profesa wole soyinka akiwa na mwenyeji wake makamu mkuu wa chuo kikuu cha university of dar es salaam profesa rwekaza mukandala akiondoka ukumbi wa nkrumah hall baada ya lekcha.

Profesa Wole Soyinka amepongeza mchango wa Mwalimu Julius Nyerere wa kuunganisha Watanzania kwa kutumia Ujamaa.
Akizungumza leo na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na wengine wa nje, Soyinka aliwaasa viongozi wa Afrika kuiga mfano wa Mwalimu Nyerere ambaye alisimamia mawazo yake kwa vitendo.
"Uite kwa jina lolote lile, Ujamaa ulikuwa mfumo wa siasa ambao Nyerere aliweza kuusimamia na ukafanya kazi," alisema.
Mhadhara wa Soyinka wa leo ulichukua zaidi ya saa moja, ambapo mambo mengi aliyozungumzia yalihusu ubeberu na chimbuko lake.
Mhadhara huo ulichokoza mjadala miongoni mwa wasomi, ambao kila mmoja alikuwa na mawazo yake na wengine kumuuliza kama Nyerere alikuwa dikteta.
Soyinka alipinga dhana hiyo akisema Nyerere hakuwa dikteta na watu lazima watofautishe kati ya anayetekeleza sera zilizopangwa na dikteta.
Msomi huyo pia aliwataka viongozi Waafrika kuacha kulindana kwa kumkingia kifua Rais Hassan al Bashir wa Sudan asipelekwe katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Alisema kama kuna mtu ndani ya familia yake atafanya kosa la jinai hatasita kumpeleka Polisi.
Tamasha hilo lilifunguliwa na Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa Rwekaza Mukandala na litaendelea hadi Aprili 17 mwaka huu na kesho mshindi huyo wa tuzo ya Nobel ataendeleza libeneke lake.

wadau walipewa nafasi kuuliza maswali
umati baada ya kumsikiliza profesa wole soyinka
mzee makwaia ya kuhenga na wageni toka algeria
maprofesa (toka shoto) f. othman, marjorie mbilinyi na amandina lihamba wakijadiliana
mkurugenzi wa UN-HABITAT profesa anna tibaijuka naye alikuwepo pamoja na watu wengine wengi mashuhuri


mh. abdurlahman kinana (shoto) na balozi christopher liundi
profesa haroub othman (kati) akiwa na maprofea f. othman (shoto) na amandina lihamba
profesa wole soyinka akitoa lekcha yake hivi sasa hapa ukumbi wa nkrumah hall, mlimani
profesa wole soyinka baada ya kuvishwa skafu maalumu ya mtoa lekcha mkuu wa tamasha la wiki ya nyerere
profesa wole soyinka akivishwa skafu maalumu ya kuwa lekcha mkuu wa tamasha la wiki ya nyerere
profesa wole soyinka, makamu mkuu wa chuo kikuu cha university of dar es salaam profesa mukandara na profesa issa shivji wakisimama wakati wimbo wa taif ukipigwa kuashiria mwanzo wa wiki hiyo ya wanzuoni
profesa wole soyinka akiwa meza kuu
ukumbi wa nkrumah hall umejaa kama inavyoonekana juu na chini

profesa wole soyinka akisalimiana na mkuu wa chuo kikuu balozi kazaura
wakuu wa idara mbalimbali udsm wakielekea ukumbi wa nkrumah
msafara ukielekea nkrumah
wole soyinka akisindikizwa na kikundi cha ngoma cha parpanda kuelekea nkrumah

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. Wanazuoni hao wenye kuheshimika sana duniani wanamuenzi Mwalimu Nyerere na kuzithamini sana kazi zake. Sasa kwa nini hamtaki kuirejesha misingi na miongozo ya Azimio la Arusha?

    ReplyDelete
  2. Huyu ni ndugu wa Morgan Freeman LOL.

