Dereva wa Mbunge wa Kyela Dr Harrison Mwakyembe amedaiwa kuwa chanzo cha ajali iliyotaka kupoteza maisha ya mbunge huyo katika kijiji cha Ihemi, Iringa Vijijini baada ya gari lake lililokuwa likiendeshwa na Joseph Msuya (30) kuacha njia umbali wa mita sitini kutoka barabara kuu iendeayo Dar es Salaam, kugonga mti na kisha kupinduka.

Hayo yamo katika taarifa ya Kamati iliyoundwa na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema kuchunguza chanzo cha ajali hiyo .
Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Barabara nchini, James Kombe alisema baada ya uchunguzi wao kamati imebaini kwamba chanzo chake hakikuwa roli lililokuwa linapitwa kama alivyopata kunukuliwa mbunge huyo, bali dereva wa mbunge huyo aliyekuwa akiendesha gari hilo kwa mwendo mkali.

“Kamati imefika eneo la tukio na kuwahoji mashuhuda walioona gari la mbunge huyo kabla na baada ya kupata ajali, kukagua gari la mbunge pamoja na kumhoji mtaalam wa magari aliyesomea uingereza, Francis Mwakatundu ambaye ameonyesha kupingana na kauli ya mbunge huyo kuwa aligongwa baada ya kuchunguza gari hilo na kuona hakuna sehemu ambayo ilionyesha kugongwa” alisema.

Alisema uchunguzi wao haukuona alama yoyote ambayo inayothibitisha kwamba gari la mbunge huyo liligongwa kwa nyuma au upande mwingine wowote. Alisema mikwaruzo iliyopo ni ile iliyotokana na gari hilo kuacha njia na kubiringika porini zaidi ya mita 60 kabla ya kugonga jiwe kubwa na kuling’oa na baadaye kuparamia mti mkubwa wenye mzunguko wa sentimeta 115 hadi kuung’oa na hivyo kupinduka.

Kamati hiyo iliundwa baada ya kuwepo na taarifa tofauti toka jeshi la Polisi, Mbunge huyo na dereva wake.

Pamoja na maelezo hayo kamati ilishauri:
-Ikumbukwe kwamba mwendo ulioruhusiwa kisheria ni spidi 80 kwa saa na kwamba ajali zinapotokea waviache vyombo vinavyohusika vichunguze
- Barabara hiyo ni mbaya kwa kuwa ina mashimo mengi hivyo inastahili kufanyiwa matengenezo.
- Magari ya viongozi yasifungwe kispoti na wasitumie matairi yasio na mipira kwa kuwa usalama wake ni mdogo ukilinganisha na matairi yenye mipira.
-madereva wawe waangalifu na kuzingatia sheria zingine zote za usalama barabarani .
Kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo ilihusisha Jeshi la Polisi, TANROADS, Wataalamu wa Ufundi wa Magari, na Daktari mmoja ambaye ni mtaalamu wa uchunguzi wa ajali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

 1. AnonymousMay 26, 2009

  Yametoka kwa mpoki.blogspot.com.Kweli tume inategemea tuiamini baada ya maswali haya??
  Anonymous said...
  Tume hii siyo professional wala haina powers za reasoning.Tume ya kufunika ukweli.Maswali haya iyajibu:

  1. Kuna dereva wa lori amehusishwa na ''ajali'' hii katika maelezo ya dereva wa mbunge. Dereva wa lori 'kajitokeza' Tanzania Daima na maelezo yake na hajajitokeza Polisi na wala Polisi haimtafuti yeye wala lori lake. Kwa nini?

  2. Kombe anamuonya mbunge asiszungumzie ''ajali'' kwenye vyombo vya habari, wakati Kombe mwenyewe anatoa onyo hilo na kuzungumzia mengi tu kuhusu ajali hii kupitia vyombo vya habari. Kwa nini asijionye mwenyewe kwanza?

  3.RPC wa Iringa saa chahche tu baada ya ''ajali'' alizungumza na vyombo vya habari na kusema hakuna mkono wa mtu katika ajali hii na stori kubwa tu ikatoka The Citizen, kwa mfano. Je Kombe amemuonya RPC? Na wakati RPC anazungumza hata mbunge alikuwa hajachukuliwa maelezo yake!!!

