THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

libeneke hoteli ya movenpik: aluta kontinyua...

Kaka Michuzi,
Ni matumaini yetu kuwa umzima wewe na timu nzima ya blog ya jamii.
Tulikutumia email hii jana ili kuweka ufafanuzi kuhusiana na maoni ya wadau waliotoa maoni baada ya kuweka malalamiko yetu hapo katika blog ya jamii.

Hatutaki kuamini kuwa umeyapuuza malalamiko yetu, kwani tunaiamini blog ya jamii kuwa haifanyi kazi kwa kulinda maslahi ya watu au kundi fulani.
Tunaamini kuwa blog ya jamii ni blog ambayo ipo kwa ajili ya jamii na jamii yenyewe ni sisi wadau wake.

Tunakuomba kwa hisani yako usiyaapuuze malalamiko yetu kwani baada ya kuweka yale malalamiko yetu ya kwanza, uongozi ulishtuka na walikaa kikao ili kuweka mikakati ya kudhibiti habari zote za zinazohusu malalamiko ya wafanyakazi wa Moevenpick kutolewa katika vyombo vya habari.

Juhudi zetu za kupeleka habari nzetu katika vyombo vya habari hazikutoka kutokana na wakubwa kupenyeza rupia katika vyombo hivyo na ndio maana tukaleta habari yetu katika blog ya jamii.

Inasemekana wakubwa hawa walihaha kutafuta hicho chombo cha habari kilichohusika kutoa hiyo habari ili wakinyamazishe kama kawaida yao.
Hatutaki kuamini kuwa Bloga ya jamii imenyamazishwa. Tunakuomba kaka Michuzi uyaweke malalamiko yetu kama ufafanuzi ili kujibu baadhi ya hoja zilizojitokeza.

Tunategemea kilio chetu kuifikia
jamii ya watanzania kupitia katika blog hiyo ya jamii.

Tunakutakia kazi njema
Ahsane sana

Ni sisi Wafanyakazi wa Movenpick
Dar Es Salaam.


MGOGORO WA MOVENPICK HOTEL,
THE SAGA CONTINUE

Kaka Michuzi,
Pole na majukumu yako ya kila siku, pia tunashukuru kwa kuweka malalamiko yetu katika blog yako ya jamii na wadau wengine wakapata fursa ya kuchangia maoni yao.

Kaka Michuzi sisi wafanyakazi wa Hoteli ya Movenpick tumesoma kwa makini maoni ya wadau wote waliochangia kuhusiana na sakata lililoikumba Hoteli yetu, pamoja na maoni mazuri lakini tumesikitishwa sana na baadhi ya wadau kuchanganya mada aidha kwa kutaka kumaliza hasira zao au tuseme kutojua kuwa sisi tunazungumzia nini.

Kwa mfano wapo waliotoa maoni ya jumla kuwa ni kweli sisi watanzania ni wezi na kutuunganisha sisi na wafanyakazi wa Bandari na wale wa Airport. Hawa naamini ni watanzania wanaoishi Ughaibuni, kwamba baada ya kutoridhishwa na utendaji kazi wa hizo taasisi mbili wamekimbilia kutuunganisha nao.

Sisi tunasema hiyo sio sawa, sisi hatuhusiki na kutoa mizigo bandarini wala kukagua mizigo Airport. Kuna mdau mmoja yeye alikwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa hata Ivory Coast ililalamikia Hoteli yetu kuwa ina huduma mbovu na vyumba na vyoo ni vichafu pia, huyu tunadhani alishindwa kutofautisha kati ya Movenpick na Kilimanjaro Kempinski. Timu ya taifa ya Ivory Coast haikulala Movenpick bali ililala katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinsk, na hayo ndio matatizo ya kudandia mada bila kufanya utafiti.

Kuhusu swala la wizi, na udokozi, tunaomba kuweka bayana kuwa ni kweli vitendo hivyo vipo kama ilivyo katika taasisi yoyote, huwezi kuendesha taasisi iliyoajiri wafanyakazi zaidi ya 300 halafu uwe na wafanyakazi wote wasafi, labda kama umeajiri malaika.

Kuna wafanyakzi wengi wamefukuzwa kwa makosa ya aina hiyo na wengine wamevuliwa vyeo kwa uzembe, pale inapoonekakana kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Hoteli yetu, na labda hili wengi hawalifahamu. Katika Hoteli zote zilizopo hapa nchini Movenpick ndiyo Hoteli pekee yenye tawi la CHODAWU na kuna kamati maalum ya nidhamu inayoshirikisha uongozi wa hoteli na wajumbe wa CHODAWU ambapo jukumu lake ni kusikiliza kesi za wafanyakazi kabla ya mfanyakazi kufukuzwa.

Kamati hii imekuwa ikishirikiana na uongozi wa Hoteli katika kukomesha tabia ya wizi na uzembe kazini na hili limekuwa likifanyika kwa ushirikiano wa Meneja rasilimali watu anayeondoka.

Tatizo lililopo ni kwamba hawa wenzetu wazungu na hasa Meneja mkuu msaidizi bwana Shousha, na mpishi mkuu Bwana Vicenzo kutaka kuindesha hoteli hii kwa mkono wa chuma, wamekuwa hawaheshimu sheria za kazi na wamekuwa na maamuzi ya kuonea wafanyakazi. Ni watu ambao wanapotaka mfanyakazi aondolewe kazini hilo lifanyike bila kufuata taratibu na sheria za kazi, na huyu bwana Shousha ndiye anayesisitiza zaidi kutaka Meneja rasilimali watu kutoka Kenya aajiriwe akiamini kuwa yeye anaweza kufanya kazi bila kufuata sheria na kanuni za kazi za hapa nchini.

Sisi hatulalamiki kwa sababu ya huyo mkenya kuletwa, sisi hatuna matatizo na yeye, kilichotusukuma kuleta malalamiko yetu katika blog ya jamii ni kupinga ile nia ovu ya kuletwa kwa mkenya huyo, yaani ile kauli ya kusema kuwa atatukomesha, pili ni kutaka taratibu zote na sheria za uhamiaji zifuatwe.

Tunaamini kuwa ajira yoyote inayohusu mgeni ni lazima idhibitike kuwa hakuna mtanzania mwenye sifa hizo. Je ina maana tangu tupate uhuru mwaka 1961 serikali yetu imeshindwa kusomesha watu wenye uwezo wa kuwa mameneja rasilimali watu?

Hotel hii inayo wafanyakazi wageni zaidi ya 10, ambao hata hivyo vibali vyao vina mashaka matupu, wamekuwa wakikitumia kituo cha uwekezaji cha TIC kufanikisha malengo yao ya kuleta wageni kuchukua ajira zetu.
Kuna siku walikuja watu wa uhamiaji kutaka kuona vibali vya hawa wageni, mbona wote walikimbia, kwani kuna ambao wanaishi hapa hotelini na vibali vyao vya kuwepo hapa nchini vinaonyesha kuwa ni watalii.