    ReplyDelete
  3. hivi jamani hii iko vipi katika kiswahili chetu?
    1.chuo kikuu cha university of Dar es salaam
    2.ukumbi wa Nkurumah hall

    Ni makosa madogo kimtazamo lakini yanakera sana tu!

    ReplyDelete
  4. Lekcha ndio nini? Hivi hatuna maneno fasaha ya kiswahili Bw. Michuzi? Huu nauita ni uchafuzi wa lugha na wewe ndio kiongozi mkuu. Unataka kuingia kwenye rekodi kuwa miongoni mwa wanaokiua kiswahili ndani na nje ya Tanzania?

    ReplyDelete
  5. Kumbe Nkrumah imepakwa rangi siku hizi Imependeza sana.

    ReplyDelete
  6. Hapo wanapomvalishia hicho kinguo ni bafuni? Hilo dirisha juu liko vipi? Bongo tunapenda sana mambo ya ki-mediocre. Just too simple and eventually stinks.

    ReplyDelete
  7. Profesa Wola ana shepu ya kisomi. Nywele, ndevu, nk. kama vile ma-genius wa Isareli.

    ReplyDelete
  8. kaka michuzi naomba kuuliza, hapo naona kuna kitu kama AFRIKA NI MOJA, pia kuna AFRIKA MUST UNITE, najua hapo ni mahala penye wasomi wengi na pengine kuna sababu ya kuandika AFRIKA katika sentensi ya kingereza, na sio AFRICA.naomba kuuliza kama kuna tofauti yoyote kati ya AFRIKA na AFRICA .

    ReplyDelete
  9. Anon 4 hapo juu, hicho unachoita kidirisha ni Kiyoyozi (AC), angalia kwa makini utaona kuna vidirisha viwili vya kutoa hewa ya baridi ili kupunguza joto la Bongo.

    Anon 5 Afrika ndio jina halisi la Kiafrika kwa matamshi, na Wamajumui huwa wanalitumia sana, rejea historia ya matumizi ya neno Afrika utaona kwa nini ni muhimu kutumia neno kama tunavyolitamka mf lugha yetu ni ya 'Kiswahilli' na si ya 'Swahili'.

    Anon 3 Kiswahili hubeba maneno ya lugha zingine na kuyafanya yawe ya kibantu hivyo 'lekcha' na 'mhadhara' yote si maneno ya asili ya Kiswahili ila yanafaa kutumika maadam sentensi zetu zinabakia za Kibantu.

    ReplyDelete
  10. Broz Michuzi,ingependeza zaidi laiti hizi picha zingeeambatana na alichoongea mwanazuoni huyo mahiri...

    ReplyDelete
  11. naona profesa haroub othman yuko na mkeo profesa saada othman.nice.nyie ni mfano wa kuigwa.wakilisheni wangazija

    ReplyDelete
  12. MediaViabiltyApril 14, 2009

    Kuhusu ishu ya Al-Bashir napata wasiwasi wa huyo mwanazuoni asije akawa front company ya neo emperialist ilhali anajifanya ant neo emperialist.

    For me DRC problem is worse than Darfur so I cant comprehend warrant issued by the ICC.

    Is this below a conlusion of scholars in afrika?

    1. In DRC we have good governance by the president and Bad rebels

    2.Darfur we have Good rebels and Bad governance by Al-Bashir

    Kwa nini hamkumualika prof mamdan? I reagrd Mamdan as best contemporary historian profesor on afrikan issues

    ReplyDelete
  13. Siku ya Nyerere? Wasomi baada ya kuzungumzia mambo ya maana mnamzungumzia sera ambazo zimefeli za Ujamaa. NO socialism in TZ; Ni FREE MARKET CAPITALISM.

    ReplyDelete
  14. Mediaviability Mamdani alishaalikwa Agosti mwaka jana na alizungumzia Darfur, sijui ulikuwa wapo ila tangazo la hilo tukio ndio hili hapa http://udadisi.blogspot.com/2008/08/public-lecture-by-professor-mamdani.html na kama unataka mrejesho nitumie email nitakutumia huo mrejesho wa alichokiongea Mamdani na tena kashakitoa kwenye kitabu chake kipya kuhusu Darfur.

