Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu Zain kudhamini mashindano ya gofu ya Zain Corporate Challenge yatakayorindima Ijumaa katika viwanja vya TPDF Lugalo, Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa Zain Tanzania, Heiko Schlittke.


Zain Tanzania imedhamini mashindano ya gofu ya kampuni yanayotambulika kama Zain Corporate Challenge ambapo wachezaji kutoka kampuni mbalimbali, wakiwemo wateja wa Zain watachuana katika viwanja vya TPDF Lugalo jijini Dar es Salaam Ijumaa ya Novemba 7, 2008.



Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha wa Zain Tanzania, Heiko Schlittke alisema kwamba Zain inafurahia kudhamini mashindano hayo yatakayowakutanisha pamoja wafanyakazi wa kampuni mbalimbali pamoja na wateja wa Zain kwa ajili ya kuburudika katika michezo na burudani.

“Zain ina furaha kudhamini moja ya mashindano ya gofu yenye msisimko Tanzania, ambayo yanajulikana kama Zain Corporate Challenge, yatakayokutanisha pamoja kampuni ambazo ni washirika na wateja wa Zain ili kucheza pamoja.

Michezo ni lazima kwa ajili ya kuimarisha afya zetu na kujiweka fiti, na Zain tuna furaha kuwaburudisha wateja wetu kupitia mchezo huu,” alisema Schlittke.

“Hatuna budi kuwashukuru washiriki wote wa mashindano haya na tunatumaini kwamba udhamini wetu utafanya mashindano haya kuwa ya kimataifa zaidi na kuongeza chachu ya ushindani pamoja na kupromoti mchezo wa gofu Tanzania,” alisema na kuongeza kwamba anaamini mashindano hayo pia yataimarisha uhudiano miongoni mwa wateja wa Zain.

Kampuni itakayoibuka mshindi katika mashindano hayo itanyakua zawadi ya kombe la Corporate Challenge, zawadi ambayo pia watapata washindi wa pili na tatu. Zawadi nyingine zitatolewa katika kategoria za atakayepiga mpira vizuri kwa umbali mrefu (Longest Drive) na atakayepiga mpira kwa mbali ukakaribia kuingia shimoni (Nearest to the Pin).

Mashindano hayo ya siku moja yanatarajiwa kuanza saa 6:00 mchana na yatachezwa katika mfumo wa mtu mmoja mmoja na pia timu itawakilishwa na wachezaji wawili kwa kila kampuni. Matokeo yatatangazwa wakati wa hafla ya utoaji zawadi itakayofanyika katika viwanja vya TPDF siku hiyo kuanzia saa 1.00 usiku.

Takriban watu 85 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo yatakayochezwa kwa kufuata kanuni za mchezo wa gofu na yatasuhudiwa na Kocha wa timu ya Taifa ya Gofu ya Tanzania, Charles Farrar.

“Itakuwa siku ya furaha, mchuano na burudani, na zawadi zitatolewa katika jingo la klabu ya gofu Lugalo wakati wa hafla ya chakula cha usiku,” alisema Schlittke.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...