Mhe. Rais Jakaya Kikwete leo, Jumatano, Oktoba 21, 2009 atawaapisha maofisa hao wawili waandamizi wa Serikali pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara za Serikali ambao aliwateua, Jumatatu, Oktoba 19, 2009.

Maofisa hao watakaoapishwa ni Jaji Frederick M. Werema kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Bwana David Kitundu Jairo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini; Bwana Sazi Salula kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa; na Bwana Mbarak M. Abdulwakil kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Wengine watakaoapishwa ni Bwana Christopher Sayi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji; Bwana Sethi Kamuhanda kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo; Bwana Prosper Mbena kuwa Katibu wa Rais, na Bwana George Masaju kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Shughuli ya kuapishwa itaanza saa sita mchana, Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

 1. HATA MWANASHERIA MKUU MKRISTU YAANI TOKA UHURU NAFASI HII HAJAWAHI KUSHIKA MUISLAM.
  MAKATIBU WAKUU WOTE WAKRISTU.TUKIULIZA TUNAAMBIWA SABABU ZA KIHISTORIA.WAISLAM KUNA WASOMI KAMA PROFESSOR SAFARI,MWANAIDI MAAJAR NI WATU WALIOBOBEA KWENYE SHERIA.

  ReplyDelete
 2. Kaka Michuzi, nakusihi usisahahu kutuweka picha za tukio hili muhimu. Hawa ni watendaji muhimu sana katika Serikali yetu. Ni vyema tuone sura zao na utashi pia. Kazi njema.

  ReplyDelete
 3. haya mambo ya dini yatawamaliza mbona husemi hakuna mwanamke? huyo maajar unataka awe AG, Balozi,Katibu Mkuu????

  ReplyDelete
 4. WEWE ANON WA KWANZA 11:41AM KWANI AKIWA MUISLAM AU MKRISTU ITAKUSAIDIA NINI? JE UNAFAIDIKAJE? AU NINYI NDIO WALE WATU WENYE KUJIPENDEKEZA KWA KUTUMIA UDINI? NINACHOELEWA HATA WAKIWA WAKRISTU AU WAISLAM WANAFAIDIKA WAO NA FAMILIA ZAO CHA MSINGI NI WEWE KUJITAHIDI KUSOMA NA KUACHA UTEGEMEZI ILI UFAIDIKE.

  ReplyDelete

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...