Kongamano la Kwanza la Wanataaluma Waishio Ndani na Nje ya Nchi 2009

Mada Kuu: Wanataaluma Na Vipaumbele Vya Taifa na Jinsi Wanavyoweza Kuchangia na Kuchochea Maendeleo ya Nchi na ya Watanzania

Mtandao Wa Wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network – TPN ) ukishirikiana na Tume ya Sayansi na Technolojia (Commission for Science and Technology Tanzania – COSTECH); Open University of Tanzania; University of Dar Es Salaam; na Serikali imeandaa Kongamano la Siku Moja (Nyumbani Ni Nyumbani 2009) siku ya Ijumaa; 18th December 2009 kuanzia Saa 2.00 Asubuhi -11.00 Jioni litakalofanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel Toure Drive, Masaki.

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Kongamano hili atakuwa Mheshimiwa Bernard Kamillius Membe (Mbunge), Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pamoja na mambo mengine Serikali itaongelea juu ya suala la Uraia wa Nchi Mbili (Dual/Smart Citizenship) na masuala mengine yahusuyo Watanzania wanaoishi nje ya nchi.

Washiriki wa Kongamano hili ni Wanataaluma Wazalendo waliopo ndani na nje ya Tanzania. Kila Mwanataaluma wa fani yoyote anakaribishwa kuhudhuria. Kutakuwa na ada ya ushiriki ambayo ni TZS 50,000 (Kwa ajili ya kuchangia gharama za ukumbi; chakula; chai, vitafunio, matangazo, makabrasha ya mkutano, Vyombo vya Mawasiliano; ulinzi nk.). Viongozi wa Vyama Vya Kitaaluma na Wanataaluma Wanaharakati wa Maendeleo wawasiliane na TPN. TPN inapenda kutoa changamoto kwa Wanataaluma wote wenye mapenzi na uzalendo na Tanzania kuwa huu si wakati wa Kulaumu bali wa vitendo. Kama unaguswa na una mawazo mazuri juu ya kusaidia kuleta maendeleo ya nchi tafadhali sana usikose kuhudhuria. Ambao hawataweza kufika wanaweza kuwasilisha mawazo yao kupitia barua pepe: president@tpn.co.tz na watakaofanya “booking” mapema ya kutoa mawazo kupitia “Skype Video Conferencing/Chat” wanaweza kufanya hivyo kupitiaSkype ID ya: TPN_TZ

Baadhi ya Mada zitakazojadiliwa, kuwekewa mikakati ya kiutendaji na ufuatiliaji ni pamoja na:
1. Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara
2. Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao
3. Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.
4. Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini
5. Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi
6. Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua za Kuleta Mabadiliko Na kwa Vipi?
7. Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka/

Kwa Kujiandikisha kuhudhuria Kongamano na kwa Maelezo Zaidi, tafadhali wasiliana na ofisi kupitia namba: 0715 740 047 na barua pepe: president@tpn.co.tz; www.tpntz.org. Tiketi zinapatikana Ofisi za TPN - TOHS Nyerere Road; Mayo 1999 Co. Ltd – Extelecom Samora Avenue; Zizzou Fashion Victoria na Africa Sana.

Imetolewa: Wednesday, December 16, 2009 na:

Sanctus Mtsimbe;
Rais; Mtandao Wa Wanataaluma Tanzania
(Tanzania Professionals Network, TPN)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Idea ni nzuri kwa kweli, hata fee sio mbaya ila taratibu za uandikishaji finyu, mara nyingi matapeli ndio wanapenda kutumia simu za mikononi, nazani ingetumika Land Line (simu ya ndani) isingeleta mashaka.

    ReplyDelete
  2. wataaluma = academicians
    wataalamu = professionals
    au kiswahili kimenipitia kushoto, nisaidie hapo

    ReplyDelete
  3. KUZUNGUMZIA URAIA MBILI NI MUHIMU...NA SIJUI KWANINI WANASITASITA SEREKALI YA TANZANIA HADI LEO KUPITISHA SHERIA HIOOO?? SIONI CHAAA AJABU.

