Wadau leo nimeona nije na hii nyingine, nimekumbuka sana ile miaka ya nyuma kidogo wakati tulikuwa hatuna radio stations nyingi kama zilivyo sasa, wakati huo station ilikuwa ni Radio Tanzania tu na ile idhaa yake ya kiingereza (External).
Fashion ya radio ilikuwa ni zile wanaita RADIO MKULIMA na brand names zake zilikuwa ni NATIONAL Panasonic ama PHILIPS. Mzazi alikuwa anainunua RTC (yale maduka ya uma).Tukirudi katika vipindi, navikumbuka sana vipindi vifuatavyo ambavyo bila shaka mdau utakubaliana na mimi vilikuwa maarufu kutokana na zile nyimbo za utangulizi kuashiria kipindi kuanza ama kumalizika.
"Sikiliza Bwana Umeme... (Bwana Umeme) - Kile kipindi cha TANESCO cha kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya umeme.
"Starehe na BP " - Uncle J. (Julius Nyaisanga) alikuwa anakimudu vyema kabisa""Kahawa ni Mali" - Namkumbuka sana yule mama wa kiashirio cha kipindi akitamka hayo maneno kwa rafudhi ya kichaga.
"Jifunze Kiswahili Fasaha" - sina uhakika kama nimeandika vyema tittle yake lakini kilikuwa ni kile kipindi kizuri kilichobuniwa kuhamasisha watu kuzungumza kiswahili katika harakati ya kuwaunganisha watu wa mikoani na wa Bara. Nakumbuka kiashirio chake kuna sehemu inasema.. na mikoani... ni kiswahili chatumika.....Bila kusahau vipindi kama..
"TTCL Simu kwa Maendeleo" kipindi cha "Serikali za Mitaa", " Afya yako /Afya ya jamii " sikumbuki vyema title ila nakumbuka kiashiria cha kipindi ulikuwa ni wimbo mmoja anaimba Kept John Komba na kundi lake wakati ule.
Ukija vipindi vya week ends kama "Club Raha leo Show", bila kusahau kipindi cha "Mama na Mwana" namkumbuka mtangazaji Edda Sanga alikuwa anakimudu vyema kipindi na zile hadithi za "Adili na Nduguze", "Kisa cha Mfalme Juha", ile hadithi ya watoto wa mfalme wanakwenda kutafuta wachumba wa kuoa... n.k wadau ongezeeni hapo kumbukumbu zenu.
Japokuwa kilikuwa ni kipindi cha watoto lakini nakumbuka watu wazima walikuwa wanazifuatilia kwa umakini sana zile hadithi bila kukosa sehemu hata moja juma moja baada ya lingine.
Wakati ule radio ilikuwa na msaada mkubwa kuelimisha jamii nzima (wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara) kuhusu mambo mbali mbali na watu walikuwa wanafuatilia sana.

Je, wewe mdau unakumbuka nini miaka hiyo hapo kunako Radio Tanzania (RTD)???
Mdau yule yule wa Dodoma,
Natanguliza shukrani Bro Michu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 95 mpaka sasa

  1. Hapo mdau kasahau asubuhi tunaamka na MAJIRA. tunapata habari toka kwa wawakilishi mikoani. Kuna kipindi nilikuwa nakichukia sana kwa sababu kikianza tu nasikia njaa MALENGA WETU. Vipindi vingine kama JENGA NA MECCO,TAIRI GENERAL na marehemu bati kombwa, Kipindi cha Michezo saa mbili kasorobo. YOTE TISA KUNA KIPINDI NAKIMISI SANA. 'MUZIKI NA HISIA' Kipindi hiki kilinivutia sana. Wadau lete vipindi vingine

    ReplyDelete
  2. Ilikuwa myeyusho tu, sisi kwetu tulikuwa tunapata mawimbi ya sauti ya Kenya kuliko RTD na kipindi alichokipenda sana mama yangu ni 'JE HUU NI UUNGWANA?'NA MAMBO MBOTELA!

    ReplyDelete
  3. Mie naukumbuka ule wimbo wa mzee Makongoro akiwaonya madereva wasinywe kileo kama gongo na kuendesha. 'Ati dereva kalewa gongo ah! sawa hiyo?!' Halafu wengine wanabwakiza 'haata hiyo si sawa dereva acha vitukoo!!. Wimbo huu ulitungwa kufuatia hotuba ya mwalimu Nyerere akiwaonya madereva kuwa wastaarabu barabarani. Hiyo ndiyo ilikuwa miaka ya chama kimoja chenye uongozi thabiti wa Taifa.

    ReplyDelete
  4. Duu hapo umasahau kulikuwa na mchana mwema, wahenga wetu,wakati wa kazi, mazungumzo baada habari, mambo mpwitompwito,pwagu na pwaguzi,kumakucha jamani kumekucha,from me to you, dial a disc,majira na zengine kibao nipe muda nitakulretea.

    ReplyDelete
  5. Mdau kuna na hivi vifuatavyo:
    Kijaluba, Kipindi cha Mashairi
    Pwagu na Pwaguzi.
    Bila kusahau kipindi ambacho kwa sasa hivi kingekuwa na kazi ya ziada cha Mikingamo. "Ndugu fulani wa jiji fulani akishirikiana na fulani walikwiba pesa za umma na kuzificha kwenye kisiwa fulani!"

    ReplyDelete
  6. Duuuuh mdau wa dodoma umenikumbusha mbali sana na kipindi cha hadithi ''KISA CHA MFALME JUHA'' kwani nilikuwa sikikosi hata kidogo zile hadithi nakumbuka niliachwa na treni kwenda Dodoma kwa kumalizia kipindi ikabidi nisafiri siku nyingine. Kweli ya kale Matamu

    ReplyDelete
  7. Mdau kipindi cha mama na mwana hapo zamani kilikuwa kinaendeshwa na DEBORAH MWENDA!Wakati huo hadithi ya Binti chura na Ua jekundu zinatukusanya pembeni mwa redio kuanzia saa 8 mchana.

    Any way.. kila mtu na zamani yake, hata mtoto wa mwaka mmoja nae ana zamani yake!


    Binafsi nakumbuka kipindi cha Mzee jangala cha usiku, kilikuwa kinadhaminiwa na "CHIBUKU"

    Zaidi ya yote kipindi cha jumapili salamu za wagonjwa hospitalini. Kiashiria ni wimbo wenye ujumbe mzito " ..Ajue bwana mungu wa mzima kuwa mfu mgonjwa kuwa salama..."

