Si kweli kila aliye ughaibuni anabeba boxi. Mfano hai ni Da' Rukia Potter-Malipula mbongo anayaishi kitongoji ya Maryland nje kidogo ya jiji la Washington DC ambaye amethibitisha kwa vitendo kwamba kuishi ughaibuni kwa malengo kuna faida. hivi sasa ni mmiliki wa kampuni ya kufanya usafi majumbani na maofisini akiwa na wafanyakazi aliowaajiri takriban 19 hivi. juu yuko na mama yake ambaye kaja kumtembelea na chini akipozi mbele ya nyumba yake, pamoja na video inayomuonesha akielezea shughuli zake.

rais wa kampuni binafsi ya American Cleaning
Company, LLC, Rukia Potter-Malipula alonga na globu ya jamii
Tovuti yake ni:
http://www.americancleaningcompany.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 74 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2009

    Asante kwa kutuwakilisha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2009

    SASA HIYO NI KAMPUNI SI SAWA TU NA MMACHINGA HAPO BONGO ANAYETEMBEZA NGUO BARABARANI, HIYO MTU YOYOTE MWENYE AKILI ZA KAWAIDA TU ANAWEZA KUFANYA SI LAZIMA UWE KICHWA. WALA HAITAJI SAYANSI YA ROKETI KUANZIA KAMPUNI KAMA HIYO.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2009

    hilo jina 'POTTER'mbona sio la kibantu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2009

    Hiyo kawaida ughaibuni kila msafishaji ana kuwa na kampuni yake, na tenda zikiwa nyingi inabidi utafute washikaji ambao wengi ni wanafunzi kukusaidia kazi zako. kwa hiyo huyo dada ni msafishaji sawa na wabeba maboxi asijipake siagi.

    ReplyDelete
  5. Hii ni Poa, Hapa UK wabongo wanaomiliki makampuni wako kibao..mimi nilifikiri kubeba boxi ni msemo tu, nipo hapa UK kwa miaka miwili sasa nilishangazwa sana kuona wabongo wanamiliki makampuni..na wengine wana jobs babkubwa kama lawyers,nk mmoja nilimtembelea kazini kwake hospitalini nikidhani lazma atakua mfagizi au muosha vibibi nikakuta ni boss wa department nzima na wazungu wamepanga foleni kumuona boss baada ya mi kutoka..kusema ukweli wabeba boxi ni wanafunzi tu na wageni kama mimi, waliokuja zamani wametulia.

    Nawakilisha mdau UK

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2009

    Ah..hebu acheni kujitetea! kwani mie nikisema ati namiliki 'disneyland'je mtaniamini?
    Sasa kama wanasafisha majumba ya wazungu yaani kuokota takataka zao zikiwemo mipira ya kupuliza na kupiga pasi,kusafisha misalani yao na kufua simizi zao ,haimanishi chochote...bali ni njia mmoja baadhi ya mengi kujitafutia riziki...pia jina hilo la potter si la kizungu au lakiniga tu? basi naipumzisha kesi yangu!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2009

    Good all the Best RUKIA, safi sana

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2009

    MFANO WA KUIGWA NA WENGI.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2009

    Asante Da'Rukia kwa kutupa ushauri mzuri watanzania wenzako,hasa sisi wanawake.kila la heri katika biashara zako...

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2009

    Ongera sana dada

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 23, 2009

    michuzi bwna,umewazungukia ma rostamu wote huko,tuonyeshe begi ukiwa airport.,

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 23, 2009

    kampuni ni yake au ni agent??

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 23, 2009

    Dada Rukia, Kuna yule Mwalimu mmoja wa chuo kikuu mzumbe anaitwa Mrisho Malipula je ni ndugu yako???

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 23, 2009

    ni matumaini yangu kuwa wapiga box wako wooote ni wabongo. usije ukawa umeajiri wamexico bure au wakenya!! achana na wakenya wao states sahivi ni kwao kaka yao obama atawapa kazi nzuri tu na uraia wa bei rahisi. saidia wapiga box wa kwenu mama, wabongo. walikimbia maisha magumu huku. walishindwa kupambana huku wakaamua kwenda kuwa wakimbizi wa kiuchumi huko na ulimbukeni flani wa kuwa states. ni vizuri uwasaidie waajiri wapige box kwenye kampuni yako ili wazichange nao waje waanzishe kampuni hata za kusafisha vyoo!!!
    Umenipa moyo nami ngoja nimtafutie nauli na viza mtoto wa mjomba wangu amelosti hapa bongo ili aje huko umuajiri apigepige box kwenye kampuni yako. manake hapa amekalia wizi tu watamchoma moto wabongo wamepinga.
    Ahsante.
    Mzee wa blingbling,chenigoldpetesilver DSM.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 23, 2009

    That's what I am talking about lady! Keep it up! you're doing great!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 23, 2009

    Good job mama
    Baambie sio wote wabeba boksi na kubeba boksi ama kusafisha wazee ni kupenda kwakuwa US is a land of opportunity.
    U can be a musician like Akon, boxer kuliko Tyson, basketballer kuliko Dikembe, anything anything and wake up a bilionea
    Baelezee mama

    Niko kwenye ze same industry hapa Texas

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 23, 2009

    Michuzi, muombe akupe angalau siku moja ya kupiga boksi/kufagia kwenye kampuni yake usikilizie boksi linavyovunja mgongo!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 23, 2009

    mjasiriamali wa kusafisha ofisi, vyoo, mbwa,barabara nk yeye hachagui sasa anatofauti gani na mimi ninayefanya kazi magari ya city NY na pia sichagui kazi mradi isihatarishe nikarudishwa bongo

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 23, 2009

    Asante dada Rukia.Mungu akubariki sana.Wengi tunaoshi ughaibuni tunapenda sana kujiita"wabeba mbox"
    Tupo wabongo wengi tunaofanya kazi za maofisini na akina dada wengi mahospitalini na pia wapo wengine wanaojifanyia shughuli zao binafsi kama vile dada Rukia.Wapo vijana waofanya kazi Fedex ambao kazi yao ni kudeliver packages kama maboxes nk.Lakini wote tunajiita wabebamabox.Nikama vile Newyork inavyoitwa Newala,Boston-Bukoba,Ulaya-majuu,Marekani-Unyamwezini nk.Kwhiyo kama kuna mtu anayetumia"wabebamabox"kutibeza tunaoishi ughaibuni,bila kutaja mishahara tunayolipwa,anahaki ya kufanya hivyo na sisi tunahaki ya kumuelewesha.Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 23, 2009

    Kep up the good work.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 23, 2009

    Michuzi wifi yetu hana wivu kabisa.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 23, 2009

