UKAHABA : MBINU MPYA YA KUCHAPUZA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

Na Ali Haji Hamad, Cape Town.
Jumuiya inyotetea haki za makahaba ya hapa Afrika Kusini imetowa wito kwa waandishi wa habari kusaidia juhudi zao za kutaka Biashara ya Ukahaba ihalalishwe na sheria za nchi kama njia ya kupunguza maambukizo mapya ya virusi vya UKIMWI.

Akizungumz na jopo la waandishi wa habari 56 kutoka zaidi ya mataifa 40 duniani, katika Kongamano lililofanyika Fountains Hotel Mjini Cape Town, Mkuirugenzi wa Taasisi hiyo inayojulikana kwa jina la Sex Workers Education and Advocacy Initiative, Eric Harper amedai kuhalalishwa kwa biashara hiyo kutasaidia kupunguza kiwango cha sasa cha maambukizi kwa makahaba na wateja wao kwa vile watakuwa na nguvu ya kisheria ya kuchukua hatua za kinga,

Mkurugenzi huyo ametowa wito huo zikiwa zimebakia siku mbili tu kabla ya wanasayansi, madakatari,watafiti, jumuiya zisizo za kiserikali na kiserikali, taasisi za dini na watu mmoja mmoja kuanza kukusanyika hapa kuhudhudhuria mkutano wa kimataifa wa Ukimwi unaokusudia kujadili pamoja na mambo mengine hali mbaya ya mambukizi ya ugonjwa wa ukimwi, upatikanaji w dawa za kutibu na hatua mbali mbali zilizofikiwa katika kutafuta chanjo ya ugonjwa huo.

Akizungumzia hali ya maambikizi miongoni mwa watu wanaofanya biashara ya ukahaba mkurugenzi huyo amesema katika hali ya sasa kiwango cha maambukizi miongoni mwaokinaonekana kuwa kikubwa zaidi (asilimia 9) kuliko kile cha jumla (asilimia 7) kutokana na ukweli kwamba wanoifanya kazi hiyo wanaifanya kwa magendo na katika hali ya kunyanyaswa na hawana muda wa kutosha walnguvu za kisheria za kujadiliana njia za kujikinga kama vile matumizi ya mipira ya Condom.

Aidha ametaja sababu nyengine inayowafanya watu wanaofanya biashara ya ukahaba kuonekna na kiwango kikubwa cha maambukizi kuwa ni kuongezeka kwa kesi za kubakwa kwa wafanyabiashara hao huku wakikosa haki ya kutibiwa mapema kwa maradhi ya zinaa na haki ya kisheria ya kuwashitaki wateja wao wanaowatendea vibaya,

Mkurugenzi huyo amabaye jumuiy yake inaendesha kampeni hiyo chini ya ujumbe wa MWILI WANGU BIASHARA YANGU amesema biashara hiyo ikihalalishwa matatizo yote hayo yataisha na wmakahaba watakuwa ni chombo muhimu cha kupambana na maambukizo mapaya ya ukimwi.

Harbert amedai kuwa nchi zote ambazo ambazo zimehalalisha biashara ya ukahaba ikiwemo Newzealand wamefanikiwa kupunuza maambukizi mapya sio tu miongoni mwa makahaba bali katika jamii kwa jumla.

Mapema mmoja wa wafanya biashara hiyo aaliyekuwa ameambatana na mkurugenzi wake ambae amekuwa akiifanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 15 (hakutaka jina lake litajwe kwenye chombo cha habari ) aliwashushia lawama waandishi wa habari kwa kuendeleza unyanyapaa kwa watu wanaofanya biashara ya ukahaba na akasema kwamaba hata pale wanapopata fursa ya kuzungumza nao huwauliza masuali yaliyojaa kebehi kama vile wao hawni haki kama binaadamu wengine.

Hata hivyo waandishi wa habari hao walielezea wasiwasi wao iwapokila mtu ataachiwa na kuruhusiwa kufanya atakalao kwa kisingizio cha haki yake ya kibinaadamu basi kizazi kijacho kinaweza kukosa mwelekeo.

"Ikiwa anetaka kuuza mwili atahalalishiwa kwakuwa tu ni mwili wake, kesho anaetaka kupanda Cocaine nae atadai haki hiyokwa vile shamba ni lake na keshokutwa anetaka kujiua nae atadai haki hiyi kwasababu mwii na roho ni yake...Jamani dunia hii itafika wapi? alihoji Amir Latif , mwandishi kutoka Redio na TV Pakistan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2009

    huyo ndugu anatakiwa kumrudia mungu wake kwanza kabla ya mambo yote. kuharalisha ukahaba maana yake ni kumkosoa mungu juu ya mpango wake wa kazi kwa binadamu na kumkosoa juu ya amri yake ya sita.
    Mungu hakuagiza kuwa moja ya kazi kwa mwanamke ni kuuza mwili wake, hakuna agizo kama hilo. wala hakuagiza kuwa kutakuwa na kazi ya kishoga kati ya mwanamme na mwanamme na mwanamke na mwanamke.
    Haya mambo yanayodaiwa kuwa yaharalishwe ni kufuru tupu.
    Ebu tufike mahali tumuogope mungu wetu aliyetuumba, na kuziheshimu amri zake.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2009