  4. Dereva wa lori nae 'aliyejitokeza' Tanzania Daima nae ameonywa asizungumzie ajali hii kwenye vyombo vya habari?

  5. Kombe na tume yake wasitufanye watoto. This is a very cheap propaganda job they are doing

  26.5.09


  Anonymous said...
  Hii tume ina spidi kweli, kuliko hata dereva wa Mwakyembe! Tume iwe na uangalifu isije ikasababisha ajali!! Polisi wangekuwa na spidi kama hii kuwashughulikia mafisadi sidhani kama hata mafisadi wangepata nafasi ya kutuhujumu.
  Inaelekea kuna spidi ya kuwashughulikia kina Mwakyembe na dereva wake na kuwageuzia kibao na spidi ingine tofauti ya kuwashughulikia kina Ro..., Sai..., Man... na washirika wengine wa kifisadi.
  Tuko macho Kombe tunakuangalia!!!

  26.5.09


  Anonymous said...
  Kombe tuko macho tunakucheki hata kama viti vyetu tumelaza!!!

  26.5.09

  ReplyDelete
 2. AnonymousMay 26, 2009

  hivi jamani ni samahani kwa usumbufu neno ni sahihi hapo ni "ROLI" au ni "LORI". lakini ndio maana waandishi wengi wa tanzania wanaambiwa elimu duni!!

  ReplyDelete
 3. AnonymousMay 26, 2009

  huyo hapo ni mgambo wa jiji, paparazi,au wataalamu wa mabomu.???
  sasa anatafuta ushahidi au anasevu laifu za watu?

  na huyu aliempiga picha je?? hahahahhah teh teh kwa kwa kwa kwa au ni bro michuuu???

  taswiiiraaaaazzzzzzzz

  ReplyDelete
 4. AnonymousMay 26, 2009

  Mzee Kombe ee, wachana na longo longo hizo.Tunakuheshimu wewe, Mzee wa Kanisa KKKT Goliondoi Rd pale Arusha. Si ajabu hata huo uliko Mzee wa Kanisa, sasa janja ulongo funika funika ya nini tena?

  ReplyDelete
 5. AnonymousMay 26, 2009

  "KUPOTEZA MAISHA KWA MBUNGE HUYO" JAMANI KWANI MWAKYEMBE AMEKUFA? HII HABARI MIMI SIJAISIKIA, NAOMBA UFAFANUZI

  ReplyDelete
 6. AnonymousMay 26, 2009

  hii tume kiboko inabidi ipewe award du!!! yani tume zote zingekuwa zinafanya kazi kama tume hii tungekuwa mbali sana! hivi na ile tume iliyoundwa kuchunguza ajali ya chenge ilishatoa ripoti vile!!! mungu ibariki Tz

  ReplyDelete
 7. AnonymousMay 26, 2009

  Hawa kina myakwyembwe nao u-bwana u-kubwa umewazidi sana, mimi binafsi sioni tatizo lolote la mbunge au hata waziri kuendesha gari yake mwenyewe.

  ReplyDelete
 8. AnonymousMay 26, 2009

  There goes another scape goat! Masikini huyo dereva!!!!
  J.
  Toronto

  ReplyDelete
 9. AnonymousMay 26, 2009

  Dr. Mwakyembe amefariki? Michuzi hii ni sawa? " ..dereva wa Mbunge wa Kyela Dr Harrison Mwakyembe amedaiwa kuwa chanzo cha ajali iliyotaka kupoteza maisha ya mbunge huyo katika kijiji cha Ihemi . . . ". Nilikuwa sijasikia hiyo. Kama ni kweli basi ni hatari sana TZ. Mimi na siasa basi tena.

  Mdau W.L.

  ReplyDelete
 10. AnonymousMay 26, 2009

  Tume zote zingekuwa zinafanya kazi kwa spidi namna hii tungefika mbali sana. Inaonekana zaidi iko kwenye kujihami kuliko kutafuta ukweli.