Tunachotaka ni sheria za uhamiaji na taratibu zote za ajira kwa wageni zifuatwe kwa mujibu wa sheria, hatuna shida na wageni, lakini ikumbukwe kuwa ni serikali hii hii iliyoahidi katika kampeni za mwaka 2005 kuwa itazalisha ajira milioni moja, sasa kama ajira zenyewe zinachukuliwa na wageni, hizo ajira milioni moja zitapatikana wapi?

Wale mliosema kuwa ni heri waajiriwe wageni kwa kuwa watanzania ni wezi, jaribuni kutafakari kauli zenu, mkumbuke kuwa hata nyie ni watanzania na kwa kusema kuwa watanzania ni wezi, ni sawa na kuuambia ulimwengu kuwa sisi sio watu wa kuaminiwa, kwa wale walioko nje mjue kuwa hata nyie mmejitia kitanzi, hamtaweza kuaminiwa kabisa.
Je hamjui kuwa kuna nafasi za ajira ambazo zingeweza kushikwa na wake zenu watoto wenu, wajomba zenu, shangazi zenu, dada zenu, na ndugu zenu watanzania ambazo zimeshikiliwa na hawa wageni?

Kuhusu kuwa wakenya ni wachapa kazi, sawa tunakubali, lakini je nao ni wasafi kiasi gani? Hivi mnajua kuwa kuna baadhi ya mawaziri nchini Kenya hawaruhusiwi kuingia nchini Marekani na Uingerza kwa sababu ya makosa ya Rushwa, je Uzalendo wao uko wapi, uadilifu wao ulo wapi? Je sisi, ni mawaziri wangapi wamezuiwa kuingia katika nchi hizo?

Hawa wazungu, wanasema kabisa kuwa katika nchi ambazo wananchi wake ni wapole na wanyeyekevu hata uwafanyie nini ni Tanzania, na ndio maana hapa Movenpick kuna baadhi ya wazungu wameongeza muda wa kuishi na kufanya kazi hapa nchini zaidi ya mara nne kwa kubadili nafasi zao za ajira ili kupata ridhaa ya kuendelea kuishi hapa nchini.

Hawataki kuondoka kwa kuwa nchi yetu ni Corrupt katika kila sekta. Wazungu hawa wanajilipa mishahara mikubwa tofauti na wazawa. Mtanzania anaweza kulipwa shilingi milioni 2 lakini akija mzungu kwa nafasi hiyo hiyo analipwa dola elfu sita, sio shilingi za kitanzania namaanisha dola za kimarekani achilia mbali malazi chakula na huduma nyingine kama kufuliwa nguo na kadhalika.
Mshahara mkubwa kabisa wa mtanzania hapa ni shilingi milioni mbili na mshahara wa mzungu wa chini kabisa ni dola elfu sita, na huyu mzungu anayelipwa hizi fedha ni nokoa tu, hajui kazi, kazi zote zinafanywa na mtanzania, rangi tu ndiyo inayomlinda.

Tunapenda kumalizia kwa kusema kuwa Mkenya aletwe lakini sheria na taratibu za uhamiaji zifuatwe.

Ni sisi wafanyakazi wa Hoteli ya Movenpick
Dar Es Salaam.


Kuna Maoni 28 mpaka sasa.

 1. Anonymous Anasema:

  wekk, nice move kuona mnapambana kuhakikisha mnaretain status yenu, mimi ni mtanzania mpambanaji kama nyie ila kinachonoboa kwenye move kama hiyo hakukosekani wapambe wanaowazunguka na ndio wanakuwa kikwazi, wazungu wanapokuja kuwekeza mara nyingi wanakuwa na scale nzuri ya mishahara in mind ila wanapokutana na baadhi ya wazawa wanawaharibu, i have good experience on that, pili kwa kweli inabidi mjiulize ni kwa nini wanangangania wageni, hakuna mwekezaji anaependa kutumia helA zaidi kununua workpermit ila anapokosa productivity lazima inabidi aingie extra charge kutafuta mgeni, watanzania productivity na hospitality yetu iko very poor, am sorry kuwa hata mimi ni mtanzania hasa katika nii fani ya hotel watanzania tuko nyuma sana, tusipojitahidi tutawapa nafasi wageni kujustfy kwa nini waajiri wageni,

 2. Anonymous Anasema:

  HAHAHAHA SAFI SANA KAZENI MSULI SIE WABEBA BOX TUNA SIKIA MAUMIVU YENU MICHUZI USIWABANIE JAMAA ZIDI KUWAPA TAFU, HAKUNA KUONEWA WANYONGE BWANA BLOGU YA JAMII TUNASAIDIANA. M

  BEBA BOX NUMBER MOJA OVERTIME MUHIMU.

 3. Anonymous Anasema:

  this is serious issue,,,ivi michuzi ili suala la ndugu zetu watanzania awa wa movenpick linafikia wakubwa?
  au ndo yaleyale ya EPA?kwanini hii nchi kuna watu wana roho za shetani za kukandamiza watanzania wenzetu na KUWAABUDU ngozi zingine au nchi zingine?
  ivi umeshawai ngaa kuishi na ao majirani zetu uone viroja na chuki dhidi yetu???

  ivi pesa ni nini asa zaidi ya UTU WA MTU AMBAYE NI NDUGUYO?

  hii news imenigusa sana,,ifikishwe basi kwa mkono ata kwa mhusika "angalao"wale waaminifu waliosalia ktk sekta ya serikali yetu....

  shenzy taipu waliopokea huu mlungula eti kuzima hii ishu
  me kila siku nasema iko siku KITAELEWEKA

  aluta kontinua,,,asante mtoa mada

 4. Anonymous Anasema:

  Natamani uzalendo na upiganaji huu wa wafanyakazi wa Moevenpick ungekuwa ndio character ya kila mtanzania. Ni kweli watanzania tuna sifa ya kuwa wapole, watulivu na wakarimu,ingawa ni nidhamu ya woga kwa sababu ilijengwa na siasa ya ujamaa na azimio la Arusha kwa mkono wa chuma,lakini sifa hii ndo kama hivi inakuwa abused, wageni wanataka watuonee na kututawala kwa sababu hiyo. Watanzania lazima tufahamu kwamba ulimwengu umebadilika. Sasa hivi hakuna undugu na ujamaa, ni SURVIVAL OF THE FITTEST! Tukiendelea kujihesabu ni wezi na wadokozi na wavivu kama viongozi wetu wapumbavu wanavyotuita na wajinga wengine waliochangia mada ya kwanza, na kutumia kigezo hicho eti kuajiri wageni ni kujitia kitanzi. Kama walivyosema wenzetu hawa, hata nchi zenye utawala wa kiimla wa kidini unaoendeshwa kwa sharia za kukata wezi mikono bado wezi wapo! Ni mbinguni tu ambako hakuna wezi na wadokozi. Ni upuuzi sana kusema watanzania ni wezi na wadokozi halafu unajifanya hujui kwamba kwanza sio wote walio hivyo na kwamba kila nchi hapa duniani ina elements hizo.

