Mdau Edgar Kaliboti  (juu kulia)  si jina geni hasa kwa waliowahi kupiga tizi katika dojo la Zanaki la Goju Ryu Karate miaka ya 80 na 90 chini ya Sensei nantambu Camara Bomani na Senpai Magoma Nyamuko.  

Hivi sasa  Kaliboti yuko Sydney, Australia, anakofanya kazi ya kufundisha sanaa mbali mbali za mapambano zikiwemo karate, boxing, kick boxing,  stick fighting n.k. 

Pia amekuwa anashiriki  kwa mafanikio makubwa katika mapambano mbali mbali ya mara kwa mara. akiwa anajihusisha mara kwa mara kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa. Hivi sasa ana mkanda wa blue katika Grace jiu jitsu. 

Katika hizi picha alikuwa  katika mechi ya fainali ya Brazillian Jiu Jitsu katika  New State Championship uzito wa juu (97kg +) hivi karibuni ambapo alikuwa wa pili. Kiu yake ni kurejea bongo na kufundisha wadau mbinu mpya ya sanaa za mapigano. 

Akiongea na globu ya jamii kwa njia ya simu anasema sanaa hii sasa imepanuka sana na kwamba wengi sasa wanafanya mazoezi ya sanaa mchanganyiko inayochanganya aina kadhaa ya sanaa kwa mpigo kama vile karate, Jiu Jitsu, kickboxing, judo na stick fighting. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

 1. Fainaly hiyo kweli, mbona kama mazoezi tu na hakuna hata watazamaji mimi naona watu wachache wamesimama na wengine wakiendelea na mazoezi yao.

  ReplyDelete
 2. Hongera Kaliboti,mafunzo hayana mwisho!!
  Kumbuka enzi zetutulipotoka na juhudi ya mazoezi?, ni contact kupitia Michuzi.
  Sensei Rumadha.

  " KARATE NI SENTINASHI" By Sensei Master Kanryo Higaonna.(Mafunzo ya sanaa ya mikono mitupu hayana mwisho)

  ReplyDelete
 3. AnonymousMay 03, 2009

  hongera kaliboti.

  ReplyDelete
 4. AnonymousMay 07, 2009

  Ground fighting is way to go!It is most effective and efficient way to finish your opponent.

  Student from Machado School.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...