  ReplyDelete
 11. AnonymousMay 27, 2009

  Inashangaza sana kuhusu lile shimo wanalozungumzia kuwa nichanzo cha ajali kukarabatiwa kwa haraka kiasi hicho.

  Ajali zote zitokeazo katika hiyo barabara wala sijawahi sikia zimeundiwa tume au kufanyiwa uchunguzi.

  Na wanahabari wetu wamekuwa wakizungumzia kila mara kuhusu hiyo barabara na hakuna hatua yoyote ilochukuliwa.

  Yangu macho, kazi kwenu tume!

  ReplyDelete
 12. AnonymousMay 27, 2009

  Tume inashauri magari ya wabunge YASIFUNGWE KISPOTI hii maana yake nini wadau?

  ReplyDelete
 13. AnonymousMay 27, 2009

  Madu mtoa maoni 8:1PM umezungumza na kutukumbusha la maana. tume ya ajali ya Chenge sijui kama imetoa ripoti. Lakini tume ile na Polisi hakika hawakufanya kazi na mbwembwe na PR na kulalia upande mmoja kama hii ya Kombe. Alafu Polisi na tume waliganagamala mpaka dereva wa bajaj aliyepotea kiaina baada ya ajali na mmiliki wa bajaj aliyejificha kwa siku nyingi wakapatikana. Sasa hii ajali ya Mwakyembe vipi mbona dereva wa lori iliyobetua Land Cruiser ya Mwakyembe hapatikani wala hatafutwi anazungumza tu kupitia Tanzania Daima (Jumapili 24May 2009)na analindwa bila kutajwa jina, bila kupigwa picha na bila hata kusakwa na Polisi.Yuko huru na anapeta. Alafu taarifa za ripoti za tume na taarifa za Tanzania Daima zinashabihiana mno. Jamani eee kulikoni???? Freeman Mbowe, Dr Slaa, Zitto Kabwe mumemuuzia fisadi fulani hilo gazeti??

  ReplyDelete
 14. AnonymousMay 27, 2009

  NASHANGAA TUME ILIUNDWA YA NINI KAMA SI KUPOTEZA PESA ZA WALIPA KODI.DEREVA BAADA YA AJALI KUTOKEA ALISHA SEMA ALIOMBA KUOVATEKI MARA TATU DEREVA WA ROLI HAKUMRUHUSU AKAMUA KUPITA KWANGUVU,MAELEZO YAKE YAMEJITOSHELEZA KUWA ANA MAKOSA NA SI DEREVA MAKINI HAFAI.PAMOJA MA UBOVU WA BARABARA SPIDI 80 KWA SAA HAIFAI,WENZETU WENYE MIUNDO MBINU YA UHAKAIKA(UK) SHERIA NI SPIDI 7O KWA SAA KWENYE MOTORWAYS,PIA SHERIA ZA LESENI ZIBADILISHWE MADEREVA WAKAE DARASANI WASOME WAFANYE MTIHANI WA WA SHERIA NA UMAKINI WA DEREVA,KABLA AWAJA FANYIWA MAJARIBIO YA VITENDO(KUNDESHA)NDIPO WAPATE LESENI.VINGINEVYO AJALI AZITOKOMA.

  ReplyDelete
 15. AnonymousMay 27, 2009

  Wadau, tuangalieni na upande wa pili wa shilingi, hivi hawa wabunge wetu wanaajiri madereva wenye ujuzi wa uendeshaji au ndugu zao ili wawape ajira? kwa sababu tumepoteza wabunge wengi sana kwa ajali za magari yao.mbunge analipwa mshahara na marupurupu ya dereva lakini wanakimbilia kuwachukuwa ndugu zao ili wawape mshahara tu, tena mdogo na marupurupu yote wanakula wenyewe.