    NI MAWAZO MABOVU KUFIKIRIA KILA MTU HAPA USA ANABEBA MABOKSI KAMA WENGI WENU MNAVYOFIKIRIA.WANAOBEBA MABOX WENGI NI WALE WALIOKUJA KUTOKA TANZANIA WAKIWA NA ELIMU YA FORM FOUR AU WACHACHE WENYE ELIMU YA HIGH SCHOOL.WATANZANIA WENGI NINAOWAFAHAMU WAMESOMA UNIVERSITIES HAPA USA KUANZIA DEGREE YA KWANZA HADI YA TATU.KUNA WANAOFUNDISHA VYUO VIKUU,WANAOFANYA WORLD BANK,IMF NA MAKAMPUNI MAKUBWA YANAYOFANYA KAZI NA GOVERNMENT KAMA LOCKHEED MARTIN,SAIC NA MENGINE MENGI.LA MUHIMU HAPA NI JUHUDI ZAKO ZA KUSOMA BASI HAKUNA JINGINE UKIZEMBEA UNABAKI NYUMA KAMA WALIVYO WATU WENGINE.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 23, 2009

    Nikweli huyo mama anavyosema kuhusu Busines, ukianzisha kampuni watu wengi wanakudiscourage, kama mimi ilivyonitokea, ila mie niliamua kufanya bila kumwambia mtu na mara nilipo fanikiwa basi watu wakanifuata wengi sana kuniuliza ulifanyaje! hivi na vile.
    ula mamaa keep it up,utakuwa mfano wakuigwa.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 23, 2009

    Thanks very much!because wabongo wanafikiri wote wanaoishi marekani wanafuta mavi.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 23, 2009

    Kazi yoyote ni kazi, kusafisha pia ni kazi ambazo zimo katika jumla ya kazi za kupiga box, pia inaonyesha hajaanza tu nakuwa na kampuni yake, kaanzia kwenye kuajiria(kutumwa)na kufikia alipofikia(kama hajamzunguka mtu),kwa miaka aliyokaa huko na ikiwa ndio kazi yake ya kwanza tu kuanzia afike basi ni hatua ya kawaida sio ya kushangaza sana, wapo watu wengi wamekaa muda mfupi na maendeleo yao ni makubwa sana, katika hao watu anaowaajiri atuambie Watanzania wapo wangapi? Pengine hakuna hata mmoja na kama yuko ni ndugu yake.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 23, 2009

    Babake,

    Zama zile kila Jumamosi jioni tulikuwa tunasikia toka Idhaa ya Biashara ya Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Uncle J Nyaisanga akisema "COCMACS: Civil Office Cleaning and Maintanance Services wapo Jengo la Umoja wa Vijana kwa usafi wa maofisi na majumbani"

    Nakumbuka mpaka signal tune ya kipindi kile ilikuwa lile funk la Pick Up the Pieces la Average White Band. Ok, Wabongo, tusisubiri mwekezaji toka nje aje kutufagilia maofis na majumba yetu.

    Dada Rukia Malipula "..Makasi? Alee?.."

    ReplyDelete
  27. Kaka Nanihii mbona aliposema anasafisha kila kitu ulistuka kidogo? Halafu na wewe haujambo kwa KUONGEZA CHUMVI ye amesema ana wafanyakazi 16 kama nimesikia vizuri,lakini we umeandika 19.
    Huyo dada nimempenda kutokana na anavyochakalika huku "manchi ya watu" mpe HONGERA zake.Huyo da Rukia ni mfano wa kuigwa sio dada zetu wengine wanaokuja huku kujiuza.
    Kaka mbona hukutuhabarisha kama keshaolewa au bado, tuchangamkie maana dada kama huyo ndio aina ya mke ninayeota kumuoa kila siku.

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 23, 2009

    michuzi ulizia vizuri wenyeji kuna wajasiriamali wa ukweli ukweli huko VA ila sidhani kama watakubali kuanikwa hapa

    ReplyDelete
  29. wabebe box hilo ni jina tu linalotumiwa na watu wanaoishi afrika kuwaita watu wanaoishi ulaya.kama ilivyo bongo tunavyawaita wamachinga kuwakilisha wafanyabishara ndogondogo japokuwa si wote wanaofanya hizo biashara wametoka kusini,ukweli si wote huku wanaofanya kazi za mabox,kuna washikaji wengi tu wanafanya professinal job na mishaara yao after tax kwa mwezi wanaweza lipa walimu wa shule nzima kama sekondary benjamini mkapa

    ReplyDelete
  30. WAKATI WAHESHIMIWA (executives) WANAJITOA UHAI WAO FAMILIA ZAO NA WATOTO SABABU HAJAZOEA VITU KAMA MKATE BILA SIAGI, KUTOKA KWENYE HEKALU KWENDA KWENYE NYUMBA YA KAWAIDA WALIOFIKIRIA MWISHO WANAPETA.
    http://www.cnn.com/2009/CRIME/01/28/family.dead.california/index.html

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 23, 2009

    acheni kujifaragua kazi nzuri wapi nyie??? wote watumwa wa wazungu tu huko. unatakiwa kila siku kusali ili upate masaa mengi. wote wabeba box hamna lolote!!! box jema!!!

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 24, 2009

    MtaHATE, mpaka mchoke, dada NI CEO, Na kaajiri wafanyakazi 16, wawewabongo wamexico au wazungu who cares, the thing is SHE IS THE BOSS OF HER OWN SELF...yeye hasafishi hayo majumba, na yuko full equiped, unaweza kuning'inia gorofa ya 20 wewe ukafuta vioo! EBO! Watu wanabwabwaja tu.... eti kama mi naown disneyLand.. haha ama kweli mjinga aliyelala usimuamshe, ukimuamsha utalala wewe... Dada Achana na waosha vinywa, hiyo ni sign kubwa ya Kushindwa maisha na kukata tamaa.... Inafurahisha sana kuwepo watu kama hao kwani wanazidi kutupa moyo sisi wenye positive mind na ni changamoto tosha ya kuweza kuonyesha matabaka katika maisha.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 24, 2009

    boksi ni boksi tu

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 24, 2009

    hata km saivi anafanya kazi kwenye iyo kampuni, lkn apo mwanzo box alipiga asikatae historia yake, ndo unataka kutuambia alipofika tu uko akaanzisha iyo kampuni? msituzingue apa.......

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 24, 2009

    Michuzi thanks for vising us....I'm just accross the football field observing you...it can never get better...welcome to DC Michuzi!!!

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 24, 2009

    WEwe mtu wa juu uliyeongelea kuajiri watz wenzake umeleta point nzuri lakini let us be honest how many of us will be ready to put out heart and sould in someone's business especially when we see them making money and they are paying us a regular income? I can guarantee you that if she wants her business not to prosper then she will have wabong in her workforce otherwise we all know who are real workers here in U.S.