    MikoJohn are you arguing for the sake of arguing or what? There is no such thing as free market capitalism - ni kiinimacho tu. Ask the bailing out and subsidizing Americans!

    ReplyDelete
  15. Chambi chachage nimekuelewa , lakini mi nauliza kwa nini katika sentensi ya kingereza , wameandika AFRIKA? nakubaliana na wewe katika kiswahili kuna uhusiano kati ya jinsi neno lilivyoandikwa na matamshi yake lakini katika kingereza there is no correspondency between orthography and pronunciation. asa hapo inakuaje?AFRIKA MUST UNITE. kuna kitu maalum hapo kimekua potrayed?

    ReplyDelete
  16. Mr. Chambi Chachage,

    Ki- ni prefix ya lugha ya Kiswahili. Hivyo huwezi kutumia neno Kiswahili katika lugha ya Kiingereza. Unapoongea Kiingereza neno sahihi ni "Swahili"

    Nitakupa mifano michache ya kukuonesha jinsi vile ki- ni sahihi pale unapoongea Kiswahili tu.

    Mfano wa kwanza lugha ya Wafaransa sisi Waswahili tunaiita "ki-Faransa", Waingereza wanaiita "French" lakini Wafaransa wenyewe wenye lugha yao wanaiita "Francaise". Je itakuwa sahihi nikiwa naongea kwa Kiswahili nikasema "Mimi napenda kuongea Francaise"?

    Haiji, au sio? Basi ndio hivyo hivyo na wewe ukimwambia mtu anayeongea kiingereza atumie neno ki-Swahili katika sentensi za kiingereza.

    Hali kadhalika lugha ya Waingereza sisi tunaita "ki-ingereza", wenye lugha yao wanaiita "English" na tuchukulie wafaransa wanaiita "Anglais".

    Kwa hiyo kama Waswahili tutang'ang'ania kiSwahili kiitwe kiswahili kwenye kila lugha basi tuache kuharibu majina ya lugha za wenzetu. Tuache kuita lugha ya Waingereza kiingereza. Tuiite "english" kama wao wanavyoiita.

    Siku njema

    ReplyDelete
  17. Chachage,

    Huko unakokwenda sio kwenyewe unless unatafuta academic arguments.

    Bail out ya USA sio kigezo cha kusema hakuna Free Market Capitalism.

    Ni kwamba walijisahau tu katika regulations.

    Lakini usilete sera za "centrally planned production" za enzi za ujamaa, na mambo ya kupanga foleni kununua sabuni na sukari.

    Binadamu ni watu tunaopenda uhuru wa kuchagua. Ujamaa huwa hautoi uhuru huo ndio maana from the word GO, ujamaa ni failure.

    Free Market Capitalism ni kama game kama mechi ya mpira, hivyo lazima kuwe na refa. Serikali kazi yake ndio huo urefarii.

    Marekani serikali ilijisahau ikalala katika kazi ya urefarii ndio maana wakajikuta katika matatizo.

    Lakini mambo ya serikali kuingia kucheza kwenye game ni hatari maana serikali ikiwa mchezaji nani atakuwa refa?

    Angalia sekta kama maji (DAWASCO) au umeme (TANESCO) mambo yako hovyo maana refa mwenyewe anacheza mpira.

    Tunashukuru kwenye sekta ya mawasiliano refa kakubali kufanya kazi yake ipasavyo hivyo mambo no mswano.

    ReplyDelete
  18. MediaViabilityApril 14, 2009

    Mr Chambi,

    Kipindi hicho nilikuwa maporini, kazi za uhandisi kuna kipindi sinatuweka mbali na ulimwengu.

    tafadhsli nitumie mrejesho hapa remera2008@gmail.com

    hasante sana kwa majibu yako

    ReplyDelete
  19. Ana Tibaijuka is no more UN Habitat Director, wazungu wameshamwaga, please update your data

    ReplyDelete
  20. There is nothing wrong in being a left-wing intellectual. However, the fact remains that though Capitalism is not perfect, it is the best system we have to get us out of poverty in Africa. Human beings will ALWAYS work for the best benefit of themselves first and then help others later.