  Wafanyakazi wa Moevinpick kazeni buti. Nawashauri kama viongozi wenu watapuuza madai na maoni yenu mwende hata mahakamani. Kama uhamiaji watachukua rushwa kama wanavyofanya Ole Naiko na TIC yake kwa kuruhusu zaidi ya wageni 10 kufanya kazi kwa vibali vyao, pelekeni menejimenti na taasisi hizo zote mahakamani. Kuna taasisi za sheria zinazotoa msaada wa kisheria na kiuwakili kwa gharama nafuu sana kama LHRC, na pale Chuo kikuu (UDSM). Watumieni hao kushitaki kukiukwa sheria za ajira na uhamiaji katika hoteli hiyo.

  Mungu ibariki Tanzania na wazalendo wapenda nchi wote. Wanaoidharau nchi hii waliyozaliwa na kukulia na kuwaita watanzania wenzao wezi na wadokozi washindwe! Shame on them!

 5. Anonymous Anasema:

  Jibu la matatizo yote hayo ni kufanya kazi kwa uadilifu wa hali ya juu, kila mmoja awe msimamizi wa mwenzake na kamwe usimlinde mwovu na watu wawajibike kwa nafasi zao! Tukifanya hivyo Watanzania tutarudisha heshima yetu. Natamani kuiona Tanzania bila Rushwa, Mizengwe. Natamani kuiona tanzania ya wachapa kazi kwa manufaa ya watanzania!

 6. Anonymous Anasema:

  ndugu zangu wafanyakazi wa Movenpick nawapa pole pia hongereni za juhudi zenu, endeleeni tu iko siku mtafanikiwa wala msikate tamaa,mimi nilikuwa naishi huko nyumbani kwa sasa niko nje nachoweza kuwambia msitengemee sanaaa maoni wa watanzania walio nje wengi wao wanakasumba na wametawaliwa na tabia ya kujiona wao wameendelea sana lakini wamesahau kwamba na wao walitokea hukuhuku lakini ndio tulivyo watanzania uzalendo ziro, na ndio maana kila siku sisi tutakuwa wa mwisho ila isipokuwa jitihada binafsi ambazo nyinyi mnafanya,watanzania wengi waliopo nje ni masikini wa mawazo na fikara

 7. Anonymous Anasema:

  huyo mpishi hana management skills zozote na yeye kuwaongoza nimkitu cha ajabu sana.
  kwa mtu yeyote aliyekaa nje ya nchi atakuambia kuwa huyo mzungu atakuwa ameenda kwenye kozi ya mapishi halafu basi.

  hata huyo mkurugenzi mkuu inaonekana management skills zake ni mbovu, hayo matatizo yenu ni raisi sana kuyatatua kama kuna uongozi mzuri.
  wasiwatishe na rangi mimi nina uhakika kabisa hao jamaa hawana qualifications zozote.

  tafuta simu ya waziri wa mambo ya ndani na pia peleka malalamiko yako kwenye gazeti la mwanahalisi na this day

 8. Anonymous Anasema:

  yale yale mambo ya Embassy Hotel

 9. Anonymous Anasema:

  Hata sijui nisemeje, ukweli ni kwamba wengi wetu tuliotoa maoni hatujakumbana na hiyo hali, unakuta mtu anatoa tu maoni ili mradi nayeye kasema basi. Mimi binafsi siwezi kukushaurini muende kwenye chombo chochote hapo nchini, kwani yalishanikuta, nilipokwenda kudai haki yangu kunakohusika nikakuta tayari jamaa wameshapenyeza rupia na nilitazamwa kama nyanya mbichi na huyo mhusika wa kunisaidia kupata haki yangu. Kwa kuwa nilikuwa naondoka kwenda masomoni ilibidi niache haki yangu ipotee hivi hivi, na tena mwajiri wangu alinilazimisha kuchagua moja, shule au kazi. Nikaamua kuchagua shule nikaacha kazi. Na HR wetu alikuwa Mkenya hajui labour laws za Tanzania hata moja, yeye kila alichokikuta ambacho MaHR waliopita nyuma yake wameweka kulinda maslahi ya wafanyakazi alikifutilia mbali tena bila kufuata utaratibu unaotakiwa katika masuala ya policy.

  Yeye na hao wageni wenziwe wali plunder kisawasawa na kujitengenezea mazingira mazuri ya kula mali za kampuni. Kwa hiyo usimuone huyo Shousha anamtaka Mkenya mkafikiri kuwa anamtaka kwa ajili ya kuwakomoa, la anamtaka ili wapate kufanya ufisadi wa nguvu, kwani Watanzania bado waoga, na akifanya naye ufisadi atawaambia watanzania wenziwe siri yao.

  Kusema sijui mkalalamike wapi, kwa kweli hakuna, kwa sababu kila mahali kumeoza, kuanzia huko uhamiaji, wizara ya kazi kunakohusika na utoaji wa vibali, TIC na hata kwenye vyombo vya habari, ukiondoa hizi blogu zetu.

  Ushauri wangu kwenu, tulieni jipangeni na mrekodi maovu yao yote, muweke ushahidi mzito, waacheni wamlete huyo Mkenya wao, lakini nyie kumbukeni kurekodi utumbo wao wote, kumbukeni pia umoja ni nguvu, lazima muwe wamoja msikubali divide & rule. Kisha with evidences za madudu yao tumeni kwa mwajiri wao. Lazima hoteli kama hiyo Movenpick itakuwa inaendeshwa na hoteli ya kimataifa kutoka nje, ambayo itakuwa na website na contact details, elezeni jinsi mambo yanavyoenda na jinsi msivyoridhishwa na utendaji wa kazi wa hao waliowaleta. Hapo mtakuwa mmelifikisha suala hilo kunakohusika. Kama mmiliki wake atakuwa makini na hataki kuharibu sifa za hoteli yake kwa kuonekana kuwa wanavunja sheria za nchi huko wanakofanya biashara basi watatuma ujumbe wao kuja kuchunguza madai yenu na kuchukua hatua.

  Mko tayari lakini, sio wakati unatumwa ujumbe kuja kuwasikiliza nyie mnaingia mitini mnamuachia mtu mmoja au wawili kwa kuogopa kufukuzwa kazi? Maana ikiwa lenu moja na wote mkiulizwa mtakuwa tayari kusema ukweli lazima wenyewe wata take actions.

  Mkiona huko kwa wenye hisa kubwa/waendeshaji hakuna majibu, basi pelekeni hiyo story yenu kwa vyombo vya habari vya huko aliko huyo mwendeshaji, kama ni UK, bbc; kama ni US basi CNN; pia tumieni blogs maarufu za nje, be creative & dramatic pengine itasaidia.