    Mwisho sikisahau kipindi cha majira asubuhi saa 12.30 kilikuwa kinanikera sana sababu ndo mida ya kuwahi namba shuleni (shule ya msingi Tandale Dar.), viranja wanoko na mwaalimu wa zamu balaa ukichelewa namba. Huku nimebeba dumu la maji ya kumwagilia bustani za shule, huku ufagio wakufagilia, huku kifuu cha kupikia uji wa shule, huku nimebeba madaftar, huku michongoma sijui yakueka kwenye uzio, huku kikombe cha uji..dah kama askari anaenda vitani!

    Ah imebaki historia wala haijirudii tena...!

    ReplyDelete
  8. (Ugua poe )JUMAPILI.wakati umewadia wasalamu kwawagonjwa hosipitalini leo tunawapa pole.....
    Mikingamo.Asiria salam.Malenga wetu,Jumanne kibao.Tumbuizo asilia.

    ReplyDelete
  9. Hivyo vingine sivikumbuki vya juu

    Ila nakumbuka mama na mwana, adili na nduguze

    mahoka,
    salamu za wagonjwa jumapili,
    zilipendwa,
    kipindi cha salamu za wafanyakazi

    ReplyDelete
  10. Mama na Mwana = Deborah Mwenda

    ReplyDelete
  11. Wakati umewadia wasalamu zawagoonjwaa, osipitaliinii leo tunawapa poole...tililii, lili. Kipindi kinaleta unyooonge!

    Afu yule babu anasoma mashairi--malenga wetu or something?, yani akianza kusoma na sauti yake ya kizembe zembe njaa ndo inazidi kukoleaaa. Sa kwanini angalau habadilishi tone, au rhythm?.

    Mama na mwana, enzi ya Debora Mwenda....unawajua Urefu, Upana, na jicho-kali?, whatcha know 'bout dat kiddos?.

    Hey, can't forget Pwagu na Pwaguzi. They funny as hell...baati mbaya kunakuwa na mbu kibao kipindi kinapokuepo. Kesho yake malaria, mambo ya chloroquine 4-4-2-2 dozi noma, afu kidonge kinakwama kooni..ughhh!

    ReplyDelete
  12. hii ni kumbukumbu yangu ya baadhi ya vipindi
    saa 5 : WAKATI WA KAZI
    saa 6: MCHANA MWEMA
    saa 7: TAARIFA YA HABARI
    saa 7.10: MATANGAZO YA VIFO
    saa 7.20: ?WAKULIMA

    saa 2 usiku: TAARIFA YA HABARI
    saa 2.10: MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI
    saa 2.15: HOTUBA ZA NYERERE (NIMESAHAU JINA LA KIPINDI)

    ReplyDelete
  13. RTD SASA TBC IMECHNGANYIKIWA HIVI SASA KWANI INATULETA TAARIFA YA HABARI KWENYE REDIO KWAKUTUMIA MTINDO WA LUNINGA! HII IMEFANYA TAARIFA HIYO KUTOKUWA NA MVUTO NA WAKATI MWINGINE HAIELEWEKI HASA WANAPOJARIBU KUIIGA LUNINGA YA BBC HUKU WAKIRUSHA HABARI KWENYE REDIO.

    ReplyDelete
  14. Michuzi umesahau kipindi kingine kilikuwa kinaitwa "UJUMBE WA LEO" kilikuwa kinaanza nafikiri mara tu baada ya taarifa ya habari ya saa 1 asubuhi na saa 2 usiku kama sikosei.

    Baadhi ya mneno yaliyokuwa kwenye wimbo wa kiashirio yalikuwa

    "...mkulima wa kweli hafikiri hayo, anajitahidi kuongeza kilimo,
    ardhi na watu, siasa safi na uongozi bora..."

    Unakikumbuka?

    ReplyDelete
  15. Tunazikumbuka au Zilipendwa, Ujuzi Hauzeeki, Mazungumzo baada ya Habari (k.m. maneno ya "...tulilima na kulimaga.....,safi safi Watanzania bara bara ninyi, wenye kupanga na kuamua....."). Kutoka mikoani, Kilimo Bora, Jungu Kubwa, Dunia ya Jumamosi n.k.

    ReplyDelete
  16. Unaukumbuka wimbo huuu? "Mpango wa pili wa maendeleo unasema kuleni kuku, mayai, mboga samaki maziwa,

    Kuleni chakula bora cha kuujenga mwili na kujenga nyumba safi pa kulala pawe bora!!!

    ReplyDelete
  17. Na huu je? Tujenge, tujenge nchi pamojax2 vijiji vya ujamaa! tujenge, tujenge nchi pamoja X2 Nyerere kasema

    Kibwagizo: wananchi , tujenge......

    ReplyDelete
  18. Mdau umenikumbusha mbali sana, mimi naongezea hapo kipindi cha "jambo" na kile maarufu kwa nyimbo na mabingwa wa salaam, "mchana mwema"

    ReplyDelete
  19. Bila kusahau pia kipindi cha "General Tyre na gari lako" kilikuwa bomba sana pia....Kingine kilikuwa ni zile ngoma za Marehemu Mzee Nyunyusa? kabla ya kila taarifa ya habari...GK

    ReplyDelete
  20. Enzi Hizo Uncle J babaake!! Juliuas Nyaisanga alikuwa juu kwenye mangoma. Miminilikuwa kijijini ningali mtoto mdogo nilikuwa tu naisikia Dar. Jamaa akija toka dar huku kijijini tulimwona kama katoka Ulaya vile??kweli tumetoka mbali!!!

    ReplyDelete
  21. Mdau wa Dodoma, mbona umesahau vile vipindi murua kabisa vya salamu vya kila siku kutoka RTD yaani Mchana Mwema na Jioni Njema; pia kile kipindi kilichotisha kwa 'mangoma' cha Noon Spine kutoka External Service?
    Naitwa Benjamin Ndaga

    ReplyDelete
  22. Mdau, unafanya vizuri kutukumbusha tulikotoka. Kuna kipindi kile cha UJUMBE WA LEO kilichokuwa maalum kwa hotuba za Mwl. Nyerere (huko kijijini Baba yangu alikuwa hakosi kukisikiliza). Kulikuwa na kipindi cha Abdallah Mlawa (sijui yuko wapi sasa) cha KIJALUBA, kipindi cha akina mama (akina baba walitaka kipindi chao kiitwe JALUBA!), vipindi kama Tanzania Stars (maalum kwa bendi mbalimbali za Tanzania) n.k.

