAMBA ya SHY hapo sell out hakuna nafasi kabisa.
    1. Madata Lubigisa/Juma mhina
    2.Yusuf Ismail "Bana"
    3.Athman Juma "Chama"
    4.Ibrahim Magongo
    5.Joram Mwakatika
    6.James Ng'ong'a"jaluo"
    7.Antony Nyembo
    8.Khalid Bitebo
    9.Amri Ibrahim
    10.Idd Watchee
    11.Abuu Juma
    Duuh hii mechi Abbas Magongo alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kipepsi kaka yake Ibrahim Magongo.
    Cha chandu -UK

    ReplyDelete
  71. Acha yote hayo, mpira ulikuwa sio mpira bila kina Charles Hilary "Mzee wa macharanga", Noel Namalowe, Mikidadi Mahmoud,Julius Nyaisangah "uncle J", Salim Mbonde, Ahmed Kipozi, Sekioni Kitojo, Ahmedi Jongo. Ukienda kuangalia mpira lazima uchukue ka-national radio kako upate uhondo both sides. Hawa jamaa ndio waanzilishi wa maneno kama songombingo, majalo nk

    ReplyDelete
  72. MUHAJI MUKI ALITOKEA LINDI KUJA YANGA, KABURU PIA ALITOKA LINDI KUJA YANGA, MARTINI KIKWA WA SIMBA,

    ReplyDelete
  73. Haya RTC Kigoma. Kule mtanagzaji alikuwa ni Chisunga Steven, mawimbi ya ziwa tanganyika, simba hapigi kucha.

    1. Patrick Mwangata
    2. Mavumbo Omar
    3. Khalid Rehani
    4. Yusuf Mfaume
    5. Juma Mkambi
    6. Hamza Maneno
    7. Dadi Phares
    8. Stanslaus
    9.Cheche Kagire
    10.Sanifu Lazaro
    11. Wastara Baribari

    Kikosi cha Kigoma Stars dhidi ya Igembensabo nani anakumbuka? Kile cha kina Kahuzu Habib, Kichochi Lemba n.k! je Relwe Eagles Kagera?

    ReplyDelete
  74. Je hawa bao mnawakumbuka?
    1. Ikupilika Mkoba
    2. Mtawa kaparata RTC Mbeya baadaye Majimaji
    3. Jobe Ayubu (kwasa kwasa) nafikiri Milambo Tabora
    4. Lindimu Muba
    5. Asangalwise Aswile (asanga aswile)
    6.

    ReplyDelete
  75. Hili nalo ni chama la timu iliokuwa ya kwanza kuchukua ubingwa nje ya Dar toka mji kasoro bahari - Mseto ya Morogoro.
    1.Hemed Mussa
    2.Vincent Mkude
    3.Ramadhani Mnyepe
    4.Shilingi
    5.Miraji Salum
    6.Spencer/Charles Boniphace Mkwassa
    7.Shiwa Lyambiko
    8.Aluu Ali
    9.Omar Hussein
    10.Hussein Ngulungu
    11.Abdallah Hussein
    Hawa jamaa waliibanjua Nyota ya Mtwara kwenye fainali ambayo Omar Hussein alikula Hat-trick.

    ReplyDelete
  76. WACHEZAJI WA YANGA WAKATI HUO,ELIAS MICHAEL,KITENGE BARAKA, BOI IDDI,HASSAN GOBBOS OMARI KAPERA,KILAMBO,ABDULRAHMAN JUMA,ABRAHMAN LUKONGO,M DILUNGA,JUMA BOMBA,ABEDI MAULIDI,AWADHI GERSON,LEORNARD CHITETE,NA WENGINEO NIMEWASAHAU

    ReplyDelete
  77. Acha niongeze...wa Uganda,,,Sadiq Waswa, Majid Musisi, Sam Timbe, Sam kabugo, ningezee tafadhali,,,

    ReplyDelete
  78. AnonymousJune 28, 2012

    Mao Mkami "Ball Dancer"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...