nyota wa filamu bongo ray na kanumba walonga na globu ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2009

    nafurahi sana nikiwaona awa jamaa wakiwa pamoja na kuwa na mawazo mazuri ya filam za kiswahili apo wazee nawapa credit! ila sikusikia vizuri maoni yenu na michuzi kwani noise nadhani kama mziki ilikuwa inasumbua, nilikuwa nasikia muheshimiwa rais nyingi na filam za kiswahili, naomba namba zenu za simu tuchangiane mawazo.

    mdau canada!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2009

    there they go again, MIE HAWA WATU WAWILI HUWA WANANIFANYA NACHEKA SANA.

    ReplyDelete
  3. mimi nimeguswa na ujumbe waliokuwa wanajadiliwa hao vijana kuhusu mt kilimanjaro.siku moja nilikuwa naangalia tv show here in uk.it was documentary,washiliki walikuwa watu maarufu. i remember on of them was alisha dixon;the purpose of their tour to kilimanjaro was to make donation for charity. kilichonishangaza uwezi kuamini kwenye show ya more than 2hour sijasikia neno tanzania,walichokifanya ni uhusisha huo mlima na matatizo ya maralia uganda as if kilimanjaro hipo uganda.kilichoniuma nilimstua mshiji mzungu sababu kila siku anasema haijui tanzania,mwisho wa show ananiuliza where is kilimanjaro,ukweli usiofichika tz haijulikani kabisa nimeshaulizwa mara mbili na waudumu wa western union tanzania hipo bara gani,huu ni msiba kwa wadanganyika wote

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 31, 2009

    Ni kweli tz haijulikani,lakini ukishakutaja neno znz watakwambia tumeshawahi kuisikia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 31, 2009

    HAHAHa Ray kanifurahisha sana ni kweli Mt Kilimanjaro si lazima watu kugombana kwamba kwanini kenya wanasema yao inajulikana Kilimanjaro ni ya Tanzania wapende wasipende hata wkaijitangazia mtu akifikiria ni ya Kenya kimpango wake. Kanumba na Ray zidini kukaza butu mwenyezi mungu atazidi kuwaongezea kipaji. Ila hilo swala mwambieni waziri wa Utamaduni sio Raisi jamani kilak itu Raisi? Juma.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 31, 2009

    wewe unayesema kuhusu Alisha Dixon umetizama kipindi UK, Inaonesha pengine lugha ilikupiga chenga kwanza walisema kabisa Tanzania mt kilimanjaro. baadae kila mmoja alikuwa anaonesha charity zake Nchi tofauti hasa Uganda kwa maswala ya Malaria. ni sehemu mbili tofauti kama ulitizama vizuri Chris moyes alikuwa akijitangaza kwenye Radio 1 yake mie nakumbuka nilisikiliza kipindi cha radio 1 akasema tupo Mt kilimanjaro Tanzania. na baadae Gazeti moja linaitwa The Mirror lilisema kwamba Toka wale jamaa kwenda Mt Kilimanjaro watalii wamezidi kwenda Mt kilimanjaro na wameweka Tanzania. kama kanumba alivyosema Haina haja kubishana kila mtu anatambuwa anayetangazia kwengine aendelee tu Ila Ramani ipo inajulisha wapi ni wapi. Kenya watawaonesha kama mfano ukiwa Arusha unaiona Mt kilimanjaro ila ukifika Bango limeandikwa Uhuru Mt kilimanjaro Tanzania. Kushne. kuhusu Kenya labda itoke kwenye Mdomo wa Kenya. Mpemba.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 31, 2009

    mimi bwana nawapongeza wasanii wa bongo kwa kukiendeleza kiswahili ila cha kushangaza ni pale serikali inapozidi kukikumbatia kiingereza na kuendeleza kufundisha vyuo na seekondari kwa kutumia kiingereza hiyo inashusha kiwango cha elimu bongo na pia huo ni utumwa wa lugha hiyo lugha ilikuja na wakoloni ni vyema ikafundishwa tuu kama somo mataifa kama china na japani yanakuwa saana kiuchumi sio kwa kutegemea kiingereza bali ni kwa technologia wanazofundishwa kwa kutumia lugha yao ukienda kwao lazima ujifunze lugha kwanza,Kingine ni kwamba serikali isimamie suala la hatimiliki kwa dhati kabisa ikiwezekana liundiwe tume na sio kuunda tume za kujadili masuala ambayo yaneleweka na kuelezeka hata mtoto anaweza akalielezea