    ReplyDelete
  4. Ufisadi ni kizingiti kikuu kwa maendeleo ya nchi. Huwezi kuzungumzia wataalamu kuwa chachu ya maendeleo bila kutafuta njia za kubadilisha mfumo wa utawala na utumishi ambao umezaa ufisadi, vinginevyo yote tutakayojadili itakuwa ni porojo ambazo watanzania wameishazizoea. Pia ikumbukwe kuwa ufisadi unafanywa na wataalamu - sio wakulima!!! Kwa hiyo basi hilo kongamano litakuwa na maana ikiwepo mada maalumu ya kuzungumza "uhusiano wa utalaamu na ufisadi nchini tanzania: jana, leo, na kesho"

    ReplyDelete
  5. Ni wazo zuri kuandaa mkutano huu, hata hivyo ninawasiwasi na mhudhurio kwani kiwango cha 50,000/= ni kikubwa.
    Nifikiri hawa mataalamu wapigiwe magoti ili waweze kuhudhuriaili kutoa mchango wao ni kw kiasi gani wanaweza wakawa ufumbuzsi wa matattizo mbalimbali, mtokeao yake h hao wenyeinputs wanatakiwa kuchangia, haiingi akililini, ili wafaidike na ninio? waandaaji walipaswa kutafuta sponsor na wala sio kuwataka wachangiaji wajilipie.
    Next time hili liangaliwe, mungeweza kupata fund kutoka mshirika ya simu, pombe serikalini nk.

    ReplyDelete
  6. Kwa kuwa sijafurahishwa na kitendo cha watu kukongamana muda wa kazi acha nitoe majibu kwa maswali yote ambayo yameoredheshwa kama mada za kongamano.

    Seriously, kwa nini tukapoteze masaa 9 wakati majibu ni mafupi mno?

    Let's begin ...

    ---

    1. Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara

    A: Kwa kugombea nafasi za kisiasa, na uongozi wa jamii. Ni viongozi tu, na wenye fedha ndio watakaoamua nini vipaumbele.

    2. Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao

    A: Je wanataaluma ni super-Tanzanians? Wakiacha kujiona super-Tanzanians wataweza kusaidia "Watanzania wa kawaida"

    3. Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.

    A: Kwa kuachana na blah-blah za makongamano tena siku za kazi, badala yake wachape kazi.

    4. Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini?

    A: Kwa kujiimarisha huko huko waliko, na kisha kuvuta Wabongo wengine wakaishi nje.

    5. Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi

    A: What's the question?

    6. Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua za Kuleta Mabadiliko Na kwa Vipi?

    A: Wakati muafaka ni sasa.

    7. Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka?

    A: Watumie barua-pepe na simu

    ReplyDelete
  7. ELFU HAMSINI PESA NYINGI SANA KWANIN ISIWE ELFU TANO?NYIE WATALAAM MNASHINDWA KUPATA WADHAMINI WA KU SPONSOR KITU HII?UTALAAM WENU UNAFANYA NINI HAPA?

    ReplyDelete
  8. I SALUTE YOU..MCHAPAKAZI

    ReplyDelete
  9. Serikali inaelewa kuwa ili wataalamu au wataaluma wa Kibongo warusi bongo lazima:

    1. Waruhusiwe pasi mbili.
    2. Waheshimike.
    3. Hali ya maendeleo iwe juu kidogo. Mfano: maji safi, umeme wa kutosha, shule inayofundishwa na walimu wasomi.
    4. Haki za wananchi ziheshimike hatika korti. Jaribu kwenda leo kufungua kesi ya kudhulumiwa, utakuta inachukua miaka 10 kumalizika na lazima uhonge upate haki. Kuna kila aina ya bodi kusaidia bubadilisha sheria lakini sheria na serikali ipo karibu sana.
    5. Sisi tulio nje hatutaki makubwa. Lakini kama wenzetu wasomi huko na serikali bado hamjawapatia maji na umeme na haki wananchi, sioni faida ya kuja huko na kuacha kazi yangu ya maana ili nije kuhangaishwa bure.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...