mdau bernard rwebangira katuletea hii picha kuonesha sehmu ya kisiwa cha pemba ambacho kwa jinsi kilivyojaaliwa rutuba unaweza kusema uko tukuyu ama bukoba. bofya jina la bernard utembelee globu yake ambayo imesheheni picha za matukio mbalimbali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2008

    Nani kasema Pemba kuzuri??

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2008

    sasa wewe huoni mazao yalivyo stawi ama unataka leta ubishi wako wakipemba?wewe wa may 24,2008,5:10 pm

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2008

    http://www.blogger.com/comment.g?blogID=16511139&postID=4460294635474807970&isPopup=true
    Post a Comment Ndio Pemba, kuzuri tena kwa daladala hizo hata kama huna pesa unapanda bure tu, makonda hawana noma wa nini, ila ukiongea nao lazima utumie lafidhi ya kipemba, ukiongea kiunguja tu, umekwisha, bora achukuliwe samaki kuliko kumchukua muungua asiyekuwa na pesa

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2008

    Uzuri hauko isipokua Ardhi ya Pemba ni nzuri na Mungu ameijaalia rutba na hichi ndicho kinachofanya wapemba kuendelea kupata kijio chao. Kwani ukizungumza uzuri unamainisha mjumuiko wa mambo mbali mbali kama: maisha rahisi na nafuu, kuwepo na umeme, maji,barabara, mashuleni kuwe na walimu, vitabu, vya kutosha, kuwepo na ajira kwa vijana lakini leo watu wote wanaondoka na kutafuta maisha sehemu nyengine huo ni uzuri.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2008

    Nakubaliana nawe anon wa may 25, 1:29.Mji mzima unanukiaaaaa saubuhi ukifungua dirisha unasikia harufu nzuri nzuri za maua, Bado pako natural na ardhi yake inakubali kila kitu mf. shelisheli, fenesi migomba ya kila aina kuna ndizi moja tu mnaweza kula mlo wa watu wawili(mkono wa tembo),shokshoki, fursadi mabungo, nazi asili ambazo utazibahatisha ukerewe mzee ruksa alipopeleka mbegu huko maana kunafanana ardh matofaa/apples,viungo/spices na maua ya kila aina ambayo ni asilia waridi, asmini, langilangi,mikadi,na mkilua,bado wajuwaji hawajayapandikiza burding zao na kuharibu harufu nzuri, na kuweka muonekano wa uwa uwe mzuri lakini harufu hamna, sipendi kweli hayo mambo ya kupandikiza, baadhi havitakiwi wanapoteza uhalisi na kuweka mageuzi ambayo baadae huleta madhara/mabadiliko,kwa mmea wenyewe.Wana fukwe nzuri asilia Ila mahitaji ya muhimu mf elimu na vitendea kazi vya kuendeleza wakaazi wao bado adimu sana.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2008

    NINI MKONOWATEMBO WA PEMBA, WA KWETU TUKUYU NDIZI MOJA NI MLO WA WATU WAZIMA WANNE, NA SHINA MOJA HUZAA NDIZI NNE AU TANO ZIKIZIDI HAPO SHINA HUVUNJIKA KWA UZITO WA NDIZI TEMBEA UONE.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2008

    ndio pemba yetu yakheeeeeee


    amina yusuf

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2008

    Anon 26 may 11:58 wahenga walisema kusikia si kuona, nimeyapenda maongezi yenu ya maajabu ya ukubwa wa ndizi moja inayoliwa na watu wawili mpaka wanne naomba munifundishe utaalamu gani unaofanyika mpaka upate ubora huo wa ndizi nimetamani sana nami nataka niboreshe ndizi zangu tafadhali.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 27, 2008

    WEWE 3:35PM NDIYO MAANA UMEAMBIWA TEMBEA UONE, HAPA SI UTAALAMU WA MAPISHI BALI NI UKUBWA WA NDIZI YENYEWE NDIO SABABU IKAITWA MKONOWATEMBO IKIFANANISHWA NA MKONGA WA TEMBO ( IVORY ). KAMA NI MSOMAJI MZURI UNGEELEWA MARA MOJA KUTOKANA NA NENO KUWA ZIKIWA ZAIDI YA TANO KWENYE MKUNGU BASI MGOMBA HUKATIKA.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 28, 2008

    anon 27, 7:37. asante kwa ufafanuzi, naelewa kuwa kinachoongelewa ni ukubwa wa ndizi ndo maana nikatamani nisaidiwe utaalamu wa kuboresha ndizi zangu hizo mkono wa tembo ninazo bali hazitoki vizuri kama kule nilikozitoa au kama nilivyosoma maelezo ya hao ndugu zangu hapo juu. ninachoomba maelekezo tangu kuipanda na kuikuza hadi kuivuna tafadhali.kuhusu kuipika ikiwa mbivu kwa nazi na hiliki, kukaanga,kuchoma, hivyo havinipi shida.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...