madhara ya moto uliochoma hoteli za paradise resort na oceanic bay mjini bagamoyo leo
wasamaria hoi baada ya kusaidia sana kuzima moto kwa mikono
kila kitu kwishney
oceanic bay nako jivu tupu
njia kuelekea kuliko na hoteli hizo
mabaki ya oceanic bay

wadau kama kawa
wapangaji wakijiorodhesha
faya likiwasili toka dar

shangingi meng'emeng'e...

askari wa faya akizima majivu
fiat likiwa hoi kwa moto getini oceanic bay

faya likiwasili wakati kila kitu kwishnehi
mdau akiwajibika
mfanyakazi wa paradise resort akiokoa masalia. imeelezwa na wamiliki wa paradise na oceanic bay kwamba jumla ya wafanyakazi 380 watakuwa hawana kazi baada ya janga hili

video ya matokeo ya moto huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

 1. Mungu kasaidia hakuna aliyeumie hicho ndio muhimu. Ila TANZANIA lazima tutizame tunavyojenga vitu vya makuti lazima na vyombo vya zima moto visiwe mbali sana Hii itafanya watalii wapunguwe. Tanzania tujitahidi vitu kama hivyo nilitakak usema labda moto umeanzishwa kwa kusudi ila sioni dalili hizo. John.

  ReplyDelete
 2. hihihiiiii faya ikizima majivu hahahaaaaa

  ReplyDelete
 3. Maskini Mahad(Owner) namuonea huruma sana kwani hoteli ilikuwa inafanya vizuri mno. Nilikuwa pale mwaka jana. Na pia nina booking ya mwezi wa tano nikija tanzania, imebaki history, ila i hope ana insurance so those things can be paid back. Anyway ndio maisha. Ila inasikitisha sana.

  Mdau Ned!!

  ReplyDelete
 4. Jamani poleni sana waathirika wa huu moto,cha kusikitisha yaani magari ya zima moto yatoka Dar kwenda Bagamoyo hii ni aibu sana kwa serikali,wahusika jamani waangalie hili,wajenge kituo cha fire.So sad tulikuwa tunapenda sana kwenda Paradise on the weekends.

  ReplyDelete
 5. Asante kwa taswira Kaka. Na kisha pole kwa wahanga.
  Lakini swali hapa ni kuwa kwanini hawa wanaoopewa punguzo la kodi ama ofa za kuanzisha ama kuwekeza wasiwekewe masharti ya kuwa na vitendea kazi vya uokozi yatokeapo majanga? Yaani kama gari la kuzima moto hoteli ya kitalii iliyo Bagamoyo linatoka Dar (na ninavyojua namna yanavyovuja sijui kama yalifika na maji huko) ina maana mtu amekubaliwa kuwekeza katika biashara inayohusu maisha ya watu na hana namna yoyote ya kukabiliana na majanga kama moto. Nadhani kunahitajika umakini zaidi katika hili. Sio tu yeye mwenye kumiliki, bali hata halmashauri ama mji ama jiji alilowekeza halina kikosi cha zimamoto kuweza kukabili hoteli ambayo inalipa kodi (ama niseme inastahili kulipa kodi) kwa serikali?
  Hapa si mali za mmiliki, bali maisha ya wengi ambao wanatembelea na kulala humo. Maisha na mali zao zinateketea kwa kuwa tu fulani hakufuata taratibu ama hakufuatilia taratibu za kumkinga "mlaji" ambaye anastahili kuwa na hakika ya usalama wake katika matukio kama haya.
  NI AIBU KWA KWELI
  Blessings

  ReplyDelete
 6. kila kitu kina faida na hasara. hata hivyo baada ya kupata utamu wa biashara hiyo ,sasa nafikiri watawekeza katika hoteli za kudumu,kuliko za aina hiyo amabzo hazina hadhi, kwani kwa picha tu inaonesha kuwa majengo kama vile yalijengwa kwa makuti tu,ambayo ndo ilikuwa hali halisi. poleni wamiliki na wapangaji,bila kusahau wafanyakazi.

  ReplyDelete
 7. kha jamani hivi sisi tumelaaniwa yaani kweli gari la zima moto litoke dar kweli mpaka bagamoyo,hawa wabunge ,wakuu wa wilaya na wakurugenzi hata mwenye hotel wanafikiria nini mi naona akipewa kibano mmoja hadi afe ndio watawajibika.