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 24, 2009

    Michuzi tupe basi update za DC weekend huko what is happening???

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 24, 2009

    Watu mlioanza michuzi juzi juzi tu mtuachie misemo yetu. Hivi mlizania kubeba box ni kama inavyofikiriwa hivyo? MBEBA BOX NI MTU YEYOTE ANAYETAFUTA MAISHA UGHAIBUNI na kama kuweka makampuni ya watu walio nje ya nchi na wenye nyumba huku mbona tutabanana

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 24, 2009

    Watanzania tuseme ukweli kuwa sisi ni wavivu sana. Kazi tunazichangua hata kama hatuna kitu mfukoni. Kuna Watanzania wachache tu Tanzania au nje wanayeweza kufanya kazi ngumu kama hizi.

    Mimi nina elimu ya Master's ya marekani lakini kabla ya sifafika hapo, nemefanya kazi zote na nakumbuka Watanzania wenzangu wengi walikuwa wananicheka nilipokuwa nasafisha vyoo, nafagia, nalinda maduka na kadhalika. Nilipokuwa Tanzania, nilikuwa na biashara yangu na nakumbuka nilitaka msaada wa kubeba virago vyangu katika nyumba mpya. Wabeba maboxi wa Bongo wanaofanya kazi kubeba maboxi ya wafanyabiashara katika mikokoteni yao nje ya duka langu, walikataa kunisaidia kwa malipo kwa kuwa kazi inabidi iwe jioni, hawataki kuchelewa kufanya starehe baada ya saa 11. Kwao ni bora kukataa elfu 3000 kwa saa moja ya kazi kuliko kuchelewa katika starehe. Tabia hii ya uvivu ipo mpaka leo na ndio inayosababisha umasikini wetu.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 24, 2009

    anoni waa 3:44 acha USHAMBA!! eti wawaachie misemo yenu!! una msemo gani, ni msemo gani duniani ulitungwa na wewe?? kama uliutunga wewe basi uliutunga sababu ya kupiga box. anafundisha michigan state uni au anayefanya kazi ofisini hawezi kuwa mpiga box??
    kwani maisha yanatafutwa ughaibuni peke yake. wanaosoma ughaibuni na wao si wanatafuta maisha pia?? kwa hiyo waliokuja mahususi kwa kusoma kisha wakarudi bongo bila kufanya kazi huku nao watasema walikuwa wanapiga box ughaibuni?? acha ushamba wewe. eti watuachie misemo yetu!!!! halooooo!!! ndio nyie mkiwa bongo mkapata kamsemo kapya ka kiswahili mkarudi kwenu huko madongokuinama ihembe karagwe mnawakoga wabushi wenzenu na vijimisemo vya mjini na hamtaki wenzenu wavitumie!!
    acha ushamba wewe!!!kula box osha wazee mwana uzichange ukirudi kwenu uwe nazo lakini nakuhakikishia wewe hata ukae huko miaka mingapi ukirudi bongonyoso we bado mshamba tu. kuku wa shamba kamba hiyo hutaivua maishani.
    haya kula maisha mwana kufa kwaja

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 24, 2009

    Kwani kuna tofauti gani kati ya "rat catcher" na "rodent officer"?

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 24, 2009

    Ninafarijika kwamba angalau comments 40 zimegusa mioyo ya watu. Swali ni je si jibu kwamba huyu mtu anafanikiwa lakini kwa tabia yetu ya watanzania ni kubebeza kila kitu na kujifanya tunajua? Tusubiri na tuone!

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 24, 2009

    Hongera mama, hakikisha una document zote za hiyo campun yako usije ukawa kama yule mama wa michigan, Kwani naye alikuwa na kampun kama hiyo yako.Tuliombwa michango ya ile apate mwana sheria wa kumsaidia katika kesi yake ambayo hatujui mpaka sasa iliishia wapi. Ni ushauri tu

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 24, 2009

    DA,RUKIA TUAMBIE UNALIPA DOLA NGAPI KWA SAA, WADOGOZAKO TUPO WENGI TAYARI KWA KAZI HIYO WE SEMA NI KIASI GANI UNALIPA KWA SAA. MDAU WA BOX ASIYECHAGUA KAZI.

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 24, 2009

    DADA RUKIA,

    FANYA HARAKA KWA SABABU KUNA RUMAZI TENDA YA KUSAFISHA VILE VIOO VYA TWIN TOWERS (LIYUMBA - KWEKA TOWERS) ZA BENKI KUU WAMEPEWA WASOUTH AFRICA NA MSHIKO WAKE SIYO WA KITOTO.

    EAPOTI YETU NAYO CHAFU KINOMA INAHITAJI SOAP SOAP LA NGUVU. UKIJA MKONTAKTI BWANA MATAKA NA MZEE NYANG'ANYI WAKUPE TENDA.

    USISAHAU KWAMBA MIMASHINE YAKO NA HIYO MIDAWA YA KUSAFISHIA ITAHITAJI WASAFISHAJI WASOMI KIDOGO. KWA HIYO KINA MZEE ZAKARIA NA BIBI KIJAKAZI UTAWAOTESHEA NYASI VIBARUA VYAO. PIA UTAKUKOSESHA MAANDAZI NA CHAPATI TULIZOZOEA KUNUNUA TOKA KWA MACLEANER.

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 24, 2009

    Duh wabongo kweli hatuna mawazo endelevu ukisoma hizi coment nyingi za wivu usio kuwa na mpango wowote
    Oya sister wewe endeleza biashara yako hata siku moja usifuate yale mabaya yalioandikwa umu badala yake yawe chachu ya kusonga mbele
    nakuombea upige hatua zaidi na zaidi.Mdau Canada

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 24, 2009

    Leo ndo nimeamini wabongo wavivu sana! Yaani kumwambia afanye physical labour "box" anaona kama yuko motoni vile! Kila mmoja anataka akae ofisini atafune vitumbua na chai siku nzima!
    Fanyeni kazi, ndo mtajua thamani yake!

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 24, 2009

    We Anonymous wa 11:29 weka address yako hapo nikufahamishe Sehemu moja hivi Box kwa saa 15usd hadi18usd Nguvu yako tu kama upo tayari sema na useme upo wapi usijekuwa unataka kupiga box kumbe upo mbagala utakuwa umechemsha, kazi kwako Mdau mwenye mapenzi mema kwa wabogo.

