mwili wa moja ya hayo majambazi ukipelekwa mochuari

shaba si mchezo. askari na raia wakiwa wamebana nyuma ya farasi mweupe wakati muziki unalia...

mtaa wa swahili ulikuwa hekaheka asubuhi ya leo

kama kawa wadau wakishuhudia shaba zinavyopigwa badala ya kukimbia hatari

jamaa wamebana karibu na hii gari kulia. mmoja wao amevaa mkanda wa risasi na anamwaga njugu kama hana akili nzuri....

MPAMBANO KATI YA POLISI NA WANAOSHUKIWA KUWA MAJAMBAZI MTAA SWAHILI UMEMALIZIKA NA FARASI WEUPE (LAND CRUISER ) ZA POLISI ZIMEONDOKA ENEO LA TUKIO LIKIWA NA MIILI YA WATU WATATU WAKIWA WAMELALA SAKAFUNI NA WATATU WANAOONEKANA WAJERUHIWA.

HAIJAJULIKANA KAMA KUNA WALIOPOTEZA MAISHA KWANI TUKIO LENYEWE LA KUONDOKA ENEO LA TUKIO LIMECHUKUA DAKIKA CHACHE MNO. HABARI ZINASEMA WALIVAMIA DUKA LA MFANYABIASHARA MMOJA NA FFU WALIMALIZA MCHEZO NDANI YA DAKIKA TANO TU.
KWA KUWA HII NI HABARI INAYOKIMBIA (RUNNING STORY) TEGEMEA ZAIDI BAADAYE.

----------------------------------------------------------------

GLOBU YA JAMII INATOA ASANTE NA PONGEZI KWA MDAU AMBAYE AMEWEZA KUTUPASHA NA KUTUREKODIA TUKIO HILI KWA KADRI YA UWEZO WAKE, YOTE IKIWA NI KATIKA KUENDELEZA LIBENEKE. KWA KUWA HATAKI KUTAJWA JINA ZAWADI YAKE NAYO UNABAKIA KUWA SIRI.



GLOBU HII YA JAMII PIA INATOA MWITO KWA MDAU YEYOTE MWENYE HABARI KAMA HIZI AZILETE CHAP CHAP KUPITIA

issamichuzi@gmail.com

NA ITARUSHWA HEWANI MARA MOJA, MRADI IWE YA UKWELI NA UHAKIKA.



-MICHUZI





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 08, 2009

    NILIKUWEPO MAENEO HAYO, YANI ILIKUWA KAMA SOUH AFRICA, NACHUKUWA NAFASI HII KUKUPONGEZA KWA KUTUPATIA HABARI HII AS BREAKING NEWS.

    ReplyDelete
  2. Ahsante mdau kwa taarifa -keep it up

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 08, 2009

    AYA TUNASUBIRI IZO VITA ZA BONGO SIKU IZI,

    jaman,Mungu pishilia mbali

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 08, 2009

    Maskini wabantu sie, kama kawaida tunakimbilia kushuhudia badala ya kuikimbia hatari! Hivi kweli serikali ianze kutumia pesa kuwaelimisha watu kuikimbia hatari badala ya kuikimbilia? When do we ever learn?!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 08, 2009

    kweli sisi tunafurahisha, zingatia askari wanavyoogopa shaba lakini wakalamba wameshika viuno wanazinusa badala ya kukimbia waache ffu wafanye kazi, hivi akili zetu zina akili kweli?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 08, 2009

    DUH........UJAMBAZI UMEZIDI KEEP IT UP JESHI LA POLISI KUMALIZA ILI JANGA LA UJAMBAZI DAR-ARUSH AND MOSHI.

    PICHA BOMBA SANA THANKS MICHUZI......DUH KALIAKOO SIO MASIALA MAJENGO MAZURI SANAAAAAAA

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 08, 2009

    MABOMU YA MBAGALA TU YALIKUA KIZAAZA UTASEMAJE UNASUBILI VITA VYA BONGO KAMA HUNA CHA KUCHANGIA BORA UKAE KIMYA.

    HONGERA MDAU KWA TAARIFA KEEP IT UP!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 08, 2009

    baadaye hao wataitwa raia wema na polisi mashitaka.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 08, 2009

    Pesa za nchi zinaliwa na mafisadi, ajira hakuna watu waishije sasa zaidi ya kibabe?

    Wananchi wa kawaida ndio wanabaki kuteseka na kuonewa wakiiba hata ua mfano yule aliyeiba ua IKULU wanashtakiwa na kuhukumiwa. Unategemea wafanye nini? Kama ni amri yangu mwizi yeyote kwanzia sasa akiiba asihukumiwe kifungo aachiwe hadi Mafisadi walio iba mabilioni wahukumiwe kwanza...Wangewaacha hao waliokuwa wanataka kuiba wapate rizki zao waondoke ilimradi wasimdhuru mtu tuu..

