Killuvya Pub, baada ya kuwachengua Wapenzi wake kwa Burudani ya Nguvu ya mwaka Mpya 2008, mara hii inakuletea Burudani ya aina yake.

Huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Miaka ya 1960 na 1980 kumekuwepo Wanamuziki Magwiji wawili waliotamba sana Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati.
Hao ni Luambo Lwanzo Makiadi (Franco) na TPOK Jazz na Tabu Ley Rochereau na Afrisa International.

Katika kuwakumbuka na kuwaenzi Wanamuziki hawa, Kiluvya Pub inaandaa Tamasha kwa Wapenzi kumtafuta Nani zaidi kati yao. Historia za Wanamuziki hawa zimeandaliwa na Miziki yao iliyotamba pia imeshakusanywa.

Wapenzi wa Burudani Kaeni Mkao wa kula ili mtakapojulishwa tarehe ya kuanza Mpambano huo usikose kushiriki. Tembelea Globu hii kila wakati upate taarifa kamili.

Mkurugenzi.
NACHUKUA NAFASI HII KUMPONGEZA MKURUGENZI WA KILUVYA PUB KWA HATUA HII YA KIMAENDELEO YA KUZINDUA GLOBU KWA AJILI YA WADAU WAKO. HII INAONESHA KWAMBA TARATIBU TEKNOHAMA INAINGIA NDANI YA DAMU ZA WABONGO NA ITAKUWA RAHA ZAIDI KILA FANI IKAFUNGUA YAKE. KWA HABARI ZAIDI ZA PUB HIYO BOFYA HAPO CHINI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2008

    "...on the road to Morogoro?"

    Sidhani kama ni kiingereza fasaha hicho.

    Ilipaswa kuwa
    "...on the WAY to Morogoro"

    Halafu angeweka na GUEST ndo atapata wateja wengi.
    Pia PARKING yake FINYU SANA!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2008

    SAFI SANA! KILUVYA PUB BADO HAIJAFA!!!!!

    NAKUMBUKA MIAKA YA 2003, 2004 KULIKUWA NA BURUDANI YA NGUVU YA MUZIKI KILA IJUMAA JIONI. NI BAA YA WATU WASTAARABU WA MAENEO HAYA, (KWA MZEE KAWAWA).

    NAWAKUMBUKA TU WACHACHE - MZEE KIMORI, MZEE MWAKIPESILE, MWALIMU JUMA HAMAD NCHIMBI, NA WENGINE N.K.

    NITATEMBELEA SI UDA MREFU UJAO. WANA NYAMA CHOMA NZURI, SUPU, NK. NA VINYWAJI KIBAO.

    Mdau wa USA

    Mr. Mwipopo, M
    Mwalimu- Kiluvya Sec.- zamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...