tabia mwanjelwa akiendeleza libeneke huko ujerumani. chini ni tabia alivyo leo
Nani anayewezeza kubisha kuwa Mwanadada Tabia Mwanjelwa kuwa ni mwenye sauti hinayoweza kumtoa nyoka pangoni?

Tabia Mwanjelwa ni lulu ya watanzania iliyopotea kwa miaka mingi bila kusikika na kuwaacha washabiki wakiwa wanajiuliza yupo wapi?

Tabia mwanjelwa! wengine walifika hata kuvumisha na kuzua uzushi labda Tabia hatunayetena! Lakini majibu yanapatikana leo labda Tabia mwenyewe alishaimba kuwa: Maisha ni safari ndefu!!! Mwisho wa Maisha ni kifo!!!

Kwa bahati njema leo juhudi zimefanyika na bendi ya The Ngoma Africa inayoongozwa namwanamziki maarufu Ebrahim Makunja kuwa Lulu hiyo ya watanzania (Tabia Mwanjelwa)imeonekana !

kama kawaida ya watoto wetu wa uswahilini wanapookota kitu uimba Po! Changu! Po! Cha kuokota si cha kwiba!Cha Mchongoma Kina Mwiba!Lakini Lulu hiyo waliyoigundua Ngoma Africa wanairudisha mikononi mwa watanzania! wenyewe mpokeeni Tabia Mwanjelwa anarudi tena uwanjani kwa Kasi mpya! Nguvu Mpya!na miondoko mpya! kaeni mkao wa kula!

Tabia Mwanjelwa kwa sasa anaishi Ujerumani, mzima wa afya na sasa yupo studio kuwaletea nyimbo mpya ambazo kwa kiasi kikubwa zimesha kamilika.
The Ngoma Africa band wanampa shavu dada yao huyo kuhakikisha katika kila hali anarudi tena kwa kasi mpya.Tabia Mwanjelwa bado ana sauti yake utafikili kazaliwa leo! Mwanadada huyo LULU ya watanzania ni nguzo ya kuhaminika katika fani ya mziki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Absolutely definitely one of the legends. If Tanzania had a culture of honouring its icons, she would not have been forgotten. I remember listening to the songs tinged with sweet and melodic voice of hers. Respect.

    ReplyDelete
  2. te!te! Bi.Tabia !furaha nyingi kusikia unarudi kwenye gemu,lakini hao vichaa ngoma africa band! je?
    huko fit na gwaride lao?? pia angalia jamaa ukiwakorofisha tu basi tusakia wanakuimba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...