THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

khadija kopa na mai hazzbendi wake wameremeta

Kaka Michuzi,
Yaani mimi nampongeza saaana Bi. Khadija! Mbona mijibaba kila siku inaoa watoto waduuuchu hamsemi???
Mwacheni atese na Dogo...LoL
Mdau Lilly


Kuna Maoni 53 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  Ingekuwa kachukua mume wa mtu ama anatembea na mwanamume tuu kwa ajili ya starehe zake binafsi, hapo kweli waosha vinywa mgepata pahala pa kuoshea!! Lakini huyu Bi mkubwa kaolewa (Halali kabsaaaa!!) - sasa midomo ya nini? Hivi vinywa vinaosha namaji yeyote tuu!!!. Hongera Khadija na wengine wafuate mfano wako, na si wafanye uharamia wa kuchukua na kuchuna hao "toy boys" (dRU)

 2. Anonymous Anasema:

  TOBA!!! HARUSI YA LINI HII? AU UMELETA PICHA ZA MWAKA 2004 WEWE LILY!!! NDOA YA 5????

  LAKINI HONGERA DADA KULIKO KUZINI, NA ZAIDI MWEZI MTUKUFU HUU SHURTI UWE MSAFI. UMEPENDEZA SANA SHOSTI!!!!

 3. Anonymous Anasema:

  YULE MWANAMUZIKI ALIYEPATA AJILI YA NDEGE WA HUKO USA ANAITWA ALLYIAH ALIIMBA "AGE ANT'NOTHING BUT NUMBER" MAANA YAKE NI NINI TENA WADAU??? SIJUI MANENO YAKE KWA UNDANI

 4. Anonymous Anasema:

  Hongereni sana la muhimu mapenzi hayo mengine hayana msingi.

 5. Anonymous Anasema:

  Yupo ndani ya maadili ya dini yake atakayechukia ajinyonge.

 6. Anonymous Anasema:

  Loh! Yahitaji Moyo, asante mdau Lily

 7. Anonymous Anasema:

  Loh! Yahitaji Moyo, asante mdau Lily

 8. Anonymous Anasema:

  Nilikuwa naipenda sana couple yao na Othman Sudi... lakini ndo hivyo. Hongera Khadija mwana wa Kopa... Unaelijua Jiji ipasavyo.

 9. Anonymous Anasema:

  Kijungu cha ngapi?

 10. Critic Anasema:

  Nothing to say, other than ... IT IS CHILD ABUSE !!! Lol !!!

 11. Anonymous Anasema:

  Duuuuu ila kajamaa katafaidii hiyo mimacho ikiremburiwa. Lakini mbona ni kama mwanae?? Jamani umri huu na wa yule marehemu mwanae si ni sawa?

 12. Anonymous Anasema:

  umefanya jambo la maana na huu mwezi mtukufu. umpikie mmeo futari, ila halahala na mdomo wako usije ukamsasambula maana mazoea yanatabu.

  je huyo umempola nani?? fanya mazoezi upungue kidogo usije ukampa kibiongo mtoto wa watu au nae kakomaa??

  mmependeza sana na hongera yenu

 13. Anonymous Anasema:

  Mhh!!nini??Hadija kopa kaolewa?basi hata mimi nitapata mchumba wangu,,,na miaka yangu 39..sasa huyo kijana kafuata ATM au ni nini jamani?Hongera sana hadija kwa kukamata kijana wako mtoto wako..mdau Norway

 14. Anonymous Anasema:

  Mimi kwa ujuml simpongezi hata toneee
  yaan jimama lote hilo linaolewa na mwanae loooo

  kashindikana huyu mama wamipasho

  ona picha ya kwanza eti nayeye anaona aibu, aibu gani nawakati kataka mwenyewe kuolewa na mwanae

  Ingekuwa mie nibora nikae bila kuolewa loooooooooohuoni hata aibu.

  Mdau Manyoni

 15. Anonymous Anasema:

  Makubwa haya.

 16. Anonymous Anasema:

  this is gud news!!
  Wala mbona kijana sura imekomaa nadhani sio dogo itakuwa wana lingana bwana au mamaaaa ana baby face... ila couple imetulia hii.
  big up kwa wana ndoa
  Dada Lao

 17. Anonymous Anasema:

  Lilly jamaa ni mdogo kimwili au nini ? Maanake jamaa huyo kazaliwa 1960 na khadija kopa kazaliwa 1961.

 18. Anonymous Anasema:

  WOW,
  Mimi wasiwasi wangu mkubwa ni je huyu dogo atalifikisha hili jimama
  kwenye safari ya kutwaa kombe la dunia na kusherekea kwa pamoja kwenye kilele juu ya mlimani kilimanjro au ataishia kuninginia ninginia tu...!!!!!
  Mdau,
  USA.

