samweli
mdau meshack mfugale (kulia) akikabidhi dola 500 kwa emmanuel nkya kama mchango wake kwa mtoto samwel nkya (pichani juu) anayehitaji kwenda india kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na matibabu katika uso wake ambao umeharibika. wanaoshuhudia ni wajumbe wa kamati ya kumsaidia mtoto samweli akatibiwe.


mdau mfugale anayefanya kazi darfur, sudan, ni mmoja ya wadau wengi waliojitokeza kumchaangia mtoto huyu kiasi sasa mchango umetimia dola 9,500 na zimebakia dola 2,500 tu kukamilisha matakwa yote ikiwa ni pamoja na tiketi ya ndege mtoto samwel na baba yake, matibabu na malazi hospitali mwezi mmoja.


Baba wa mtoto huyo, emmanuel nkya, ametoa shukrani sana kwa wasamaria wema wote waliochangia kwa hali na mali. safari ya kwenda india inatarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa.
Kwa habari kamili bofya hapa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Thanks bro! Mungu akuongezee ulipotoa. My dear Samwel with God's sake everything will be alright.

    ReplyDelete
  2. Michuzi, ile dola yetu 500 iliyoahidiwa mshindi wa mil 4, tunaomba umwambie mdhamini aitoe kwa mtoto huyu. Manake hakupatikana mshindi, na kwa sababu blogu yetu ni ya jamii, basi tunaomba zawadi ifanye kazi ya jamii. Natanguliza shukrani

    ReplyDelete
  3. Mimi nakupongeza wewe mwenyewe kwa kuwa mwanakamati wa kamati ya kusaidia mtu. Inaonyesha jinsi unavyoijali jamii si kwenye blog tu bali hadi kwa vitendo. Naamini wadau zaidi watajitokeza kwa sababu tu wewe uko kwenye kamati.
    Nakutakieni kila la kheri na naamini kijana atapatiwa matibabu na mambo yatakuwa shwari.

    ReplyDelete
  4. Jamani kuuliza si ujinga. Hivi mtoto huyu mpaka leo jajaenda huko India Bado. Mbona kuna waliopata matatizo baada ya tangazo lake la kwanza walishapelekwa mara moja na tumeshuhudia wengine wengi tu. Hata sasa kuna wengine hata haijuilikani watarudi lini. Je utaratibu huwa ni tofauti kiasi kwamba hauwezi kumuingiza huyu kijana? Badala ya kumtembeza na kumzalilisha matangazoni kila siku?
    Naomba kuwasilisha.
    Muungwana.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana mr.Mfugale kwa moyo wako.Hebu niandikie globaldetective@lycos.com kwa mawasiliano zaidi.
    Met wako,
    Majita

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...