    ReplyDelete
  23. Mdau umenifurahisha sana, jana tu tulikuwa tunajikumbusha hivyo vipindi. Mimi nikukumbushe MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI. ilikuwa kila baada ya taarifa ya habari ya saa mbili unapata hiyo kitu, was so nice nilikuwa sikosi hata siku moja. Lakini wadau mnakumbuka enzi za kuanika betri za redio juani ijichaji kwa ajili ya matumizi ya jioni tu. Tehetehetehetehetehe

    By Belas

    ReplyDelete
  24. Panga pangua, matangazo ya mpira Jongo & Charles Hilary yalikuwa mwisho wa mchezo hakuna mtu mtu aliyefikia mpaka sasa..

    ReplyDelete
  25. Jamani mimi nakumbuka saana kile kipindi cha mikingamo na kibwagizo chake kilikuwa kinasema ...Mbinu gani wanazotumia?Kinannani?na wanafanya nini ili kuhujumu uchumi,tuambie nasi tutasema hewani na kwa wanaohusika....
    na kile cha rushwa na tangazo lake...Liangalieni limbukeni hiri,harina haya ,rinakura mari ya uma...wewe?acha kujitafuna mwenyewe kama punguani,wewe acha kuharibu mali ya uma,wewe wacha kuiba mari ya umaaaaa..
    jamani bila kusahau kale kawimbo ka chama..chama chama kimetukomboa chama x2,watanzania,wanamapinduzi ni c c eeeem yajenga nchi.dah .

    wakati ule muziki ulikuwa unakuwa unanogeshwa na nyimbo kama Ifre wana frelimo zooona inapaswa ku mozambique,au magaidi wa msumbiji nilazima walaaniwe kwa unyama wao na uushenzieeh,kusabaishwa kwao kifo cha samora Masheliiii,tanzania tunaahidi tuko nanyi bega kwa bega matatizo yenu ndio yetu eeeh,tutapigana nao mpaka damu ya mwishoooo.

    Kusema kweli mambo ya zamani yalikuwa mazuri mnoo,na shukrani sana kwa mwanakijiji Michuzi kwa kutukumbusha ya nyuma.

    TMMM call a spade a spade

    ReplyDelete
  26. Mmhh jamani mnanikumbusha mbali mie!! ZILIPENDWA Jumapili - wakati huo uko kwa msusi unasukwa mistari ya shule - gwaride Jumatatu...

    ReplyDelete
  27. dhuuu kweli nchi imepotea ilikuwa redio ya wantanzani ,kwa ajili ya watanzani sasa kuna redio tangu hiyo redio ya taifa mpaka zawatu hakuna tafauti ipi inawakalisha taifa na ipi ni redio tu yakusikiliza hata tv ni hayo hayo kazi zilikuwa na wenye wito kweli tumekwisha

    ReplyDelete
  28. ee bwana ee mimi nilikuwa sipendi wimbo ule unaosema kumekucha sasa kumekucha wazalendo amkeni tufanye kazi sasa ukipigwa huo wimbo ujue umechelewa namba kwa mwalimu yeyeye kipeuo cha pili NYAKABUNGO mwanza na usiku nilikuwa sipendi wimbo wa mikingamo maana ukisikia tu huo wimbo mnaambia kwenda kulala si unajua tena enzi hizo tv hazikuwepo basi mkimaliza kula mkaa nje kuadithiana hadithi

    ReplyDelete
  29. KULIKUWA NA TANGAZO MOJA CKUMBUKI VIZURI LILIKUWA LA NINI ILA LINASEMA HIVI" WEWEEE WACHAKUCHAFUA MALI YA UMA WEWEE WACHAKUHARIBU MALI YA UMMA WEWEEEEEEEEEE WAAAACHAAAA MALI YA UMMAA WEEWEEEEEEEEEE.

    ReplyDelete
  30. Mnakumbuka mabingwa wa salamu kama kina ISSA HASSAN MAJESHI wa Ukonga---wengine nimewasahau

    ReplyDelete
  31. Mimi nakumbuka pia Kipindi cha Mkonge ni Mali! Kilikuwa na wimbo wake " Sisi wafanyakazi wa Mkonge mkituona sisi miamba..." Sasa hivi hakuna umwamba wowote Zao la Mkonge limepoteza mwelekeo, watu wamelifilisi Shirika na mashamba yote!

    ReplyDelete
  32. Michezo ya redio
    Njechele
    Ngoswe ( penzi kileo cha uzembe )
    Mkwawa na wajerumani
    mwaka wa watoto
    Mshamu ( mzee Jangalu )n.k

    ReplyDelete
  33. Kweli mdau umetukumbusha mbali. Maisha yalikuwa safi sana maana tulikuwa hatujui mambo mengi ya duniani tuweze kufananisha. Kwanza sio wote waliokuwa na redio kwa hiyo hata mashuleni yalikuwa tunasimuliana! Enzi zile watuma salamu walikuwa maarufu sana kama Limonga Justine Limonga, marehemu Athumani Michuzi na wale mabwana wa Mahuta shimoni Newala!!!. Michu tupe post nyingine kama za magazeti ya zamani, shule, urafiki wa kwanza shuleni...lol kweli ya kale ni dhahabu

    ReplyDelete
  34. yule mtangazaji wa kipindi cha majira, alikuwa maarufu sana, toka dodoma, nimeshahau jina lake, wadau nikumbusheni.

    ReplyDelete
  35. Jamani hivi TIDO ana maana gani kuziondoa ngoma kumi za mzee morris nyunyusa ambazo zilikuwa zinaashiria kuanza kwa taarifa ya habari? Tunamuomba hizo ngoma zirudi kwa vile zinawakilisha utanzania wetu. Au mnaonaje wadau?

    ReplyDelete
  36. Ilikuwa redio haikeshi ...basi ikifika saa sita usiku inapigwa "Mungu Ibariki ....." halafu ikiisha Miungu ibariki tu redio mitambo inazimwa kimyaaaaa....mpaka kesho asubuhi tena
    (Machozi yananilenga)

    Halafu kulikuwa na kipindi cha "Bima yako ...kwa mali ... Bima yako kwa ajali ...Bima yako ...."

    oooohhhh tumetoka mbali jamani Mungu tunamuomba atusaidie tufike salama huko tunakokwenda

    Nimepatwa na hisia sana jamani

    ReplyDelete
  37. Mmesahau kipindi cha "Tumwabudu Mungu" kila jumapili

    ReplyDelete
  38. 1)umesahau na kina mzee jongo na matuga
    2)huduma bora zuri kwa wateja wetu,na ushirikiano kwa mara ya kwanza na kila wakati na maelewano ya watu wawili*2 TTCL simu kwa maendeleo

    ReplyDelete
  39. Lady JD wetu kipindi hicho alikuwa ni Tabia Mwanjelwa na kibao chake "Kweli Maisha ni safari ndeeeefuu eeeehhhh x 2"

