Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe akitangaza matokeo hayo

Asilimia 80.73 ya wanafunzi 433,260 waliofaulu darasa la saba wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza katika shule za serikali ambapo wasichana ni 188,460 sawa na asilimia 82.13 na wavulana 244,800 sawa na asilimia 79.69 .

Akitangaza matokeo hayo leo mchana kwa waandishi wa habari, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe (pichani) alisema kuwa kati ya wanafunzi wote 1,017,967 sawa na asilimia 97.51 ya walioandikishwa walifanya mtihani huo mwaka huu na wanafunzi 536,672 sawa na asilimia 52.73 wamefaulu.

Katika matokeo hayo ambayo yataanza kutangazwa na kila mkoa kesho, wavulana walifanya vizuri zaidi ambapo walikuwa 307,196 sawa na asilimia 59.75 huku wasichana waliofaulu ni 229,476 sawa na asilimia 45.55.

Aliitaja mikoa iliyofanya vibaya na kiwango cha ufaulu kwa asilimia kwenye mabano ni Shinyanga(34), Lindi(40.7), Mara(42.6) na Tabora asilimia 43.2.Kwa Mikoa iliyofanya vizuri ni Dar es Salaam(73.9), Arusha(69.2), Iringa(64.1) na Kagera 63.5.

Kwa upande wa wanafunzi waliobainika kufanya udanganyifu alisema “watahiniwa 102 wamefutiwa mitihani wakiwemo wasichana 41 na wavulana 61”.

Akifafanua juu ya ufaulu wa masomo ya Hisabati na Kiingereza ambayo kwa miaka miwili mfululizo umekuwa wa chini, Profesa Maghembe alisema kuwa Hisabati ni asilimia 18.07 huku Kiingereza ni asilimia 31.5

Ameongeza: “matokeo ya Kiingereza ni sawa na mwaka jana na Hisabati mwaka jana ni asilimia 18.72, tumeweka mikakati ya kuboresha masomo hayo ikiwemo vyuo vyote vya ualimu kutoa nyenzo kwa wanafunzi wa ualimu kuweza kufundisha masomo hayo, kuwapa mafunzo walimu waliopo na tunatoa wito kwa wanafunzi wasiyaogope masomo haya”.

Ufaulu wa masomo mengine na kiwango katika asilimia ni Kiswahili(73.4), Sayansi(68.24) na Maarifa(61.03).
Waziri Maghembe alisema kati ya wanafunzi 346 wenye ulemavu waliofanya mtihani huo, wanafunzi 221 sawa na asilimia 64 ya watahiniwa wamefaulu na wote wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. WAALIMU WAO WENYEWE WALIFELI HATA FORM FOUR (FIV) WE UNATEGEMEA NINI?

    ReplyDelete
  2. Wataalam wa HAKIELIMU Tusaidieni kutathmini taarifa ya matokeo y mtihani huu. Ni vipi tunaweza ku kabili kudorora kwa elimu ya hisabati na hiyo lugha ya Kingereza?

    ReplyDelete
  3. Ndo matokeo ya kutumia walimu wa UPE (Ualimu Pasipo Elimu)....kama kawaida yetu tunajali wingi na si ubora!

    ReplyDelete
  4. Inasikitisha. Lakini sijui ndo tumeshazoea?

    kwanza kabisa wadau hizo asilimia za kufaulu mbona hazijumlishiki?

    "wavulana walifanya vizuri zaidi ambapo walikuwa 307,196 sawa na asilimia 59.75 huku wasichana waliofaulu ni 229,476 sawa na asilimia 45.55." - Jumla hapa ni 105.3%, inakuwaje?

    Pili reaction ya serikali inanitia huzuni. Ni ile ile ya kila mwaka. Nyenzo kwa walimu-wanafunzi, sna kuwaasa watoto wasiogope hayo masomo!!! Reaction hii ina miaka mi4 sasa, bado mambo ni yale yale, serikali inafanya nini?

    Arhg!

    ReplyDelete
  5. SI HISABATI NA KIINGEREZA TU, BALI HATA KISWAHILI PIA HAKINA MATOKEO MAZURI! HII NI AIBU KWA TAIFA.

