JK akiangali baadhi ya vipande na mabaki ya mabomu vilivyookotwa katika makazi ya watu wanaoishi karibu na kambi ya Jeshi la wananchi Mbagala jijini Dar ambapo nyumba kadhaa ziliharibiwa vibaya na kwa mujibu wa taarifa ya polisi  watu sita kupoteza maisha na 236 kujeruhiwa wakati ajali ilipotokea katika ghala la kuhifadhia silala za kivita katika kambi hiyo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa usalama na utambuzi Jeshini Brigedia Jenerali Paul Meela,Naibu Waziri wa Ulinzi na jeshi la kijenga Taifa Emanuel Nchimbi,Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Said Mwema.
JK akimpa pole mtoto Mariam Isihaka(8) aliyelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Temeke baada ya kuathirika kwa mshtuko kutokana na ajali iliyotokea katika ghala la kuhifadhi silaha katika kambi ya jeshi huko Mbagala jijini Dar jana mchana.Pembeni aliyeketi na Mtoto Miriam ni mama yake Husna Selemani mkazi wa Mtoni Mtongani, jijini Dar
Madaktari Bingwa katika Taasisi ya Mifupa ya Moi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbil(kulia) wakimpa  JK (shoto aliyevaa mavazi maalum) maelezo ya mgonjwa aliyejeruhiwa vibaya na moja ya mabomu yaliyolipuka katika ajali iliyotokea katika ghala la kuhifadhia dhana za kivita katika kambi ya jeshi la Wananchi wa Tanzania huko Mbagala, jijinji Dar es Salaam.Mgonjwa huyo amepoteza mguu wa kulia na amepoteza damu nyingi na napumua kwa kutumia mashine maalum (Life Supporting machine ). JK  alirejea jijini Dar es Salaam leo akitokea mjini Arusha ambapo alihudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulimalizika jana jioni na kwenda huko moja kwa moja
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein  akipata Maelezo toka kwa Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania Brigedia  Jenerali  F N Ulomi  Wakati alipotembelea Kambi ya Jeshi hilo eneo la Mbagala ambapo milipuko ya mabomu ilitokea jana na kusababisha madhara makubwa ya mali na watu.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akimfariji mtoto Thabit Abdallah aliyelazwa katika Hospitali ya Temeke, mmoja wa majeruhi wa ajali ya mabomu yaliyolipuka katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania eneo la Mbagala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Mwenyezimungu atawapa Uzima inshallah! Watanzania tujaribu kuelimishana muda kama huu, kwa kila makosa na bahati mbaya zinazotokea Kwenye TV. Kama ukitokea jambo tunapoambiwa tuwe mbali na eneo la Hatari tusitake kusogelea tusikilize, Mambo ya Usafi wa Jiji, Tufanye nini kukitokea matatizo kama hayo. Kuliko kutumia muda mwingi kuonesha Bongo Flava peke yake na Kilimanjaro Award na Miss Tanzania.

    Elimu ya Kuonesha Matokeo na tuyakabili vipi ni muhimu Tanzania itatusaidia watu wengi, Kama zile ajali anaotuwekea michuzi kwenye Blog Matu baada kuwa mbali Gari la mafuta wao ndio wanazidi kulisogelea. Inshallah mwenyezimungu atatunusuru na mabalaa mengine. Pazi.

    ReplyDelete
  2. Muda mfupi tu uliopita nimetoka kumwambia rafiki yangu kwamba tutaona picha ya Rais kamshika mtoto hospitali. Piccha nyingine itakuwa ya Rais akiwa katika maeneo ya tukio huku katinga suti na shati lake la drafti (hapo nilikosea). Akiambatana na mawaziri wa wizara husika na wanajeshi. Nilimwambia hii ziara itakuwa photocopy ya ile ziara aliyofanya Mererani.

    Kitu kingine nilichomwambia rafiki yangu katika habari nzima hututaona makambi ya dharura ya waathirika wa mabomu haya. Pia hatutasikia takwimu kamili za idadi ya watu waliokufa na kujeruhiwa na mabomu. Hasara za mali (majumba/majengo na vilivyokuwemo majumbani/majengoni humo, mashamba na mazao ya mashambani humo, magari na mali zingine zilizosababishwa na mlipuko mabomu hayo pamoja na athari za mabomu hayo kwa mazingira. Halafu ikiwa kama waathirika wa mabomu haya watapata fidia za hasara walizozipata kutokana na milipuko hii kama kufiwa, kubomokewa majumba na kuharibikiwa mali zingine kama mashamba nk. Na endapo watapata msaada wowote wa dharura kukarabati majumba/majengo yaliyobomoka au kujenga upya nyumba zilizoharibika kabisa.

