Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Classic kipanya hehehehe

    ReplyDelete
  2. Right on the point kp

    ReplyDelete
  3. Ha Ha ha ha haah! Ki-mouse nimekukubali. You've made my day ahsante !

    ReplyDelete
  4. Helikopta ya polisi inapopita level ya chini maeneo ya uswahilini kwa lengo la kuhakikisha usalama inaleta kero kwa wakazi wa kawaida. Hii ni kweli na ni kinyume cha haki za binadamu. Maana mtu aweza kuwa uani anajisetiri ghafla helikopta linapita katika anga za jirani. Je hii ni halali kweli? KP good move!

    ReplyDelete
  5. Helikopta ya polisi inapopita level ya chini maeneo ya uswahilini kwa lengo la kuhakikisha usalama inaleta kero kwa wakazi wa kawaida. Hii ni kweli na ni kinyume cha haki za binadamu. Maana mtu aweza kuwa uani anajisetiri ghafla helikopta linapita katika anga za jirani. Je hii ni halali kweli? KP good move!

    ReplyDelete
  6. Sasa kova afanyeje na vyoo vyenu vya passport size mjielimishe hasa maeneo ya manzese na mwananyamala kisa uchafu

    ReplyDelete
  7. yaani wee acha tu mtu mzima unachunguliwa hata watoto huwa wanapanda kwenye miti sio kova tu anaewakosesha raha

    ReplyDelete
  8. lakini kipanya una vihoja umejuaje watu wameazirika

    ReplyDelete
  9. Kipanya umenimaliza hapo

    ReplyDelete
  10. yani nimecheka sana pia wapika gongo misituni wanalalamika

    ReplyDelete
  11. this is one of da best of KP!

    ReplyDelete
  12. Kweli Kipanya wewe unaijua Jamii ya Dar haswa. hii inanikumbusha hapo Mtoni Mtongani wakati Kanisa katoliki walipotaka kujenga nyumba ya mapadre na ofisi, jengo likiwa na ghoraofa moja; kwanza waliwekewa pingamizi na majirani wao. Kisa, walidai kuwa itakuwa vigumu kwao wakati wa kujisitiri bafuni na chooni, maana watakuwa wanachunguliwa na wakazi wa ghorofani. Pia jengo la ghorafa litapunguza thamani ya nyumba zilizo jirani, kwani wapangaji wengi watakimbia eneo hilo kwa kuogopa kuonwa wakati wanafanya shughukli hiyo muhimu chooni na bafuni. Baba paroko ambaye alikuwa mgeni katika mazingira ya Tanzania na haswa uswahili alipatwa na mstuko, tulipojadili hoja zao za msingi kweli tuliona kuna mambo ya msingi ya kufanyia kazi; Hivyo suala lilifanyiwa kazi na baraza la serikali ya mtaa; uamuzi parokia iliwapatia majirani mabati ya kuezeka sehemu zao hizo Muhimu! Pingamizi kama hili pengine lisingewza kueleweka katik mji wa NYC, ambapo kila ghorofa jipya linalosimmama daima upata kwanza pingamizi, bahati jirani anaweza kuuza "air space" kwa mshiko mzuri. Katika busara ya Biashara ya Airspace ndiyo ilitatua tatizo la jengo la Parokia ya Mtoni kichangani! majirani waliuuza airspce kwa mabati 2 au 3 hivi kila mmoja. Kipanya ika eneo hilo uone. Hivyo kamanda KOVa elewa wakazi wa Dar au wape wapatie mafundisho mazuri Polisi wa kikosi cha Elikopta kuwa kupiga chabo ni kosa la jinai!

    ReplyDelete
  13. Tehe Tehe..
    Haki ya nani vile!

    ReplyDelete
  14. Big up ,Kp gud job,keep on entertaining while educating people!

    ReplyDelete
  15. Tutafakari namna ya kujitoa katika 'vyoo vya stamp-size'. Vyoo vya wazi vinahitaji mabati mawili, 2X2 mbili na misumari ya bati 12 ili kujikinga na mvua, jua na stara ya wapiga chabo.

    Tunahitaji maisha bora tulioahidiwa katika kampeni za JK.

    Pamoja na umaskini wetu, tunahitaji kukabili hali hii hata kwa michango, sadaka, zaka na msaragambo.