  ReplyDelete
 8. Mdau wa 7:47 sikuelewi unavyosema wajenge hoteli zenye hadhi, kwa ufupi hiyo hoteli ilikuwa na hadhi hasa, na pia makuti yalikuwa yemeezekwa juu tu. Haimaanishi hoteli kuwa na makuti haina hadhi, hapo walichokuwa wanajaribu kukionyesha ni kuwa na uasili flani wa kitanzania. So kuwa na vigae au whatever u think ndio hadhi kwa upande wako, umechemsha. Hoteli ilikuwa na standard inayotakiwa au kwasababu hujafika na umesikia ni bagamoyo? tembea uone ndugu yangu sio kuandika vitu visivyoeleweka.

  Mimi nimelala pale na hakuna tofauti yoyote na mahoteli ya hadhi ndani na nje ya tanzania.

  Ni hayo tu

  Mdau Netherlands

  ReplyDelete
 9. Dah ndugu zangu wa oceanic bay poleni sana na jirani zetu Paradise pia polen sana!!
  Muhmin sijui yuko kwenye hali gani huko aliko!!!

  ReplyDelete
 10. Wakati umefika watanzania Tuamke!

  Tangulini ukazima moto kama huo namaji ya bomba kwenye ndoo!!##$$#@$??????

  Amkeeeeni??????

  Maji yana Oxygen,hapo hyo jamaa afanyi kitu sanasana anaongeza tu!

  Tangu lini gari lazimamoto likatoka Dar kwenda kuzima moto bagamoyo, hivi hawa wausika huko serikalini wanafikiria kweli? mimi naanza kua mini usemi wawazugu kwamaba waafrika wanamapungufu fulani kwenye akilizao, na ndo maana wazungu wataendelea kutu tawala tu,

  SASA KAMA HUU SI UJINGA NININI?
  NIMEONA HAPO LUKUVI ANAENDA KUZINDUA MIUNDOMBINU YA MAJITAKA, AMBAYO NIWAZUNGU WAME TOA HELA! SASA KAMA WAZUNGU WANAFIKA HATUA YA KUKUJENGEA CHOO WEWE MTANZANIA UNDHANI NINI KINAFUTA OHOOOOO SHAULIZENU! MISIMO!WATANZANIA AMKENI?

  ReplyDelete
 11. anon 23, 7:45.
  kama hujafika paradise, nyamaza!
  hapo ushaambiwa kuwa kila kitu "kwishney", ulitaka uone hadhi gani tena?
  kumbuka hizo nyumba za makuti ndizo walokulia babu na baba zako na wakaishi kwa furaha na wakiheshimika kama sasa waziona hazina hadhi!

  ReplyDelete
 12. hoyeeeeeeeee...
  si hoyeee ya moto ila ni shangwe ya kupata mwekezaji wa umeme wa upepo
  kampuni ya akina nani yapiga baoooo!!

  bro misupu soma mwenyewe afu wape wadau wa jamvi!!
  http://www.bloomberg.com/apps/news?pid=20601116&sid=asaM3zg.jdvk&refer=africa

  ReplyDelete
 13. Poleni sana wawezekaji.

  But........

  No tourists, canceled bookings, increased competition from Mombasa, Zanzibar etc, a possible reluctance to "invest" on local tourism because it will mean a reduction of prices even up to half or more, and many more reasons. You got 380 employees, overhead is kicking your butt, PM Pinda is trying to put a stop to the "local tourist workshops", global credit crunch etc etc etc then why the hell not put a flame to the ever-dry makuti?

  Burn, baby burn!!!

  Ok, ok, ok, I may be a little harsh but deep in the minds of many, (I know in my mind) insurance fraud idea is lurking up in there. Hopefully they are insured.

  Well, just thinking aloud.......

  ReplyDelete
 14. MUNGU UTUSAIDIE TU...FIRE TOKA DAR????? NI MASAA MANGAPI ILITUMIA KUFIKA HUKO...HIZI DEVELOPMENT TUNAZOZIFANYA BILA KUFIKIRI....WATU WANAINVERST MABILLION BILA KUFIKIRI...KAMA SERIKALI HAISAIDII KATIKA KUANYISHA NA KUJENGA VITUO HIVYO KWANINI WANAOJIJENGEA MAJUMBA NA MAHOTELI WASIJIKAMUAE WAKAJENGA PRIVATE FIRE STATION ZAO.....KAMA THEY COULD AFFORD ALL THAT MONEY ...NAJUA WAKICHIP IN WATAWEZA KUWA NA KITU CHA KUPUNGUZA PRESSURE ZAO.....SIO KUNGOJA GARI LA FIRE KUTOKA DAR