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 24, 2009

    Watanzania acheni kujifanya wajuaji. Wivu nao ndo unachangia watu kubwabwaja ya kuwakatisha tamaa wengine.
    Walala hoa wasiobahatika kufika unyamwezini na wale waliofika wakarudi bila kuambulia walichokusudia ndo wivu unawakata maini kama hadithi ya Sungura kuzikosa mbivu kisha singizia sizitaki mbichi hizi.
    Huwezi kabisa mlinganisha huyu unayemwita mbeba box na wewe unayajitdai eti mkaa ofisini bongo.
    Mbeba box pato lake la mwizi ni ni zaidi ya pato lako la mwaka mbongo unajebwabwaja manono yasiyokuwa na fikra za kimaendeleo na kiuchumi.
    Kwa taarifa yenu wabongo wengi walio Unyamwezini wana kazi nzuri na hata wanaona wakirudi zao bongo hawawezi pata ajira kama walizo nazo huku. Kumbuka jamaa anaoperate robot sasa akirudi bongo robot ziko wapi? Nilirudi bongo kutafuta kazi nilichoshuhudia sikurudia tena nikaamua nirudie kazi yangu ya unyamzezini kwani bongo hata pato halitoshi hata ghrama za usafiri. Ndo maana ufisadi unazidi kuota mizizi.
    HONGERA D-RUKIA, NAMI NIKO NA YANGU NILIYOFANYA NIKIWA NIMEWAAJIRI WENGINE WANIFANYIE WAKATI NAENDELEA PIA NA AJIRA NYINGINE YA KUPIGA BOX ILIYONIFIKISHA NILIPO.
    Asante Nanhii kwa kutuunganisha wabongo katika hii global villege

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 24, 2009

    Dada Malipula yuko mbali sana kiuchumi.wafanyakazi 16 * 32hr/week * 7 usd/hr unapata = usd 3584 per week.

    kwa makadirio ya chini kabisa Dada Malipula anatumia usd 3000 kwa wiki kwa ajili ya payroll tu.

    hapo hujaongeza mafuta gari, vifaa vya kazi, mawasiliano ya kiofisi etc.

    biashara ya usafishaji haiathiriwi na mitikisiko ya uchumi ya USA. tena kama ana wateja toka taasisi za serikali au mahospitali basi biashara yake ni stable kuliko kuajiriwa.

    hongera sana Dada Malipula.

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 24, 2009

    Watanzania tuna wivu sana. Ukimuomba mtu ushauri jinsi ya kuanzisha mradi fulani atakwambia haiwezekani. Acheni wivu. Huyu dada anapata anapata faida kubwa sana. Watu hatuna chochote lakini wivu tuuu. Marekani kila kazi inalipa. Mkiwa na wivu kamwe hamtasonga mbele. Starehe tu.

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 24, 2009

    anoni wa 3:18 unacheza makidamakida wewe!! eti wafanyakazi wote wa ofisini bongo hawawafikii wapiga box kwa kipato!!! eti kipato cha mpiga box kwa mwezi ni sawa na cha mfanyakazi wa ofisini bongo kwa mwaka mzima!!! mh usinchekeshe mie!! hivi ingekuwa hivyo si wabongo wote wangekimbia nchi wakaja kuunga libeneke la box huko!! hujui ukisemacho wewe. wewe ninaweza kukuweka katika kundi la malimbukeni wa nchi za watu na sijui kwa staili hiyo kama utarudi kwenu wewe!!! nyie ndo wale mkisikia hata baba zenu wamekufa hamji mnaishia kutuma hela!!!
    eti kipato cha mpiga box cha mwezi ni sawa na cha mfanyakazi ofisini bongo kwa mwaka!!! you seem not to even know the shit you talkin'.
    Ipo siku utarudi bongo na kuishia kupata presha tu kwa jinsi watu wanavyosonga mbele. Kwa taarifa yako huku kuna watu wanalipwa hadi $7000 kwa mwezi na wanapigwa viyoyozi ofisini!! wewe kama unalipwa sana kwa mwezi basi itakuwa $3000 sasa hapo ndo pakusema mshahara wako ni wangu wa mwaka??? umechemsha. mimi kwa mfano kwa mwaka nafunga $36,000 na niko ofisini kiyoyozi kwa kasi, safari mikoani za kufa mtu hiyo ni nje ya mshahara, safari za nje ya nchi napata karibia safari 5 kila mwaka we unasema nini bwana!!! kwa taarifa yako sahi bongo tambarare kwa wenye shule. neda kaone mambo ya Afisa Mipango wa wilaya, nenda kaone mambo ya afisa manunuzi na ugavi wa ofisi za serikali na wanakula kiyoyozi kila siku hawabebi box ka wewe, kikubwa zaidi wako nchini kwao amani amani sio wewe mkimbizi huko kila siku kiroho juu unahofia usijitele ukaaribu ukarudishwa bongo!!!! kaangalie watu vodacom, zantel, tigo, TBL, vyuo vikuu, ESRF, REPOA, mawilayani, mikoani, hapo bado hujawatembelea wale wanaofanya makampuni ya madni kama barrick, bila kusau wale walioko mawizarani utachoka ukae chini mwenye. sahvi watu watoto wadogo wametoka vyuo juzi wanadrive magari makali na wanamajumba we unasema nini bwana!!! we hata kama umejenga si ni baada ya kijasho cha kufa mtu huko!!!!
    kwa taarifa yako sahvi vijana maofisini bongo huko state na UK na kwingine wanakujaga likizo tu. round ticket kwa emirates airline ni nusu mshara wangu kwa kifupi mshahara unanunua ticket na kulipa hoteli. binafsi juzi kati hapa nilikuwa atlanta likizo ya wiki mbili tena na demu wangu basi.
    unacheza wewe!! eti mshahara wa mpiga box kwa mwezi ni mshahara wa mwaka bongo!!! inawezeka ni kweli kwa baadhi ya sekta lakini usifanye generalizations!! kama unamaanisha mwalimu wa shule ya msingi au polisi hapo sawa laki kuna ofisi zinalipa mavumba huku usifanye mchezo wewe!!! kwa taarifa yako sahivi watu wanapewa hela ya kwenda shule wanakataa kwa kuona kuwa kipindi atakachokuwa shule atakuwa amekosa mavumba!!!!
    we wafa'mchezo nini!!! kuna mshikaji wangu anakula $8,000 kwa mwezi pale USAID hapahapa dar. na ni professor pia. kwa mwaka hizo ni $96,0000 wa unaongea nini bwana!!!
    hebu ngoja nikuache utanpotezea muda wangu bure limbukeni wa states wewe!!!!
    Ahsante
    Mzee wa blingbling, Chenigoldpetesilver, DSM.

