paul scholes baada ya kufanya kile tulichokuwa tunataka. ngoja tumalize mtu kesho darajani, mtakoma ubishi moscow...

nenda BBC uone ndondocha hii ilivyokuwa kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. Duh Zeruzeru kawamaliza wa CATALAN(Barcelona) mie yangu macho kesho kama liverpool wakipita ujue yale mnayosema liverpool mnamtaka sababu watakuwa wabovu basi msahau, kama tukifika moscow tunauwa tu final. Babel na Torres kesho wanauwa kama Chelsea akipita bora wachukuwe Chelsea kuliko Shetani Wekundu, Shetani ni Shetani tu wanakuwa Haramu ngoja Angel Tuje Tuwauwe mashetani nyie. Wale Barca siwanajifanya mpira wa Arsenal Gonga mpaka Ndani ya Box, Chenga twawala sie hatuna sie Zaidi ya mashuti ya schole labda SG achukue njano.

    ReplyDelete
  2. Bwawa La MAini Kaa Mjue Bwawa Lenu Juu Kuna Daraja hatutozama kwenye hilo BWawa Leno, Mnajuwa kama Sie hatufungiki Darajani Briji. Kesho Tunawapiga 3-0. tukitoka hapo tunaenda kuwanyoa wale jamaa zenu wa kasikazini mwa uwengereza. Shetani Wekundu Manchester United. Mnajuwa kama Chelsea mpira wa chini juu butuwa nguvu vyote tunaweza. michuzi na william wa UK mkae mkao wakufuta machozi.

    ReplyDelete
  3. hahahahhahahahaahahhaahha

    wadau mliokuwa mnanitafuta menipata Liverpool na Chelsea mpo
    kweli tactics ni muhimu in europe sasa wale walio lalamika kuwa manchester tumefundishwa mpira nou camp mpo?naomba kusema kwamba mechi ya leo manchester united wameonesha unity and maturity,passing was good we should have won even by 4-0 but well no luck and mind you Vidic & Rooney out lakini Babu yetu Scholes kaonesha kwanini hadi leo anakuwa regarded as one of the best midfielders of all time in the world ,uzuri nilishakata ticket mapema ya moscow ngoja nitangulie alafu ni waache watoto wagombanie nafasi moja iliobakia
    haya bwana ngoja sasa tumalize league uzuri ntakuwepo ndani ya old traford jumamosi haya wadau poleni sana wapinzani,

    Ila Ronaldo inabaidi next season improvement kwenye big games inabidi ajitahidi sana maana leo kajitahidi kucheza kama timu lakini we need to see him do big things an who
    we are happy united family

    William uk(united for life)

    ReplyDelete
  4. OK now "Arsenal fans" stop talkin bullshit about Red Devils koz we r heading to MOSCOW........I mean SHUT da f@$ked up hehehehehehehe
    Mdau T-Dot

    ReplyDelete
  5. Wachongaji mko wapi??? Kile Chombo [Scholes] Sijui mtamlinganisha nani sasa??! amefunga sana magoli ya aina ile katika umri wake wa ukijana bado anaonyesha uwezo wa kumiliki kiungo na jinsi ya kugawa mpira! Ahsante kwa kuwaita mandondocha, nadhani ya hapo bongo bado yapo kichwani mwako!
    Kila la kheri kesho yeyote!

    ReplyDelete
  6. Ndugu yangu Mishuzi nyie moscow hamuione usijipe moyo saana, wale jamaa wa darajani wananyuka bakora sio mchezo, yaliotukuta jumapili tumeshika adabu, hivi ninavyokwambia tunajuta kwanini tumeingia fainali, tunawaombeeni muingie nyie fainali ili tupate ubwete kidogo lakini wakija wale nuksi chelsea watachafua hali ya hewa.

    Man U for Life.

