Bwana Michuzi,
Mimi Nimefurahi sana Kuiona hii blog yako, kwani kweli ni ya maendeleo.
Kuongelea maendele napenda niwataarifu Watanzania kuwa Wachina sasa wako tayari kununua mali kamili kutoka Africa.
Mali kamili namaanisha bidhaa ambazo zimetengenezwa na ziko tayari kutumika (Finished products). Miaka yote wamekuwa wakitaka tuwapatie bidhaa wazitengeneza (Yani RAW materials).

Nawasihi sana Watanzania wanotaka kujaribu biashara ya kuuza bidhaa zao China waangalie website hii
www.cantonfair.com
Hapa watapata maelezo yote ya jinsi ya kuingia na kuonesha bidhaa zao katika China Import Export Fair.

Hizo Picha ni mwaka huu mimi kwa niaba ya Multimodal nilishirika katika Maonesho hayo, kweli mafanikio ni makubwa.

Mwaka huu Kutoka East Africa Tulikuwa sisi wenyewe lakini kwa msaada wako bwana Michuzi nadhani watanzania wengi zaidi watanufaika mwaka kesho na miaka ijayo

Nakushukuru,

FREDDY MLAY
Branch Manager.
Multimodal Sourcing and Logistics Company LTD.
Guang yuan xi road,
Xiushan building 4th floor Room 4021.
TEL:+86 20 86508207
FAX:+86 20 86507207
CEL:+86 132 42807212 (8:00AM - 10:00PM CHINA TIME)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

 1. Yakhe sisi wabongo hatuna chochote cha maana kuwauzia hao wachina...labda bidha pekee tuliyonayo ni hao watoro wakimbizi yaani wabeba maboksi waliyodoea kule marekani na ulaya,wapelekwe kula uchina na wafundishwe kilimo bora!!!

  ReplyDelete
 2. Anon wa 7:20 una chuki binafsi unanikumbusha hadithi za sungura nilizoma soma darasa la pili Sizitaki Mbichi Hizi. Ni kweli maisha ya Ulaya ni magumu inabidi kufanya kazi kubwa kufanikiwa. Kazi nyingi zinakuwa ni za kima cha chini. Wenzetu walioanza kuja miaka ya zamani mfano west africans au hata Kenya wanakuwa wako ok kidogo. Tanzania yetu passport zimeanza tu kutolewa miaka ya karibuni kwahiyo unakuwa sisi ndio tulikuwa wa kwanza hapa unafika huna pa kuanzia
  Nyumbani nako maisha ni magumu watu wanavyeti vyao lakini ajira hakuna na mara nyingi ni kwa mwendo wa kujuana. Inasikitisha unategemea wazazi mpaka kukuozesha, mitaji ya bishara na kila kitu. Maboksi inakuwaga ni process ukifika huku hakuna office inakusubiri. Kibaya tu mahali kama huku ni ubaguzi na kuwa ugenini lakini maisha ni mazuri. Nimefanya kazi na wachina wawili katika sehemu tofauti na sio watu. Na wenyewe wanaubaguzi wao na watajipendekeza kwa mzungu. Kuna pride katika nchi yao hivyo huwa wanajiona. Wakikufuata ni kwasababu wanataka kitu.

  ReplyDelete
 3. Namna hivi ndio watu wanatakiwa kupigana tafu sio kumwagiana mitusi na midharau tu. Kidogo kidogo tutafika, wakati umebadilika, na akili za watanzania zinazidi kuielewa dunia.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...