    Mshikamano: chumba kwa chumba, nyumba kwa nyumba, mtaa kwa mtaa nk. Tusisubiri fedha za EPA, Meremeta, Kiwira kwani hatutaziona.

    Hata kodi zinazokusanywa na TRA zitaenda kwenye MMEM, mikopo kwa wanafunzi, allowance za walimu, mkono wa kwa heri kwa wastaafu wa EAC na wahanga wa VVU.

    Maisha bora yapo mikononi mwetu, tusaidaiane.

    ReplyDelete
  16. Hahahahhaaa teh tehehehee!! Hakika KP umenifanya nimalize mwaka huu kwa tabasamu na kukumbuka sana nyumbani. Hapa tatizo sio uchumi, ila ni ukosefu wa elimu ya afya, hakika nimemkumbuka sana Banza Stone aliposema kama unadhani "Elimu ni ghali, basi jaribu Ujinga". Nakumbuka kijijini nilikotoka Wazee walikuwa wanajificha wasikamatwe kwenye msako wa Maafisa wa Afya kwa kutokujenga na kutumia choo. Tanzania safari bado ni ndefuuu, lakini tutafika tu msihofu.
    Tuwekeze katika elimu vya kutosha mambo yawe mswanozzz

    Teheheeeee, hahahahahaaaa
    Mdau Oslo, Norway

    ReplyDelete
  17. tetetetehhh hii funga mwaka haswa.

    Pitisheni nyingi tu ili watu wajue kujenga mabafu mazuri sio kila siku kujenga vijitu vya kujisetiri setiri tu. Kama unaweza kuweka kuta nne nadhani hata juu unaweza kutafuta makuti na kumaliza kazi ya kuweka juu.

    Tatizo letu sio umasikini ni uvivu, lack of creativity na tunaridhika kirahisi sana.

    ReplyDelete
  18. Zote kali. Ila Hii kali kabisa.

    ReplyDelete
  19. hahahaahahaha euwiiiiiiiiiii , lol KP hapo umenimaliza, hili la kufunga mwaka, wapi watu wa mwananyamala na manzese na vitongoji vyake!!!!!!

    ReplyDelete
  20. hhahhah! big up kipanya u real made my day! hii kali kinoma ya funga mwaka. nimekukubali kp.

    ReplyDelete
  21. Naungana nawe anon wa dec 31, 12:41 kweli ni wengi ni uvivu tu si umaskini wa kiasi hicho na kukosa ubunifu hata nyasi utakuta hicho choo chenyewe kimezungukwa na nyasi kubwa na ndogo basi hata mtu kuchukua hata siku moja kukata hizo nyasi nakuzitumia kama paa anashindwa, nakumbuka kipindi niko mdogo sana tulienda likizo kumtembelea shangazi yangu kijijini , tukakuta kadhia hiyo ya choo ukiingia badala ya kupata pumziko au burdani unapata udhia wa jua linakutandika kisawasawa na huku unahofia kupigwa chabo kwani matundu kwenye, mzee wangu aliiona hiyo, hakulalamika alitoka kimya kimya na kuanza kurekebisha choo yote kukandika na kuezeka na nyasi pakawa na stara na kila mtu alitoa pongezi.

    Viva kipanya umenichekesha hadi machozi.

    ReplyDelete
  22. aha aha ahaaaaaaa mbavu zinaniuma kwa kucheka, kipanya we sikuwezi haya ni maisha ya kweli kabisa yapo hapa uswazi kwetu, tatizo nawaza hivi, ndo umeshikwa na tumbo la nanihii alafu inakubidi kila dakika unatoka na ukitoka unakutana na hiyo hedikopta, na wao wanahisi kunaishu wanazidi kuganda hewani yaani sipati picha.

    ReplyDelete
  23. KIPANYA SAWA KAZI NI NZURI, LAKINI SUALA LA DOLIA KWA RAIA NI MUHIMU KWANI MUKIIBIWA MANASEMA OOHH POLISI WETU HAWAFANYI KAZI,

    VYOO VYOTE VINATAKIWA VIEZEKWE HIYO NI LAZIMA NA ITASAIDIA HATA KUPUNGUZA HATA KIPINDUPINDU WAKATI WA MVUA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...