 10. Anonymous Anasema:

  ndugu wafanyakazi wa movenpick,ningekushauri uzingatie zaidi hayo malalamiko yako kufika kwa vyombo husika kama uhamiaji,wizara ya kazi tic n.k ningekushauri usijibizane na wadau kwani hutaweza kubishana na watu usiowaona,kuhusu kugeneralize kuwa nyinyi wote ni wezi si sahihi na poleni sana....ila na wewe umekosea kugeneralize kuwa watu wa ughaibuni wametoa maoni hayo sio wote,mimi niko nje na naumia jinsi mnavyonyanyasika,nafikiria niko nje wazungu wananinyanyasa na nyumbani kaka na dada zetu wananyanyaswa na hao wazungu kwa kweli hii inauma,hii yote ni kwa sababu viongozi wetu ni corrupt kama ulivyosemak, kuhusu wizi airport na bandari ni mifano kumbuka airport wanapita watu wote sio wanaishi ughaibuni tu, kwahio usijali sana baadhi ya watu wanaserma nini take the positives,hakikisha malalamiko yenu mnafikisha kunakohusika yasiishie hapa tu

 11. mtanga Anasema:

  jamani watanzania tuamkeni,hayo yaliyosemwa na wafanyakazi wa moven pig yameniuma kiasi cha kulia,sabbabu na jua ni ukwlei mtupu wnayosema,mimi ni mbongo ambae niko ughaibuni,huku usome hata mpaka upate phd.lakini hupati kazi ya hayo uliyosemea utaishia kubeba box wanaajiriwa wazawa, sasa sisi wabongo tunaacha kuaajiri wabongo tunaajiri wakenya ,jamani tuamkeni,mi mkisema wakenya nakumbuka jinsi walivyotutesa enzi za bluband,tuamken wabongo,hao wazungu ni waezi kuliko wabongo kama kuna mtu anajua hilo wala hatabisha ila kama hujui hataamini lakini hao wazungui kwa rushwa ni namba 1,wabongo tuamkeni.

 12. Anonymous Anasema:

  Ndg zangu, nimesoma vema ujumbe huu tangu wa kwanza na huu wa leo. Nimewaelewa vizuri sana. Kuna hoja za msingi na kama kweli tunaipenda nchi yetu ni lazima tuwe pamoja.

  Kuchangia.

  1. Sikubaliani katu na hoja ya kumleta Meneja Rasrimali Watu kutoka Kenya kwa sababu zozote zile. Huu ni upuuzi na ni matusi kwa Serikali ya Tanzania. Tangu zamani UDSM wanafundisha taalamu za uongozi wa biashara ikiwa ni pamoja na human resource management. Baadaye Chuo Kikuu cha Mzumbe wakafuata nyao achilia mbali wale wote waliosoma kupitia taasis mbali mbali za ndani na nje ya nchi. Kama tunaajili wageni kwa kazi hizi, basi hakuna sababu ya kuwa na vyuo hivyo maana itakuwa ni kupoteza fedha bila sababu. Lakini hao hao wageni watapata sababu ya kututukana Watanzania kwa kutuona ni wajinga.

  2. Kusema kwamba Wakenya wanachapa kazi kuliko Watanzania, hii ni hoja isiyokuwa ya uwazi. Unapimaje uwezo wa Mameneja? Ni viashiria vipi vinatumika kuijenga hoja hii na kuifanya kuwa na uhalali wa kuwasuta Mameneja wa Tanzania. Wengi waliochangia hoja hii, naweza kusema si tu kuwa wamekurupuka, lakini pia wana mtazamo mfinyu wa kifkra. Mimi ni Mtanzania, nimeona kutoka Kenya, ninawafahamu vizuri. Anayesema ana hoja aleta utafiti, au kama utafiti haupo, tuandike mpango utaoatuwezesha kufanya utafiti kuwa kutathmini uwezo wa utendaji kazi wa Mameneja Rasrimali Watu kutoka Kenya na Tanzania. Hata kama fedha za kufanyia kazi hii hatuna, tutachangishana. Tukiujua uwezo wao kwa viashiria sahihi vinavyopimwa kwa muda usiopungua miaka 3 hadi 5, itatusaidia kujua ni jinsi gani wanaonekana wanauwezo mdogo watafutiwe msaada. Maana hii ndiyo kazi ya Wizara ya Afrika Mashariki, Wizara ya Kazi, ILO, Wizara ya Elimu na wadau wengine. Kukaa nje ya nchi, kusitufanye kutamka kila neno linalotujia mawazoni.

  3. Hapa Tanzania, nimefanya kazi na Wenye Viwanda. Kuna matatizo makubwa pengine kuliko hili la Movenpick Hotel. Nafurahi tu kuwa wamekuwa jasiri kueleza hali halisi. Tanzania yetu ni kama nchi iliyomateka. Haina mwenyewe, uongozi wetu ni mazingaombwe. Niliwahi kuambiwa na Prof. Wangu wa Uchumi kutoka Japan kuwa nchi yetu ina kila kitu, isipokuwa Uongozi wenye uzalendo. Nilijisikia vibaya sana kuwa kumbe tunajulikana hadi katika ngazi ya Kimataifa. Na zaidi, aliniahakikishia kuwa nchi yetu haiwezi kuendelezwa kwa njia ya "ku-import" watu kutoka ng'ambo. Hapa binafsi nakubaliana. Ambaye anapinga hoja hizi, alete mifano ya nchi iliyoendelezwa na wageni hadi ikawa nchi tajiri duniani??

  4. Kwamba Watanzania ni Wezi!!! Maswali" (a) Kwa nini wezi?? (b) Ni akina nani?? (c) Sheria ya Nchi inasemaje?? Maana ya Watanzania ni wote hata kama ni wekundu! Hata kama wapo nje ya Tanzania. Hoja hii ya wizi, imeshabiokiwa sana na watu ambao bila shaka wapo nje ya Tanzania. Wanadhani kwa kuwa nje wao hawahusiki. (d) Ukweli ukoje kwa mtu mmoja mmoja?? Nashangaa kuona watu wanakosa uzalendo ktk hili. Pia ni dalili ya utapiamlo wa akili mtu kwenda kutangaza madhaifu ya watu wa nyumbani mwake. Sijawahi kuona. Kama kuna haya mapungufu, si kwamba tukae kimya, bali tukanyane sisi kwa sisi ndani ya nchi yetu kwa kutumia sheria na taratibu zilizopo.

  5. Nina uhakika endapo Movenpick wataajili huyo wanayedhani atafanya kazi ya kukukomoa watu, kitakachofanyika hapo ni migogoro ya kila siku. Kama hamuamini nendeneni pale East African Cables, mtajifunza ninyi wenyewe. Hata hivyo, kinatharia na kivitendo, mtu mwenye uelewa mzuri wa wafanyakazi ndiye anayeweza kuwasimamia vizuri na si mgeni. Ninyi mliopo nje ya Tanzania, fanyeni kuangalia ni makapuni mangapi kwenye nchi mlizopo wameajiri wageni kama Mameneja Rasrimali watu??