    ReplyDelete
  7. wewe michuzi hamna lolote sisi tunajua tunacheza na chelsea tuna hamu nao kweli...wewe ukiingia fainali ujue umekwisha
    mdau manchester for life

    ReplyDelete
  8. SILENT STALKER SAYS...........MIMI NAMTAFUTA YULE NDINDI ALIEANDIKA UPUUZI WAKE HUYU HUU HAPA CHINI KWENYE ILE ISHU YA RONALDO MISSING A PENALTY .....NATAKA NIONE ATASEMA NINI SASA??? DOGO UWE UNAFUNGA MDOMO KAMA HUNA UHAKIKA NA ISHU UNAYOTAKA KUZUNGUMZA, WATU TULIKWAMBIA VIJANA WALIFANYA KITU INAITWA PROFESSIONAL DISPLAY IN NOU CAMP, MADHARA WAMEYAONA LEO....NYANGAU MKUBWA WEE NA UKOME USIRUDIE TENA


    Tarehe April 24, 2008 12:40 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Hapo ndo ninapomuona CR kwamba bado hajafikia hatua ya kuitwa bora kabisa duniani, kwani katika mechi kubwa, wakati ambao timu inamuhitaji zaidi huwa haonekani kabisa. na sio hapo Man U tu, hata timu yake ya taifa la Ureno ni hivyo hivyo, anapokutana na timu zinazocheza more technical game huwa anapotea kabisa. Nakumbuka hata bosi wa soka la Ulaya Platin alimwambia kwamba ajitahidi kufanya vizuri katika mechi kubwa 'big matches' ndo hapo ataanza kufikiriwa kuhesabiwa kwamba ni bora duniani. tehetehetehe, najua wapenzi wa timu yake na mpira wa uingereza mtaungana kupinga, lakini habari ndo hiyo kwamba CR kiwango chake ni mwisho robo fainali ya mashindano yeyote, ikishafika nusu fainali anashindwa, labda kama ni nusu fainali ya FA cup na sio mashindano makubwa kama Uefa, mtakumbuka mwaka jana dhidi ya AC Milan, ilikuwa hivyo hivyo. hivyo badala ya kuzidi kumsifia kijana, inabidi kumpa maelekezo muhimu ili aongeze bidii zaidi

    ReplyDelete
  9. Tunatishatunatisha!Navybouy uko wapi.Bado Moscow tunachapa mtu moja tu inatosha!Hatuongei tunachapa.kama vipi Michuzi tuweke dau,wee weka jiwe mi hela,kwa kuwa ni uhakika.nina furaha siwezi lala!Danny.UDSM

    ReplyDelete
  10. Utabiri (prediction)!?
    Kwa wataalam wa tafsiri na semi wanakubaliana kwamba predictions are never wrong unless they are proven false.
    Nyerere alisema ataishi hata miaka mia na watu hawakumpinga mpaka alipofariki ndipo tunajuwa he was wrong.
    so sidhani kama kuna mtu atapoteza muda kubishana kwa prediction kama hizi! why abishane? last week walisema leo ndio mwisho, leo wanasema moscow! By the way HONGERA ARSENAL 6-2 mwakani mutauwa mtu.

    so MOSCOW will decide! kama unaweza go and bet huone kama walambwa or not....

    G7
    UK

    ReplyDelete
  11. MCHUZI MIMI MAN U SIIPENDI KWANI MI NI BARCA, NA TUMETOLEWA KWA HIYO NAWAOMBEENI DUA MSHINDE HAPO KESHO KILA LA KHERI....
    KANSAS CITY

    ReplyDelete
  12. kwa NBA kila la kheri BOSTON CELTICS najua ma boi KG will not let me down

    ReplyDelete
  13. Home advantage counts! 21 may ni Chelsea vs Man U na Chelsea kama kawa kwa Man. Ila da yule Messi hafai,hafai.Yule ni Maradona wa leo

    ReplyDelete
  14. Mdau William hongera kwa kufanikisha safari ya Moscow. Hebu tupe maono yako (honestly) kuhusu fainali kati ya MANU Vs LPOOL au MANU Vs CHELSEA. Ni ipi itakuwa mechi ngumu kati ya hizo mbili. Ungependa ukutane na nani kati ya hao wawili?