    The recession and bail outs will be over and forgotten and people will go back again to make money anyway they can just like before and I am sure along the way, we will experience another economic crisis. That's the cost we pay to reach high standard of living.

    I would take Capitalism any time of the day. Socialism is only great as a system if the country is already rich and can use the taxes to help it's most needy citizens. You can't help the poor and the needy if you don't have greedy capitalists running the economy. Without the growth of goods and services, the governments in Africa will never take off economically, let us not kid ourselves here.

    I have asked our respectful intellectuals here what Nyerere has done to the nation for us to be so ever grateful. This country's economy was destroyed by Nyerere's Socialism. I am still waiting for a reply.

    Ironically, when many Tanzanians were living without any freedom under his dictatorship, he spent our resources to help his fellow African freedom fighters to free themselves from colonialism.

    The elite left-wing intellectuals can trick the masses with their messages of hope under socialism but the world is being run by Capitalism, with all it's deficiency. The very fact that we are communication in this medium is thanks to a Capitalist entrepreneur.

    Mdau wa Tokyo, Japan

    ReplyDelete
  21. socialism failed, so is capitalism (bailout plans,stimulus packages). I feel that socialism failed because then we did'nt have resources(e,g skilled labor)to implement it effectively.

    With regard to Nyerere, he committed a good number of mistakes. So have other great leaders of the world. When we jugde our leaders, we have to "put them on the balance"-wole soyinka. That is, if we look at the likes of bokassa,pinochet,and mkapa, we can say that Mwalimu was selfless, visionary and democratic (this is subjective).

    ReplyDelete
  22. Je tunaweza kupata papers au video recordings za wazungumzaji wa siku hiyo?

    ReplyDelete
  23. "UBEPARI NI UNYAMA"

    ReplyDelete
  24. Hivi jamani kila siku tunasikia sifa za UDSM kupitiwa na watu maarufu kama kina Marehemu Walter Rodney, Profesa Ali Mazrui, Marehemu Kanali John Garang, Rais Yoweri Museveni, Marehemu Shihabudin Shiraghidin, Mwalimu Abdilatif Abdalla na wengineo wengi.

    Naomba kuuliza wanazuo wa Kitanzania wanaovuma kwenye anga za kiamataifa kwa sababu nimejaribu kukumbuka nikashindwa kumkumbuka hata mwanazuo mmoja wa Kitanzania aliyezalishwa na UDSM anayetambulika katika anga za kitaaluma za kimataifa kama hawa kina Profesa Wole Soyinka, Chinua Achebe, Ali Mazrui, Dan Wadada Nabudere, Mahmood Mamdani, Ahmed Mohamed Haidar, Ngugi Wa Thiong'o, Adebayo Adedeji, Adebayo Olukoshi, Philip Ameagwali na wengineo toka Afrika.

    Pili, Kumbukumbu zangu zimenikumbusha wanazuo wa UDSM ambao wanaojulikana katika anga za kimataifa kina Profesa Anna Tibaijuka na Dr Asha-Rose Migiro. Hata oa ni wanatofautiana kwa sababu mmoja ni Profesa Anna Tibaijuka wa kutafuta mwenyewe(through Application) na Dr Asha-Rose Migiro ni wa kuteuliwa.