    Cha mwisho tulichoongea kuhusu mlipuko huu ni jinsi gani tusivyokuwa na muundo kamili wa kushughulikia dharura kama hizi kwa mfano zimamoto, ambulance, helikopta, special police and army emergency units, wataalamu wa kutathimini hasara, emergency relief team, reconstruction team.

    Fundisho jingine ni umuhimu wa kuwepo na simu za majumbani na barabarani na kuwepo emergency call free number kama ilivyokuwa zamani kwenye mitandao yote ya simu. Tukakumbushana enzi za namba 999 polisi, 990 dharura, na 994 mlio wa tindo ambao ulikuwa unatueleza saa kwa Kiswahili na 993 kwa Kiingereza.

    Hivi sasa hivi Tanzania kuna namba ya polisi na emergency?

    ReplyDelete
  3. Huyo bibi aliye na JK hospitali mkononi ana mikwaruzo ya mabomu au ni mimi tu?

    ReplyDelete
  4. bado sijasikia uwajibikaji hapo, sio kwenda tu kuangalia wagonjwa. i want to see somebody stepping down dont care ni waziri au mkuu wa majeshi, want to see all the stones turned to find out who pressed the button, or who didnt change temperature as required, or who fell asleep on a job, or who smoked a cigarette to ignite the fire....somebody do something dont leave all the burden to these innocent people that left this world or will have to leave with scars and disability for no fault of their own!!

    ReplyDelete
  5. Nakuunga mkono Mdau PAZI hapo juu, Umenena vya kutosha na inaonyesha kero hii si peke yako uliyenayo. Ntatoa mfano mmoja wa kuonyesha uwajibikaji wa vyombo vya habari, Hapa Uingereza kuna kipindi kinaitwa PANORAMA, kinarushwa na BBC, kila Janga, tatizo, Makosa, Uchunguzi nk, huonyeshwa kwa muda muafaka kabisa na kuelezea watu nini kimefanyika, nini kilitakiwa kufanyika, nini kifanyike hapo baadae kuzuia tatizo nk, vipindi kama hivyo ni Muhim sana kuliko kuonyesha mambo yenye kunufaisha wachache (waandaaji wa vipindi kama miss TZ, Kili awards nk).. Wenye TV wanaweza kuhoji kwamba tunajitegemea kwa kila kitu kuendesha vipindi vyetu, SAWA lakini revenue si wanapata kutokana na matangazo?? wakiwa na business module nzuri watapata hao hao watangazaji wa kudhamini vipindi muhimu kama hivyo.
    Serekali za nchi nyingi sana zinatumia vyombo vya habari kutangaza kuonya na kuelimisha raia kwa manufaa ya Uma. Sometimes uzalendo unanijia na nawaza kurudi nyumbani nikafanye mabadiliko, lakini nikikumbuka kwamba wengi wanafanya kazi ili walipwe na waendeshe maisha yao na si kunufaisha taifa, naona ntachezea shilingi chooni, kwani kuangushwa na watu wenye tamaa maishani kwa kufanya kazi pasi na uadilifu ni hatari kuliko kubaki nilipo na kuendeleza niwezao kwa uwezo wa Mungu.
    Mungu Inusuru nchi yetu kwani inazama. To me Tanzania Is a partial failed state... hakuna vita wala balaa za asili lakini utadhani Somalia vile.

    ReplyDelete
  6. Allah Awape subra na uvumilivu wafiwa na majeruhi wote.

    N.B. Michuzi nawe unapotosha lugha yetu nzuri; dhana za kivita si sahihi. Sahihi ni zana za kivita ai vifaa vya kivita.

    ReplyDelete
  7. Hivi hawa watu walioathirika na mabomu kama waliopoteza miguu na waliokufa kwa hio serikali itawalipa au inakuwaje????

    ReplyDelete
  8. Yaani Anonymous(Tarehe April 30, 2009 7:08 PM) kwa kweli ingekuwa jamii forums basi ningecoppy comment yako na kuitolea maelezo.

