Jumatatu wiki hii JK alifungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania mjini Washington DC lililonunuliwa kwa dola milioni 10.415, sawa na shilingi bilioni 13.5.
Akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi, Rais Kikwete alisema jengo hilo mbali ya matumizi ya ofisi, lakini pia ni ishara ya kisiasa na kidiplomasia kuonesha kuwa uhusiano wa Tanzania na Marekani unakua vizuri.


Akizungumza wakati wa kumkaribisha Rais Kikwete, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Member, alisema jengo hili ndilo kubwa kuliko majengo yote ya balozi za Tanzania duniani.


Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Ombeni Sefue, jengo hilo la ghorofa sita lina eneo la futi za mraba 26,240 na litagharimu dola 367,593.54 (shilingi milioni 477) kulitunza kwa mwaka.

Kutokana na kuwepo katika eneo zuri katikati ya Jiji la Washington, serikali imeuagiza ubalozi kupangisha ghorofa tatu ili mbali ya kipato kwa serikali, upangiashaji huo usaidie kulitunza jengo hilo kwa gharama.

Awali mtathimini anayetambuliwa kisheria, Riley & Associates LLC, alikadiria jengo hilo kuwa na thamani ya dola milioni 11,200,000, wakati Jiji la Washington lilitoa thamani ya dola milioni 11,456,200 kwa ajili ya makadirio ya kodi kwa mwaka 2009.

“Tumefanikiwa kulipata jengo hili kwa bei rahisi zaidi kuliko thamani yake, hivyo tumeokoa dola 1,585,000,” alisema Balozi Sefue na kuongeza: “Tulifuata taratibu zote ambapo wizara na ofisi zote husika za Tanzania na Marekani zilihusishwa katika manunuzi.”

Kwa wastani jengo hilo limenunuliwa kwa dola 397 kwa futi moja ya mraba kulinganisha na bei ya majengo mengine katikati ya Jiji la Washington ambayo hugharimu kati ya dola 400 na 900.

Ndani ya jengo hilo lililo kwenye Mtaa wa 22 mkabala na hoteli ya Marriot, kuna picha ya Rais Kikwete na Rais George wa Marekani wakiwa Ikulu Dar es Salaam; picha ya Rais Kikwete na Rais Barack Obama wakiwa Ikulu ya Marekani, Washington DC; picha ya Rais Julius Nyerere wa Tanzania enzi hizo, akiwa na Rais wa Marekani enzi hizo, Jimmy Carter kwenye Ikulu ya Washington DC.

Pia kuna picha rasmi mbili za sura za viongozi, Rais Kikwete na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere pamoja na picha zingine za mapambo ya fahari ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Tumeokoa dola 1,585,000 au tumetumia dola milioni 10.415?
    Jengo kubwa hilo, lazima patakuwa na shughuli nyingi zinazohitaji wafanyakaiz wapya. Nataka kuwa mmoja wa wafanyakazi wapya ubalozini hapo. Lini hizo kazi zitatangazwa?

    ReplyDelete
  2. just try to confuse us with those numbers.....but we know that there is more to it than whats being said.

    ReplyDelete
  3. Naafiki uamuzi wa kununua jengo hili. Tungeweka pia ile picha ya Mwalimu Nyerere na Rais John Kennedy. Katika kukumbushia historia ya uhusiano wa nchi zetu mbili, ile picha ni muhimu sana, kwani ni ya miaka ya mwanzo ya Uhuru wetu.

    ReplyDelete
  4. Nina imani pia wafanyakazi wa ubalozi wetu wataacha uzembe na uvivu na kufanya kazi jinsi inavyotakiwa sio kwa mazoea.
    Hilo jengo lipo mtaa gani hapa DC?
    Mbona gharama ya kuliendesha kwa mwaka karibu nusu bilioni ni kubwa sana? je hiyo ni property tax tu? au wamekadiria umeme na maji pia?

