Kwa niaba yangu na kwa niaba ya familia,ndugu,jamaa na marafiki wa Abdulhameed Bafagih, nasikitika kuwafahamisha kifo cha mpendwa wetu,kaka yetu, mwenzetu, rafiki yetu Abdulhameed Bafagih, kilichotokea Jumatatu March 31st, 2008 majira ya baina ya saa nane na saa tisa na nusu mchana, katika Hospital ya Interfaith Brooklyn New York baada ya kuuguwa kwa muda mfupi.


Sala ya maiti itasaliwa leo baada ya salat Maghrib. Masjid Taqwa, Brooklyn-New York, na maziko yatakuwa kesho saa nne asubuhi katikamakaburi ya waislam yaliyopo New Jersey.


Hakika sisi sote tunatoka kwa Allah na kwa yeye ndio marejeo yetu,naomba tumuombee marehemu safari ya kheri na Mungu amuondoshee adhabu zakaburi na za kesho akhera, ameen.


Nasi tuliobaki Mungu atupe mwisho mwema.
Ameen.


Kutakuwa na hitma kwa upande wa wanawake ambayo tutamuombea dua mwenzetu na kaka yetu, inatarajiwa kuwa Jumamosi april 5th saa nane mchana Brooklyn new york.


Kwa maelezo zaidi tutawasiliana.


Tafadhali wafahamishe watanzania wenzetu habari hizi .


Ahsanteni sanawenu

Katty

NYC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Ina lilah wa ina ilah rajiun (sisi wote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea) Tumuombee mwenzetu awekwe mahala panapostaili kutokana na matendo yake
    amina

    katochi)

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu mbona hiyo comment yako inatisha...yaani awekwe mahala panapostahili kutokana na matendo yake????

    ReplyDelete
  3. mungu aiweke roho yake mahali pema peponi amin

    ReplyDelete
  4. INNA LILLAHI WA INNA ILAHI RAJIUN.

    ReplyDelete
  5. michu sasa huyu katty ndo nani? nimekufowardia mail leo katty kawekwa jina lake

    ReplyDelete
  6. Mungu aliumbwa Mungu ametwaa jina la bwana libarikiwe.
    Abulhamid umetutoka kama mchezo

    ReplyDelete
  7. jazzakallah!!! Inna lillah wa ina illah rajiun....
    Allah amrehemu mahali pema peponi..amina..

    ReplyDelete
  8. POLENI SANE!!! lakini huyu alikwa Brooklyn ya wapi mbona simfahamu??
    Wala sijawahi kumuona ktk michanganyo ya Wadau wa NY/NJ
    Mimi ni mdau wa NJ pia...

    ReplyDelete
  9. INNA LILLAHI WA INNA ILAHI RAJIUN.
    R.I.P.
    NAMKUMBUKA SANA ABDUL ENZI ZETU ZA CARE BOYS PALE KINONDONI B.

    ReplyDelete
  10. Mungu amlaze mahali pema peponi

    Wewe wa april fool...yaani wewe unajua kila mtu wa NJ/NY??? Who are you? Kada wa nyumba kumi au!!!?? Naamini ni wengi tu huwajui watu wapo wanaishi tu kama wewe unavyoishi na sio lazima uwafahamu wote...Na michanganyiko ya wabongo ipo mingi tu labda uliyokua unakwenda yeye alikua anakwenda mingine

    ReplyDelete
  11. Mdau wa 11:18pm inaelekea wewe ndio sio wakujimix maana Abulhamid mashallah alikuwa mtu wa watu si wazenji wenzake wala wabara he was a good quite guy!
    RIP Abdulhamid.

    mdau unakaa NJ ya wapi?

    ReplyDelete
  12. huyu katty siyo yuko bongo vakesheni?

    ReplyDelete
  13. MICHUZI.....HUYU JAMAA NI BABA YANGU MDOGO..NA NIMEPATA HABARI YA KUWA KWENYE MSIBA WAKE WALIFURIKA WATU VIBAYA MNO...MSIKITI ULIJAA MPAKA NJE WAUME KWA WANAWAKE...KWAHIYO NINGEPENDA KAMA INAWEZEKANA UIPOST VIDEO YA MAZISHI YAKE KWENYE TV YEYOTE YA HUKU ILI WATANZANIA WANAOENDA KULE WAJIFUNZE KUTOKANA NA HUYU NDUGU YETU ALIVOISHI NA WATU HUKO MAPA AKAPATA WATU WENGI KIASI HICHO....NIKIIPATA VIDEO YAKE NITAKULETEA KAMA INAWEZEKANA KWAKO WEWE UKAIPOST KWENYE TV ITAKUWA VIZURI ZAIDI....ILI SISI WATANZANIA TUJIVUNIE KUTOKA KWAKE YEYE KUISHI KWAKE HUKO NA WATU VIZURI MPAKA AKAPATA WATU WENGI SANA....NAMBA YA KAKA YAKE NI 0784859013 ALIYEKUWA HUKU NCHINI ILI UJUE ZAIDI KINACHOENDELEA ZAIDI.....

    ReplyDelete
  14. True mimi binafsi sikutegemea kama watu wangeweza kujitokeza kwenye mazishi kwa wingi kutokana na schedule! maana mazishi yalikuwa saa 10am. Lakini ma'ashallah Abdulhamid kapata watu msafara wa magari ulikuwa zaidi ya ishirini.
    RIP Abdulhamid

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...