Home
Unlabelled
mhandisi makini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Tehe teh tee!
ReplyDeleteBwana Kaijage si useme tu umetaka tu droo atenshen yetu kwenye hizo gramatiko eraz hapo?
Eti Construction ARE CONTINUES.
Tehe teh tee!
khekhe that s a good one construction are continues.halafu unategemea majengo yasidondoke
ReplyDeletekwanza kingera bomu lakini hata angekua kapatia watu wangapi wanaopita na kufanya shughuli zao hapo wanaojua kingereza
ReplyDeletekweli makini maana hicho kiinglish kimeenda shule naona ni kiinglish toleo jipya!
ReplyDeleteWadau mmeliona hilo tangazo nanukuu "Construction are continues" !!!! hicho ni kiingereza au kiswaEnglish ????? Kosa liko wapi hapo WADAU ????
ReplyDeleteKiingereza kwa hapa kwetu jamani ni Janga la kitaifa. Linafuata baada ya ukimwi!!
ReplyDeleteHuyo mwandisi lazima atakuwa mrusi ay mchina. Vinginevyo kama mtanzania degree yake kainyakia Urusi au china! English not beepable!
ReplyDeleteKaka, hao wachina tu kama sio wahindi.
ReplyDeleteNI kweli kabisa,
ReplyDeleteMtu makini huyu. Construction are continues!!
"Construction are continues"....kama gramma haijatulia ujenzi inakuaje?
ReplyDeleteTUSHACHOSWA NA HAWA WAHANDISI FEKI(CJUI MAKANDARASI)VYOVYOTE VILE WANABOA KWANI WANAANGALIA MASLAHI YAO BILA KUJALI UZIMA WA WATUMIAJI AMA HATA NDUGU ZAO KWANI HATA WAO PIA NI WAATHIRIKA WAKUBWA SANA WA HILO.
ReplyDeleteBONGO NCHI IMEJAA USANII KTK ELIMU YA UHANDISI WATU WANAFOJI VYETI KWENDA MBELE YAANI FULL USANII CJUI LINI TUTABADILIKA!
NADHANI IFIKIE MAHALI HUKUMU YA KOSA LA MKANDARASI AU MHANDISI ATAYESABABISHA MAAFA YA VIFO AHUKUMIWE KIFO ILI IWEPO WARNING SIGN,NA NDIO MAANA HAWATAKI MAHAKAMA YA KADHI SABABAU WANAJUA KUNA MIJIHUKUMU YA VIFO PIA HATA UNAWEZA MHANDISI WAKAKU........XXX SABABU YA VIJI asilimia 10 TU VITAWAPELEKA AHELA SHNZZZZ ZENU.
HEBU MJICHUNGUZE JE MAJENGO MNAYOYASIMAMIA YANA UBORA SAWA NA NYUMBA MNAZOISHI? KAMA SIO TUNAANZISHA VITA NCHINI NANYINYI WASHNZZZZZZ SANA.
TUTAANZA NYUMBA KWA NYUMBA NDO LAZIMA TUPATE SULUHISHO. NAWE WAZIRI WA UJENZI KAMA SI MIJENGO FEKI NA UFISADI KIDOGO KOMAA NA HEAD KTK HILI UTAUMBUKA CHEO MAANA BWANA MKUBWA JK ANATISHA SIKU HZ NI INGIZA TOA KTK BARAZA LA MAWAZIRI,HONGERA KWAKE PIA HONGERA MISSUPU KWA BLOG YA JAMII.
NI MIMI MZEE WA UK,MASTER P INGAWA NIMEJIANONYMOUS
hee jamani lugha inatushinda, "construction are continues" wakipita wageni sii aibu!
ReplyDeletemhandisi makini kweli CONSTRUCTION ARE CONTINUES. makini my @@@@
ReplyDeleteNAKATAA,KATAKATA,HILO BANGO HALIJAANDIKWA NA MHANDISI BALI LIMEANDIKWA NA MWANDISHI.....OTHERWISE CRUSH PROGRAMS SHOULD COMMENCE VERY SOON...BUT SORRY,IT IZ TOO LATE,SO WHT TO DO????ALWAYS ENGINEERZ BUILD THE WORLD...FULL RESPECT TO ALL ENGINEERS..
ReplyDeleteEeeiish!!!
ReplyDeleteCONSTRUCTION ARE CONTINUES??
what english is that?he he he
O M G....
Hapo hakuna Mhandisi...tuna wasiwasi na uimara wa jengo hata kabla halijajengwa!!!
ReplyDeleteBora ujumbe ufike, gramatical mistakes doesn't matter. Huku kwa waingereza wenyewe yaani kuna watu wanaongea broken kinoma ila wanachojali ni je umemuelewa anchosema?. Hapo engineer kafikisha ujumbe japo katika broken English. "Construction are continues", angesema tu "Construction works on progress" ingesound vizuri zaidi lakini ujumbe umefika.
ReplyDeleteDuuu!!! Hicho kingereza jamani, contractor inabidi abadilishe kabla credibility yake haijatiliwa mashaka
ReplyDeleteMwambie mhandisi makini aandike "construction in progress" sio kuandika broken swanglish
ReplyDeletehicho Kiingereza hapo kinanitoa uchangamfu kabisa hebu wadau angalieni hiyo Sarufi i.e "CONSTRUCTION ARE CONTINUES".
ReplyDeletendio wasomi wa kibongo hao kiinglish zeroooooooooo
ReplyDeleteWilliam mikono ya dume la nyani!