    Tupo ukurasa mmoja kaka haiwezekani janga zito kama hili limetokea alafu akina Nchimbi wana kenua kenua meno tu we need to see some one anakuwa fired kwa uzembe uliotokea roho ya mtu inathamani kubwa sana sasa uzembe wenu mmesababisha watu kupoteza maisha wengine viungo alafu hao majeruhi mtawaangalia kwa miezi mi tatu tu mtaendelea na shughuli zenu na hivi 2010 inakaribia dah.... Hapa tunataka kuona watu WANAKWISHNEY waziri wa wizara usika, Naibu wake, mkuu wa kikosi cha maafa yalipotokea Mwamunyange ooooops huyu jamaa smart kidogo aendelee kutumikia nchi yake lakini hao wengine niliowamention tunataka kuona uwajibikaji wenu sio pole sizizokuwa na manufaa kwa wahanga wa tukio husika.

    ni mimi MTANZANIA mwenye uchungu na uzembe wenu na urafi wenu kiasi kwamba mnasahau wananchi wenu.
    ni hayo tu...........

    ReplyDelete
  9. hizi gharka jamani kuna watu waowana wanaume kwa wanaume tz alafu serikali haichukui hatua,mungu atusamehe.
    oya annonymous 7:10 waswahili wanasema usitukane mamba kabla ya kuvuka mto, we mwenyewe mungu kakuangaza.

    ReplyDelete
  10. UZEMBE HALI YA JUU!

    ReplyDelete
  11. UJENZI HOLELA...DUNIANI KOTE WATU HAWAJENGI KARIBU NA KAMBI ZA KIJESHI. POLENI WAFIWA NA MAJERUHI

    ReplyDelete
  12. SARAWILIMay 01, 2009

    Mdau WA hapO juu
    namba za emergence POLIS NA FIRE zipo na ni bure tu na hata kama simu imejilock au imelokiwa bado unaweza ukapiga na unapokelewa.labda udhaifu uwepo kwenye urasimu wa kupokelewa sim yenyewe
    jaribu 911 na 112

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 01, 2009

    masikini poleni. nikiwa mdogo niliambiwa vifaa vya kivita vinafichwa chini ya mlima kilimanjaro.

    lakini kweli tuache mambo ya kuelimishana kwa mambo ya entateiment tu. kuna emergency plan ya jiji yeyote, evacuation route etc etc god forbidden yakitokea mambo kweli hapo? siku hizi huwezi jua

    poleni wafiwa lakini lazima watu wawajibishwe hapo. ni joto lilizidi,yameexpire au niaje a bomb kugo off just like that?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 01, 2009

    TUNATAKA KUJUA ILIKUWAJE HADI HAYO MABOMU YAKALIPUKA LIPUKA.TUNATAKA HATUA ZICHUKULIWE KWA WATU WALIOHUSIKA NA HASARA HIYO NA MAISHA YA WATANZANIA WASIO NA HATIA.
    KWANZA,TUNATAKA TUJUE YAFUATAYO;
    1.0 KAMA MABOMU HAYO MUDA WAKE ULIKWISHA KWA NINI HAYAKUTEKETEZWA?
    2.0 KAMA JOTO NI KALI KWA NINI HAIKUFANYIKA TARATIBU ZA KUPUNGUZA,JE WAHUSIKA WALIKUWA WAPI KUTIMIZA WAJIBU WAO?
    3.0 TUNAPENDA KUJUA WATANZANIA WALIOATHIRIKA WATALIPWAJE,HAITOSHI KUSEMA KUWA SERIKALI ITAGHARIMIA MAZISHI TU...SERIKALI ISIJARIBU KUTUMIA UMASKINI WA WATANZANIA KUTOA AHADI NDOGO NDOGO KAMA ZA MAZISHI,HOSPITALI N.K (INAPASWA ILIPE FIDIA KWA WOTE WALIOATHIRIKA)
    4.0 ITOLEWE RIPOTI YA WAZI TUFAHAMU WATANZANIA WOTE KWA SABABU INAHUSU NCHI HAIHUSU SERIKALI AU VIONGOZI PEKEE.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2009

    Waliokumbwa na hii ajali nawapa pole sana. Poleni sana wafiwa.
    Kingine. mimi nachukulia ni kama uzembe wa kulimbikiza yaani kuanzia jeshini na hata wizara husika. Inakuwaje vitu hatari hivyo vinawekwa karibu na makazi ya watu?? Mfano, zamani kiasi kama sikosei pale kimara baruti, nyuma ya bahama mama kulikuwa ulinzi mkali na hata hakuruhusiwi watu kupita/kwenda kwasababu inasemekanaika kulikuwa kuna baruti I guess so, ila siku hizi akhaa shwari tu sijui zimetolewa ama ndo mwendelezo wa uzembe?