    Alikuwa anaimba kwa kiswahili lakini kwa accent ya Kinyakyusa .......
    mweeh tumetoka mbali

    ReplyDelete
  40. Kipindi cha michezo kilikuwa kinaturusha roho kweli kwani habari muhimu zilikuwa hazitangazwi mwanzoni zilikuwa zinatangazwa mwishoni mwishoni mwa kipindi

    ReplyDelete
  41. YOTE TISA MAMA NA MWANA KILA JUMAMOSI DUH HIZO IMAGINATION CBBC AU DISNEY CHANNEL ZILIKUWA HAZIONI NDANI.HAPO HADITH ILISOMWA NAFIKIRI ALIKUWA BETY CHALAMILA- MKWASA BAADAYE. REDIO YETU ILIKUWA NESHNO YA MBAO. BETRY NESHNO AU PAKA POWER ZA KENYA!!! KIBOKO

    ReplyDelete
  42. SALAMU ZA WAGONJWA WOTE TUNAWAPA POLE.... HAYA NIKO KWENYE WODI YA KINAMAMA WAJA WAZITO.... JINA LAKO NANI... MEN IT WAS LIKE KUWA KWA X FACTOR . LOL

    ReplyDelete
  43. Mdau wa kwanza nashukuru kwa kutufungulia dimba vyema,
    Umenikumbusha sana hivyo vipindi ”JENGA NA MECCO”, ”GENERAL TYRE na Gari lako”,
    Mdau Nov 14, 2008 4:14 AM na Nov 14, 2008 4:43 AM nashukuru kwa kuniweka sawa ”Mama na Mwana” alikuwa ni Deborah Mwenda , Edda Sanga alikuwa ni mwakilishi (reporter) wa RTD wa kanda ya Kaskazini sina uhakika vyema wadau watakumbushia

    Wadau wamekumbushia kipindi cha ”Malenga Wetu” kile kipindi kiliwekwa wakati mmbaya sana (mid day ) mara nyingi ilikuwa ni muda ambao ndio nilikuwa natoka shule. Nakua na njaa sana halafu mara kadhaa unakuta chakula bado hakijawa tayari sasa ukisema uwashe radio tu unakumbana na ”Malenga Wetu” yaani dahh ...njaa ndio ilikuwa inaongezeka.

    Naungana na Mdau hapo juu kuwa tumepoteza uelekeo... hii ilikuwa ni Radio Tanzania kwa Watanzania. Ukiangalia kwa makini vipindi vyote vilikuwa so organised pamoja na kuwa hakukuwa na technologia nzuri kama ilivyo sasa. wasanii waliimba nyimbo zenye ujumbe sambamba na vipindi hii ilikuwa ni kichocheo cha hali ya juu cha kujenga Uzalendo kwa raia. Sasa tupo katikati hatujui tufuate lipi tuache lipi,radio zimekuwa nyingi na TV lakini control na ubunifu umekuwa wa hali ya chini sana kulinganisha na wakati ule.

    wadau mnaweza kutoa maoni yenu pia ya hali halisi wakati mkikumbushia hapa na pale enzi hizo.
    Mdau wa Dodoma.

    ReplyDelete
  44. MMESEMA VIPINDI VENYE KUONGEZA NJAA... KUNA HIKI SIKUMBUKI JINA KILA IJUMAA BILA KUKOSEA SHEKH MKUU BIN HEMED BIN JUMAAAA.....DUH ILE SAUTI SIKUWA MUISLAMU LAKINI NAKIKUMBUKA MPAKA LEO... ALLIIIIKUWA NA MVUUTO WA SAUTI.

    ReplyDelete
  45. Mdau, Nov 14, 2008 12:45 PM, Mtangazaji wa RTD Dodoma kwa muda mrefu kulikuwepo na Mohamed Kipozi na Mkewe Sango Kipozi pia kuna kipindi alikuwepo yule mtangazaji machachari Beni Kiko nafikiri mnakumbuka na style yake iliyovutia wengi na mara nyingi habari yake iliwekwa mwisho wa kipindi.
    Mdau, Nov14, 2008 1:02 PM, umenikumbusha sana kipindi hicho ”Tumwabudu Mungu” pia kulikuwepo na kipindi cha ”Nyimbo za injili” vilikuwa vinafuatana. Hivi ni miongoni mwa vipindi ambavyo hajibadilika sana mpaka hii leo.

    ReplyDelete
  46. ....shambani shambaniiiiiii!ni mazao bora shambani!haya twendeni shambani....

    ReplyDelete
  47. mimi nakumbuka sana kipindi cha
    Mazungumzo baaada ya habara(nilikipenda sana)
    Maneno hayo (nilikipenda sana)siku moja kinaanza kama hivi "Komba nadhani mlio wengi mnamfaha na kwa wale wasiomfahamu basi wanamsikia usiku akilia kana kwamba anapigwa kumbe anafurahia chakula alacho usiku palipo giza ni chakula cha wakulima walitolea jasho kulima mazao kwa takribani mwaka mzima ila komba yeye ni mwenye furaha kama ................"

    Wosia wa baba

    Mama na Mwana jumamosi saa nane kamili mchana (adili na Nduguze, Uwa jekundu, binti chura)

    Mzee jangala jumamosi saa tatu na nusu usiku (wadhamini Chubuku kibwagizo tutumie chubukuuu uuuuh ni pombe bora, tutumie chibuku uuuuh ni pombe bora) nakumbuka siku moja niko kitandani nimelala nikasikia kimeanza kama hivi "mmmmmmmh croooooo crooooo alafu unasiki "we Kiatu yani mchana wote huu umelala baradhani uchuro mtupu"

    General Tyre na gari lako (kibwagizo " tairi General kutoka arusha. Tairi tayari"

    kipindi cha michezo ambacho mwanzo wake niliupachika wimbo huu hapa
    "baba yake juma amevaa viraka.. vinaulizana umekujalini...?
    nimekuja jana nimekuja juli nimekuja leo taaaaa taaaaa taraaa.

    yanii we acha tu utamu mtupu siwezi kuweka vyote ni vingi sana vya kukumbuka

    ReplyDelete
  48. dah hii sio mchezo wadau mnanikumbusha kipindi cha jeshi letu la police....kibwagizo chake kinaanzia hapo kati sijui mara.."kurekebisha misafara ya magari barabarani..kuwakamata wahalifu wote na kuwafikisha mahakamani..."wapi bwana hakuna cha mahakamani ni usanii tu wakati huu.kipindi cha twende na wakati tunu na mkwaju enzi hizo,mzee makusanya sio mchezo.kipindi cha BP "kwa ulainishaji wa mitambo ya viwanda..Tegemea BP,kwa Oil za magari,trekta,treni,meli ,ndege na vyombo vinginevyo tegemea BP..."