 19. Anonymous Anasema:

  Dogo atafaidi masongi kitandani lakini aangalie asije kutembelea mkongojo siku za zake.

 20. Anonymous Anasema:

  Ongereni maharusi hacheni wivu wabongo jamani hasa akina mama km hujapata subiri na muombe mungu,kuna kipimo gani cha kusema huyu bwana ni mtoto wakati mtu mzima??au kwasababu huyu kopa kajazia ulizeni umri wao kabla ya longolongo zenu mjue wivu unauwa hamjui wametoana wapi.

 21. Anonymous Anasema:

  JAMANI HAYA MAMBO YA AKINA MAMA KUOLEWA/KUTOKA NJE NA (VIJANA WADOGO) HAYAJAANZIA KWA HADIJA KOPA..HUKU NCHI ZA WATU TUNAWAKIMBIA AKINA MAMA KABILA HII NA SASA HIVI WANAJUA KUJITUNZA NA WANA MAUMBO MAZURI SIO KAMA HADIJA KOPA NA (SURA NZITO).(HILI WIMBI LINAKUJA KWANGUVU SANA)

 22. Anonymous Anasema:

  Suali linalokuja hapa hapa ni je dogo atahitaji kupata watoto?. Kama hana haja ya watoto poa ila kama nia kupata familia yaani watoto ajihesabu maumivu. Biologically menopouse start at the age of 45 for women. Otherwise wamefanya jambo la busara kuoana badala ya kuzini. Ila Jamaa namsifu kwa kweli ana roho ngumu. Yupo kama kandege tunduni vile

 23. Anonymous Anasema:

  Haya mambo ya kuchaguliwa rangi ya mashati na akina ma-bibi harusi halafu sisi akina baba tunakubali mara nyingi yanaishia kwenye kuchemka. Ona saha huyu bwana harusi kavaa shati kumechisha na rangi ya ukuta... Tusikubali kila tunachoambiwa wanaume wenzangu. We jiulize, ukimwambia bi harusi avae gauni la zambarau siku ya harusi just because wewe bwana harusi wazipenda zambarau unafikiria atakubali? Wake up guys!!!!!!!!

 24. Anonymous Anasema:

  OK, bora maisha!!!
  Q niseme nini hapa mie!!, nina kiu
  lakini lakini mmmh.Haya, nawatakieni ndoa yenye kheri na baraka.


  Q

 25. Anonymous Anasema:

  kumbe cougar imeshaingia bongo. That is nice....

  Sioni wanachokiona kibaya hapo kwani wazee wakioa vibaby mbona midomo haifunguliwi?

 26. Anonymous Anasema:

  Dogo chunga uti wa mgongo manake kilima kirefu hicho, kutundika bendera hapo sio mchezo.

 27. Anonymous Anasema:

  hivi jamani yule mume wako bwana othman waliachana lini mbona sikusikia jamani yule mtunzi wake wa siku nyingi

 28. Anonymous Anasema:

  Haluuuu!!!! mambo ya ving"asti yahoooo huku Huston tunaita ADUDUUU!!!! kula raha mama maisha umeyapatia kalee katoto kako!

 29. Anonymous Anasema:

  Haloooo!!
  Mama Mipasho umeopoaaa? Eeeh hatari ila salama hongera shosti kwa kujipatia pumziko la roho. Naona jimbo lako la NIMEMRIDHI MWENYEWE ndo wakati wake huooo, kukuruka mtu mzimaaaa!!

  Huyo mjamaa wala si KISERENGETI BOY, hamuoni Sura ilivyomshupaa nae?

  Kazi kwenu waosha vinywa!!

 30. Anonymous Anasema:

  NYIE WABEBA MABOX HADIJA KOPA ATAWATUNGIA TAAHARABU AMABAYO HAIJAWAHI KUTOKEA ACHENI KUMSIMANGA..HALAFU HUYO KIJANA WALA SIO MDOGO NI MWEMBAMBA..WAKO KARIBIA UMRI SAWA...MBONA KUNA WAZUNGU WAZEE WA MIAKA 65 WANAOWA WANAWAKE WA KIAFRICA WENYE UMRI WA MIAKA 25?MIE HAPO SIONI CHA AJABU HATA KIDOGO...UMRI MZURI WA KUISHI KWA SASA NI KUANZIA MIAKA 45-70

 31. Anonymous Anasema:

  wadau mimi naweza kulala na huyu Maza one night stand ila vya kuoana lazima aniogeshe VX na RAV4 na kila siku niwe na hela ya kuhudhuria bar niwe narudi home niko tingas everyday.
  Na asiniletee kiherehere eti lazima tuende kila mahali tukiwa tumeshikana mikono,hiyo ni big NO.Siku nikitoka naye tunaenda mbali sana viwanja sijulikani kabisa

 32. Anonymous Anasema:

  DU WANAMEREMETA KWELI AAAAH! NGOJA NIWAIMBIE WIMBO... Akanana akana........., wana meremeta wanamere......,

  mmmmmh! Natamani nichangie lakini mdomo mzito, inatosha kuwapongeza kwa wimbi tu.