    ReplyDelete
  25. Muungwana sijaleta akademiki agumenti hapo, nimetoa fakti tu. Naona hata wewe pointi yako inajifunga unaposema walijisahau kwenye 'regulation' Sasa Free Market gani hiyo inakuwa regulated? Free market gani hiyo inakuwa subsidized? Free market gani hiyo inakuwa na bailed out? Naam Free Market gani hiyo inategemea state intervention kwenye international trade negotiations za GATT,WTO,EPA n.k? Alafu sijasema nafagalia centralization. Ujamaa Orijinali sio centralized bali ni decentralized at the village assembly level. Huo ndio naufagilia mimi katika muktadha wa third way au mixed economy. Mabyurokrati wa chama waliusaliti Ujamaa wa kweli kwa kufanya decentralization by deconcentration badala ya kufanya decentralization by devolution. tupeleke madaraka vijijini badala ya kuyahodhi mikoani au wilayani tuone watu watakavyokuwa free ku-trade na kufanya mambo mengine bila rungu la centralization!

    Mboma hoja zako zimetulia ila sikubaliani na hitimisho. Isizulu ni lugha ya Wazulu. Huwezi kusema someone is speaking Zulu. Utasema someone is speaking Isizulu. Waingereza wametambua hilo. Na wameanza kurekebisha lugha yao ili iache Ubeberu wa lugha. Angalia dictionary mpya. Utaona wamegundua Swahili sio lugha. Lugha ni Kiswahili. Ila sisi bado tuna kasumba ya kunga'ang'ania tu anglicization!

    Mediaviablity nitakatumia mrejesho haraka iwezekanavyo ila kwa ufupi inaonekana Soyinka anapingana na Mamdani kuhusu Darfur!

    ReplyDelete
  26. Anon wa April 14, 2009 8:01 AM nitawauliza waandaaji kama walitumia Afrika badala ya Africa makusudi au la ila kama nilivyosema nachojua mimi ni kuwa wanaharakati ngangari wa Umajumui wa Afrika wanapenda kutumia Afrika yenye 'K' badala ya yenye 'C' hata kwenye Kiingereza 'to make a statement' yaani kuonesha msimamo fulani - I am talking about the militant Pan-Africanists and Afrocentrists.Kwa ujumla wanafanya hivyo kupingana na Ukoloni na Ukoloni Mamboleo uliohodhi mamlaka ya kuwapangia wengine waitwe nani, miji/nchi zao ziitwe majina gani na rasilimali zao ziitweje. Google 'Afrika' uone hoja zao.

    ReplyDelete
  27. Anon wa April 14, 2009 10:17 PM anga za Kimataifa ni zipi hizo maaana kama ni za IMF/WB basi tunaye Benno Ndulu wanamheshimu sana huko na alikuwa huko pia ndio aliyewaandikia ripoti yao ya growth challenges za Afrika - bila kumsahau Ibrahim Lipumba anayeitwa huko Geneva kuwa kwenye timu za wataalamu wa taasisi za kimataifa za UN. Kama ni za Afrika basi Issa Shivji wanamtambua sana huko, anatoa lekcha kibao kwenye nchi mbalimbali za Afrika na wanampa honorary doctorate - pia hata huko Ulaya na Marekani huwa wanamtafuta sana. Na kama ni anga za Amerika kina Julius Nyan'goro wanakubaliwa huko mpaka wanapewa uenyekiti wa ASA. Sasa sijui unatumia kigezo gani maana kwa vigezo navyovijua mimi hawa kina Haroub Othman, Farouq Topan na wengineo ni wanazuoni maarufu kwenye medani za kimataifa za hapa Afrika na nje ya bara la Afrika.

    ReplyDelete
  28. Yaani Muungwana nimekufagilia ile mbaya na posting yako hapo juu. Lazima utakuwa na silika za u-genious. Moja ya silika za genious ni kuongea based on well considered facts na kukwepa kuongea based on mob psychology.

    Nimefuatilia sana matamshi ya Wole Soyinka katika huu mdhahalo na ninasikitika kusema kuwa ameni let down. Ni kama vile he is playing to the crowd. Mara anasifia Ujamaa, siasa bankum kabisa iliyoshindwa hata kwa waanzilishi wake. Mara anazungumzia Imperialism - kitu ambacho kimesha evolve na kuwa Globalization. Whats wrong with Soyinka? Halafu kali kuliko yote ni pale aliposema inabidi Kiswahili kiwe lugha ya Africa (#*@#!?) - kwa aje? Kwanza Kiswahili ndiyo kilichofanya mpaka wasomi wa TZ wapate shida ku-compete katika job market hata Tanzania kwenyewe. You simply cannot expotulate abstract concepts, or even discuss complex issues in Kiswahili as well as you would in English.