    ReplyDelete
  49. Asubuhi tunaamka na kipindi cha kumekucha, na wimbo wa shaaban marijani "kumekuucha jama kumekucha, majogoo vijijini yanawika hata na jua mbinguni linatoka, wazalendo amkeni tufanye kazi sasaaa!
    Bila kusahau kipindi cha ombi lako, yaani vijana siku hizi wanaita request, jioni njema, kipindi cha Ukulima wa kisasa, pamba yetu n.k.

    ReplyDelete
  50. mdau w auk nakuja hivi,
    kuleni kuku mayai,mboga samaki maziwa,kwa kulinda afya zetu pa kulala pawe bora!!!

    hata sabuni zimepotea,hata sukari zimepotea,kumbe kuna vyura wanao meza!!!

    palikuwa na kipindi kinaitwa misakato,kombora,

    mnamkumbuka fundi mitambo damsoni msonga reli?ahhh tumetoka mbali bwana.
    kuna mtu aliitwa ben kiko,akitangaza vita vya idd amini.

    wadau wote wa kukaye dodoma
    tuwasiliane titusboniface@yahoo.com

    ReplyDelete
  51. Ama kweli hii ni blog ya jamii, maana tunakumbushana mambo ya jamii ya kipindi kilichopita! MDAU WINDY-CITY mtangazaji wa Majira enzi hizo Dodoma kama sijakosea anaitwa BEN KIKO! Mdau wa saa 10.38 umenikumbusha wimbo wa "kumekucha sasa kumekucha, majogoo vijijini yanawika, hata na jua Mbinguni linatoka, wazalendo amkeni ..." jamani tumetoka mbali!!!

    ReplyDelete
  52. Nyimbo zilizotamba kipindi hicho

    "Mwanameka eeeh ...mwanameka jirani yangu ....mimi naona vibaya ...umemponza mwenzioooo"

    Sikinde

    " Tufurahi leo tufurahi na wana sikinde ...tucheze leo ngoma ya ukaeeeee"

    Sikinde walikuwa na basi lao kubwa limechorwa vyombo vya muziki na picha za wanamuziki

    Halafu

    Kulikuwa na Mabondia kama Emanuel Mlundwa, Habib Kinyogoli, Stanley Mabesi, Somwe Patauli

    Basi kwenye magazeti kulikuwa na matangazo ya Mapambano mbalimbali ya ngumi na matangazo ya muziki na kumbi za cinema kama vile Odeon, Drive in, Empire, Empress basi zilikuwa sinatoa matangazo kwenye magazeti kuhusu picha mbalimbali zitaanza saa ngapi na kusha saa ngapi

    Looooh

    Maisha ni safari

    ReplyDelete
  53. Nyimbo zilizotamba kipindi hicho

    "Mwanameka eeeh ...mwanameka jirani yangu ....mimi naona vibaya ...umemponza mwenzioooo"

    Sikinde

    " Tufurahi leo tufurahi na wana sikinde ...tucheze leo ngoma ya ukaeeeee"

    Sikinde walikuwa na basi lao kubwa limechorwa vyombo vya muziki na picha za wanamuziki

    Halafu

    Kulikuwa na Mabondia kama Emanuel Mlundwa, Habib Kinyogoli, Stanley Mabesi, Somwe Patauli

    Basi kwenye magazeti kulikuwa na matangazo ya Mapambano mbalimbali ya ngumi na matangazo ya muziki na kumbi za cinema kama vile Odeon, Drive in, Empire, Empress basi zilikuwa sinatoa matangazo kwenye magazeti kuhusu picha mbalimbali zitaanza saa ngapi na kusha saa ngapi

    Looooh

    Maisha ni safari

    ReplyDelete
  54. Gazeti la mfanyakazi lilikuwa liko juu sana na Waandishi maarufu kama James Nhende .... na kulikuwa na hadithi nzuri " Simulizi za Agoro Anduru"

    Halafu EPA ya kipindi hicho ilikuwa kashfa ya "Loliondo Gate"

    ReplyDelete
  55. Scout Boy na Chipukizi(vijana wa CCM) ilikuwa dili

    ReplyDelete
  56. Mmesahau kipindi cha ijue "IDM Mzumbe"

    ReplyDelete
  57. "Mbiu ya Mikoa"

    ReplyDelete
  58. Mbiu ya mikoa .... utasikia "Eeehh leo Tuko mkoani Iringa ...mkoa huu uko sehemu ... kuna makabila ya...."
    Halafu vinawekwa vibwagizo vya nyimbo za makabila ya mkoa huo ...
    kama
    "Siwainogela munu ki .... siwainogela muuuunuuuhhh"
    au
    "Sagula madulu na mapilipili x 2"

    ReplyDelete
  59. Jamani taarifa za habari za RTD zilitufundisha sana watoto miji mikuu ya nchi, utasikia mtangazaji anaianza habari kihivi.."Sansalvador, Rais wa nchi ya El-Salvador amesema..."...au... "Colombo, Nchi ya Sri-Lanka imetoa msaada..."
    Yaani watoto wa siku hizi ukiwauliza mji mkuu wa nchi ya Mali au South Afrika hawajui...RTD walikuwa wanatufundisha bila kujijua.

    Na kipindi cha mama na mwana kikianza, ukisikia mama anakuita tuu unatamani umpige maana anakunyima uhondo.

    Klabu raha leooooo, shooooooow...hichi kipindi hadi leo sielewi walikuwa wanakifanyaje fanyaje, nachojua ni kama vile kunakuwa na watu kibaooo hapo wamekusanyika.

    Mnalikumbuka tangazo saa moja kasorobo kabla ya kipindi cha Majira..."mologolo mologolo darisalamaaaa wahi basiiii (Mabasi ya Aboud ya Morogoro to Dar es Salaam)

    ReplyDelete
  60. kipindi cha chaguo la msikilizaji, kama hutoi sababu za kuupenda wimbo hupigiwi! Utasikia ujumbe ni mzuri sana, vyombo vimepangwa vikapangikika, na sauti ni murua....

    yote tisa kumi utaalamu wa watangazaji wa kipindi cha michezo mbili kasorobo. Huwezi kujua kwa vidokezo mpaka ukae mpaka mwisho kabisa.

    Wako wapi, Michael Katembo, Nazir Mayoka, Jackob Tesha, David Wakati, Malima Ndelema, Mbonde, Abdalahaman, Kisengo, Kipozi, na yule bosi wao wa mazungumzo baada ya habari??

    Ila ilikuwa raha yake.