    Nashindwa kuelewa ni vipi kuhalalisha ukahaba kutapunguza magonjwa ya ukimwi? kwani ukimwi unapatikana kwa kuwa tu ukahaba umepigwa marufuku? wangapi walioathirika na ukimwi hawajawahi hata mara moja kutembea na makahaba? kwani ni makahaba peke yao ndio wenye kuambukiza ukimwi. sasa ukahaba ukiwa halali ndio tuseme anaekwenda kwa kahaba hatapata ukimwi?


    Mbona hii issue inanitatiza? hebu nieleimisheni hapa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 23, 2009

    ANONY WA KWANZA UPO RIGHT
    LAKINI NATAKA NIKUELEZE TU MSIMAMO WA DUNIA NA NGUVU YA DUNIA ILIVYO ''UNIPOLAR'' SASA.KWA KIFUPI BWANA ERIC NI MEMBER WA FREE MANSORY.ILE DINI YA MHESHIMIWA ''RASTA WA MAZIZINI'' NA MTANDAO WAKE TZ.KWA KIFUPI JAMAA WANATAKA KUHAKIKISHA WATU WANAKUFA KWA NJAA,MAGONJWA YA MAKUSUDI(UKIMWI,MAFUA YA NDEGE,NGURUWE,N.K) VITA ZA KUANZISHA KWA NGUVU AMA KWA KISINGIZIO CHA DEMOKRASIA,UBABE WA KUUZA SILAHA KATIKA MATAIFA MACHANGA NA KUMALIZA WATU WASIO NA HATIA,KUWEKA NA KUPANDIKIZA MBEGU ZA FITNA,CHUKI,UADUI KATI YA PANDE MBILI ZENYE TOFAUTI ZA KIMSIMAMO AU KI-IDEOLOJIA,AU MATABAKA(UISLAM-UKRISTO,WEUSI-WEUPE,MAKABILA(MFANO WAHUTU-WATUSI),MAENEO AU PANDE(KASKAZINI-KUSINI mf.SUDAN,) MASHARIKI-MAGHARIBI Mf.TURKEY),KOO(SOMALIA),TABAKA(KASKAZINI MWA IRAQ),LUGHA(BELGIUM)...ILI KUFIKIA MALENGO YAO WANA VYOMBO VYA HABARI VYA KUTOSHA NA WANAHAHA KUPATA VINGINE NA VYA WENYE UCHU NA TAMAA YA SARAFU,WATAHAHAKIKISHA WANAPATA WANACHAMA WAO WA KUTOSHA,,NA KWA KIFUPI WANAKUBALI MTU WA DINI YEYOTE AINGIE KWAO..POLEPOLE HUMPIKA KAMA CIA WANAVYOMCHUKUA MTOTO AKIWA MDOGO HADI AKUE WAKIMPIKA...HAPO SASA UTAJUA DUNIA INAELEKEA WAPI
    SAM LULA DA SILVA
    RIO DE JANEIRO-BRAZIL

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 23, 2009

    Jamani hivi tunaelekea wapi watanzania?
    Mbona tunataka kupelekwa pelekwa tu na watu weupe?
    Ivi byashara ya kuuza mwili ni byashara gani iyo ya kishenzi?
    Tunashindwa kukaa chini na kufikiria jinsi ya kujikwamua kimaisha tunafikilia kuharalisha zinaa! Acha wazungu wafanye mambo yao ya ki-firauni na sisi tufanye mambo yetu ya kumpendeza mungu.
    Mbona hatuwaigi wazungu kutokupokea rushwa? Eti tunawaiga kufanya ngono! Its me Mbeki 4rm St.Joseph College of Engineering and Technoloy-DSM

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 23, 2009

    Tuharalishe tu ili TRA iweze kukusanya kodi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2009

    hizi ni dalili za kiama...

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2009

    Ndugu umetokea wapi wewe,kuharalisha siyo kiswahili ni kuhalalisha. But u have a good point

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 24, 2009

    annon #2 toka juu...

    hujui ni hiviii:unapolala na mke au mume wa mtu,au na mtu asiye mume wako ni UMALAYA kamili

    so ukimwi ndivo unapoenea kwa kasi kwa kulalana-lalana,kutokuwa na mwenzi wako mmoja tu for the rest of your life

    kwanini unataka kulalana na mtu tu?why usiwe na wa kwako tu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...