  ReplyDelete
 16. AnonymousMay 27, 2009

  Mimi nashindwa kuwaelewa watzd kwa ujumla wao kwani hupoteza muda kujadili jambo ambalo limeshapita wapo wahusika kulifuatilia tunabaki kufikiria masuala ya ajali na kusahau ufisadi unnaotutafuna kila kukicha jamani tufunguke akili na waandishi wa habari tumechoka kuyumbishwa na mihabari yenu ya kutuchanganya halafu magazeti yenu tukisoma kila baada ya maneno mawili matatu lazima unakuta maneno yamekosewa jamani shule tulizosoma mnawaangusha waalimu au mlinyakwa

  ReplyDelete
 17. AnonymousMay 27, 2009

  mm nashangaa sana , we have a lot of our tanzanian wanakufa kwa ajali na hatufuatilii kwa tume kuundwa kama hizi za waheshimiwa. mfano: Tanga-muheza early this year wa2 26 walifariki na wengi kujeruhiwa, mbona hawa hatukuwasemea??? Arusha mto nduruma wa2 zaid ya 11 walikufa pia...... ni wengi etc. kwa nn huyu m2 mmoja tu tena hata hajafa lakin tume inaundwa na mijadala inakuwa mikubwa???
  kwa nn tusiamini Dr. mwakyembe nae kapata ajali kama watanzania wengine wanavyopata ajali??
  honestly serikali yetu haiko fair pamoja na ss wenyewe.
  nikitazama comments za wa2 wengi hapa ni kama mwakyembe hastahili ajali!!
  we r all human being, 2 me i c az an accident not otherwyz

  nevava

  ReplyDelete
 18. AnonymousMay 27, 2009

  mm nashangaa sana , we have a lot of our tanzanian wanakufa kwa ajali na hatufuatilii kwa tume kuundwa kama hizi za waheshimiwa. mfano: Tanga-muheza early this year wa2 26 walifariki na wengi kujeruhiwa, mbona hawa hatukuwasemea??? Arusha mto nduruma wa2 zaid ya 11 walikufa pia...... ni wengi etc. kwa nn huyu m2 mmoja tu tena hata hajafa lakin tume inaundwa na mijadala inakuwa mikubwa???
  kwa nn tusiamini Dr. mwakyembe nae kapata ajali kama watanzania wengine wanavyopata ajali??
  honestly serikali yetu haiko fair pamoja na ss wenyewe.
  nikitazama comments za wa2 wengi hapa ni kama mwakyembe hastahili ajali!!
  we r all human being, 2 me i c az an accident not otherwyz

  nevava

  ReplyDelete
 19. AnonymousMay 27, 2009

  Mkuu Anonymous May 27, 2009 12:31 PM
  Si kweli dereva aliomba mara tatau na hatimae alikubaliwa baada ya kukataliwa kwanza.Alipofika katikati kumovateki lori likabana tena upande wa gari lililokuwa likiovateki na kuongeza mwendo. Ikabidi gari nayo iongeze mwendo maana ilishafika katikati na mbele kulikuwa na Coaster.
  Ilipokuwa ikmalizia kuovateki ikabetuliwa na lori, gari ya mbunge ikayumba kushoto na kulia kutokana na kubetuliwa huko na hatimae ikaangukia upande wa kushoto wa bara bara.
  maelezo ya dereva aidha kwenye Mwana Halisi ya leo yanasema traffic hawakuwa na msaada baada ya ajali na walikuwa wakimshawishi dereva aende mjini akapate matibabu amuache mbunge pale kwenye tukio maana walisadiki ameshakufa, kumbe kazirai.Dereva hakukubali na akatoa first aid kwa kupump kifuani na mbunge akazinduka hatimae.Sasa haya maelezo hayamo kwenye ripoti ya tume Kombe kwa maana Dereva wa mbunge wala mbunge mwenyewe hawakuhusishwa na tume katika utafiti tume.
  Zaidi dereva wa ile lori hakusimamishwa, kwa road block labda mbele ya safari, wala hatafutwi na Polisi, wala hajachukuliwa maelezo na traffic, wala gari yake haijachorwa kwenye mchoro wa ajali, wala hajajitokeza polisi; lakini dereva wa lori alitimua mbio zaidi baada ya gari ya mbunge kupinduka na akajitokeza gazeti la Tanzania Daima (Jumapili Mei 24 2009) kazungumza nao na kutoa maelezo yake gazetini huku akilindwa bila jina lake kuandikwa wala picha yake kutolewa. Na dereva wa lori hajaonywa na kamanda Kombe asiszungumze na vyombo vya habari lakini amemuonya mbunge asizungumze na vyombo vya habari.
  Alafu ajali ya Mbatia haikuwa na tume, ajali ya Sokoine haikuwa na tume, ajali ya Namfua haikuwa na tume. Vipi hii kiongozi kaoswakoswa in tume? Lakini tume isiyomhoji mbunge wala kumshirikisha yeye wala dereva wake? Vipi ?
  Linganisha na tume ya ajali ya Chenge aliyegonga (tofauti na wengine hakugongwa wala maisha yake hayakuwa hatarini yeye ndiye alihatarisha maisha na kupoteza ya wengine), dereva wa bajaj aliyepotea kwenye tukio kapatikana na mwenye bajaj kapatikana baada ya polisi kuchakarika kwa siku chache tu.
  Yote haya unaona sawa tu na tume na traffic imefanya kazi yake vizuri tu?? Wewe bado umeridhika tu na mwenendo huu wa mambo? Mimi naona tangu mwanzo polisi na tume vilidhamiria kumuangamiza mbunge.