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 24, 2009

    WEWE MZEE WA BLING BLING HATA UTUPANGIE TAKWIMU SIJUI MISHAHARA YA RAFIKI ZAKO, UKWELI NI KWAMBA HATA KAMA UNA EARN MAMILION TZ KWA KUKAA OFISINI NA KUFUNGA TAI, BADO UNA HALI MBAYA KULINGANISHA NA MBEBA BOKS, DIGIST ZINAWEZA ZIKAWA NYINGI LAKINI KWA TZ THEY DON'T MEAN A THING, JE WEWE ZINAKUSAIDIAJE HIZO MILIONI WAKATI KILA MTU ANAZIPATA, POINT NI KWAMBA UTAKUWA NA MAMILIONI UNAYOPATA KWENYE MSHAHARA IKIJA KWENYE MATUMIZI HUNA KITU, KILA SIKU MIFUKO IMEPAUKA, KWANI KULIPWA MILLIONS BONGO SASA HIVI NI ISSUE BWANA? JE WEWE UNAISHIJE NA HIZO MILIONI ZAKO, SANA SANA UNA GARI NA NYUMBA, WAKATI HATA MTU WA KAWAIDA BONGO ANAVYO, DO YOU SAVINGS FOR THE FUTURE, UNA INVESTMENT YOYOTE INAYOELEWEKA AU NDIO DALADALA NA DUKA LA UJENZI, USITAKE KUTUBOA HAPA!

    ReplyDelete
  54. SurvivorDMay 24, 2009

    Ndugu zangu anonymous wa 3:18 na 6:06 (mzee wa bling) pamoja na wabongo wenzangu wengine wote wenye mind set kama za hawa ndugu zetu wawili, mimi ningewashauri hivi:

    Maisha ni popote pale ndugu zangu. Whether uko Houston Texas, Watford Junction England, au K'Koo Dar es salaam Bongo maisha ni popote! Lakini kupata hayo ni MAJAALIWA ya Mwenyezi Mungu pamoja na utulivu, planning, na smartness yako.

    Unaweza ukawa huku nchi za nje ukawa unapata maelfu ya dollars/pounds kwa mwezi lakini yote yakawa yanaishia kwenye bills, kuvaa pamba za gharama, bling bling, na luxury za kila namna zisizo na mwisho huku first world na hivyo kulipwa kwako pesa nyingi kukawa illogical.

    Na vivyo hivyo unaweza ukawa back home (bongo) unafanya kazi ya ofisini kama hiyo ya bw. blingbling na unalipwa mamillion ya sh. lakini pesa yote inapitiliza usikokujua for some unknown reasons (pengine wanawake, umenunua gari limekula mzinga nyang'a nyang'a ukitoka kulewa coz home hawadhibiti usalama barabarani kama huku.. n.k.).

    Wala sioni kama kujivunia mishahara mikubwa whether uko bongo au ughaibuni kwa kazi inayotokana na KUAJIRIWA na mtu au watu ni hekima hata kidogo, kwani kazi ya kuajiriwa inaweza kuisha wakati wowote. Mtu aliye na initiatives za kujiajiri ndiye aliyelenga mbali zaidi hapa, awe Bongo au ughaibuni, hata kama hapati pesa nyingi per annum lakini yuko katika long objective. In a long run huyo yuko more likely kuwa stable & wealthy kuliko hawa ndugu wawili wanaobishana hapa.

    All in all mimi naona badala ya kubishana hivyo in a negative way, tungeelekeza hiyo fierce negative energy ya ushindani kati ya African Diaspora na Ndugu zetu mlioko huko nyumbani, tukashirikiana badala ya kushindana, kifikra, kielimu,na hata kiuchumi, tukawa more supportive to each other rather than hateful - Tungefika mbali sana kama Taifa!

    Hivi ndivyo Wanamibia na Wanigeria walivyo na ushirikiano, Wanigeria saa hizi wana launch mpaka financial instutes zao hapa UK wakiwashirikisha wananchi wao waliowaacha Nigeria na hizi zinawawezesha kurahisisha zaidi funds wire transfers ncjini kwao!! Sisi Watz je tutafikia lini hatua hiyo kama kazi yetu ni kulumbana tu eti nani ana-earn zaidi kushinda mwenzie??

    Wakati sisi tunatembea na kulumbana kama vile tunasindikiza harusi au ngoma ya mdundiko, wenzetu wanakimbia mchakamchaka wa "aliselema alija" huku wakiwa wameshika mikono kwa mshikamano - objective - kuwachomolea capital wazungu na kujijenga kwao!!

    Tuamkeni ndugu zangu Wabongo! Yangu ni hayo tu. N'gwabeja banamhala.

    Survivor
    Mdau UK (Rep. Rock City)

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 25, 2009

    anoni wa 9:40 pointi yako iko wapi??!!! mbona huna point we mama mdogo?? kwanza haileweki uko wapi mi nimesema niko bongo wewe je?? kama ukpo majuu je hizo za box unafanya savings. na kama ndio basi iweje sisi tushindwe kufanya savings? wewe kwa box lako umefanya kipi cha maana kama kujenga nyumba kumiliki magari na kuinvest sio vya maana?? au mwenzetu zako za box zitakupeleka mwezini??? huna point kaa kimya na uendelee na ulimbukeni wako ukitemea kuwa ukizeeka na wewe utaanza kuoshwa kama unavyowaosha wenzako huko!!!! eti ukija kwenye matumizi unabaki huna kitu!!! enhe sasa hiyo kazi itakuwa ya kazi gani kama hatusave??? tunafanya savings na nje tunzitumia kwenda vilevile?? wangapi walikaa states wakafanya kazi maofisini na sasa wamezeeka wako home hapa tunawaona?? akili zako tu bwana maisha hata hapa bongo tambarare tu mbona!!!! we ka' unapata $3500 kwa mwezi huko za box au ofisini basi hata watu wengi tu tunalipwa hizohizo na tuko home, magari makubwa nini!! safari nyingi, na siku hizi bongo ukiwa na kazi nzuri ukawa unazikamatakamata basi ni mamtoni tu yani shwari tu. wengi tumepiga skuli ughaibuni tumerudi tuna kazi bomba na mshiko hevi. $3500 states na $3500 bongo zipi nyingi??? we hizohizo ulipie apartment ambazo ni aghali wapi na wapi bwana!!! kaa ukichoka urudi uone watu na maisha yao huku kama hukuishia frustrations wewe.
    huna point bora yule wa kwanza!!!
    ahsante, karibu.
    Mzee wa blingbling chenigoldpetesilver, DSM.