  Niishie hapa, naamini watu wengi wenye mapenzi mema na Tanzania watatoa mchango wenye maana ya kuliokoa Taifa letu na sio kuloloma tu bila hoja zenye uzalendo. Kumbukeni, kila hoja tunayiotoa ilenge kulisanua Taifa letu na udhaifu wa kitaasisi na kimfumo tunaoushuhudia leo. Hapa ndipo tutakuwa kweli tunamsaidia Rais wetu kwa changamoto nyingi zinazomkabili.

  Mdau.

 13. Anonymous Anasema:

  Kuna siku nilitoa comment ya kuwataka watanzania kuwa wazalendo, kwa mtazamo wangu jamii yetu haina uzalendo kabisa na wamekuwa kama vilema wa kuabudu mataifa mengine, hili swala linakera sanaaaa. Kwa maoni yangu ni upuuzi uliopitiliza kuthamini mataifa mengine maana kwa kufanya hivyo tunajiangamiza wengewe na ili tatizo ni kubwa kwa maana hata viongozi wetu nao wameathilika. "Funika kombe mwana haramu apite" maana ya msemo huu ni kwamba linapokuja swala la uzalendo tunasahau tofauti zetu au kasoro zetu kwanza maana kasoro hazikosekani katika jamii na hapo ndipo watanzania tunapokosea kwa kuanza kuabudu mataifa mengine hii inatia kichefuchefu sana, kwanini tusiwe na tamaduni ya kujivunia utanzania wetu??? ni utumwa wa kiakili kuthamini mataifa mengine. Nawatakieni kila la kheri, hakuna mapambono rahisi kazeni kamba mtafanikiwa, hii ni nchi yetu!!!
  Mungu ibariki Tanzania

 14. Anonymous Anasema:

  Wadau naomba nianze kwa kuwapa pole ingawa sioni tatizo lolote kutokana na maelezo yako.Umesema haiwezekani katika taasisi iliyoajiri wafanyakazi 300 kuwa wote ni waaminifu,sijui hiyo conclusion umeipata kutokana na reseach ipi.Kwa maelezo hayu tu umejustify kuwa wizi ni halali hapo kazini kwenu.Jaribu kufanya utafiti utagundua kuna makampuni mengi makubwa yaliyoajiri zaidi ya watu milioni moja na wote wapo safi.Kuna hotels ambazo ukisahau pesa au electronics chumbani utatafutwa ili urudishiwe,mdau tukubaliane kuwa huu utamaduni haupo siyo tu hotelini kwenu bali hotels nyingi hapo nyumbani.Malalamiko yako ya awali ni kuwa hamkutaka kabisa kuongozwa na mgeni.Baada ya mashambulizi ya watoa hoja sasa mko tayari kuongozwa na wageni waoishi kihalali.Tatizo letu watanzania ni ile siasa ya ujamaa na kujitegemea ndiyo imetuharibu.Katika mfumo wa kibepari ni kuwa hiyo ni private sector.Muajiri anahaki ya kuajiri mtu wa taifa lolote ingawa ni lazima asilimia fulani wawe wazawa.Hayo ndiyo mambo ya globalization,lazima tukubali ku-intaract na global community kama vile mamilioni ya watanzania wanaoishi nje,hususan Arabuni,USA,UK Scandnavia nk.kupata ajira na kusaidia nyumbani wakati wapo raia wa nchi hizo ambao hawana kazi.Kumbukeni kuwa mnayoilalamikia ni mali binafsi ya muwekezaji kutoka nje.Ukitaka watanzania pekee wapate ajira basi pengine watanzania pekee ndiyo wawe wawekezaji.Mkiukubali ubepari acheni malalamiko fanyeni kazi vizuri.Mkiwa na good customer service mauzo yataongezeka na viwango vyenu vya mishahara vitapanda.Kama udokozi utaendelea wateja watakimbia mtakosa mishahara.Hakuna waziri wa kenya wala wa Tanzania anayefanya kazi hotelini kwenu hivyo mifano ya mawazili hao haihusiani kabisa na udokozi hapo hotelini.Ukiona mazingira ni magumu kwenye sector binafsi ndani ya ubepari acha kazi katafute kazi kwenye chama cha ushirika ambako mali haina mwenyewe.Kwahiyo ndugu zangu fanyeni kazi acheni siasa.Wateja wakiingia changamkeni wapokeeni with smile and remember customers are always right.CEO na wafanyakazi wa ngazi za juu kulipwa six figures na bonus lundo wakati wafanyakazi wa ngazi za chini three figures is ok in capitalist system.kumbukeni kuwa Nyerere aliwahi kusema kuwa ubepari ni unyama alikuwa na maana hiyo.

 15. Anonymous Anasema:

  Jamani Bongo yetu.Inaumaaaaa.Wadau mtazunguka mara wabongo mara management ila wafanyakazi wala management haina shida.Kiini kikubwa hapa ni system nzima ya serikali inasababisha kwani naapa kutafuta haki tanzania ni ngumu ni adimu hasa ukikabili mtu mwenye Rupia.Ukiwa na kesi nenda polisi wewe ndo unakuwa mradi wao.kimbilia mwanasheria ndo utakiona cha moto.Mifumo yetu haina sheria.la kama mifumo ingekuwa inafanya kazi huyo mwekaezaji angepata chake na mwajiliwa akafurahia kazi yake.hao wanaojiita wabeba box ni wabongo nami nimmoja wao tunajiona tofauti kwa sababu tumefika sehemu ambako sheria inafanya kazi.tungekuwa hapo hata sisi tungekuwa wale wale.serikali IBEBESHWE LAWAMA ZOTE.HUU MZIGO ITAUBEBA MPAKA YENYEWE IJIAMBIE KUACHA UBABAISHAJI IWEKE SYSTEM SAWA.SIELEWI UGUMU UNAKUJAJE.Viongozi wetu walivyoanza kazi waliweza kuonyesha jamii kuwa Tanzania can make a bit of change.Tanzania inatakiwa mbabe mwenye roho ya kijeshi.hayo mambo hayapo hapo tu yaposehemu zote kuna watu hawajui hata kama kuna haki.Kagame anawezaje?wadau nendeni web ya Rwanda muone sehemu ya ruswa watu wanavyong'olewa kwa tips za wafanyakazi.KWA NINI SISI WATANZANIA?????.Wachangiaji ningewashauri walie na mifumo feki ya nchi yetu yenye mkono butu.Nilishawahi kwenda Ardhi kutafuta commercial area wakati ndo ramani za kigamboni na Buyuni ziko busy naapa hazitajwi hata kama ziko ndani ya plan.kwa nini????.samahani wadau nachukia mifumo ya Rushwa to death.NASHAURI TENA WALE WENYE UCHUNGU TUELEKEZENI NGUVU ZETU KWENYE MIFUMO.SI MBONGO WALA MWEKEZAJI.TUTAFIKA TU.NAMWOMBEA MICHUZI WETU MUNGU AZIDI KUMPA UZIMA KWANI ANA MCHANGO MKUBWA SANA KWA NCHI YETU.NAWASILISHA.

