Juu na chini Babu Seya na wanawe wakiwasili Mahakama ya Rufaa leo


Nguza Viking a.k.a Babu Seya (kuume) akijaribu kumfariji mwanae Papii Kocha mtoto wa mfalme baada ya rufaa yao kuhukumu kwamba wao wawili waendelee na kifungo chao cha maisha jela wakati watotot wawili wa babu seya wakiachiwa huru leo mahakama ya rufani dar
Nguza na mwanae Papii Kocha wakirejeshwa lupango kutumikia kifungo cha maisha
baada ya kuachiwa huru mwanae Babu seya aliangua kilio


wakili aliekuwa akiwatetea Mh. Mabere Marando akiwapongeza walioachiliwa huru


Babu Seya na wanawe wakisikiliza rufaa yao


Papii Kocha Mtoto wa Mfalme akimtuliza mdodgo wake alieachiliwa huru






Walioachiwa huru ni mshitakiwa wa tatu Nguza Mashine na mshitakiwa wa nne Francis Mbangu (Chichi).Warufani hao walikuwa wakitetewa na mawakili wa kujitegema Mabere Marando na Hamidu Mbwezeleni. Serikali ilikuwa ikiwalishwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Kassim Robert.

Hukumu hiyo iliyoandaliwa na Jaji Natalia Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk , ilisomwa kwa niaba yao leo asubuhi na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani kuanzia saa 3:02- hadi saa 4:08 asubuhi huku ukumbi wa mahakama hiyo na nje ya viwanja vya mahakama hiyo ikiwa imefurika umati wa watu waliojitokeza kufuatilia hukumu ya rufaa hiyo ambayo ilikuwa ikivuta hisia za watu wengi.Miongoni mwa walioudhuria ni wanamuziki bendi za muziki wa dansi ambao ni Rais wa Kongo.

Akisoma hukumu hiyo Chusi alisema kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyotumika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Mahakama Kuu, kuwatia hatiani washitakiwa hao ,ilikuwa ikionyesha warufani walikuwa wakikabiliwa na makosa 23. .










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 87 mpaka sasa

  1. hii issue bado haikukaa sawa. mimi nakubaliana na theory inayozungumzwa mitaani, jamaa amemuudhi mkubwa serikalini.

    kweli kuna watu wanaoweza kufanya makosa waliyoshutumiwa, lakini mtu kufanya makosa ya aina hii pamoja na wanawe hii haiingii akilini, tena sio mmoja bali watoto watatu? no way! haiwezekani kabisa!!!

    ReplyDelete
  2. WATANZANIA HATUNA USHIRIKIANO WENZETU KENYA, WAPO RADHI KUFA KWA AJILI YA KUTETEA HAKI YA WENZAO KWA NINI TUNAFANYIANA HIVI????????????? NASEMA WATANZANIA TUSIPIGE KURA, MPAKA HAWA WATU WATOKE RAISI WETU YUOP NA ANGALIA VITU KAMA HIVI KWELI NANI KIONGOZI??? TUTAFIKA KWELI??? HAKIMU WA WAPI HUYU??? SHULE YA WAPI HIYO KWA KUTOA HUKUMU YA NAMNA HIYO???? JAMANI TUFUNGUE MACHO??? LEO HII TUPO HAPA KESHO TUTAKUA WAPI? TUNAWAFUNDISHA NINI VIJANA WA TAIFA LA KESHO MICHUZI UTUSAIDIE..HAKI IKOWAPI HAPO?

    ReplyDelete
  3. so sad kwa kweli kama kuna tatizo kwenye mlolongo mzima wa kessy tafadhali waupitie tena na tena,

    sasa hao wawili walioachiwa je watalipwa fidia kwa kufungwa kimakosa?

    kifungo walichopewa kinatosha tafadhali fikirieni kupitia upya baadhi ya vipengele vya kesi hii

    ReplyDelete
  4. hii kesi anajua mungu na washitakiwa, ni kwanini hao wawili waachiwe na hao wengine waendelee kusota wkt makosa yao walikuwa wakishirikiana kuwatenda watoto wkt mmoja?
    malipo hapa hapa duniani,sipo upande wowote
    kwa kweli wamenisikitisha sana afya zao na zaidi yule dogo..

    ReplyDelete
  5. inasukitisha sana machozi yamenitoka! waachieni watu hawa jamani wameteseka sana tayari kwa kesi isiyoeleweka! wahalifu wa kweli hamuwafungi< mnawaonea hawa, au sijui kwa sabab si watanzania? jamani majaji hebu muwe na roho jamani!