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 25, 2009

    Profesa Bling Bling: sasa unazo pesa nyingi tu. Je, zinakupa maji safi katika bomba? zinakuletea umeme wa uhakika? Zinakusaidia kuleta usalama kama kuita polisi katika simu au kuita daktari nyumbani wakati wa dharura? Ukiumwa, hizo pesa zako zitakusaidia kukutibu au utalazimika kukimbia India kutibiwa (baada ya kutafuta viza, ndege na barua ya daktari)? Pamoja na pesa zako, kama unaishi Afrika, miaka yako duniani pia imeshapunguzwa. Data za WHO zinasema kuwa average life expectancy Tanzania ni miaka 50.

    Kwa kifupi, fedha zako kama alivyosema anony 9:40 juu, hazikusaidii kuishi vizuri kama yule anayepata fedha kidogo lakini yupo nchi tajiri.

    Mimi naishi Japan na sina mamilioni ya fedha kama wewe. lakini watoto wangu wanafundishwa na walimu waliosoma chuo kikuu. Madaktari wanakuja shule kuangalia afya ya watoto mara 3 kwa mwaka. Watoto pia wanafundishwa kuogelea, kuimba, kupika, kupiga kila aina ya kinanda na kuelimishwa nchi yao kwa kusafiri kuona nchi na wenzao. Nikitoka nje hata saa nane usiku, sitegemei kukabwa na wizi. Polisi na daktari anaweza kuja nyumbani ukimpigia simu ndani ya dakika tano. Usafiri wa kwenda popote upo masaa 24. Naweza kutibiwa na mabingwa wa kila aina ya ugonjwa hapa hapa Japan. Haya mazingira ndio yanayotufanya sisi twende nje kufanya kazi, sio pesa tu. By the way, kama ukiishi hapa, tegemea kuishi zaidi ya miaka 85. Tuna watu 3500 ambao wana umri zaidi ya 100 au zaidi.

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 25, 2009

    mnamwambia mzee wa blingbling asitake kuwaboa. na amewapa ukweli. mnapiga box huko mmkimbia makwenu, wengine mkifiwa mnapandisha maiti kwenye ndege nyie wenyewe hamji kuzika mkidhani bongo ni ile mliyoikimbia!!!
    mzee wa blingbling umewapa ukweli big up mwana wanune wapasuke lakini hiyo ndo ilivyo. dola zenu 3000 kwa mwezi ni sawa na mtu anayelipwa dola 1000 bongo ukiangalia gharama za maisha jamani hata hilo linahitaji muwe na shule kulielewa?? we ukilipwa dola 3000 huko na mimi nikilipwa kama hizo tanzania au kenya tutalingana. tofauti ni kwamba wewe uko mamtoni na mimi niko tanzania lakini kwa kusave mi naweza kusave nyingi zaidi yako.
    huyo mshikaji kawaambia ukweli muache dharau na kujiona mko kwenu huko wakimbizi nyie siku mwenye akichukia kila mtu akatakiwa kurudi kwa si mtakuja nyie. acheni ushamba bwana!!

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 25, 2009

    Rukia habari yako? ni wewe mtoto wa mzee malipula aliyekuwa NAFCO, na kuishi Tabata? Kama ni wewe Botswana umetoka lini? Je Peter hajambo? Kazi njema.
    Kazi ni kazi mradi humwasi mwenyezimungu.

    Dada Mariam.

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 25, 2009

    Nduguzangu waoshavinywa acheni ghadhabu,yanayoongelewa hapa jaribuni kutafakari ndipo mtoe comments zenu,siyo kushambuliana tu, huyu analipwa hivi huyu analipwa hivi, kwanza mgekuwa mnakumbuka kwamba nyie wote ni marehemu watarajiwa,kwamaana saa na dakika yeyote mnawezakutoruhusiwa kucomment hata herufi moja hapa,nafikiri msingetambiana kiasi hicho.Ninacho waomba peaneni taarifa,kwani halingumu yeyoteile iwe ya kukosa pesa,kukosa mahindi,kukosa dhahabu,kukosa mke,kukosa biashara,kukosa,pesa,kukosamchumba,nk nk huwa sababu yake kuu ni kukosa taarifa au ukiritimba wa taarifa. Kwamba wewe unatambua sehemu ambayo pakichimbwa kisima maji yatapatikana lakini taarifa hiyo unakaanayo bila kuwaambia wenzako ambao mgeshikiana kuchimba kisima matokeo yake wote mnakufa kwa kiu, Tarifa,taarifa taarifa jamani ndiyo maana wenzetu wamataifa mengine wanaendelea ni kwa sababu ya kupeana taarifa bila ya kujali utafaidika vipi kwa kumpa mwenzako taarifa.Tusiwe wachoyo wa taarifa kuna wengine wanakaa na taarifa bila kusema ilhali haimsaidii chochote.Wewe unaejiita blingbling japo sielewi unajiita hivyo kwamaana gani,nasidhani kama kweli unalipwa kiasi ulichotaja hii inatokana na jinsi unavyojiita lakini pia ninamashaka na kabila lako na lini umeingiamjini.Anyway ninachotaka kukwambi mh blingbling binafsi sipendinitamke hiyo bling kwasababu naona kama nakutukana lakini kwasababu mwenyewe umependa haya. Wape na wenzio taarifa ninaimani unawafahamu wabongo wengi'tu wapo hapo na wana elimu na hawana kazi na hata wenye kazi wanafanya kazi zisizolingana na elimu walionayo, wengine ni miongoni mwa ndugu zako lakini kupitia unavyojiita ninaimani huwezi na hujawapa taarifa yeyote itakayoweza kuwasaidia. Na hata nyie ndugu zangu mliopo huku ughaibuni kuweni wepesi wa kuwapa wenzenu taarifa,siyo kukaahapa kwa michu na kujidaituuu,haisaidii Nanyie wala vumbi msiwe na dharau kwawabeba box, Kodi tunazolipa huko ndizo hizo mnazoletewa misaada kujengewa miradi ya maji na barabara zisokwisha. Hizo nikodi tunazolipa huku kwa kazi hizohizo za box.Halafu msisahau kuwa "KIDOGO CHA HALALI SI KIKUBWA CHA KABALI" Mdau Majuto-Sweden.