    ReplyDelete
  5. Hongera, lakini dola 30,000 kwa mwezi za kulitunza!! Ama tarakimu zimekosewa?
    Wanohoji kwamba lazima kuna kitu ni wale wale ambao hawana mchango wowote na wanashukuku kila kitu bila sabubu za msingi. Hatuwezi kuendelea na watu kama hao.

    ReplyDelete
  6. Mzee Mbele ile picha ya Mwalimu na Kennedy ipo IKULU. ukiingia tu corridors of power unaikuta hiyo picha. Ila pale ndio tuliharibu manake sasa hivi tungekuwa mbali sana tukaenda kufuata mambo ya Urusi

    ReplyDelete
  7. Gharama la kuliendesha kwa mwezi inaweza kutatua tatizo la maji, kwa kuchimba visima zaidi ya kumi kwa mwezi.

    ReplyDelete
  8. Hata ufunguzi wa jengo jipya hawaukutangaza.

    Pia Kikwete, Ubalazo na Wafanya kazi wa Ubalozi wana chuki na Watanzania wa DC, kwani hawataki kujihusisha nao.

    ReplyDelete
  9. MBONA TUMEWASHINDA WAINGEREZA, WAJERUMANI, WAFARANSA NA HATA WAJAPANI, WOTE HAO VIJENGO VYAO VILIVYOPO NCHINI NI SAWA NA SERVANTS QUARTERS TU, SASA WAMEREKANI NA DUNIA YA KWANZA NI LAZIMA WAJUE KUWA TANZANIA NI NCHI TAJIRI NA HAIHITAJI MISAADA TENA.

    ReplyDelete
  10. Wangu Macho tuu, Dola Million 10 ?

    ReplyDelete
  11. UPUUZI MTUPU!!KUNA NCHI NYINGI AMBAZO TANZANIA HAINA UBALOZI LKN ZINAFAIDA KUBWA KWA TANZANIA!!ZINATUSAIDIA SANA KISIASA NA KIUCHUMI.
    IMEPITWA NA WKT KUABUDIA KISICHO NA FAIDA MAREKANI INAATHARI KUBWA SANA KTK NCHI ZA KIAFRICA KULIKO FAIDA.

    HUYO ANAESEMA TULIIKOMBATIA RUSSIA TUNGEIKOMBATIA MAREKANI TUNGEKUWA MBALI SANA NADHANI HANA UPEO AMAHAJUI SIASA YA DUNIA INAVYOKWENDA!!HIVI KUNA NCHI NGAPI ZINAURAFIKI WA KARIBU NA MAREKANI NA HIVI LEO ZIPO MASKINI SANA NA HATA KUZOOFIKA KWA KUPANDIKIZIWA VITA?
    MAREKANI HAINA URAFIKI BALI INAMASLAHI TU.

    ReplyDelete
  12. roho yaniuma saaana!!

    kununua jengo USA???

    ReplyDelete
  13. Najua umesema kuwa lipo karibu na Hotel ya Marriot, lakini ingekuwa vizuri ukatupa street address na zip code.

    ReplyDelete
  14. Unayesema mengi, pamoja na, "Ila pale ndio tuliharibu manake sasa hivi tungekuwa mbali sana tukaenda kufuata mambo ya Urusi", kumbuka kuwa Urusi ilitusaidia sana kuikomboa Kusini mwa Afrika wakati Amerika ilikuwa ni rafiki mkubwa na Makaburu!

    Someni historia! Je, mmesahau kuwa Amerika ilikuwa ni mojawapo ya Nchi za Magharibi kusaidia na kulipia gharama za ma-"terrorists"...the so called dogs of war au mecernaries katika kuziangusha nchi za Afrika...

    Umesahau ya Lumumba wa Kongo, Nkrumah wa Ghana. Olympio wa Togo, na kadhalika!

    Shame on you!

    ReplyDelete
  15. KUNA MSEMO USEMAO KWAMBA.....
    "KUVUJA KWA PAKACHA FAIDA YA FAIDA YA ....MICHUZI....KUNRADHI FAIDA YA MCHUKUZI"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...