    ReplyDelete
  6. KAma mimi ningekuwa Prof Majembe ningestep down...mfumo wa elimu ni mbovu kuanzia msingi mpaka huko juu...harafu tunatarajia viongozi waadilifu na wabunifu....tusahau.

    ReplyDelete
  7. Serikali inapof*ck elimu ya msingi inategemea nini huko mbeleni.Somo la kilimo bado lipo mashuleni?Vitabu vya JUMA NA ROSA JE?DAMASI NA LUSI(LUCY)?bado vipo?

    ReplyDelete
  8. Hii itaendelea kusababisha wanafnzi wa wamaskini kuendelea kutawaliwa na watoto wa vigogo wasomao ktk shule nzuri sana nje ambapo walimu wanalipwa vizuri na shule zina mandhari bora ya kujisomea... La msingi tu ni kuboresha shule zilizopo na kuondoa kero na migomo ya walimu isiyo na sababu.. Walimu watajituma zaidi na results zitaonekana tu..
    Takribani wote waliochaguliwa kujiunga ni kuishia kumaliza kdato cha 4 ktk shule za kata..na FFFFFFF. Msemaovyo.

    ReplyDelete
  9. mkandamizaji unaonekana wewe pia ulifeli hesabu au ni mwalimu wa upe. hizo asilimia ni kwa watahiniwa wote ktk hiyo category na sio jumla. kwa maana kwamba 59.75 ya wavulana wote na sio watahiniwa wote n.k.

    ReplyDelete
  10. Udhaifu wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) ulionza mwaka 2002 umeendelea kuonekana baada ya nusu ya wanafunzi waliofanya mitihani ya kumaliza darasa la saba mwaka huu kufeli.

    Kati ya wanafunzi 1,017,967 waliofanya mitihani ni wanafunzi 536,672 tu sawa na asilimia 52.73 waliofaulu, wakiwemo wasichana 229,476 sawa na asilimia 45.55 ya wasichana waliofanya mtihani na wavulana 307,196 ambao ni sawa na asilimia 59.75 ya wavulana waliofanya mtihani.

    Matokeo haya ni kipimo cha pili cha MMEM baada karibu nusu ya wahitimu wa kwanza toka mpango huo uzinduliwe kufanya vibaya kwenye mtihani wa darasa la saba.


    Katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana, ni asilimia 54.18 ya wanafunzi 773,550 watainiwa waliofanya mtihani wa darasa la saba waliofaulu, hivyo mwaka huu kiwango cha ufaulu kimezidi kushuka kwa kuangalia asilimia.


    Katika matokeo ya mwaka huu, Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kitaifa kwa kufaulisha asilimia 73.9, ikifuatiwa na Arusha, Iringa na Kagera.

    ReplyDelete
  11. Dar-es-salaam Shule nyingi kwasababu pengine ila Lindi lazima wajitahidi na Mara hata nimetizama sehemu yani hata kisarawe wamejitahidi sana tena si kidogo wanaanza kwenda shule kisarawe ilikuwa chini sana, ni sehemu ambaayo ilikuwa chini mno, ila ikitowa wasomi ni wakubwa safarihii wamejitahidi.

    Serikali lazima waisaidie na Mara na Lindi pia kama ilivyokuwa kisarawe Tabora ni maajabu si kawaida ku fail tabora kuna tatizo watizame pia. Dar-es-salaam na Arusha shule nyingi miji mikubwa walimu wenye juhudi ndio wapo hapo ile mikoa midogo wanakataa kukaa lazima wajengewe nyumba wakae wawasomeshe wanafunzi sehemu kama Mara na Lindi. Mpaka sasa siwezi amini Lindi na Mara inapitwa na KIsarawe.

    ReplyDelete
  12. je ni website gani naweza kuona hayo matokeo?

    ReplyDelete
  13. Wtoto wa watu wamejitahidi kadri ya uwezo wao. Walimu hawalipwi mishara na muda wote wanatumia kufanya miradi yao ili waweze kuishi. Sasa serikali inategemea nini? Nani wa kulaumiwa?

    Halafu cha aibu ni kumasema matokeo ya .......ni "kama mwaka jana" ouch!!!!! Kwa hiyo mwaka jana hamkulearn chochote au it is okay hiyo asilimia waliyopata.

    Bila msingi bora wala huko juu hakutakalika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...