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 25, 2009

    Nduguzangu waoshavinywa acheni ghadhabu,yanayoongelewa hapa jaribuni kutafakari ndipo mtoe comments zenu,siyo kushambuliana tu, huyu analipwa hivi huyu analipwa hivi, kwanza mgekuwa mnakumbuka kwamba nyie wote ni marehemu watarajiwa,kwamaana saa na dakika yeyote mnawezakutoruhusiwa kucomment hata herufi moja hapa,nafikiri msingetambiana kiasi hicho.Ninacho waomba peaneni taarifa,kwani halingumu yeyoteile iwe ya kukosa pesa,kukosa mahindi,kukosa dhahabu,kukosa mke,kukosa biashara,kukosa,pesa,kukosamchumba,nk nk huwa sababu yake kuu ni kukosa taarifa au ukiritimba wa taarifa. Kwamba wewe unatambua sehemu ambayo pakichimbwa kisima maji yatapatikana lakini taarifa hiyo unakaanayo bila kuwaambia wenzako ambao mgeshikiana kuchimba kisima matokeo yake wote mnakufa kwa kiu, Tarifa,taarifa taarifa jamani ndiyo maana wenzetu wamataifa mengine wanaendelea ni kwa sababu ya kupeana taarifa bila ya kujali utafaidika vipi kwa kumpa mwenzako taarifa.Tusiwe wachoyo wa taarifa kuna wengine wanakaa na taarifa bila kusema ilhali haimsaidii chochote.Wewe unaejiita blingbling japo sielewi unajiita hivyo kwamaana gani,nasidhani kama kweli unalipwa kiasi ulichotaja hii inatokana na jinsi unavyojiita lakini pia ninamashaka na kabila lako na lini umeingiamjini.Anyway ninachotaka kukwambi mh blingbling binafsi sipendinitamke hiyo bling kwasababu naona kama nakutukana lakini kwasababu mwenyewe umependa haya. Wape na wenzio taarifa ninaimani unawafahamu wabongo wengi'tu wapo hapo na wana elimu na hawana kazi na hata wenye kazi wanafanya kazi zisizolingana na elimu walionayo, wengine ni miongoni mwa ndugu zako lakini kupitia unavyojiita ninaimani huwezi na hujawapa taarifa yeyote itakayoweza kuwasaidia. Na hata nyie ndugu zangu mliopo huku ughaibuni kuweni wepesi wa kuwapa wenzenu taarifa,siyo kukaahapa kwa michu na kujidaituuu,haisaidii Nanyie wala vumbi msiwe na dharau kwawabeba box, Kodi tunazolipa huko ndizo hizo mnazoletewa misaada kujengewa miradi ya maji na barabara zisokwisha. Hizo nikodi tunazolipa huku kwa kazi hizohizo za box.Halafu msisahau kuwa "KIDOGO CHA HALALI SI KIKUBWA CHA KABALI" Mdau Majuto-Sweden.

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 25, 2009

    Tupeni data . Kuna watu wangapi Tanzania wanapata fedha kama za Profesa Bling Bling? Tusidanganyane hapa. Ni muhimu kujua kuwa sio kila kitu ni pesa tu. Quality ya maisha ndio muhimu zaidi. Asililia ngapi ya Watanzania wanalipwa dola 3000 au 8000 kwa mwezi? Kama kuna mishahara hio kwa nini basi watu wanaenda nje kutafuta kazi kila siku? Tembelea ubalozi wowote wa nchi tajiri utaona mstari mrefu wa wasomi wanaomba visa na kuondoka kila siku. Mimi nilikuja huko 2007 na sijaona tofauti yoyote na 2006, 2005. Pia, maendeleo sio tu mishahara mikubwa ya watu wachache. Niliishi miaka mitatu baada ya kumaliza chuo kikuu Marekani na nilikuwa nalipa gharama sawa sawa na huku. Umeme wa Luku dola 100-150 kwa mwezi kama upo. Kustarehe nje ni gharama pamoja na VAT 20%. Kila mwezi natumia dola 2000 kuishi. Karibu kila kitu Tanzania kinatoka nje. Sasa kuna wangapi Tanzania wanaweza kuishi hivi? Kama unataka uone umasikini nenda kijijini, usidanganyike na majumba mepya ya ghorofa na kudanganya watu hapa sijui mnapata mishahara mikubwa. Ni asilimia chache tu ya Watanzania wenye elimu ya chuo kikuu, na wengi wao ni kama mimi, wanaishi nje kwa sababu wanataka quality ya maisha sio Quantity. Nimefunga biashara yangu kwa mahangaisho ya TRA kila siku pamoja na gharama kubwa ya kufanya biashara kwa kuwa kila kitu lazima tuagize nje na ushuru mkubwa. Nimechagua kuishi nje sio kuwa nilikuwa na shida ya fedha Tanzania, ila nataka kuishi bila kero.

    ReplyDelete
  62. AnonymousMay 25, 2009

    Rukia Malipula hongera shosti....kwa sura nisingekutambua ili kilichokutambulisha kwangu ni the way unavyosimamaga...hilo pose ulilosimama nalo nalikumbuka tangu tukiwa kifungilo....Hongera mwana.

    ReplyDelete
  63. AnonymousMay 25, 2009

    we issa michuzi uweke comment za walala hoi usijifanye matawi ya juu utakufa na ndege shenzi type.Huyo mwenye kampuni ya usafi naye mshamba tu hana kanuni yoyote wenye BillGates hawajitoi lakini maskini hohehae wanajitoa

    ReplyDelete
  64. AnonymousMay 25, 2009

    Ubebe box au usibebe who cares?? As long as you can pay ur bills. Wenzetu wazungu wanaendelea kwa sababu hawabagui kazi. Kwa taarifa yako wabongo wengi tu tunaoishi Marekani tumegraduate na tuna professional jobs. Na ndiyo hizo pesa unazoziita za maboksi tunawatumia wazazi wetu nyumbani kila mwezi na kukukarimu ukija marekani. Owning a cleaning company is okay but nothing compare to what she has to deal with - as a matter of fact if people don't show up to work she has to clean up herself so what's a different from carring a box - jamani pole kwa umbumbumbu.

    ReplyDelete
  65. AnonymousMay 25, 2009

    kweli Bongo kuna watu wanatengeneza pesa ya kufa mtu. mumesikia wenyewe kwamba wabunge wanapata mil 7 kwa mwezi. msije mkashangaa kwamba Kikwete anatengeneza pesa nzuri kuliko Obama per year.

    pia ni ukweli usiopingika kwamba mbeba box wa ughaibuni analipwa vizuri kuliko watumishi wengi sana walioko Bongo.

    uzuri wa hizi kazi za kubeba box ni kwamba walau unapata pango la nyumba, usafiri, TV, na vitu vingine vidogo vidogo. unaweza usifanye mambo makubwa lakini walau uko comfortable.