  ReplyDelete
 15. LABDA HUYU MDAU WA 7:47 ANGEELEKEZA MAELEKEZO YAKE KATIKA SUALA ZIMA LA USALAMA-KWA KIMOMBO HEALTH AND SAFETY, NA SI HADHI.
  HUKU KWA WENZETU WA DUNIA YA KWANZA KILA PENYE MKUSANYIKO WA WATU KITU CHA MWANZO KUZINGATIWA NI USALAMA NA AFYA ZAO. HIYO INAKUSANYA KILA KITU KUANZIA HUDUMA, HADHI, MAZINGIRA NA KILA KINACHOHUSIKA.
  KWA HUKU KWA WENZETU KWA MFANO, USIHANGAIKE KUDAI BIMA KIWANDA CHAKO KINAPOSHIKA MOTO ENDAPO HUKUTIMIZA KWANZA MASHARTI YA USALAMA WA WAFANYAKAZI, WATEJA NA MALI. HUWEZI HUKU KUKUTA KIWANDA, OFISI AU HOTELI IMEJENGWA BILA YA KUWEPO VIFAA NA HUDUMA ZA ZIMAMOTO ZA KUAMINIKA. WENZETU HUKU WANAAMINI KATIKA "KINGA NI BORA KULIKO KUPONYA". KINYUME CHAKE, SISI HUKO TUNAISHI ETI KWA REHEMA YA MUNGU, MAANA AJALI IWE NDOGO AU KUBWA ITAACHA MAAFA YASIYOSEMEKA.
  LAWAMA WASITUPIWE WAKUU WA WILAYA, WABUNGE AU MAWAZIRI. HUO NI UPUUZI. WATU WAWE NA MENTALITY!! NA HILO NDILO GUMU MNO KULIFIKIA.INABIDI KAZI YA KUELIMISHANA IFANYIKE HASA.
  BAADA YA MIAKA 10 TU YA KUISHI NJE, NILIPOKUJA LIKIZO TZ JULAI ILIYOPITA, KILIKUWA KIZUNGUZUNGU KITUPU, MAISHA YA NYUMBANI NI ROHO MKONONI, WACHACHE MNO WANAOJALI NA KUTHAMINI SI TU MAISHA YA WENGINE, BALI HATA YAO BINAFSI. MAJANGA KAMA HAYA YATAENDELEA KUTEKETEZA MALI NA HATA MAISHA BINAFSI MPAKA PALE TUTAPOKUBALI KUBADILIKA NA KUACHA TABIA YA KUTUPIA VIONGOZI LAWAMA. ILA PIA KWA WABUNGE WETU, WAJITAHIDI KUSOMA KUTOKA KWA WENZETU WALIOENDELEA, NA BUNGE LIPITISHE MISWADA YENYE LENGO LA KUNUSURU ROHO NA MALI ZA RAIA.
  NAJIULIZA KWANINI KUWE NA HOTELI KUBWA KAMA HII ILIYOTEKETEA KABLA YA KWANZA KUWEPO NA HUDUMA ZA KUAMINIKA ZA ZIMAMOTO. I WAPI HEALTH AND SAFETY HAPA!
  Mndengereko, Ukerewe

  ReplyDelete
 16. Kama kuna aliyekuwa ameenda kusaliti nanihii haki ya mungu harudii tena wallah ila sijui utadanganya nini kama gari limebabuka na moto. Pole zao wote waliokuwepo na wenye hoteli moto sio experience nzuri. Ila serikali inabidi iweke huduma muhimu kila mahali sasa hii ni hatari siajabu hata kigamboni fire lazima itoke dar

  ReplyDelete
 17. Duh hatari kweli,askari wa zimamoto kavaa kama anaenda disko

  ReplyDelete
 18. hahaha...anon wa March 23, 2009 11:49 PM umenivunja mbavu. Na ni kweli kabisa. hii ni hatari. Sasa hapo ni kula na insurance company, alafu nayo ile na faya na serikali. Hapa yani vichwa lazima viliwe town/city council. Sio kazi ya hotel ku-provide infastructure, ni kazi ya serikali. Sasa kama unataka kuendelea bila kujenga infastructure, itawezekana kweli? Lakini ndo tunajifunza sasa. Acha JK apige kelele tena na kusema lazima tufanye hivi na vile. Hiyo ndo imekuwa kazi yake tu...kutoa maagizo bila utekelezaji.

  mtoto

  ReplyDelete
 19. Ama kweli bongo ni tambarrrarrre... ha ha ha

  Nilishangaa sana waziri wa zamani Mramba aliposisitiza kwamba hata kama watanzania watakula nyasi ndege ya mkapa itanunuliwa tu. Mwishowe ndege ikanunuliwa na kuishia kutengeneza skendo ya first class.