 16. Anonymous Anasema:

  Kwanza poleni na hayo majanga ndungu zanguni,sasa mimi nataka kuuliza haya huyo mpishi yamemkumbayapi kuingilia ya watu wa position nyingine?km yy ni chef basi yabidi awe anadeal na watu waku wa huko jikoni hadi restaurant,na nyie km ni housekeeping then mkuu wenu sio sasa hao wengine wanavalianjuga yawatu wengine kivipi.Then jaribuni pia kuwa chunguza hata hao viongozi wenu zaidi kwani huwezi jua wanajidai kuwa wagumu kwenu kumbe wenyewe ndio wezi wakubwa kama msemavyo kuwa huwa chukuwa wenzao wengine kwasababu ya ngozi then lazima wenyewe huwaibieni,then na km wote mpo hapo nchini kwanini na nyie msilipwe dollars basi km wao wanavyo walipa wenzao?kwasababu ukiangalia hiyo ni ujinga km ni hivyo basi kila mtu alipwe in dollars,sio wengine Tshs wengine Us$?Ahh poleni sana ndugu zanguni...

 17. Anonymous Anasema:

  mimi nimeshateseka sana na kuzungushwa na viongozi watatua matatizo,sasa nimeamua sitaki tena njia za kupanga foleni kutizamwa kama sanamu,sasa njia yangu ni yamkato tu sheria mkononi na nawaomba na wengine njia hii tuitumie ndani ya mwaka mmoja tu mambo yataanza kunyooka.
  haki kwa tanzania ni ngumu kupatikana sana maana kila muhusika ni mungu mtu sehemu yake,na asilimia karibu na mia wote wanajali anafaidikaje nawewe anapokusaidia.sasa basi mimi nimesha choka,haki yangu sitaiomba nitaidai hata kwa mabavu na atakaye niwekea kauzibe nitazaanaye jino kwa jino.

 18. Anonymous Anasema:

  NINGEKUA RAIS WA NJI NINGEISHA AMUA KUINGILIA KATI TATIZO HILI BINAFSI ILI NIJUE KILICHOJIFICHA. HILI SIO SUALA LA HOTELI TUU BALI HATA USALAMA WA NCHI. SASA HAPA KAMA KIONGOZI WA NCHI UTAFUNIWE KIASI GANI?

 19. msemakweli Anasema:

  Mimi simuonei MTZ yeyote huruma eti kwa kuwa wanaajiri Mkenya katika hoteli ya Movenpick.
  kama kuna malalimiko ambayo wawekezaji wanayapata kutoka katika huduma na wanaaamua kuajiri watu wenye sifa za kurekebisha hilo tatizo sioni kama ni kosa.
  kama wanaamini kuajiri MTZ HR na hataweza fukuza WATZ wavivu na wadokozi basi ni bora kuajiri Mkenya ili awafukuzilie mbali.
  Kama mnataka kubakia kazini ndugu zangu ningewaomba muongee na uongozi, m-wataje wezi WATZ wanaoibia hoteli ili wafukuzwe na mbaki na wTZ wafanyakazi wema. Muongeze bidii ya kazi muombe kusoma customer service na mtabki kazini bila shida. Hii kulalamika kwamba mmekuwa generalize na watu walio nje kwamba nyinyi ni wezini kosa ambalo hata wewe mwandishi umelifanya kwa kusema eti" waliowakashifu wako nje". Huna facts za kuonyesha hivyo kwani mtu anaweza andika yuko nje wakati yuko hapa TZ.Na kusema eti kuna mawaziri Kenya hawaruhusiwi kwenda nje pia ni kuondoa hoja yenu ya wizi na kuondoa kutoa mada inayohusu ajira zenu.
  Mnatakiwa mmfukuzwe tu, huwezi taka kupata mshahara zaidi ya milioni mbili, wakati hujui siku hizi katika mahoteli makubwa wapishi wakuu (Chief Chef)ndio wanaoleta wateja, ndio wanaokuwa na hisa ya asilimia 40 kwa kudhaminiwa na matajiri wenye pesa za kuanzisha hoteli kama wawekezaji.
  Mnatakiwa muelewe upande wa pili wa biashara na faida za kuongoza hoteli na sio kulalamikia mishahara. Maana hio milioni mbili mnayopta ni asilimia 200 zaidi ya kima cha chini cha mfanyakazi wa TZ wa serikali anayelipwa kima cha chini. lazima pia muelewe kwamba mara nyingine rangi au uraia hufanya mtu kulipwa zaidi na ndio neno "expatriate" likatokea.
  Watu walio huko nje watawalamikia kwa kuwa hiyo milioni mbili kama hamridhiki nayo wao pia wanaitafuta kwa hali na mali. Nasikia huko wanapata hiyo fedha kwa kutokulala na kwa kufanya kazi mbili au zaidi. Hivyo nakubaliana nao kwamba wamewalalamikia kwamba mnatakiwa kujirekebisha.
  Tumieni mda huu kujirekebisha na kufanya kazi kwa bidii na nimeona kwani mmeogopa sana kusikia mkenya anakuja kuwaondoa kazi.
  Mwisho nimekaa sana hapa TZ na nimeona siku hizi tuna mtindo wa kuita wizara ya mambo ya ndani kwenda kukagua wafanyakazi wakenya, ili wafukuzwe. Hii haitasadia lolote kwani wenye matatizo ni sisi na tusipokubali kwamba tuna matatizo basi tutabaki na matatizo.
  Nimekwenda hapa hotelini movenpick Royal palm leo na tabia hii ya kutoku-saviwa kwa kuwa mimi ni MTZ mweusi nimeona bado ipo. Nimekaa hapo Kibo bar kwa dakika 35 bila kueletewa huduma niliyoiomba na nimeona wazungu pembeni yangu wanachangamkiwa sana kwa kutoa tip na kusahau kwamba hata mimi ningetoa TIP kama mngekuja kunihudumia haraka. hivyo kulalamika kwamba eti rangi ndio inwafanya wanatamba wakati nyinyi mmnionyesha wazi kwamba rangi inatamba kwa kuchelewa kunihudumia.
  Kwa tarifa yenu ningependa muondolowe tu au kama ikiwezekana wawekezaji waondoke na nyinyi mkose ajira maana hamjui mlichonacho mkononi mpaka muwe hamnacho.

