Kamati ya Zenjydar Community Association imekutana na Mhe. balozi wa Tanzania nchini United Kingdom, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar leo hii ubalozini mjini London.

Pichani kutoka kulia Bw. Farid Ahmed Said (katibu wa Zenjydar), Bw. Saleh Jaber (mwenyekiti wa Zenjydar), Mhe. balozi Mwanaidi Maajar, Bw. Mrisho Senga (muweka hazina Zenjydar), Bi. Sofia Issa (elimu ya jamii kwa watoto na wanawake Zenjydar) na Mhe. Athman Mashanga (mkuu wa elimu na utamaduni Tanzania High Commission).


habari zaidi nenda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Duh sasa hii jumuiya inawakilisha nani? Dah Naona Farid umo kwenye jumuiya.Mwenzangu nakukumbuka tulipokuwa Shangani tukisota, kwa Rahma Taarab, Tiptip nk. Nakufagilia mwenzangu.Majuu kumekufaa.

    ReplyDelete
  2. huyu saleh jabir ndie msanii wa kwanza kuimba bongo flava kama mnamkumbuka,ice ice baby

    ReplyDelete
  3. wenye jumuiya kumbukeni kusaidia Tanzania kwa vitu mbali mbali hasa elimu. pia wazanzibar acheni ubaguzi sisi wote ni viumbe wa Mwenyezi Mungu tusiwabague wabara.

    MAMA MAAJAR WEWE KIBOKO SANA UTAFIKIRI ULIKULIA KWENYE DIPLOMATIC umewafanya wapemba waingie Ubalozini na wao walikuwa wanaona ni kituo cha polisi au HOME OFFICE.

    Mwanaidi umewafunika mabalozi wote wa ulaya na marekani.

    umedhihirisha kuwa Wanawake wanaweza.

    Balozi KIBELLOH alishindwa kufanya haya unayafanya.alikuwa kazi yake kuongopa tu hakutani na waTZ wala nini.

    JK mtunze huyu mama ni makini sana ukweli lazima usemwe.

    najua tarehe 17 april umeeandaa Tanzania Diaspora kitu ambacho hakijawahi kutokea.

    mama unapatika ofisini bila AHADI wala mizengwe. unapokea mobile yako bila matatizo.

    JK alikiibua kipaji hiki wapi?
    najua wako wanaoumia wache waumie na wajinyonge.

    WATASEMA LAKINI UKWELI UKO HAPO HAPO MAMA UMEJICHANGANYA FAHARI KWA WATANZANIA.

    ReplyDelete
  4. Saleh Jabeer NDIO MUASISI WA NYIMBO HIZI ZA KIZAZI KIPYA. TUNGEKUWA NA COPYRIGHT HUYU JAAMA NI TAJIRI.

    NASHANGAA KINA MR.SUGU WANAJIFANYA NDIO WAASISI. NAKUMBUKA KIBAO CHAKE CHA KWANZA 1991 ALIKUWA NA MAREHEMU BLACK MOSES. MZEE MICHUZI UTAKUWA UNAKUMBUKA SANA.

    JEE WAKATI HUO MR.TWO(SUGU) ALIKUWA HAJAINGIA HATA DAR.MR TWO ACHA KUDANGANYA WATU HISTORIA TUNAYO.

    ReplyDelete
  5. sasa huyo wa pili kulia ndo nini kuvaa white shoes?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...