  Kama ndege ya mkapa isingenunuliwa huyo ndugu Mkapa angeweza kutumia usafiri mwingine tu, maana tumeona hata Waziri mkuu wa Uingereza akisafiri nje akitumia British Airways, na akisafiri na wateja wengine kwenye ndege hizo. Kwa uwezo mdogo wa kufikiri wa viongozi wetu na kushindwa kugundua priorities dhidi ya raia wanaowaongoza, na kuweka mbele maslahi ya matumbo yao (10 percent) ndipo tunaishia hapa tulipo. Tanzania yetu miaka 40 baada ya uhuru bado tunapiga steps kurudi nyuma badala ya kwenda mbele.

  Tukirudi kwenye suala la moto. Hii ni aibu sana kwa serikali yetu. Msimtupie mpira huyu mwekezaji kwamba kwa kuwa ameweza invest mamilioni kwenye hoteli hiyo basi angewajibika kuweka na fire station pale karibia na hoteli yake... Hii ndio mitizamo ambayo imetufanya watz tuendelea kuwa masikini wa kutupwa leo hii miaka 40 after independence. Tusijaribu kukwepa the reality na kuanza kuwa wazembe wa kufikiri.... Lets ask ourselves... Hivi serikali imepokea kiasi gani cha pesa kama kodi kutoka kwa wawekezaji kama huyu jamaa? Je, serikali imezitumiaje hizo pesa kumtengenezea mazingira mazuri huyu mwekezaji aliyelipa mamilioni kadhaa kama kodi kwa serikali hiyo? Unajua huyu mwekezaji ana kesi nzuri sana hapa... He can sue the municipality for not responding to this simple disaster. I know kuna watu watabisha, ila ukweli ni kwamba wewe kama mlipa kodi una haki ya kutimiziwa basic needs na yule unayemlipa kodi, yaani serikali. Ndugu mwekezaji, tafuta lawyer wa kueleweka (sio wale wanaopigana disco) halafu sue the municipality. This will be a very straightforward litigation proceeding, I tell you... The government has to pay for this. Hatuwezi endelea kulipa kodi halafu pesa zinaishia kwenye kampeni.

  On top of that, ukiangalia suala hili na masuala meeengi yanayotokea nchini kwetu utagundua kwamba matatizo yote haya ni ya kujitakia wenyewe. Kama mawaziri wetu na timu nzima ya bajeti ingekuwa makini na wangekuwa wanajua wanachokifanya, basi TZ yetu ingekua mbali sana kimaendeleo. Gari la kuzima moto kutolewa Dar kwenda Bagamoyo kuzima moto ni matunda ya maamuzi mabovu ya mawaziri wetu, ambao kwa mfano waliona ni bora kununua ndege ya rais wakati gharama hiyo ingeweza kununua mazima moto kadhaa ama kununua ambulance kwa kila wilaya ya Tanzania yetu. Shame on those involved in maamuzi yasiyo na mielekeo.

  Ama kweli bongo ni tambarare... Duh!!!

  ReplyDelete
 20. hii inamaanisha kwamba maisha ya raia wa bongo sio kitu muhimu

  ReplyDelete
 21. Kweli bongo Tambararez!

  ReplyDelete
 22. I don’t think there would be any conspiracy here, but it remains to be seen what has caused this fire. Of course accidents do happen, but we shouldn’t rule out a ‘malicious act’ here!

  Whilst my thoughts are with those ‘bread winners’ who have to face a gloomy future on how they’re going to make their ends meet especially during this time of credit crunch, I feel sorry for owners of these hotels for 'lost business'.

  I know, they took some good years to build such investments but it’s out of any one prediction on to how long they’re going take to rebuild them. I hope, it's not going to take too long as nearly 400 people need to get back to work [in these hotels] as soon as it takes.

  Bagamoyo is my place (born and bred!), so whichever bad thing happens there, it really hurts me. Of course, there is one consolation comes along with this bad news; so, far, NO life has been lost because of this fire!


  But we should put record straight that ‘Bagamoyo, just like anywhere in the country needs fire-brigade’, not only to rescue tourist resorts like these, which are now imaging like mushrooms, but to save lifes of people of Bagamoyo in case of fire etc.

  It’s time to observe ‘health and safety’ issues to avoid more serious catastrophe!

  Jua Kali

  ReplyDelete
 23. Pole sana owner na my friend ELIZABETH KIBONA plus wafanyakazi wote kwa kupoteza ajira,Eliza ukiona maisha yanabana jirudie zako Ufaransa.