    ReplyDelete
  29. Kiswahili nacho ni bankum. Kinafaa kutumia nyumbani tu. Lugha gani amboyo kila kitu ni either "kula" au "kupiga"? Angalia hizi;

    Kupiga Simu = Call
    Kupiga Ramli = Bewitching
    Kupiga Soga = Chat
    Kupiga Usingzi = Sleeping
    Kupiga kengele = ring a bell
    Kupiga Kura = vote
    Kupiga mtu = beat a person
    ...


    Kula raha = enjoy
    Kula kushoto/ kulia = take a right/ left turn
    Kula hasara = make a loss
    Kula kitabu = read
    Kula reki! = WOW!

    Ni vipi utaweza kurusha chombo cha anga za mbali kama Pioneer, kilichoshapita sayari ya Pluto kwa kutumia hii lugha yenye maneno mawili tu? Au ni vipi utaweza kushiriki katika utafiti wa dawa ambapo una-deal na madaktari wa ulimwengu mzima kama wewe unachojua ni kula na kupiga tu?
    Kula

    ReplyDelete
  30. Mr. Chachage,

    Siifahamu vizuri lugha ya Kizulu lakini maadamu kuna maneno kama "isizulu" na "isindaba"... bila shaka "isi-" ni prefix ya aina fulani pia katika lugha yao.

    Kama ilivyo prefix ya "ki-" katika Kiswahili.

    Kama Waingereza wameamua kurekebisha lugha yao na kuingiza prefix za lugha nyingine katika kamusi yao well, who am I to stop them?

    After all nadhani lugha yao ndio maana imepanuka sana maana iko democratic wanabeba maneno mengi tu toka lugha nyinginezo.

    Ila hoja yangu ilikuwa ni kwamba hizi prefix kama "ki-" au "isi-" ziko specific kwenye lugha husika, na sio kwenye kiingereza.

    Nashauri na sisi turekebishe Kamusi yetu tutoe neno "Kiingereza" tuweke neno "English" kama njia ya kureciprocate ukarimu waliotuonesha Waingereza kuweka "ki-Swahili" badala ya "Swahili"

    ReplyDelete
  31. All i can read in this USDM forum is C.O.M.M.U.N.I.S.T.S.

    ReplyDelete
  32. mmemsahau dr gharib bilal ni mwanazuoni anayeheshimka sana duniani kwembe mambo ya nuclear.marekani wanamuogopa sana huyu mzee

    ReplyDelete
  33. Anon wa 4/15 9:02 ninakushauri utembelee dictionary.com utafute neno la Kiingereza "take" kama mfano mmoja tu utakaokufumbua kidogo jinsi lugha zote hai duniani zinavyofanya kazi!!!!

    ReplyDelete
  34. Chambi Chachage, asante kwa majibu mazuri. Hata hivyo hujaikidhi majibu ya maswali yangu.

    Umesema nanukuu "kama ni za IMF/WB basi tunaye Benno Ndulu wanamheshimu sana huko na alikuwa huko pia ndio aliyewaandikia ripoti yao ya growth challenges za Afrika" Naomba kukuuliza ripoti hii inatumika wapi? Ni rejeo la mchakato wa shughuli za za IMF/WB? Kama ndiyo, ripoti hiyo imewahi kutumika katika shughuli gani za IMF/WB? Ni Rejeo katika mitaala ya kufundishia vyuoni? Kama ndiyo ripoti hiyo inatumika katika chuo/vyuo gani na kozi gani?