    ReplyDelete
  61. Daaaah, Anko J alikuwa akikaa mtamboni anashusha vigongo vya nguvu, utamsikua anasema "Fundi mitambo vituuuuuuuuuuuuuuu", ...basi kipindi kikiisha utamsikia anasema "ni mimi Anko J Nyaisangaaaa, Adiosssssssssssssss"

    aaaaah that life sitasahau jamani, those were the old good days kwa kweli

    ReplyDelete
  62. Jamani mnalikumbuka Tangazo la CRDB ( CRBRBBBBBBB... CRBD ni benki ya ushirikaa, na maendeleo..vijijini, ni chombo cha umma kinachotoa mikopo, kwa ajili ya kuendeleza [..nimesahau hapa..]...piaaa, hutoa huduma za kibenki pamoja na ushauri wa kitaalaam, ni chombo kilichoundwa kwa sheriaaa iliyopitishwa na bungee Julai themanini na nne)......ahahahahahahah

    ReplyDelete
  63. Dah wadau nimefurahi sana leo, big up mzee wa Dodoma.

    Mnakumbuka kipindi cha BP kikiisha utasikia ...BP ni Zaidi D D D D....
    Basi sis zile DDD tulikuwa tunaambizana ati zinasemwa na Shetani, jamani utoto rahaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  64. Wadau vipi wimbo ule wa X-mas na wa eid?

    Heeepi krismass, hiyo hiyooo, heepi new year hiyooo hiyooo

    Mpenzi wangu ninakupaaa mkono wa idiii, tupeane mkono wa idiii jamani tupeane mkono wa idiii

    ReplyDelete
  65. WALIMU WA WALIMU

    ReplyDelete
  66. NAKUMBUKA KULIKUA NAKIPINDI CHA MASOMO KUANZIA SAA2-4,5 KWA SHULE ZA MSINGI REDIONI, NAUJIFANYA KUSAFIRI NCHI MBALIMBALI KAMA MAREKANI KUANGARIA KILIMO CHA MAHINDI,BRAZIL MIWA SUKARI NK

    ReplyDelete
  67. Du kumbuka mbali sana kuna kipindi nilikuwa nakipenda sana kinaitwa PHILLIPS RAIO CLUB na Julius nyaisanga we acha tu nilikuwa nariokodi caseti zangu kutokea hapo na kipindi cha Amboni Group kwa nyie watu wa mikonge Alafu ikawa NOmaaaa wakati wa vita vya Nduli Idd Amin Dadaaa ikawa RTD hawapigi muziki ni maombolezo tuuu usiku taa za nje haziwashwi basi tabu tu marufuku Disco basi shidaz juu ya mawazo enzi za nyuma ilikuwa hakuna mwanamke anasoma taarifa ya habari du tumetoka mbali kuna yule mtangazaji anakuja studio na manyanga yake ktk kile kipindi cha ngoma za kienyeji si unajua tena enzi hizo vijana hatupendi ndoma za kienyeji lakini yule jamaa alifanya tuzipende nipeni jina lake nimesahau

    ReplyDelete
  68. Wandugu je mwakumbuka kipindi kile kilikuwa kinasema.....Chuo Cha Ushirika Moshi kinawalete......wananchi tujifunzeni ushirika.....wananchi tujifunzeni ushirika......

    ReplyDelete
  69. Wale tuliokuwa tukifuatilia soka letu la bongo hatutamsahau Marehemu Dominic Chilambo aliyewapa sifa TP Lindanda Pamba ya Mwanza wana Kawekamo. Vipi fundi mitambo Lando Mabula?
    Anko J alikuwa anamalizia kipindi na alamsiki wasikilizaji.
    Tumetoka mbali, enzi hizo nyimbo zilikuwa zinahamasisha kilimo na kufanya kazi, kutohujumu mali ya umma na mambo kama hayo. Siku hizi ni nyimbo za demu wangu kafanya vile, demu fulani kafanya hivi, mademu namna gani nk. Tumetoka mbali kweli kweli.

    ReplyDelete
  70. Club Raha Leo shoooooooooooow!!!! long time sana!! tumetoka mbali

    ReplyDelete
  71. ...nimegundua kuwa wachangiaji wengi ni wa 'juzi juzi' tu kutokana na kukitaja kipindi cha 'mama na mwana'. waliobugia chumvi watakumbuka kuwa kilikuwa kinaitwa simply 'kipindi cha watoto' na nadhani ilikuwa kila jumapili na tune yake ilikuwa;

    (Karibuni) watoooto wa Afrika!
    (karibuni) kipiindi cha watoto!
    (msikie) nyimbo hadithi na vicheko
    (mengineyo) maambo muhimu ya masoomo!
    (sogeaa) karibu ushirikiane nasi!
    (ufurahii) na watoto wenzako radioni)
    (karibuni) watotoo wote!
    (muwe nasi) kipindi cha watoto!

    halafu mwisho wa kipindi inakuwa:

    (kwa herini) watotoo wote!
    (muwe nasi) juma liijalo!
    (asanteni) kwa heriini nyote!
    (kwaherini) watotoo wote!
    (kwa herini) watotoo woteee

    ...halafu kuna fuata sauti za watoto kama waliotoka mstarini!!!
    Those were the days.

    ReplyDelete
  72. ...wale wa zamani zaidi pia watakumbuka vipindi vya salamu vya jioni kama 'Hongera' na 'Pole' cha marhum Salama Mfamao na 'Wakati wa kazi', 'Inuenii Mioyo','Umoja wa Mataifa Wiki Hii', Karibu RTD', 'Misakato' nadhani pia mzee David Wakati alikuwa na kipindi cha kila jumapili saa nane mchana nadhani kilikuwa kikiitwa 'Duniani wiki Hii' na kadhalika na kadhalika. ajabu siku hizi tuna marundo ya vituo vya redio lakini hakuna vipindi vya kaliba hii. kelele tu.

    ReplyDelete
  73. Matangazo ya vifo baada ya taarifa ya habari.

    club raha leooo...shooooooooooooooo!

    ReplyDelete
  74. MIKINGAMO NI SAUTI YA UMMA, TUAMBIE NI NANI NA YUKO WAPI, AKIENDELEZA RUSHWA NA MAGENDO. hapo utasikia bomu limekwisha pasuka mabepari wanahangaika wahujumu wanatangatanga, ulanguzi nayo iko ndani....

