hiki ni kikosi cha yanga kids chini ya kocha wao mzee kwala (shoto) ambaye sasa ni marehemu. wengi katika wachezaji hao waliibuka kuwa nyota wakubwa nchini katika kile ambacho wadau wanasema endapo kama mtindo huu wa kulea vipaji toka awali ungeendelea bongo tungekuwa mbali sana. wenye data za enzi hii pamoja na majina ya hao yosso msaada tutani. mie naanza kwa kumtambua gordian mapango (wa nne kulia mbele) na saidi mmanga (shoto mbele)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. nami naongezea Adolph Rishard wanne kutoka kushoto

    ReplyDelete
  2. Duuh sio mchezo watoto walikuwa wanakipiga hawa. mimi niliowatambua ni adolf rishad wanne toka shoto waliokaa. mohamedi mkweche wa tatu toka shoto waliosimama na wakwanza toka kulia ni juma pondamali mensha
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  3. Duh kweli tumetoka mbali . Michuzi kwa kusaidia tu mimi nimekuona wewe hapo wa kwanza waliochuchumaa kutoka kulia hahahahahaha.

    ReplyDelete
  4. mkweche wa tatu ,kassim manara wa tano waliosimama, wa kwanza kulia juma pondamali. waliokaa wapili kulia ni marehemu mwarami mohamed shemeji wa jumanne hassan masumenti. nawakilisha mdau wa dom

    ReplyDelete
  5. Jamaa Ana Convers ya nguvu. Vijana wa Sunderland wapo wapi?

    ReplyDelete
  6. wa tatu chini toka kulia ni, Jafari Abdulahamani

    ReplyDelete
  7. kweli Tanzania kichwa cha mwendawazimu hii program ilifanikiwa ile mbaya hawa jamaa walikuwa tishio africa namaanisha waliweza kupambana na timu yoyote ile katika africa ilikuwa tunakwenda kuangalia mpira kifua mbele na matumaini makubwa ya ushindi lakini kilichotukuta mpaka leo tumekuwa nyuma kimpira mungu anajua watu wanakwenda mbele sisi tunarudi nyuma hata mtu akitaka kubisha mfano hai huo hapo juu nakumbuka tulikuwa tunamzomea juma pondamali akipita kuelekea jangwani saa saba mchana wewe jua kali saa hizi mpira utakuua akaja kuwa mmoja kati ya makipa mashuhuri nchini haihitaji mambo ya ajabu vile vile alivyofanya coach victor mtu mwingine afanye miaka mitano au kumi na sisi tutaonekana kwenye world cup

    ReplyDelete
  8. Eh bwana eh! Huyu Wa pili (Walio simama kutoka kushoto)anafanana na Mohamed Saidi Sululu (ARUSHA), Mapango, Jaffari Abdurahman,Mkweche, na Pondamali.

    ReplyDelete
  9. Dah kweli nimewakubali wa enzi hizo,mimi hapo hata sina dalili ya kuzaliwa.ila nimefurahi nimemuona kocha wangu wa timu yangu ya mtaani care boyz pale kinondoni DSM Gordian Mapango.Yanga endelezni huo mpango wa yosso!!!!!!!!!mdau Uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...