    Umesema nanukuu "bila kumsahau Ibrahim Lipumba anayeitwa huko Geneva kuwa kwenye timu za wataalamu wa taasisi za kimataifa za UN." Umesema kaitwa kama kweli kaitwa na nani? Ninavyofahamu mimi katika shughuli kama hizi aidha unaomba au unateuliwa. Halafu katika hiyo timu unayoizungumzia anaenda kufanya nini?

    Umesema tena nanukuu

    "Kama ni za Afrika basi Issa Shivji wanamtambua sana huko, anatoa lekcha kibao kwenye nchi mbalimbali za Afrika na wanampa honorary doctorate - pia hata huko Ulaya na Marekani huwa wanamtafuta sana." Rejea swali langu wanazuo niliowataja wanatamba kweli kwenye anga za vyuo kimataifa kwa kuwa wahadhiri waandamizi au kwa maandiko yao kutumika katika mitaala ya kufundishia kwenye taasisi za elimu ya juu za kimataifa. Unaweza kutaja andiko (course book) lolote la Profesa Issa Shivji linalotumika kufundishia kozi kwenye chuo/vyuo kikuu kingine zaidi ya UDSM?
    Umesema pia Ulaya na Marekani huwa wanamtafuta sana. Ulaya na Marekani ni mabara ambayo yana nchi au majimbo. Nchi zipi za Ulaya au majimbo gani ya Marekani huwa zinamtafuta Profesa Shivji na kwa minajiri gani?

    Nakunukuu tena:

    "Sasa sijui unatumia kigezo gani maana kwa vigezo navyovijua mimi hawa kina Haroub Othman, Farouq Topan na wengineo ni wanazuoni maarufu kwenye medani za kimataifa za hapa Afrika na nje ya bara la Afrika."

    Natumia vigezo vya kuwa
    1: Wahadhiri waandamizi katika vyuo vikuu vingine nje ya Tanzania.

    2: Kuwa wakuu wa vitivo au idara katika vyuo vikuu vingine vya nje ya Tanzania.

    3: Maandiko yao kutumika katika mitaala ya vyuo vikuu vingine zaidi ya UDSM.

    Je unawafahamu wasomi wowote kutoka UDSM ambao wanakidhi hivyo vipengele vitatu? Naomba usinitajie wale wahadhiri waliotoka UDSM ambao wapo Botswana, Namibia, Lesotho au Swaziland. Naomba unitajie wanazuo toka UDSM na mambo wanayoyafanya vyuo katika vyuo kwa mfano Makerere, Nairobi, Fort Hare, au huko Marekani States University of Columbia New York, Stanford, Havard, UCLA, Yale, Wilson Woodrow nk. Uingereza vyuo kama Oxford, Leeds, Cambridge, SOAS, LSE, Edinburgh, Glasgow, Dublin nk. Ujerumani vyuo kama Berlin, Luebeck, Dresden, Aachen. Sweden vyuo kama Upsalla, Stockholm, Lund, au Gothenburg. Finland vyuo kama Helsinki, Otaniemi, Turku, au Tampere. Denmark; Roskilde, Aalborg, au Copenhagen. Norway vyuo kama Bergen, Trondheim, Lillehammer, au NLH. Na vyuo vingine kama vya Australia, Canada, New Zealand, Japan, China, Russia na kwingineko lakini siyo Botswana, Namibia, Lesotho au Swaziland.

    Ndugu Chambi na wadau wengine nitashukuru sana kwa majibu yenu. Kwa sababu ninfanya utafiti juu ya suala majibu yenu ni msaada mkubwa kwangu. Asanteni sana.

    ReplyDelete
  35. Anony wa 9:59, April 16, umeongelea la maana kabisa. Kuitwa kutoa lekcha sio kitu cha ajabu kabisa. Kama ulivyosema, profesa anajulikana kama vitabu vyake vikitumika katika madarasa ya vyuo vinanyojulikana kama ulivyovitaja.