    ReplyDelete
  75. Hivi Nkwabi Ng'wanakilala, Paul Sozingwa wako wapi? TBC haina mwelekeo, hatuoni utaifa katika TBC bali kuna kuua utaifa na utamaduni wetu wa kutuletea mambo ambayo hayatujengi. TBC ya sasa inaua utamduni wetu. Mfano ngoma za mzee Moris zimekosa nini hadi zikatolewa. Ile mbiu ya mgambo ya TVT ilikuwa na mapungufu gani? Westernization na brainwashing hiyo. Tafakari

    ReplyDelete
  76. tuimbe sote na wananchi wote karibuni kwenye kipindi chenuuu cha radio cha makao makuu dodomdd,mpango wa liishe twaomba uzingatiwe mmm kweli ya kale ni dhahabu
    kuna maigizo mkwawa ndige kwa mkwawa aee tiyendelele sijui ndio hivyo nakumbuka natamani kulisikia tena hilo igizo
    na lingine kipara lete chai ya bwana mkubwa

    ReplyDelete
  77. Pia kipindi cha utalii, nakumbuka mwimbo wa Mbaraka Mwinshehe Mwaruka "maonyesho Japani yalifana sana, Mzee Morisi na ngoma zake tisa", Na ule mwimbo mwingine wake "Tanzania ndio nchi pekee yenye wanyama wengi tena wa kuvutia, watalii kutoka ng'ambo mwakaribishwa, mje kuona mengi mnaporudi kwenu mkasimulie"...

    Pia mdau umenigusa kwa watangazaji mpira wa miguu, SEKIONE KITOJO, DOMINICK CHILAMBO (akiwa CCM Kirumba)

    Mnakumbuka Ahmed Jongo kama Yanga ikifungwa Goooooooooooo yake inakuwa soooo weak, na kama Yanga ikifunga basi Jongo anachanganyikiwa anweza akasema goooooooooo mara 4!
    Those were good old dayz.
    Sue

    ReplyDelete
  78. yaani mdau unatukuna kweli
    RTD was the only station nimeikuta nilipozaliwa,nilikua napenda sana kipindi cha ugua pole
    wagonjwa wanapoambiwa wachague wimbo,yaani u reminded me so far away mdau
    duuuuuuuuuuuuh Tanzanania raha kweli,tunaimis sana RTD

    ReplyDelete
  79. tutaimiss sana redio radio yetu..
    those good days man!!!
    naskia wamefanya changes kibao, ni bora wangeikeep kama ilivyokuwa zamani..!

    ReplyDelete
  80. Mi mdau mbegu,UK Reading, nakumbuka vipindi vingi nikivitaja nadhani nitajaza kurasa hata tano ila nachotaka kusema kipindi ambacho favourity kwangu ni kile kiitwacho Wiki Ya Nenda Kwa Usalama

    ReplyDelete
  81. Mdau unaesema kipindi cha watoto ni cha zamani sana na cha mama na mwana ni cha karibuni unakosea. Mie nilibahataika kushiriki vipindi vyote hivyo, live! Kabisa live, Kipindi cha watoto wetu nilishiriki shuleni kwetu na hiki kilikuwa kinarushwa siku ya jumamosi asubuhi kama sikosei baada ya kurekodiwa. Basi walikuja watangazaji wakaja kurekodi kipindi hicho shuleni kwetu, tufurahi watotooo wote. Hiki ni kwa watoto wakubwa kidogo wa shule za msingi.

    Kipindi kingine cha watoto kilikuwa mama na mwana, hiki kilikuja baadae sana ubunifu wa Deborah Mwenda, nacho nilienda studio za RTD pamoja na watoto wengine wa shule ya msingi Miburani kurekodi hapo nilikuwa darasa la 4 mwaka 1979.

    Kipindi kingine cha watoto wadogo wa chekechea kilikuwa kinaitwa 'Chei Chei Shangazi' hiki kilikuwa ni kipindi cha Sara Dumba siku hizi Mkuu wa Wilaya moja huko Tanga, basi utasikia wakati kikianza
    " Chei chei shangaziX 2
    Shangazi chei Shangazi x1

    Tufurahi Shangazi x 2
    Shangazi chei Shangazi x 1.

    Kikiisha, wanaimba
    " Uje tena ShangaziX 2
    Shangazi shangazi chei Shangazi

    Kisha nakumbuka mtoto mmoja kwetu alikuwa anaiga ile sauti ya mazungumzo baada ya habari
    basi yeye anasema "Mazungumzo baali ya habali" yaani hicho ndicho alichokuwa anakisikia!

    Yaani we acha tu! Those were old good days! Siku hizi kuna redio au matwipwitipwi?!! sijasikiliza redio sijui nina miaka mingapi maana sioni kipindi cha kusikiliza!

    Ila bandugu leo nimecheka sana na nimekumbuka mbali kweli, kusubiria mchezo wa redio wakina jongo,. basi tu, watoto wa siku hizi wanamiss sana, ndio maana kuna study imefanywa uk na results zinasema iq za watoto wa sasa ziko chini ukilinganisha na za wa miaka ya zamani.

    ReplyDelete
  82. Yaani we acha tu,mdau kanikumbusha kipindi cha salamu za wagonjwa sijui ugua pole, katika juchagua wimbo, mgonjwa si kachagua apigiwe zile kelele zilizokuwa zinasikika wakati kipindi cha matangazo ya kifo kikianza,ilistaajabisha hata mtangazaji ila alitekeleza matakwa ya mgonjwa. Enzi hizo mdingi anazo lakini hata duduproof hakununua sijui kwa nini mi nilikuwa nadoea kwa jirani yetu ambaye alikuwa mkunga kijijini na watoto wake ndoo mabest wangu,basi hata kifo cha Sokoine(RIP)nilifanya kusimuliwa nikadhani utani,oooh ilikuwa 'msiba na nyemi'.
    tawile.

    ReplyDelete
  83. Wadau/wafanyakazi wa TBC tunajua kuna baadhi yenu mmeziona comments hizo zaidi ya 80, zote ni positive comments! tunaomba ziwafikie viongozi wa TBC hasa TIDO MHANDO ili wazifanyie kazi na waone wanaweza kufanya nini kuturudishia Raha! Wadau/wafanyakazi wa IPP MEDIA mlioziona hizi comments tunaomba mumfikishie Julius Nyaisanga in case hajatembelea bloguni ili aone watu walivyokuwa wakimfuatilia miaka hiyo ya 80!
    Thanks na Ashukuriwe mdau wa Dodoma!

    ReplyDelete
  84. Wadau,

    Mmeonyesha kukumbushwa mbali sana na RTD. Na mimi nimekumbuka mbali sana.