  ReplyDelete
 24. he he he he he! Nachekaa! Wabongo bwana wanafiki..Leo sababu tatizo kama hilo limejitokeza basi kila mmoja atasema nyumba za makuti hazifai...Mkumbuke pia kuwa hizo nyumba za makuti ndizo zilizokuwa zinaleta kivutio na kuweka mandhari nzuri ya hoteli ile.. hebu angalieni kabla haijaungua ile hoteli ilivyokuwa inavutia..inaonyesha uasili wa Mwafrika. Kitu chochote kilichojengwa kwa asili fulani ya Mwafrika kinavutia.. Mnasema hiyo hoteli hamufikirii kijiji chenu cha Makumbusho kikiungua leo hiyo hoteli makuti yake ndio yamekuwa gumzo tuu. Angalieni kijiji cha Maisha plus kinavyovutia pia. Pale wazungu wakiona vile ndio kivutio kikubwa...Kikubwa tujue tu ajali tu imetaka kutokea tu.. kwani hizo nyumba ambazo sio za makuti mbona zinaunguaga vile vile na kila kitu kinateketea? Chamsingi ni tuimarishe vyombo vya kuzuia majanga kama hayo kila mkoa bila kubagua, wilaya hata ikiwezekana kijiji Mfano Bagamoyo naamini wangekuwa na gari karibu mfano Palm beach hotel wangeweza kutuliza moto huo kwa haraka angalau...Huwa viongozi wetu wanaangaliaga mijini hawakumbuki vijijini kama huko..

  Pia Tanesco (watendaji) wanatakiwa wawe makini katika utendaji wao wa kazi kwani pia wao wamekuwa ni vyanzo vikubwa vya majanga nchini. Wanarudisha maendeleo nyuma sana.

  Hakika mimi navutiwa sana kuishi katika nyumba kama zile na kuishi maisha kama yale..Utamu kweli kweli.

  Mmang'ati Original.

  ReplyDelete
 25. ooh my God .........my beloved places kwishiiiiiiiiiiiiii. hope nobody died

  mdau netherlands

  ReplyDelete
 26. Nyie baadhi ya watanzania mnaniudhi sana ndio mnaosababishaga maujinga yanatokea katika nchi yetu then likitokea janga ndio mnachoonga kumbe hakuna lolote akilini mwenu. Najua baadhi yenu nyie mngepata chance au fedha ya kujenga hoteli huko bagamoyo mngeweza kuiga hivyo hivyo...Pumbavu zenu…Mnalalamikia hoteli hamjifikirii majumba yenu mnayoyajenga katikati ya miji inabanana hata njia ya kupita gari la zimamoto, mnachonga kuhusu hoteli.. Imarisheni pia miji yenu hebu angalia msasani Mabondeni, hebu angalia nyumba Mkwajuni zimebanana ni uchochoro tuu wa kupita. Je hapo moto ukitokea na nyumba zingine ni mbavu za mbwa itakuwaje? Wangapi watapoteza makazi? Wangapi wataanza kulalamikia serikali licha ya nyie wenyewe ndio mlio jenga hakuna aliyewatuma? Mungu asaidie tu moto usijitokeze sehemu kama hizo mtalia wengi... Hebu acheni unafiki msimnyooshee kidole mwenzenu au serikali tuu jinyoosheeni na nyie wenyewe kwanza. Jifikirieni mnapojenga kitu.. Hata mnaojenga mabondeni fikirieni mafuriko kwani ajali sio moto tuu..

  Mmang'ati Original

  ReplyDelete
 27. Duh Pole yale mmliki lakini ana insurance kwa hiyo sio big issue sana,
  jamani sehemu ya kubonywezwa kizenji na kibara ndo hivyo tena, tutatafuta sehemu nyingine baba naniniiiiiiii, mnaka nitaje alafu iweje ushahidi sitaki, alafu huyo mwenye gari nae kama ilikuwa kimeo imekula kwake,
  Alafu wadau wa netherland inaonekana ndo wanalalaga sana hapo comment zote sijaona wakerewe wala wapi, au nyie hamrudigi kwenu nini,
  ni hayo tu

  ReplyDelete
 28. POLE KWA JANGA.USHAURI WA BURE KWA WAWEKEZAJI WENGINE WA NAMNA HII.NUNUENI PAMPU ZA MAJI ILI KABLA MAGARI YA ZIMA MOTO HAYAJAFIKA ANGALAU MUANZE KWA KUTUMIA MAJI YALIYOMO KWENYE SWIMING POOL AU HATA YA BAHARI...

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...