    ReplyDelete
  15. Mdau William hongera kwa mafanikio ya jana. Hebu tupatie maoni yako (honestly and professionaly)kuhusu fainali kati ya MANU Vs LPOOL au MANU Vs CHELSEA. Ipi itakuwa mechi ngumu na ipi itakuwa mechi ya kufurahisha zaidi interms of tactics, creativity na maturity

    ReplyDelete
  16. Mi MAN U lakini yule Messi loh kiwangom kiko juu.Sijui kwa nini Ronaldo kwenye mechi kubwa anashindwa kuonekana.Kuna mwanablog alilionglea juzi watu wakamrukia na leo kuna mwingine ameligusia hapo juu.Anapashwa kusaidia timu pale inapomuhitaji.Ona Messi,I think he was man of the mactch.Anaweza kupangua defence,kutoa pasi na alkiwa hatari kwa Man.Mpira wa kujiangusha wa Ronaldo hata mimi siupendi.Ronaldo kwenye UEFA azidiwa na yule Park bwana!!.

    ReplyDelete
  17. Ningeshangaa sana katika Comments zote hizi isiwepo ya William,

    Maan siku ile pamoja na kuzamishwa pale darajani bado jamaa alipata uwezo wa kuchonga, itakua leo.

    Sawa bwana, ila kumbuka mkiingia fainal na jamaa wa stamford kanuni ni ile ile tu, kula kichapo then unakula kona,

    Ila nawahakikishieni kua Next session lazima Ghala lifanye mambo, tuna mpango wa kuleta silaha kali na ambazo hazijawahi kutumika popote duniani, kudadadadeki

    Mshika bunduki original

    ReplyDelete
  18. Ukitaka kujua utamu wa bwawa la maini ndio hapo leo tunaenda kulia maini yetu juu ya daraja hatuna wasiwasi. 21 may tunaenda kuwapunga mashetani pale moscow si unajua kaka michuzi ukututaka ubaya ubaya njoo kwenye mashindano yetu sio yao yale ya kueana magoli ya kujiangusha kina CR iliwapewe peneti, harafu mnatupa red card zisizo na mapangilio. MSIWE NA WASIWASI BWAWA LA MAINI WANAKUJA WENYEWE MMOJA MMOJA TUWAPE HUDUMA YAO.

    ReplyDelete
  19. wewe unayejiita Silent stalker ndo mpuuzi kabisa, huyo aliyesema CR bado anabaki kuwa mkweli, wewe unaongelea ushabiki usiokuwa na maana, kwani hiyo jana CR alifanya nini cha kutisha? au nikumbushe kuna bigmatch gani CR kafanya kitu cha pekee, hapa atleast Mdau William anakubali ukweli na tena kasisitiza kwamba CR anapaswa kuonekana kwenye big matches na sio wewe unayekuja na kuleta ujinga wako bila kujua unaongea nini? unaujua mpira wewe au unaropoka tu kwa vile mmeshinda? maana kama kucheza vizuri ni bora hata Messi alionekana akitisha kuliko CR, acha ushabiki usiokuwa na maana NDINDI mwenyewe!!


    SILENT STALKER SAYS...........MIMI NAMTAFUTA YULE NDINDI ALIEANDIKA UPUUZI WAKE HUYU HUU HAPA CHINI KWENYE ILE ISHU YA RONALDO MISSING A PENALTY .....NATAKA NIONE ATASEMA NINI SASA??? DOGO UWE UNAFUNGA MDOMO KAMA HUNA UHAKIKA NA ISHU UNAYOTAKA KUZUNGUMZA, WATU TULIKWAMBIA VIJANA WALIFANYA KITU INAITWA PROFESSIONAL DISPLAY IN NOU CAMP, MADHARA WAMEYAONA LEO....NYANGAU MKUBWA WEE NA UKOME USIRUDIE TENA

    ReplyDelete
  20. BRAZA MISUPU KAMA ULIKUWEPO mwanangu mwenyewe YAANI HAWA MASHETANI WEUSI WAMEJILETA WENYEEEWE HUKO MOSCOW MAANA LAZMA BWAWAZ WATAIBUKA VIDUME

    NAJUA WAPENZI WA MAN U WATADAI KUWA HUWA WANATUFUNGA BUT MIND YOU KWENYE CHAMPIONS LEAGUE WE ARE A DIFFERRENT PROPOSITION MEN!!