    Tumekumbuka vipindi. Hebu tukumbushane na wale waliokuwa wanavirusha vipindi. Mimi naanza na Khalid Ponela (this is encyclopedia), Elli Mbotto, Mustapha Nyang'anyi, Paul Sozigwa (full command ya kusoma taarifa ya habari, mazungumzo baada ya habari na uhamasishaji umma au propaganda/siasa), David Wakati (full command ya usomaji habari, mazungumzo baada ya habari na uchambuzi wa mambo/siasa), Abdul Ngalawa (taarifa ya habari), Mshindo Mkeyenge (social issues), Salim Mbonde(taarifa ya habari, michezo na salamu), Abdallah Mlawa (habari na social issues), Abisai Stephen, Chris George(salamu), Abdul Masudi Jawewa(taarifa ya habari na michezo), Danstan Tido Mhando(michezo), Gothalum Kamalamo, Mikidadi Mahmoud(taarifa ya habari na uchambuzi wa masuala/siasa), Jackob Tesha(nacheka kidogo nikimfikiria anatangaza mpira au tukio la lolote la haraka haraka), Batholomeo Kombwa(Taarifa ya habari na wakati wa kazi), Sekioni Kitojo, Dominick Chilambo, Ahmed Kipozi, Ahmed Jongo, Julius Nyaisanga (he has a voice and talent. Sauti na diction vingeweza kutumika kama signal tune ya watangazaji wa Tanzania), Hendrix Libuda (Club Raha Leo), Charles Hilary(All weather habari, salamu, michezo, salamu, social issues), Eda Sanga, Thecla Gumbo, Sango Kipozi, Salama Mfamao, Fauziat Aboud, Shida Waziri, Betty Chalamila, Mwanaisha Diwani na .....

    Haya wadau wengine kina nani katika safu hii?

    ReplyDelete
  85. Mdau wa Tandale umenikumbusa mbali sana, miaka ya mwanzo ya tisini nilikuwa Mburahati shule ya msingi. Kifuu, fagio la chelewa, na dumu la maji muhimu. Ukisahau fagio unaomba washkaji wakuchomolee chelewa unatengeneza wa kwako.
    Mdau wa hapo juu nakuunga mkono...hivi vipindi ndio asili yetu watanzania. vilikubalika na kila mtu kwenye jamii...kila rika na kila hali. Turudi kwenye "Identity" yetu and turudishe vipindi kama hivi.
    nawakilisha

    ReplyDelete
  86. Wote mliochangia mmechangia kwa hisia. Mna kitu kinaitwa "positive flashback syndrome" (Kwa Kijapan: Natsukashii kimochi). Hii hali humfanya mtu kujisikia vizuri anapofikiria mambo ya nyuma hata kama yalikuwa mabaya. Kitu kama vile ugumu wa maisha ya shule ya msingi, sekondari au chuo mathalani kula maharage almost kila siku yaweza kumfanya mtu mwenye syndrome hii kujisikia vizuri anapo yafikiria. Watu wengi huwa wanayo hali hii. Kwa hiyo haimaanishi kuwa vipindi vya Tido ni vibaya ikilinganishwa na vya wakati huo. Amini usiamini, yule anayezaliwa leo wakati wa vipindi vya Tido na kukua navyo atajisikia hivyo hivyo mnavyojisikia ninyi leo siku vipindi vya Tido vitakapo badilishwa na mtu mwingine.

    Anonymous Dr. Najaga

    ReplyDelete
  87. michael katembo na muziki wa asili "ukinipenda usinipendeeeh na mume wangu jembe" hiyo ngoma kutoka visiwani

    ReplyDelete
  88. kwaresma wakati wa pasaka

    ReplyDelete
  89. Jamani Blog yenu ni nzuri sana

    ReplyDelete
  90. Kisondella, A.AApril 15, 2009

    Duh! Jamani mimi mmenikumbusha mbali saaaana! wakati huo RTD ilikuwa redio ya kizalendo kweli, na ambayo ilikuwa ikiangalia sana maadili, hata nyimbo zilizokuwa zina rekodiwa zikionekanamashairi yana utata aidha unambiwa ubadili mashairi au uuchomoe wimbo unaotaka kurekodi. Mimi ni mpenzi sana wa zile nyimbo zetu Hivyo nilikuwa navi-mind sana vipi vya Kumekucha, Asubuhi njema, Wakati wa Kazi, Karibu Redio Tanzania, Mchana Mwema, Chaguo La Msikilizaji, Jioni Njema, Usiku Mwema, Club Raha Reo Show, Misakato (Kipindi ambacho Julius Nyaisanga "Uncle J" alikuwa anatambulisha nyimbo mpya ambazo zimerekodiwa na Bendi Hapo RTD. Basi katika vipi hivyo nilijua sitwakosa kuwasikiliza Sikinde, Msondo, Uda Jazz, Urafiki Jazz, National Pansonic, Biashara Jazz, Bima Lee, OSS, Maquiz n.k . Hivi sasa nahisi kama vile RTD imekosa mwelekeo au nao imekumbwa na mtikisiko wa Biashara Uria, Nyimboi za ujabu ajabu ni kitu cha kawaida pale RTD (au siku hizi TBC-Taifa)

    ReplyDelete
  91. Kisondella, A.AApril 15, 2009

    Kipinsi cha Malenga wetu loh! kilikuwa kinanipa njaa; yule mzee alikuwa analenga kichooooovu;

    ReplyDelete
  92. Kisondella, A.AApril 15, 2009

    Jamani kuna mtu anakumbuka kiashirio cha kipindi cha Mkulima

    "Mkulima wa kisasa, mkulima wa kisasa...........". Kweli RTD ilkuwa redio ya kisiasa

    ReplyDelete
  93. jungu kubwa haijatajwa ikiongozwa na mikidad mahmud kila jumamosi majira ya alasiri

    ReplyDelete
  94. nakumbuka majira ya saa 3 usiku ukisikia '''kibuku oyee, oyee hongera hongera hongera kibuku oyeee hongeraaaaa''' hapo popote nilipo nilikuwa namuwahi mzee Jangala, Mama Siyawezi, Siyawezi, Bi.Nyakomba...... Unasikiliza mchezo wa kuigiza kwa hisia ni zaidi ya Bongo Movie
    namkumbuka Dominic Chillambo, Khalid Ponela, David Wakati na kipindi cha duniani wiki hii, malima Ndelema, Bujaga Izengo Kadago, Beni Kiko, Abdul Ngalawa, Albert Msememb. Ama kweli life its an experience

    ReplyDelete
  95. AnonymousMay 13, 2014

    Dah japo sio wazaman sana ila nimekumbuka mbali mno….!
    wadau mnakumbuka vyema vipindi vya RTD je mna weza kunisaidi kunikumbusha vipindi vya TVT kabla haijabadilishwa kuwa TBC1….mdau wa dodoma naomba msaada wa karibu tafadhali!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...