  ReplyDelete
 20. AnonymousMay 28, 2009

  Jamani turudi nyuma twende mbele, mie nashindwa kabisa kuwaelewa hawa watendaji wetu wa serikali pamoja na viongozi, kwa sababu kuna yule askari aliyepigwa risasi akipambana na majambazi pale kariakoo mpaka kufanikisha kupatikana kwa pesa kiasi zilizokombwa na hao majambazi.Baada ya kupelekwa hospitali ya muhimbili wakamwambia kuwa hawawezi kumtibu kutokana na jeraha lake lilipo (begani) na badala yake wakamruhusu arudi nyumbani akapumzike mpaka mwisho wa uhai wake na kushindwa kufikiria hata labda kumpeleka nje ya nchi eti hawana uwezo,ila hili la mwakyembe wamelivalia njuga mpaka kuundiwa tume wakati mtu mwenyewe hajafa bali ni mzima. hebu tutafakali, mie naumia sana japokuwa hata mie ni mtu wa huko huko kwa Mwakyembe!!!!

  ReplyDelete
 21. AnonymousMay 28, 2009

  Huu ni ubabe usiyo na akili bwana anonymous May 28 2:04. Kama hoja yako mpaka itegemee unakotoka basi hoja yako dhaifu.Argument ad hominem wanasema wataalam wa sheria na lojiki.
  Mwakyembe wako kapangiwa ajali, lengo lake limeshindikana sasa kuna tume ya kufunika mambo na kumsulubu:kaambiwa asizungumze na vyombo vya habari na Kombe wakati Kombe mwenyewe na RPC Iringa na dereva wa lori wanachonga sana kwenye vyombo vya habari kuhusu ajali hii hii. Dereva wa lori wala hatafutwi na polisi wala tume, hata dereva wa costa na abiria wake waliyoshuhudia 'ajali' hawashirikishwi kwenye uchunguzi wa tume wala Mwakyembe wala dereva wake.
  Kwa hiyo umeliwa mara mbili Mwakyembe wako na huyo polisi wako mwenye risasi mwilini.
  alafu kwa taarifa viongozi wangapi wam wamepata ajali lakini hakuna tume iliyoundwa: Sokoine, Namfua, Mbatia, Wangwe hakuna tume.

  Labda ajali ya Chenge lakini polisi walichakarika kweli kumtafuta dereva wa gari ingine ilikuwemo kwenye ajali yake wa bajaj na mwenye bajaj mpaka wakawapata- lakini kwa mwakyembe hakuna cha kumtafuta dereva wa lori wala mwenye lori.
  Kuna namna hapa mwanangu umeliwa mara mbili kwa Mwakyembe wa kwenu na polisi unaemhurumia!!!!!Pole kaka.

  ReplyDelete
 22. AnonymousMay 29, 2009

  Press release ya Fk mbona umeiminya Michu. Mi nadhani inaeleza vizuri maoni yake kuhusu hili sakata? Tena inaumbua tume ya jali ya Mwakyembe na polisi na watu wanaweza kuelewa nini maoni yake hasa.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...