    Anyway, cha Muhimu waziri husika KUACHIA NGAZI, jeshini pia kuna mtu au watu pia waachie NGAZI nyadhifa zao.Hii ndo demokrasia na kuonyesha kujali wananchi pia.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 01, 2009

    PICHA ZOTE ZINAONESHA JK ANATABSAMU. NINI HASA KINAMFANYA MHESHIMIWA JK ATABSAMU??? ANACHEKELA HATARi? INABIDI UWAWAJIBISHE HAO ASKARI WAKO WA MIAMVULI

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 01, 2009

    TAFSIRI YA PICHA: Ngoja NiwekePozi Huyu Si Ndio Walewale Wanatuyeyusha tu

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 01, 2009

    Picha ya kwanza inawaonyesha Rais na Mkuu wa Majeshi wakitabasamu kana kwamba ni funny. So sad, RIP Mwalimu Nyerere na Edward Moringe Sokoine, Tanzania is missing you.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 01, 2009

    Kila jambo lina mwanzo na mwisho wake. Ajali hii imeashiria umuhimu wa nchi yetu kuangalia muundo mzima wa utunzaji silaha nchini. La maana kwa sasa sio kulaumu au kuadhibu wazembe, hilo ni wazi na halina mjadala, wawajibishwe. Bali la maana zaidi ni kaungalia ni jinsi gani kutakuwa na ufumbuzi wa kudumu wa kutunza silaha nje na makazi ya watu, au watu wakae mbali na bohari za silaha. Kuweza silaha mjini kunaweza kuwe na faida zake za kijeshi, mie sio mwanajeshi siwezi kujua sababu hasa, bali inawezekana sehemu hizo hazikuwa na makazi ya watu wakati wa awali. Hivyo, naomba vyombo vya usalama vihakiki maeneo yetu tusije tukaanza mambo ya Iraq hapa, silaha mpaka uani. Pole kwa wote walioadhirika kwa njia moja au nyingine. Mlahabwa

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 02, 2009

    From Wikipedia, the free encyclopedia
    (Redirected from BM-21)
    Jump to: navigation, search
    BM-21 "Grad"

    BM-21 on display in Moscow
    Type Multiple rocket launcher
    Place of origin Soviet Union
    Service history
    In service 1964–present
    Used by See Operators
    Production history
    Produced 1963–present
    Specifications (9K51)
    Weight 13.71 tonnes (30,225 lbs)
    Length 7.35 m (24 ft)
    Barrel length 3.0 m (9.84 ft)
    Width 2.40 m (7.87 ft)
    Height 3.09 m (10.13 ft)
    Crew 4

    --------------------------------------------------------------------------------

    Caliber 122.4 mm (4.81 in)
    Barrels 40
    Rate of fire 2 rounds/s
    Muzzle velocity 690 m/s (2,264 ft/s)
    Maximum range 40 km (25 mi)
    Sights PG-1M panoramic telescope

    --------------------------------------------------------------------------------

    Engine V-8 gasoline ZiL-375
    180 hp (130 kW)
    Suspension 6x6 wheeled
    Operational
    range 405 km (251 mi)
    Speed 75 km/h (47 mph)
    The BM-21 Grad (Russian: БМ-21 "Град") is a Soviet truck-mounted 122-mm multiple rocket launcher, developed in the early 1960s. BM stands for boyevaya mashina, ‘combat vehicle’, and the nickname grad means ‘hail’. In the West, the system was initially known as M1964. Several other countries have copied it or developed similar systems.
    Naomba umsahihishe huyu mwanajeshi aliyesema kwamba BM-21 ni aina ya mabomu,this is kind of truck kama inavyojieleza hapo juu.
    I will be happy bro

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 02, 2009

    ooooooooh,""\|%**#,/"=":,

    nyambafu,baladhuli,kenge,pepoz

    natetemeka kwa hasira siwezi ongea

    annons #2 juu,7.08pm,12.21 am,5.39am-ASANTENI SANA

    natetemeka kwa HASIRA SIWEZI ONGEA NTACHAFUA HEWA HUMU

    ReplyDelete
  22. Poleni sana wafiwa na mliojuruhiwa.
    Mmmh hivi ni wananchi walojenga karibu kambi ya Jeshi au ni kambi ilojengwa karibu na wananchi? na Je,serikali inafanya nini kuzuhia isitokee tena?maana si mara ya kwanza kama sikosei au....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...