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 31, 2009

    Watanzania bwana kila kitu wanataka Raisi aingilie kati. Sasa wewe mtu mzima unasema Raisi aingilie kati maswala ya filamu ya nini kwani hakuna chama cha filamu Tanzania? Waziri wa mambo ya habari na Utamaduni? tuweke utaratibu ili mambo yawe yanaenda kirahisi sio kumrundikia Raisi maswala ambayo ni madogo sana

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 31, 2009

    SI NDO HAPO, RAISI WA NINI KWENYE MOVIE. HAPO KANUMBA KAONYESHA UPEO WAKE WA KUTOKUONA MBALI. NDO MAANA KUNA BARAZA LA MAWAZIRI, RAISI IS ONLY A REPRESENTATIVE. RAISI SIYO WA KILA KITU, WATU INABIDI MUISOME KATIBA NA KUIELEWA. BEFORE U KNOW UKIGOMBANA NA MKEO UTATAKA RAISI AINGILIE, JAMANI!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 31, 2009

    Hivi watu wanadhani raisi ni Mungu? Mambo mengine mgambo tu wanatosha kushughulikia, utasikia Raisi!. Mtu kaombwa rushwa pale mahakama ya mwanzo, Raisi!!!, Vibaka wamejaa mtaani kwenu, Raisi!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 31, 2009

    Mie nakubaliana na anayesemakuhusu Kusoma secondary Kiengereza ingetolewa wakasoma kwa kiswahili, au kwasababu Dunia mambo mengi ni kiengereza basi waanza kusoma kwakiengereza kutoka la kwanza shule zile za msingi za serikali ya tanzania. Watoto wanafeli sababu mtu toka la kwanza masomo kiswahili akifika Sekondari wanaanza kiengereza kichwa kishakomaa kuelewa inakuwa ngumu ndio maana wana feli wengi. James.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 01, 2009

    mkorogo umetulia yaani ni wanangaa lakini sio kwa vibaya chunusi hakuna

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 01, 2009

    Utajiri ni vitu 3 ARDHI, MAFUTA na ALMASI, Kwishnee!! Ndio ukisikia mijinchi ya watu wenye akili zao wameenda kupigana ujuwe kipo kimoja kati ya vitu hivi vitatu. Sijui utalii na vyengine vyoote ni kupoteza muda,tunapoteza muda kugombea sijui Kilimanjaro ipo wapi?
    Tanzania ni nchi tajiri kwa vile tuna Ardhi kubwa yenye rutuba kulinganisha na nchi nyingi Africa, tatizo watanzania hatuna upeo na utaalamu wa kuitumia ardhi yetu kwa faida yetu, angalia ardhi ya Zimbabwe alipokuwa nayo Kaburu na hivi sasa! Rhodesia ilikuwa tajiri kutokana ilikuwa na wataalamu wa kuiendeleza ardhi yao, chakula kibao mpaka chengine walikuwa wanatusaidia akina sisi, leo hii Zimbabwe watu wanaishi kwa mlo mmoja wa bakuli ya uji?
    By the way hawa Wakenya wakisema Kilimanjaro ipo Kenya ni free advertisement kwa vile hao watalii wakija kuukwea huo mlima kipato kinaingia kwenye Bweta la Bongo, hivi mnataka kuniambia eti wanaweza kupanda Kilimanjaro bila kuwa na kibali cha Wizara ya Utalii ya Bongo?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 01, 2009

    eti mnajichubua????

    Ray umeokoka au??

    michuzi ivi AYA MADUBWANA YA WORD VERIFICATION what on earth did yu bring them back????unakera

    ni hayo tu

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 03, 2009

    hao jamaa wote wangekuwa wanaongea hivyo hivyo kwenye sinema zao, haipendezi kwa jinsi wanavyoongea sasa hivi trying to be so structured and stiff, kama kuna ushauri wawe wenyewe tu, wanaonekana kabisa kama wanaigiza katika filamu zao wakati actor mzuri ni yule anayeonakana kama hana habari kuna camera na hatumii msuli usiohitajika naomba hii iwafikie Michuzi zaidi ya hapo wanajitahidi hii fani bado ni changa kwa hiyo mambo mengine tunavumilia na yanaeleweka.

    ReplyDelete
  16. Siwezi sikiliza hii video kwani imejaa kwikwi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...