    MOSCOW HAKUTAKUA NA MAREFA WANAOHONGWA NA A. FERGUSON KULE NI MPIRA TU SHENZ TAIP...ETI REFA ANAMTOA J. MSCHELANO KWA KUMZONGA MWAMUAZI WAKATI W. ROONEY NDO BINGWA WA KUZOMEA NA KUWAFOKEA MAREFA NA HAJAWAHI KUTOLEWA NA MWAMUZI MWINGEREZA..ANY WAY NGOJA JION TUONDOKE NA MTU PALE DARAJANI AFU 21 MAY 08 TUFANYE MAMBO PALE MOSCOW

    its me SMALL BENITEZ

    ReplyDelete
  21. KUNA WANGA WANADAI ETI CHELSEA HUWA HAWAFUNGWI PALE DARAJANI HIVYO BWAWAZA LEO NI KICHAPO TU..NYIE WOTE MLIO SUPERSTITUOS SIJUI MNAISHI DUNIA GANI ETI MNADAI HISTOORIA INAONYESHA HIVYO..NYIE KENGE KWELI!!

    KAMA NI KUFUATA HISTORIA MBONA HAMUANGALII HISTORIA YA BWAWAZ KUA HAIJAWAHI KUFUNGWA NA TIMU YOYOTE YA UK KATKA CHAMPIONS LEAGUE??? PIA MBONA HAMUANGALII HISTORY INAYOSEMA BWAWAZ MWAKA HUU IMEFUNGA WALAU GOLI MOJA KATIKA KILA KIWANJA KWENYE MECHI ZA CHAMPIONS LEAGUE? KUNA KENGE NYINGINE TULIPOPANGIWA NA INTER MILAN WAKADAI ETI NDO MWISHO WA SAFARI ETI INTER HUWA HAWAFUNGIKI NA WANAONGOZA LIGI YA ITALY..WHAT HAPPENED?? TULIWAPIGA MIBAO HADI WAKASAHAU MLANOGO WA KUOKEA UPO WAPI..TUMBAF KABISA

    its me SMALL BENITEZ

    ReplyDelete
  22. Nahshukuruni wadau wote mlionipongeza mimi na washabiki wa manchester united,kwanza napenda kusema Paul Scholes ndio English Man anayeongoza kufunga magoli in European football what an archievment ameweka record.Kuna mdau aliniuliza ningependa tukutane na nani kwenye final,ukweli ni kwamba yoyote atayepita kati ya Liverpool vs Chelsea mechi itakuwa ngumu bora ungekuta ni Barcelona tunakutana nao final. Chelsea ni timu ambayo mimi binafsi sipendi kukutana nao maana wana match winners wengi sana na they never say die lakini kama wachezaji wetu tisa hawa van,Brown,ferdinand,vidic,evra,scholes,carrick,ronaldo,rooney wakiwa fit lazima tushinde ukiangalia ferguson ana bench kubwa la kuchagua nani wa kumuweka sub: tevez,anderson,Hargreeves,park,saha,Nani,oshea,fletcher wote hao ni class palyers Saha hope fully atakuwa fit maana final unahitaji attacking power.LIVERPOOL hi timu haina record nzuri against manchester lakini on Euorpean nights you can never never predict. Mimi ningependa Final ya Manchester united Vs Liverpool kwajili ya upinzani uliokuwepo na ticket tutapata sawa lakini wakienda chelsea Abromovic atachukuwa tickets nyingi kwahiyo washabiki wa man utd watukuwa wachache ambayo ni mbaya. Hivi mnajua manchester united ndio timu ya kwanza kushinda european cup(siku hizi champions league) 1968 the Busby Babes .Jana men of the match was the all team but Evra,Brown,Ferdinand,Tevez and Park were out standing. kuhusu msimu ujao nadhani mnamjua MANUCHO mchezaji wa Angola aliye sign manchester united yuko Panathaikos anaprogress vizuri ana features za ETO ambazo powerfull,fast and scoring ratio iko bomba lakini sorry Saha has to go in the summer tumlete Eto then team ndio itakuwa kamili. Najua kuna watu watapinga lakini mnajua nani ambaye amefanya tunakaribia kushinda premier league na champions league ? Ni Tevez kumbuka mechi hizi muhimu amabzo tungeshindwa ingekuwa basi
    dakika sio exactly lakini almost
    Man vs Spurs -tevez 90 min
    Man vs Chelea - Tevez 45 mins
    Man vs Liverpool- Tevez 35 mins
    Man vs Lyon - Tevez 88 mins
    Man vs Roma- Tevez 75 Mins
    Man vs Black Burn - Tevez 85 mins