ReplyDeletehahah naona unawapiga madongo wenzako.
Mdau WA AZANIA - USA
Poor language sio kigezo cha uduni wa fani ila ina-indicate mambo mengi yanayotakiwa kuangaliwa kwa umakini katika mhandisi huyo ikiwapo pamoja na uhalali na uwezo wa elimu yake.
ReplyDelete-Mtui.
Ha ha ha nimefurahi sana, sasa hao jamaa wanafanyakazi kila siku na hawaoni kuwa lugha katika hilo bango haijakaa sawa....!!!??? Hii tayari inaweza kuwa kigezo kimojawapi cha kutilia mashaka wataalam wanaohusika na ujenze huo.
ReplyDeleteBongo kweli tambalale
sasa cha kushangaza nini hapo?kwani huyo mdau hajui kuwa sie wabongo tupo down sana kingereza?kwanza tukijue cha nini wakati lugha ya taifa kiswahili/wewe michuzi mwenyewe lugha haipandi
ReplyDelete"Construction in Progress" ingependeza zaidi hapo...
ReplyDeletehiki ni kiingereza cha wapi jamani....sikutiana abu tu....!!!!
ReplyDeleteVizuri, lakini wapitao hapo kwa miguu wengi wao kiinglishi is not rechaboo! inambidi kwa umakini zaidi aongeze kibao kwa lugha ya taifa kiswahili ili wenzangu namie kina kajamba nani tusije pigwa na "vitofa" hapo!
ReplyDeleteHicho kimombo ndicho kinachonivunja mbavu.
ReplyDeleteSawa mdau, naona mhandisi yuko makini ila lugha aliyotumia kachapia ni heri angeandika kiswahili tu!!
ReplyDeleteNdio maana magorofa yana anguka kila siku. Kama kingereza kimewashinda, watawezaje ujenzi wakati lugha waliyo tumia wakati wakijifunza mambo ya ujenzi ni kingereza? Mimi sidhani kama hawa jamaa wali elimika.
ReplyDeleteKAMA ANASHINDWA KUWEKA SENTENSI INAYOELEWEKA, NAKUWACHIA NDUGU MDAU UJIBU MASWALI YAFUATAYO:
ReplyDelete1-ELIMU YA UHANDISI ALIIHITIMISHA VIPI ?
2-NANI AMA MSIMAMIA NANI, JE WASIMAMIZI HAWAONI?
3- UMAHIRI (QUALITY) YA KAZI YAKE).USISHANGAE JENGO HILI BAADA YA MIEZI 3 HALIPANDISHI MAJI JUU.MWAKA MMOJA MBELE---MWELEKA WA MGUVU
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
MTANZANIA # 1.
Nimecheka "Contructions are contibues" but hii lugha ilikuja na meli hata mimi huchemsha. Just a thought though, i think now we should be translating announcements in both swahili and english.
ReplyDeleteWe annon 14 1252 ulikuwa unacheka nini wakati na wewe ni kundini!
ReplyDeleteAnother photoshop output! beware guys
ReplyDeletemi mwenzenu naona kingereza kipo safi tu.
ReplyDeleteMnawasakama bure wahandisi si ajabu huyo Mhandisi au Mkandarasi hata hajaliona hilo Tangazo lake!Mana labda litakuwa limeandikwa na Foreman. Aidha,Lugha nafikiri si kigezo kikubwa sana ktk Uhandisi; kinachodaiwa zaidi ni mahesabu!Lakini pia mnaojiona mnajua vizuri lugha mkumbuke siku za kwanza mlipoingia Majuu, na kama mliingia mkiwa mahodari wa lugha labda wengi wenu mlikuwa watoto wa vibosile kwahiyo mlisoma shule bora, na kama unaishi Bongo basi ni kati ya watoto wa waliojiweza ambao mlisomeshwa kwenye shule za International au Kenya au Uganda; vinginevyo tuliosoma shule za Mwalimu Nyerere hatuwezi kucheka au kudharau wenzetu katika suala la Lugha!
ReplyDeleteKusema Rahisi!
ReplyDeletehivi jamani kutojua kiingereza ni kosa?message si imeeleweka lakini?hii kasumba ya kutukuza mambo ya watu itaisha lini lakini?kwani kuchanganya michanga,kokoto,cement na maji kunahitaji kujua kiingereza?wachina,wajapani na wasukuma hawajengi vizuri kwa sababu hawajui kiingereza?hebu changieni mambo ya maana jamani.....hayo ni mkosa ya grammar tu.
ReplyDeleteHapo sioni kosa. "CONSTRUCTION ARE CONTINUES" Hapa anamaana yaani akitumi ARE means one construction too many. yaani Construction nyingi. CONTINUES yaani hizi CONSTRUCTION hazijaisha, still continueing, They are going somewhere..hivyo anawatahadharisha hizi CONSTRUCTION zikiwa njiani ni HATARI yaani DANGER. Sijui mmenielewa?
ReplyDeleteDah, heri mimi sijasema! Ila Kaijage inaonekana mkandarasi alikuwa na nia njema. na aliona bora FEDHEHA kuliko LAWAMA. BTW Usikute pia EPA-approach imetumika kugharamia hicho kitangazo. MDAU WA AZANIA-Kigogo
ReplyDeletembona mnayafanya makubwa>nani asiejua sie wabongo tupo down sana kwenye lugha!
ReplyDeleteTEH TEH...bonga bonga hivyo mwayego..
ReplyDeletehata ambao leo ni wataalamu wa huyo lugha..walianzia huko huko!