    Aibae kuku anaonekana, aibae ng'ombe haonekani WHYYYY

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 08, 2009

    Big up majambazi...VITA NI VITA....Kila mtu aibr katika sekta zake....Za mafisadi serikalini za majambazi majumba ya biashara...Mwalimu shuleni..Konda na dereva ktk daladala. Ngoma droo...Wizi tuuuu...

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 08, 2009

    Hawa FFU Nao Sifa Za Kijinga .Watu Tunataka Kuanza Kurudisha Kilicho Cha Wananchi. Na Bado Kama Vita Ya Kugomboa Nchi Kwa Mapapa na manyangumi Mnaogopa Bola Tuchapane Kurudisha Japo Mrithi

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 08, 2009

    Kitu cha kwanza polisi walitakiwa kufanya ni kuzuia watu wasiwe karibu na tukio na sio kushirikiana nao.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 08, 2009

    Maskini nchi imeharibika jamani, du juzi mabomu mbagala, sasa vita katikati ya mji, tutafika!!??. Jambazi anapata wapi SMG, au ndio madili ya kulipua ghala ili waibe silaha? Hii inasikitisha sana, haiwezekana hizo silaha wanazotumia majambazi zikaanguka kutoka mbinguni, watakua na ushirikiano na jeshi.

    Mdau Trd norway

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 08, 2009

    DAH! MICHUZI UNAHITAJI UPEWE PONGEZI KUBWA SANAAAA KWA KAZI YAKO UPO MAKINI SANA NA KAZI MZEE BIG UP ILA NINYI WATU AMBAO MNAULIZIA VITA HIVI MNAKUWAJE AKILI ZENU MBONA HAZIELEWEKI JUZI MABOMU YAMELIPUKA YENYEWE TUU INSHUUUU JE VITA.

    MISUPU HONGERA SANA.
    MDAU KUTOKA TEMEKE.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 08, 2009

    BABU KUBWA KASI MPYA NGUVU MPYA

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 08, 2009

    wewe anonymus wa may 8/2009/saa12:57 sikubaliani na ushauri unaotoa wa watu kuchapana,maana hujawahi kuwepo ktk maeneo ambako kuna machafuko ya watu kuuwana ukaona inavypkuwa taabu!!wanaoteseka ni watoto wasio na hatia[innocent children who knows nothing about the war and its source!] na wazee watu wazima vikongwe wasioweza kujiokoa.
    USHAURI WAKO ULAANIWE!!
    **************************
    Njia pekee ya kupambana na kuweka utawala bora wa haki sawa na sheria,ni pale unapo ondoa ujinga ktk vichwa vya watu,sasahivi hata wengi wanaodai wameelimika bado wana NUNULIKA! na hapa ndipo mzizi wa mambo na fitna zote ulipochimbika.
    unatakiwa ulewe kuwa ubepari sikuzote unazingatia maximum profit under the expens of the weak! na law ya darwin inasema ukiweka viumbe zaidi ya mmoja ktk kushindania kujipatia malighafi ya kuvifanya viishi tokea chanzo kimmoja cha malighafi, basi chenye nguvu ndicho kitakasho stahimili.
    mapapa mnawanenepesha wenyewe!maana ukiambiwa agiza bidhaa toka ng'ambo UNALIA OOH MTAJI SINA! ukiambiwa haya zalisha basi kwa kutumia teknolojia yako UNALIA OOH SINA VIFAA! ukiambiwa BUNI basi vifaa vyako UNALIA OOH sijui MIMI MASKINI-wa akili!!
    bidhaa zikikosa OOH serikali inatuuwa,mbona bidhaa hazipo madukani!!
    HADI NASHINDWA SASA JINSI GANI WANANCHI WASAIDIWE,MAANA HATA PA KUANZIA PANACHANGANYA, sijui elimu kwanza,na kama ni elimu ni elimu gani hasa maana hii ya kutokea kwingine inaonekana nimzigo haieleweki,walio ileta wako kilomita milioni kadhaa mbele sisi ndo tunajikongoja walikopita karne kibao zilizopita.
    ***********************************
    USHAURI WANGU:-
    1)amani idumu watu wapate muda wa kujipanga kufikiri ninikifanyike
    2)ukinunuliwa kubali kuteswa pia ili kulipa gharama.
    3)walioendelea walipata shida ndiyo iliwafungua macho,historia haikwepeki na huwezi kuruka stage ktk maisha,vinginevyo utairudia tu!sasa ndio wakati muafaka wa kuchemsha ubongo ili mwenye wazo la kimaendeleo aliweke mezani kuwashiikisha wenye mtizamo sawa na yeye waliweke ktk vitendo