    ReplyDelete
  66. AnonymousMay 25, 2009

    HONGERA RUKIA KWA KUJIKUNA UNAPOWEZA....... MIMI NAONA KWAMBA WABONGO WOOTE WALIO USA HATA KAMA UNA DEGREE TATU , KWA UFUPI SHUGHULI ZA HAPA KIKAZI NI (BEBABOKSI)... KWANI HATA KAMA UNA KAZI NZURI KIASI GANI USINIAMBIOE WEWE NI MALAIKA UMEKUJA MOJA KWA MOJA SHULE UKAPATA DEGREE UKAWA NA KAZI BILA KUPITIA MISUKOSUKO YA BOKSI..NI ASILIMIA CHACHE SANA.... KUMFANYIA KAZI MMAREKANI NI KUBEBA BOKSI... KWANI HATA VAKESHENI ANAYOPATA MBUNGE WA NANIHIII WENGI WAO HAPA MAREKANI HAWAPATI...LAZIMA UTIE MASAA,UKIPUMUA UNAPEWA KAWIKI KAMOJA....ANGALIA WENZETU WALIO NCHI ZINGINE SIO MPAKA UFANYE MWAKA KUPATA WIKI MOJA...MMAREKANI BWANA ANATUBEBESHA BOKSI MTAKE MSITAKE...THAT IS THE FACT...AS LONG YOU WORK IN THIS COUNTRY U ARE A DARN "MBEBABOKSI"

    ReplyDelete
  67. huyo jamaa mchangiaji hapo juu nafikili atakuwa na matatizo kiakili itakuwaje wewe ulipwe dola 30,000.halabu bado unaendelea kuwa mtumwa wa mtu.ukizingatia hupo bongo

    ReplyDelete
  68. AnonymousMay 26, 2009

    This is non-sense.who cares kama una company ya kusafisha,unabeba maboksi,unalipwa $7000 kwa mwezi.Yaani watu tunajisahau sana.wapo watu wenye mamilioni ya pesa but life zao ziko miserable.Na kila siku watu wanalumbana over money. It's all about happiness and being content.wether uko Abroad au bongo.
    na mdau aliyetoa statistics za WHO kanichekesha. Life is too short.Recipe ya long life ni work hard,eat healthy,exercise,marry someone you love mengine yote yatafall in place

    ReplyDelete
  69. AnonymousMay 26, 2009

    bela dada kamwene bee,makasi,unoge?
    sa ukooo,

    safi sana sana wa'kubomaaa,mwanamke maendeleo kwa kwenda mbele,wahehe juuuuu

    jina la POTTER ina mana ushaolewa nao uko??ni vema sana

    wahungile kukae ukoo

    ReplyDelete
  70. AnonymousMay 26, 2009

    Anony 12:23, Unajisahau kuwa unaishi katika nchi masikini. Kuna watu wangapi wanaweza kununua chakula bora? Ni rahisi kuongea kuwa statistics za WHO zinachekesha lakini ni za ukweli. Watu wangapi wanao magonjwa yanayoweza kutibika lakini hawawezi kwenda kulipa kuona daktari au kwenda nje kutibiwa. Nend akijijini uone kama kuna mwanakijiji mwulize lini amekwenda hospitali kama hio hospitali ipo kijijini. Hao ndio watu wanafanya data zionyeshe kuwa unaishi miaka 50 tu, sio tajiri anayekula vizuri na kuwa na mke bomba anayempenda. Statistics is statistics, it's diffrerent from wishful thinking.

    ReplyDelete
  71. AnonymousMay 26, 2009

    Serikali inazidi kuomba omba kila mwaka kwa kuwa Watanzania wengi wanakwepa kodi. Wakilipa kodi halali angalau serikali itapata fedha zaidi kidogo kugharamia walala hoi. Hao wanaopata mshahara wa dola 8000 utakuta wanalipa dola 100 ushuru au wanaonyesha kuwa wana mishahara midogo serikalini.

    Sisi tulio nje tunalipa kodi na tunaona kodi inavyotumika. Huko hamjui hata meya wa Dar Es Salaam analipwa kiasi gani. Kila kitu ni siri ya taifa.

    Angalia kodi ninayolipa serikali ya Japan. Gharama hizi huwezi kuzikimbia kwa kuwa lazima ujiandikishe katika halmashauri ya jiji, lasivyo umevunja sheria na hapo ndipo wanatuma kodi zote posta na wanataka pesa zao zitoke automatic kutoka benki yako. Bahati nzuri ni kuwa wao pia wanakusaidia kama ukikwama na pia wanatuzawadia mara kwa mara.

    1. State tax: $200 kwa mwezi.

    2. City Tax: $70 kila mwezi.

    3. Safety Car Tax: $2000 baada ya miaka mitatu ya kununua gari ili upate stika inayoonyesha gari lako si bovu na halihatarishi maisha. Bila stika ukikamatwa unatiwa ndani. Kila Miaka miwili kama la zamani. Marekani wanatinga na dola 50 kila mwaka tu kupata stika.

    4. Car tax: $400 kwa gari langu jipya kila mwaka.

    5. Kodi ya ardhi: $100 kwa mwezi.

    6. Pensheni: $175 kila mwezi mpaka miaka 60.

    7. Kadi ya afya: $250 kila mwezi. Nikienda hospitali nalipa %30 ya matibabu yoyote na dawa.

    8. Income tax ya mshahara kila mwezi: $400

    9. Unataka lesensi ya gari? Nenda shule ya kuendesha gari, lipa dola 2000. Utafundishwa miezi sita. Lakini una uhakika wa kupata leseni ukimaliza. Watoa leseni wanaangalia macho tu na kukupa mtihani wa maandishi ya lugha saba. Leseni za kanada, australia, NZ na Uingereza wanapewa leseni za hapa bila kufanya mitihani wala nini. Marekani hamna, ni rahisi sana kupata leseni Marekani. yangu ilinigharimu dola 15 tu na majaribio matatu.

    Hii ni tofauti ya nchi changa na nchi tajiri. Lipa kodi endeleza nchi yako.

    ReplyDelete
  72. Endelea na kazi nzuri Da Rukia! Represent!

    ReplyDelete
  73. AnonymousMay 28, 2009

    keep it up dada rukia...

    hio biashara nadhani ni nzuri ukiwa huko huko US...materials i mean hizo washing products/chemicals ziko available abundantly!

    huku kwetu miji mikubwa kama DAR,ARUSHA..MWANZA...ama ukaenda kwa miji jirani NAIROBI-KENYA,KAMPALA-UGANDA...pia biashara yako...ingetoka vizuri sana,sema hizo chemical products za kuoshea ni lazima U-IMPORT..KUTOKA NJE...which means itakucost...which also means bei zako zitakuwa juu...na bei zikiwa juu...utampata nani??au ndio kupata tenda moja in six month???,,,

    i think km mtu wa nje..unataka kuinvest tanzania then jaribu...kutumia utaalamu/teknolojia/vifaa vya nje...ila ukumbuke mazingira ya hapo nyumbani...na upatikanaji wa raw materials ulivyo...then utadetermine...BEI zako...then ndio utajua kama bussinezz yako iko viable ama hapana...!

    ney-birmingham.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...