 20. Anonymous Anasema:

  Poleni sana wafanyakazi wa Movenpick. Kwanza mmejikanyaga sana katika habari hii, nina wasuport kwa kilio chetu lakini kwa habari hii mmejikosoa wenyewe na sijui mnachikipigania ni nini hasa kwani inaonyesha kwamba mnakubali makosa yenu ya udokozi, uzembe, na utovu wa nidhamu kazini. Wahenga walisema samaki mmoja akioza....." utamalizia wenyewe hapo. Kuhusu swala la kulipwa mshahara kati ya mzungu na mtanzania hilo ni tofauti kwani mgeni analipwa kama expert na wewe unalipwa kama kibarua. Inategemeana na elimu uliyonayo. Kwa jinsi ninavyoelewa mtu yeyote anayetoka nchi za magharibi hata kama hajakaa sana darasani likini ananidhamu ya kazi. Ukae ukijua kwamba nchi za nje sio wote walioenda shule wanafanya kazi kwenye makampuni mbalimbali wengi wa wafanyakazi wengi wameishia High school ni sawa na form four ya Tanzania lakini wengi ndo manager(supervisors) na hii ni kutokana na experience za kufanya kazi kwa muda mrefu na kuheshimu kazi. I hope kama mngepata visa ya exchange workers mje kwenye nchi kama marekani muone jinsi watu wanavyofanya kazi zinazofanana na zenu mtajiona huko ni hamfanyi kitu. Heshimu kazi ya mtu anayetoka nje ya nchi nidhamu yake ya kazi ni ya hali ya juu. Mimi ninachoona kama bado mnaendelea na kazi mjirekebishe na kujituma. Mnachopigania hapa ni kuwa na manager wa Human Resources mtanzania atakaye wapa fevours katika kutekeleza matakwa yenu binafsi sio kwa faida ya kampuni! watu wamesoma malalamiko yenu na kila mtu spoke his/her mind ni juu yenu kuchuja. Na unaposema hawa vigogo wenu wamehaha sidhani kama kuna ukweli ndani yake! Tukisema wafuate sheria za kazi hakuna mfanyakazi atakayebakia kazini.
  Kwahiyo muwe makini katika kutoa malalamiko yenu lazima mwandishi ayapitie kwa makini ili msijiingize katika mitego.
  Mdau wa Damu

 21. Anonymous Anasema:

  KAMA NILIVYOSEMA HAPO JUU TATIZO LA WATANZANIA NI NIDHAMU YA UOGA!INAYOSABABISHWA NA MAMBO YA KUWEKEANA VIFUA KWA KUWA TU KILA MTU ANAPATA CHEO KWA KUJUANA!! MIMI SIAMINI KAMA HOJA KUBWA KAMA HII HAIJAWAFIKIA WAKUU NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI!!! OF COURSE YES! LAKINI KILA MTU ANAJIFANYA HAONI! MIMI HAPA INANIFANYA NIMKUMBUKE MPIGANAJI MMOJA ALIYEPOTEZA MAISHA YAKE WAKATI ULE WA HOJA YA LOLIONDO!! MNAKUMBUKA?? MIMI NASEMA SASA WAKATI ULE UMESHAPITA NA IKO SIKU VIONGOZI WATATIA AKILI NA HIVYO VIJIMANENO VYAO VITAMU WANAVYOTUMIA KUWARUBUNI WANANCHI VITAWATOKEA PUANI! HAYA..HATUKO MBALI SANA NA HIYO SIKU!! NINACHOJARIBU KUSEMA NI KUWA HOJA KAMA HII LEO ILITAKIWA IWE GUMNZO KATIKA MAGAZETI, RADIO NA VYOMBO VYA HABARI LAKINI WAANDISHI NA WAHARIRI WANAJIFANYA KAMA HAWAONI! UPUUZI HUU!! MNAKAA MNAKINGA MISHAHARA TU NA HABARI HAMTAKI KUZIFANYIA KAZI. HEBU ANGALIENI HUKU NCHI ZA WATU VYOMBO VYA HABRI VINAANDIKA HABARI HADI INABAKI HAKUNA CHA KUANDIKA!! NA SOMETIMES INABIDI WATOE HATA FEDHA ILI KUPATA HABARI WAKATI NYIE HAPO MNAKAA OFISINI MNAJAMBA JAMBA TU!(KUTOA ANKAL TU HAPA WENGINE WOTE HOVYOO)

 22. Anonymous Anasema:

  Waziri mwangunga kuwa na tabia ya kusoma vitu kama hivi na kupata maoni toka sehemu mbali mbali. usikae kusoma mails za wawindaji wa loliondo na wanyama wanaosafirishwa nje ya nchi. Hii ni moja kati ya kazi zako wala huna sababu ya kumtuma katibu wako. Mbona Loliondo imekodishwa kwa miaka 33 wala hujatuuambia kupitia njia yoyote??? wake up mwangunga na big up blog ya jamii na wabeba box kuweni wakweli acheni utumwa.

  Mkereketwa wizarani

 23. Anonymous Anasema:

  Salamu kwa wote.
  Nilipoona malalamiko ya wafanyakazi wa Movenpick kwa mara ya kwanza, niliyatafakari na kuona kwamba si ajabu kwa uongozi kutaka kubadili wafanyakazi kwa sababu ya matatizo ya uadilifu kazini. Binafsi, imenitokea mara nyingi katika hoteli kama hizi nyumbani ambapo mfanyakazi anakuletea bili halafu unakuta kwa mfano sahani mbili za chakula hazijawekwa kwenye bili. Ukimuuliza anasema "Nilisahau, kwa hiyo jumla itakuwa Tshs 30,000 siyo Tshs 20,000". Lakini siyo kweli kwamba alisahau - ni njama ya kupata zaidi. Hali hii huwa inaudhi sana na NIMEKATAA kuwa mshiriki. Huwa nafurahia huduma nzuri na ninafikiri wafanyakazi wa mahotelini wanaotoa huduma nzuri wanastahili BAKSHISHI inayoendana na huduma waliyoiyoa; na hivyo ndivyo ninavyofanya nikienda hotelini labda mtu ajaribu kufanya michezo ya wizi.

  Zaidi ya masuala ya uadilifu kazini, kuna jambo muhimu zaidi ambalo watanzania inabidi tulitafakari nalo ni "JE NI KWELI KUWA KUFUNGUA SOKO LA AJIRA NCHINI KUNAWAUMIZA WATANZANIA?". Binafsi nina maoni yafuatayo:

  1. Changamoto ya ushindani kazini, yaani, kufahamu kuwa utapoteza kazi kama usipoifanya vyema kunampa mtu msukumo wa kufanya kazi kwa uadilifu na jitihada zote.

  2. Kufanya kazi na mtu mwenye uzoefu tofauti (kutoka nchi nyingine) au kushindania nafasi za kazi na watu kutoka nje ya nchi kunatupa msukumo wa kupandisha viwango vyetu vya kazi katika hadhi ya kimataifa.

  Sisemi kuwa tusiwasaidie watanzania kupata uzoefu kazini ila ninachosema ni kwamba tusikumbatie ajira Tanzania kwa muda mrefu na kukataa ushindani kutoka nje kwa sababu kufanya hivyo kutatudumaza kimaendeleo. Wachumi wanasema "kulinda masoko ni vyema lakini ulinzi ukiendelea kwa muda mrefu unadumaza maendeleo".