 33. Anonymous Anasema:

  Mdau wa Manyoni hizo si aibu ndugu yangu, hapo keshajikorogea uji wake wa kungu kaunuiziaaaaa atakavyo, ndo matokeo yake hapo kalewa ndugu yangu humuoni hiyo picha ya pili jicho limekuwa zitoooo pamoja na kuwa macho yake ya kuwa anamacho ya kurembua ila ile khabar lazima ameweka (kungu)uliza uambiwe. wanawake wa pwani wanaelewa khabari hizo,ili bi harusi asitie aibu kwa kuhashukwa na kupepeta mimacho kila upande mila zetu nyingi zinafunza hivyo bi harusi ainame chini , we tangu lini kopa akatulizana kama maji ya mtungini, hapo hajiwezi ndo mana kataadab nanna hiyo.

  Mmependeza malkia wa mipasho yote maisha. kuolewa ni jambo la kheri ni vema kuwa na mme wako kuliko kuokoteza okoteza mwisho uje ushikwe ugoni bure,

 34. Anonymous Anasema:

  Wivu kidonda jamani,mbona bi Kopa kafuata suna ya mtume-kuoa au kuolewa nadogo sio kosa.Kikubwa bora mapenzi na isitoshe haanzi yeye

 35. NARUBUMENYE Anasema:

  jamani na BI ZAI kungwi wetu katokea wapi tena?upo juu bi ZAI.Wa waaa.hongereni

 36. Anonymous Anasema:

  WANA MEREMETA SI UTANI!!ata kama..
  HADIJA KOPA V/S MIRIAM MAKEBA
  HOngera Taarabu Queen-AU MAlikia wa MIPASHO! kwa Kupata Mume wa NNE,Mtoto wa kiisilamu kuolewa muhimu,Miriam makeba Au MAMA AFRICA! Mwenzio ana mume wa SABA,Malikia wa MIPASHO mkiachana mume unatabia ya KUMSASAMBUA V/s Mama Afrika anatunza Heshima ndiyo maana aliyekuwa Mume wake Hugh Masekela ana msaidia akikwama kifedha .Malikia wa Mipasho Grammy Awards (tunzu) 2 v/s Mama afrika nyingi tena za kimataifa.Hadija kopa Nakutakia kila la kheri jitahidi utukwamua kimuziki.

 37. Anonymous Anasema:

  Bi Khadija anakwambia kabisaa...... "Ni chaguo langu nimemchagua yumo yoni mwaaangu.....sitaki mafumbo " Nanyi hapa mwakaa kumpa mafumbo sijui yumzee sijui yumnene. Ah binadamu tuna mambo.......Michuzi umebana comment yangu

 38. Anonymous Anasema:

  Bi Khadija umethibitisha usemi aliowahi kusema mwl. mkuu wa Mlimani Shule ya msingi Pendo Kujerwa kwamba "Mtoto wa mwingine mkubwa mwenzio, ukicheza......", wadau malizieni hiyo

 39. Anonymous Anasema:

  Khadija acha kuonea watoto wa watu sivyo hivyo shosti utauwa dada. Mdau Hollanda

 40. Anonymous Anasema:

  Jamani tuleteeni picha za chiken party pia, sio za harusi tu. Chondechoonde tunaziomba sana tuone huyo mwanamwari alivyofundwa.