    Kumbuka mechi ya blackburn tungefungwa na chelsea walivyotufunga ingekuwa basi,japo Ronaldo amefunga magoli mengi lakini huyu kijana Tevez ndiye alionesha class kwenye mechi kubwa kama mnavyoona nadhani nimeandika novel hahah, any way jana nimesimama mechi nzima kukaa ilikuwa tabu . COME ON RED DEVILS LET DO THE DOUBLE(Inaniuma ile ya portsmouth maana ingekuw treble)

    Nawatakia kila la kheri washabiki wa liverpool na chelsea mgoane meno haha

    William uk(United for life)

    ReplyDelete
  23. - CECH

    ESSIEN A.COLE

    CARLVALHO TERRY

    MAKELELE

    J.COLE BALACK LAMPARD KALOU

    DROGBA

    Hiki ni kikosi alichotayarisha mwenyewe Maalim Jose Mourinho.
    Maalim kajikata lakini squad bado inatesa. Pangeni yenu Bwawa tuone.

    The special One Mourinho Jr.

    ReplyDelete
  24. haahaahha naona watu wanapenda sana kuosha vinywa kazi kwenu mnaijua LIVERPOOL au mnaisikia acheni kusema sana baada ya matokeo ndio muanze kuosha vinywa maana mnaona chelsea kuna mpira sana au sio mlishasema mara MAN U anatolewa na barca sasa hivi hamna la kusema tena au sio hahaha subiri leo muone liverpool watakavyofanya nyumbani kwenu hahaha haya kazi kwenu.

    ReplyDelete
  25. MAN UNITED OYEE,TUNAWATAKA CHELSEA TULIPIZE KISASI,LIVERPOOL HAWARUKI KWA MAN

    ReplyDelete
  26. Mdau Willim wa UK,
    Nadhani sasa umelewa sifa baada ya kukusifia kwamba huwa unakubali ukweli wa mambo basi ukaamua kutudanganya. umesema Man U ni timu ya kwanza kuchukua ubingwa wa Champions league wakati huo ikiitwa UEFA cup, mimi ni mdau wa Real Madrid na jinsi ninavyofahamu mimi ni kwamba hili kombe lilipoanzishwa 1955 ni kwamba Real Madrid ya akina Alfredo Di Stephano ndo ilikuwa timu ya kwanza kulitwaa, ililitwaa miaka mitano mfululizo bila kupumzika na kulichukua jumla. Sasa inakuwaje tena Man U wawe wa kwanza kulitwaa wakati ni Real Madrid tena sio msimu mmoja, ni misimu mitano mfululizo, ningekuelewa kama ungesema kwa timu za uingereza, lakini kwa vile hukusema hivyo na mimi ni Real Madrid damu na wiki ijayo nitakuwa El Santiago Bernabeu kusherekea ubingwa wa la liga kwa mara ya 31 sikubaliani na wewe hata kidogo, itabidi uje kurekebisha kauli yako na kwa vile huwa unakubali kukosea natumaini nitakusoma tena. kwanza mashindano yameanzisha mwaka 1955 na Real walilitwaa hilo kombe mpaka mwaka 1960 bila kupumzika japokuwa walikuwa wamechoka kutwaa kombe zito kama hilo, lakini vijana wapi, waliendelea tu. na kama unabisha basi bonyeza hapa uone hadithi ipoje http://en.wikipedia.org/wiki/UEFA_Champions_League#Champions_League_finals
    Mkuu siku nyingine uje na habari za uhakika, mie nawashabikia nyie kwa vile sipendi Liverpool watukaribi na mara tisa zetu ni hivyo tu,