  3. Kuhusu mishahara: Ninaamini kuwa mtu alipwe kutokana na mchango wake kazini. Anayefanya kazi kwa juhudi alipwe vizuri na anayezembea alipwe kidogo. Mara nyingi (sio mara zote), ukiona kuwa kampuni iko tayari kutafuta mtu kutoka nje, kumtafutia kibali cha uhamiaji na heka heka zote za uajiri na pia kumpa mtu huyu mshahara mkubwa; kuna uwezekano kuwa wanategemea kuwa mtu huyu ana ufanisi zaidi katika kazi hiyo. Yote hayo ni kwa sababu ya kufunga soko la ajira - hatuna ushindani hivyo hatuna msukumo wa kufanya kazi kwa juhudi. Simaanishi kuwa tufungue soko la ajira Tanzania kesho. Inadidi tuwape watanzania nafasi ya kujiimarisha na kufikia viwango vya kimataifa lakini pia inabidi tuanze kuweka mikakati ya kufungua soko la ajira.

  Mtazamo wangu hauna maana ya kuhalalisha mishahara ya wanayolipwa watanzania au wageni ila ninasema kuwa "Ukifanya kazi vizuri, utapata kazi itakayokulipa kutokana na ufanisi wako. Zaidi, mwajiri wako hatataka uondoke".

  4. Mbona sisi tunafanya kazi nchi za watu. Kuna watanzania wangapi wanafanya kazi nchi za nje ikiwemo Kenya? Hatuwezi kutegemea nchi nyingine zikubali kuajiri watanzania na siji tusikubali kuwaajiri watu wao.

  Mwisho, nawapongeza wafanyakazi wa Movenpick kwa kujisimamia lakini pia nawapa changamoto "TUSIOGOPE". Kama tunajua kuwa watanzania tuna uwezo wa kufanya kazi na tunaweza kudhihirisha hilo basi hata kama tukifungua soko la ajira bado tutaajiriwa kwa sababu UFANISI WETU NI WA HALI YA JUU.

  Kila la Kheri,
  Mdau

 24. Anonymous Anasema:

  Sisi Watanzania tunajua kulalamika tu. Kwenye kazi ni zero kabisa. Hakuna bidii, uadilifu wala uaminifu. Imefika wakati sasa lazima tujiangalie na tujirekebishe. Nyie wafanyakazi wa Movenpick mnalalamika sasa, je mipaka ya East Africa ikifunguliwa itakuaje? Tusubiri tuone. Mtarudi vijijini wote nyie. Chapeni kazi, kama hamumpendi mwajiri wenu, ondokeni. Kwani mmelazimishwa? Mbona kuna hoteli nyingi za wazawa mnaweza kwenda kufanya kazi? Acheni hizo!!!

 25. Anonymous Anasema:

  jamani poleni sana ndugu zangu ila natakakuwakumbusha ya kwamba movenpik ni sector binafsi hivyo basi masuala ya ndani hayawezi kuletwa kwenye umma nawaomba kuwa wavumilivu kwani hivileo tupo kwenye soko huria na ukizingatia tupo kwenye jumuia ya africa mashariki tuache kutupa lawama lazima tupambane nazo kwambinu ya vitendo haswa elimu asante

 26. Anonymous Anasema:

  JAMANI UKISIKIA KUWA TANZANIA NIA NI VICTIM WA PROPAGANDA:SIJAWAHI KUONA WATU WASHAMBA WA KIMAWAZO KAMA WATANZANIA!!WATANZANIA KWA MUDA MREFU TUMEJAWA NA INFERIORITE COMPLEX NA NDIO MAANA HATUJIAMINI NA NI RAHISI KUTAWALIWA.
  HIVI KUNA MIJITU MIJIZI KAMA WAKENYA?
  SIJAWAHI ONA MIJITU MIJIZI MIPENDA RUSHWA NA UKABILA KAMA WAKENYA!!SASA HII LEO MTU AKIWAAMBIA WATANZANIA WEZI!!HII NI POLICY YA MPE MBWA JINA BAYA UMTANDIKE,JIVUNIENI KUWA WATANZANIA NAWALA MSITISHWE NA WALOWEZI WACHACHE WANAOTAKA KUFAIDIKA VINAVYOSTAHILI KUFAIDIKA NA WANYONGE WAKITANZANIA!!
  HAO WAZUNGU KUJIWEKEA MISHAHARA MIKUBWA HIYO TU PEKE YAKE NI WIZI MKUBWA.
  HIVI KUNA NCHI IMETAWALIWA NA RUSHWA NA WIZI KAMA KENYA?NA NDIOMAANA HILI NENO UFISADI KWENYE SIASA LIMEANZIA KWAO!!WANANCHI WAO WALIO WENGI NI MASKINI KABISA

 27. Anonymous Anasema:

  Watz kwanza tuna roho ya kutokupendana,tupendane kwanza alafu hayo yote yafuate.watu kila leo wanatabu hii mara hii.tufanye kazi kwa bidii,tuheshimu kazi,na kuijali,watanzania tupende kuambiwa ukweli,tupende kuheshimiana maana watu wanadharau kazi za watu,kama ww ofcn kwako ni manager basi ukija kwangu mimi receptionist uniheshimu kama unapokuwa kazini kwako.ukija kwangu me ni hotelier niheshimu pia,kama mimi ni pump attendernt niheshimu pia jamani,kama me ni muuza genge tuheshimieane jamani.sio kwasababu ww ni boss basi unaenda ofcn kwa mtu unadharau kama nn.hischo ndio kinachotushushia hadhi watz jamani

 28. Anonymous Anasema:

  Mimi naamini malalamiko ya wafanyakazi wa Movenpick ni ya msingi kabisa, nchi yeyote duniani ina sheria na taratibu ambazo lazima zifuatwe, ninavyofahamu mimi pamoja na kufungua soko la ajira kwa nchi za Afrika Mashariki lakini bado nafasi za Human Resourses Managers lazima zishikwe na wazawa na sababu zake ziko wazi, ni lazima azijue sheria za kazi za nchi husika, sasa Movenpick wanapotaka kumwajiri mkenya wanataka huyo jamaa a-apply labour laws za Kenya hapa nchini kwetu?! Hata hivyo hoja wanayokomalia baadhi ya wadau ya kugenarise kuwa watanzania wote ni wezi kwa hiyo bora aletwe mkenya ambaye hatakuwa na huruma kwani atawatia adabu wa-TZ!! Hivi ikitokea wadau wengi wakatoa pendekezo kuwa kutokana na wimbi la uhalifu kama ujambazi na uhalifu mwingine kama vile wizi wa kwenye mabenki uvamizi wa visiwa kama ilivyotokea huko Ukerewe na vibaka kuwapora watu kila kukicha bila kudhibitiwa,je tuajiri mkuu wa jeshi la polisi toka nje? je Serikali yetu tukufu italiafiki nakulipitisha pendekezo hilo?! NAOMBA KUWASILISHA HOJA