 41. Anonymous Anasema:

  Kaka Michu
  Wallah mimate iminitoka, ninatumia fursa hii kumpa hongera dogo na Kopa na vile vile ninatumia nafasi hii kutangaza kutoa drooo!! ninaomba unifikishie salaam zangu za ushenga (wewe) kwa Bi Kidude. Umri wangu kama wako kakaangu!! Hakika mapenzi hayana mipaka nitafurahi kusikia jibu la ushenga huu kwa Bi Kidude. Asiwe na hofu kwani hata mimi ninavuta sigara kwa jaaaamu!! (dRU)

 42. Anonymous Anasema:

  Huyo jamaa anafana na baba yake na Lewis Hamiliton duniani wawili wawili kweli

 43. Anonymous Anasema:

  Mdau wa Holland umesema kweli maana da Khadija ni vizuri aachie frii staili, lakini akileta zile za kata na kufunua atauwa kweli mtoto watu na wakikufungukia mada usiseme hukuuwa kwa kukusudia. Mademe

 44. Anonymous Anasema:

  Hongera bi Khadija maana naona umefuata suna ya wajina je na mahali umetoa mwenyewe? mmependeza sana, basi hebu jitahidi huyo awe wa kufa na kuzikana, maana hesabu inazidi mpenzi.Coolmammy.

 45. Anonymous Anasema:

  Duuuuuuuuuuuuuuuu nikubali Khadija hiyo kweli mada mweeeeeeeeeeee!!.

 46. Anonymous Anasema:

  Da Hadija kumbe mliachana mtoto wa bi dedi, yule mlipendeza sana tena, na huyu ata haiji, kama wanavyo sema wadau wenzangu unamuonea bwana, hadija acha izo sivyo mamalikia hawawi hivyo, wanakuwa na huruma kwa watoto. mwana Ilala.

 47. Anonymous Anasema:

  Njaa, Njaa, Njaa, bwana mdogo hana dili kaamua kujichukulia bibi la Mipasho. Sura nzito kama nini.
  Brother umechemsha kwani ungeweza kuwa unajipigia kwa pembeni na kuvuta kidogodogo kuliko kubeba jizee mojakwamoja.
  Inahitaji moyo lakini kuivalia njaa kibwebwe.
  Labda huyo bibi kizee kwako wewe ni Whitney Houston.
  Huna dili bwana mdogo tafuta maisha ya kweli.

 48. Anonymous Anasema:

  HIVI NYIE MBONA HAMPENDI KUJUA UKWELI HALIsI WA HABARI? Kwanini msimuombe michuzi hawatafutie umri wao.
  Habari za huakika ni kwamba huyo jamaa kamzidi khadija kopa ki umri kwa mwaka mmoja sasa sijui mnapiga domo kwanini.

 49. Anonymous Anasema:

  Anonymous wa 8.14 we nani kakwambia umri wao, ka si umbea. watu wengine bwana!!!

  Halafu siku nyingine kabla ya kutuma comment preview kwanza, sio HABARI ZA HUAKIKA ni "HABARI ZA UHAKIKA.
  Watu hawapigi domo ka unavyosema, wanatoa hisia zao, sasa sijui wewe inakuuma nini.Hayakuhusu kabisa.

 50. Anonymous Anasema:

  Wanameremeta ndiyo mara milion ..
  Namshukuru mdau aliyeandika Malikia wa Mipasho v/s Mama Africa, nimefuatilia maisha ya kina Mama hawa yametaka kufanana.Swali kaka Michuzi na wale wanaofahamu english:*Nimesoma aliyekuwa Mume wa Miriam Makeba ni LIFE HUSBAND Hugh Maselela,* Nani LIFE HUSBAND wa Hadija kopa?Nini maana ya LIFE HUSBAND/WIFE Mtu mwenye sifa gani anapewa cheo hicho????

 51. Anonymous Anasema:

  watanzania acheni tabia ya majungu na kashfa ndio maana hatuna maendeleo. kuweni kama mmekwenda shule.hakuna haja ya kupiga maneno machafu na kashfa bi khadija kopa. kila mtu ana choice yake kimaisha. we only live once.let her enjoy her life while she is still alive.hongera mama. u look faboulous na ur hubby wako. wish u fantastic life and happiness

 52. Anonymous Anasema:

  Punguzeni hasira hii ni Blog ya Jamii,ya kuelimisha,Mimi ktk kufuatilia habari ya mdau,Malikia wa Kupishana V/s Mama Afrikana ktk Miriam Makeba-Weekpedia encyclopedia.Nimekuta neno hilo Life husband Mtu ambaye aliachana naye!!ina maana Mke/mume aliyeolewa mara nyingi kuna hilo?? kama hicho ni cheo nani? anakitoa Mwolewaji au Mwandishi wa habari???

 53. Anonymous Anasema:

  Mdau,uliyeuliza swali?jibi huyo hugh masekela ameitwa Life husband nafikiri kwasababu Mama afrika alimlipia nauli kwenda U.S.A kwenda kumwoa.life husband wa malikia wa Mipasho Soma www.khadija kopa-week peia utaona mtoto wa bi dedi anaitwa .....kwani Dogo ni kwaajili ya mwezi mtukufu.