    Halla Madrid! Halla Rual!!
    Mdau wa Real Madrid

    ReplyDelete
  27. William Uk leo ana mudomo mureefu, subiri kiama chenu moscow, vijana wa darajani huwa wanafanya kweli wakiamua, na kwa vile chelsea hawajawahi kuchukua champions league naona itakuwa jihadi hiyo moscow. Kuhusu leo hatusemi saana kama nanihii wiliamu, mazungumza baada ya dakika 90 za darajani.

    ReplyDelete
  28. mdau William mie nakufurahia sana leo, hivi huyo Scholes kafunga mabao mangapi ya kumsifia, hivi unajua hii ni champions league? ongelea zaidi ulaya, uingereza kitu gani bwana sisi tuna RAUL na Di Stephano mpaka leo wapo juu! vipi umeshachagua na timu ya kushangilia kwenye Euro, maana jinsi unavyochonga ni lazima utakuwa unashabikia uingereza, maana uingereza kila mmoja ni mwandishi wa habari, kuanzia shabiki, mwokota mpira mpaka wachezaji na kila mmoja ni kocha ndo maana "walipata tiketi mapema ya kwenda kwenye Euro" ya mwaka huu. tehetehetehe!
    Viva campeone Real de Madrid l'équipe de la capitale d'Espagne!
    Halla Madrid! viva Robinho, Casillas, Diarra!

    ReplyDelete
  29. samahani wadau maana yangu manchester united ndio first English club to win the cup it was against Benfica ,sio sio kulewa sifa this is an open dialogue so watu tunaruhusiwa kujadili mambo mbali mbali, if your talking about real madrid thats another issue waache kama walivyo ndiyo maana ni Galacticoz historia yao ni nzuri. sijamdanganya mtu ila it was a typing error "english club" mpo wadau

    William uk(United for Life)

    ReplyDelete
  30. He leo tuna waspanish ile mbaya humu poleni madrid kwa kutolewa na Roma japo sis ndio tulioweza kuwatoa wababe wenu haha,kumbuka we are the best in europe at the moment not england only un beaten in the champions league 2007/2008 na kuna uwezekano wa kushinda ,unasemaje hapo? Bingwa wa france- lyon tumechapa in form team in italy Roma - tumechapa Ambao waliwabugiza nyie madrid,Barcelona well ovyo -tumechapa, NAJUA madrid timu inaundwa sasa hivi na msimu ujao wakimchukua Villa(Valencia) na Hantelar(Ajax) mtakuwa bomba kwa sasa acha wenzenu tujidai kidogo maana last week mlituandama ile mbaya

    William uk(united for life)

    ReplyDelete
  31. William uk,
    sasa umeongea, kurekebisha kauli hiyo ndo ilikuwa muhimu, maana mimi nilishtuka sana maana kama ujuavyo mzee wa timu bora ya karne! pia kama ulivyosema kwamba Chelsea wana match winners, lakini pia Liverpool usiwadharau kwani kama ni match winners hasa fainali wao ndo wana ongoza, wana mtu kama Steve Gerrard ambaye kila mchango wake unapohitajika yupo na unaonekana, unakumbuka kaishindia fainali ngapi Liverpool au ni mara ngapi kaibeba timu toka kufungwa na kuja kushinda, yaani hapo ndo tofauti kubwa inapoonekana kwa mchezaji wenu anayewika sasa hivi CR kwamba haibebi timu inapohitaji ushindi kwa udi na uvumba, na pia nakusifu kwa kuchambua, hasa uliposema safari hii aliyewashindia "kama mtatwaa makombe basi ni Teves", kwani kafunga mabao muhimu wakati ambao mlikuwa mnahitaji ushindi. Tatizo la mashabiki wengi ni kuja kuzungumza bila kuchambua mambo vizuri,
    safi sana William, ngoja nikuulize pia, hivi wewe kabla ya kuja Uk ulisoma Tumaini Iringa?