    MWISHO:
    UKISIKIA MLIPUKO KIMBIA SANA USIJE JIKUTA NA ULEMAVU WA MAISHA AU UKAJIKUTA AKHERA WITHIN AFRACTION OF A SECOND
    XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
    3)

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 08, 2009

    "....kavaa mkanda wa risasi,anamwaga njugu kama hana akili nzuri..."

    na watu wamejaa wanamshangaa "shujaa-rambo" jamabaz uyo alobeba mkanda wa njugu,ivi wangeamua kumfanya mtu ngao apo???

    yan watu wanashangaza sana!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 08, 2009

    hivi wewe anoy wa 1:04 unayesema askari wangezuia watu kwanza una ubongo? Shughuli nzima ilikuwa dk takrbani 5 halafu ulitaka watumie 15 kuondoa wajinga hao. safari ijayo FFU beba maji ya upupu usambaze watu, kati yao si ajabu kulikuwa na majambazi wanatumia kinga. Ifike muda watu watumie ubongo kufikiri sio miguu.Hili lilikuwa tukio la ujambazi na sio mchezo wa kidalipoo

    ReplyDelete
  19. Mim naipenda blog ya jamii kwa nyuz bin nyuz bin fastar kama leo niko hapa Darwin nikaona nipitie blog yetu nikaona nyuz hiii kwa kuwa hilo she she liko karibu na mtaani kwetu ngoja niwapigie simu wengi wao walikuwa hawajui kulikon ingawa walisikia milio ya risasi mwengine alikuwa msalani akaona abanishi uko uko hahahahah safi michuzi na mleta habari hii

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 08, 2009

    SMG

    ????????

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 08, 2009

    Mmoja kati ya hao majambazi hao alizama katika nyumba ya mshkaji wetu mmoja mtaa wa Swahili mwenyewe alikuwa kalala hana habari, alivyosikia njugu zikilia akatoka ili achungulie polisi walivyokuwa hawana busara wakaendelea ku-shoot bahati aliwahi kurudi ndani ndio majirani wakawafahamisha watoto wa Kova kuwa huyo aliyekuwa natoka si jambazi wakamwambia atoke kisha wakazama ndani na kumdokoa mzee wa kazi kiulaiiini baada ya kuishiwa njugu na kurushiwa bomu la machozi juu ya dari alipokuwa kajificha. Polisi kuweni makini kwenye matukio kama haya mtakuja kuua raia wema!

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 08, 2009

    wAMETOA WAPI SILAHA? AU NI JWTZ?

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 08, 2009

    Raia Wema na Majambazi ni rahisi kung'amua kama upi ni mchele na upi ni pumba. Huhitaji kwenda shule kujua hilo hivyo mdau hapo juu tumia ubongo wako ipasavyo !!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 08, 2009

    Raia wema na majambazi ni rahisi kungamua======
    Nakubaliana na mdau
    Good guys wear white hats
    Bad guys wear black hats
    Just like in cowboy films
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 09, 2009

    Michuzi

    Unasema habari iwe ya ukweli na uhakika, kwani habari inaweza kuwa ya ukweli lakini haina uhakika?

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 09, 2009

    Kweli ni majambaz kutokana na habari inavyoonyesha Hata kama Je Vipi binaadamu anaburuzwa kwenye gari kama mzoga!hana haki ya kiibinaadamu kuhifadhiwa vizuri?Inaumiza kuona jinsi watu watendao makosa wanavyokuwa treated na hasa hasa kwetu afrika.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 09, 2009

    Niliwahi kusikia kuwa Polisi wamepatiwa vifaa vya kisasa kupambana na majambazi nikimaanisha mavazi ya kuzuia risasi wawapo katika mapambano ya ana kwa ana ,lakini hapa naona wengine vipara kofia za kawaida na nguo za kawaida za kiaskari,Je Mkuu wa polisi vipi anaweza kuwatelekeza vijana hawa katika kazi hii ya kurushiana risasi ,na ilivyokuwa wao ni polisi walitakiwa wawe wamekamilika kivifaa hata zile bunduki zilizofungwa darubini ili kuweza kumpiga jambazi kwa mbali na pia kuweza kuchagua sehemu ili waweze kuwapata wengine wakiwa live ,au ndio askari wetu hawahitaji visaidizi katika kumtunga jambazi ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...