    Mimi binafsi hata doctorate sina, lakini kiji master changu cha Marekani kimenisaidia kupewa kazi za kulekcha hapa Japan. Sio lazima ujulikane au uwe mkaali kualikwa au kuomba kazi kama hizi. Karibu kila chuo duniani kina program za kuwaalika wasomi mbali mbali katika vyuo vyao, na sio lazima uwe na Ph.D au hata Master's kutoa lekcha. Mara nyingi tunapata wanasiasa wasiojulikana na hata wanafunzi wa sekondari kutupa maoni yao katika mambo mbali mbali yanayohusu jamii.

    Ukisoma magazeti ya nje kama The Econonist, The New York Times, Japan Times, The Wall Street Journal n.k utaona maprofesa na wanasiasa wengi wanaandika maoni kila siku kuhusu maswala mbali mbali yanayohusu jamii. Ni mara chache tu nimeweza kuona maoni ya maprofesa, wanasiasa wetu, au madon wetu katika magazeti ya Tanzania, labda wenzetu hawana presha ya kazi zao. Ulaya na Marekani, kama profesa hajaandika maoni au kuchapisha vitabu basi huwa hapewi tena cheo na mwisho hatakuwa na kazi kwa kuwa contract yake inamlazimisha achapishe ("Publish or Perish"). Ndio maana kila siku unasoma maprofesa wao wanachapisha katika magazeti ya elimu yao kama New England Journal of Medicine / Science (madaktari), Foreign Affairs (Siasa) na kadhalika.

    Kazi njema Balozi na shukurani.

    Mdau wa Tokyo, Japan

    ReplyDelete
  36. ....wavulana husifia ukubwa wa maumbile yao nyeti. Wasichana wanasifia ukubwa wa makalio yao. Wasomi watu wanasifia vyuo vyao walivyosoma(e.g.UDSM vs the rest).Kazi ipo!!

    ReplyDelete
  37. tatizo professorz,,wanaona vitu vidogo sana ambavyo mtu wa akili timamu havioni,,,

    kazi kweli,,,

    Tanzania tutafika tu

    ReplyDelete
  38. wasomi juu!!!

    ReplyDelete
  39. Tatizo nyumbani wasomi wetu wana maringo na uvivu pia. Nchi nyingine, hata uwe na elimu gani, lazima ufanye kazi yako kwa bidii na heshima kwa wote.

    Mzazi wangu alipopata mshutuko wa moyo usiku mmoja (tulijua siku ya pili), nilienda kwa Dr. Mtulia Upanga miaka ya nyuma. Nikaambiwa kuwa amelala japokuwa mimi ni jirani na nikawaeleza kuwa mzazi wangu ni taabani (hapo nipo ukumbini sio getini).

    Baada ya muda mfupi nikampeleka mzazi kutibiwa London na nikajikuta naongea na mwalimu wa Dr. Mtulia Uingereza. Jina lake ni Dr. Webb-Pepploe wa St. Thomas Hospital, westminster, London (bingwa wa moyo).

    Aliniuliza kama namfahamu Dr. Mtulia alipojua kuwa tumetoka Tanzania. Dr. Mtulia alisoma chini yake hapo St. Thomas Hospital na alifanya kazi hapo, London. Alisikitika sana baada ya kumweleza matukio.

    Huyu mzee wa Kiingereza alimtibu mzazi kwa heshima na alihangaika kutupatia kila aina ya huduma yeye binafsi na dada wake wa ofisini. Sitamsahau kabisa.

    Huu uchungu dhida ya Dr. Mtulia utakuwa na mimi mpaka kaburini.

    ReplyDelete
  40. The University of Dar es Salaam Vice Chancellor Professor Rwekaza Mukandala said of the UDSM lecturers:

    "You are lazy, money-hungry, teaching staff"

    "Time and again you have been reminded to submit revised curricula of the programmes you teach, but out of sheer laziness, deadlines come and go with no one living up to his responsibility. We currently have almost 1,200 faculties, but only about five or six faculties have submitted theirs"

    Quoted from IPPmedia, April 20th.

    If the university management have lost confidence of our learned lecturers to do their job with integrity, then, what hope is there for the future of our graduates?

    Mdau from Tokyo, Japan.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...