    Halla Madrid

    ReplyDelete
  32. team sheet ya moscow
    1
    2
    3
    4
    5
    6
    7 CR
    8 PAULI MFUNGAJI
    9
    10
    11
    KUDADEKI WANAOSEMA CR SIYO WA MECHI KUBWA : WILLY KESHAWAAMBIA IT WAS TEAM WORK KUMBUKA TULIKUWA TUNACHEZA NA BARCA MESSI, ETOO NA WENGINE NDANI NA WANAJUA CHENGA KULIKO MTU YEYOTE EUROPE SASA ULITAKA RONALDO ACHEZE KAMA MESSI ALAFU IWEJE? JANA ALIKUWA ANAPIGA ONE TOUCH KULIKUWA HAKUNA ROOM YA CHENGA . MIAKA 22 YA UKOCHA SIYO KITU KIDOGO TULIJUA JANA TUNAHITAJI KUWA FIT 90MIN NDO MAANA SIR ALEX AKA GAMBLE PALE DARAJANI . ULITAKA TUSHINDE DARAJANI HALAFU JANA IWEJE? TUNA MAGOLI LUKUKI NA SAFARI HII TUNA MALIZIA PALE TULIKO ANZIA 1-0 WEST HAM , 0-1 WIGAN KAZI KWISHA . WILLY IWILL C U AT THEATRE OF DREAM.

    ReplyDelete
  33. naona wote wapuuzi wanaoongea ovyo kuhusu ronaldo! anaongoza kwa magoli premier league,champions league na ukija europe golden boot anaongoza yeye(inacombine anayeongoza kwa magoli ligi zote za europe)!! hapo tu tayari ana three golden boots this year! tayari ameshatangazwa PFA player of the year,na na uhakika atachukua pia europe player of the year na WORLD PLAYER OF THE YEAR!!! sasa kuna mchezaji gani anaweza kua na record kama hiyo kwa mwaka mmoja??tehe tehe najua kinawauma kwa sababu hii yote ni wivu,ila kwa yeyote anaejua mpira lazima ataliona hilo..hao ndo RED DEVILS BANA!!!!

    ReplyDelete
  34. oooyyyyeeeeaaahhhhhh...
    guys i have little thing to add to wat u have being saying, real very little. bt first am MAN U......, that is "off the pressure club" to be fun off ofcourse, i believe u all know... then guys, i real feel that u bwawa la maini and u guys of the bridge HAMNA SHUKRANI KABISA..... MNASHINDWA HATA KUTOA HONGERA KWA MAN U KWA KUWEZESHA KIKOMBE KUBAKI HOME?????
    PLEASE GUYS SHOWS A LITTLE BIT OF CONCERNS PLEASEEEEEE

    ReplyDelete
  35. will kuongeza kwenye kitabu chako naomba uongeze kwamba: umefika wakati wakurudisha heshima ya hiki kikombe manake kilipoteza maana kwa kama miaka tano iliyopita kimekuwa kikichukuliwa na watu ambao siyo mabingwa nchini kwao. wakati ni champions league angalia timu zilizo izunguka manuu wote wanastrugle kwenye ligi zao.

    BREAKIN NEEEEEEEEWS
    kudadeki drogba keshamaliza watu. waje waje tunawasubiri red square.

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 01, 2008

    Mdau wa Madrid hapana mimi nimesoma university dar then ndio nikaja huku ,then ntarudi bongo muda si mrefu,Duh mechi ilikuwa nzuri kwa kweli ya liverpool vs chelsea . Drogba ,Lampard ni top class huyu mtu nimekubali. kama nilivyowaambia kabla champions league mimi binafsi nahisi kama Man utd tunalikosa lakini Ferguson leo alikuwa uwanjani anaangalia mechi ,jamani itakuwa shughuli haya tuombe mungu


    William uk(united for life)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...