    ReplyDelete
  6. Kwa vigezo vya hekima ya mfalme suleiman, kijana anayelia ni kweli hakutenda kosa. Mahakama asante kwa kulitambua hilo. Wengi tulisema kuwa haiwezekani familia moja wote wakafanya tukio hilo isipokuwa kama ni vichaa.

    Lakini huyu sijui Nguza mimi huwa nina doubt kama eti alisingiziwa.

    Hata pause zake mahakamani huwa mimi naona tu kuwa watu wanakuwa na huruma eti kwa sababu ya kipaji cha muziki.

    Hakuna kitu hapo, mtu akibaka mtoto wako utatamani usimwone maishani.

    ReplyDelete
  7. BINADAMU HATA SIKU MOJA HAWEZI KUTOA HUKUMU YA HAKI KWA BINADAMU MWENZAKE NI MUNGU PEKEE NDIYE MTENDA HAKI najisikia uchungu sana kwa hukumu hii na jinsi nilivyokuwa naifuatilia rufaa yao

    ReplyDelete
  8. hapo bado ni kitendawili tu hatujia serikali na babu seya nani mkweli tunamuachia Mungu atatoa hukumu ya haki ile siku ya PARAPPPPPPANDA itakapolia

    ReplyDelete
  9. ni kweli naungana na mtoa maoni hapo juu kuna watu walikuwa innocent katika hiyo kesi haotie

    ReplyDelete
  10. haya serikali iwalipe hao FIDIA iliowafunga kwa makosa ndio maana watu wa haki za binadamu wanataka serikali ya zote dunia kufuta hukumu ya KIFO kwani kwa nchi kama IRAN HAWA JAMAA WOTE TAYARI WANGEKUWA WAMENYONGWA WAKATI ULE ULE KUMBE WENGINE NI WATU SAFI HAWANA HATA KOSA WALA HAWAKUBAKA HAYA NDIO MATATIZO NA MAPUNGUFU YA HUKUMU ZA WANADAMU

    ReplyDelete
  11. ANGALIZO: anony wa 07:10:00 PM huyo mtoto sio kwamba analia kwa furaha na kuona katendewa haki sio hivyo, ni kwamba huyo mtoto aliangua kilio baada ya hukumu kuwa BABA na KAKA yake wanafungwa maisha. na ilibidi ifanyike jitihada kumnyamazisha. mimi jnilikuwepo mahakani. Michuzi samahani lakini hapa unawapotosha watu. huyo mtoto hakulia kwa sababu ya kuachiwa yeye bali ni kwa sababu ya mzazi wake na kaka kupokea kifungo cha maisha gerezani. ilibidi hata baba na kaka waliohukumiwa kifungo cha maisha kuanza kumbembeleza.
    hii kesi haiko sawa, inajulikana wazi, lakini huyu bwana anayefanya hivi dhambi yake haitofautiani na dhambi ya mauaji. kweli kabisa inatia uchungu sana. it's all about revenge basi lakini kosa hilo hawa viumbe hawakulifanya!!!

    ReplyDelete
  12. WATANZANIA WENZANGU TULIOKUWA NJE NA NDANI SASA TUKATE RUFANI YA KIMATAIFA SASA NA NAOMBA KILA MTANZANIA MWENYE MAPENZI MEMA ATOE PESA KWA AJILI YA KUKATA HII RUFANI.SASA IMEFIKA MWISHO WA KUIHAMINI MAJAJI ,MAWAKILI NA VIONGOZI WA SERIKALI WOTE NI HAO HAO..NA NASEMA ITALIPWA TU HII ISSUE ,KAMA KAMUZU BANDA NAYE ALIWEKWA NDANI SASA HAO WOTE WALIOUSIKA TUTAONA LEO WEWE KIONGOZI KESHO SISI.WATANZANIA WOTE TULIKUWA WASHINGTONI DC.TUKUTANE NA KUPANGA MIKAKATI SASA IMEKUWA TU MUCH .NAOMBA TUKUTANE TUJUE TUFANYE NINI ,HAO WATU WACHACHE WANALETA NA WANAHARIBU UTLIVU WA NCHI YETU KWA VIJISENTI VYAO.
    MDAU WASHINGTON DC
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.MWISHO UMEFIKA ,TUMEVUMILIA SANA

    ReplyDelete
  13. SALA ZETU BADO ZINAENDELEA.NA MUNGU ATAWATOA TU WAJA WAKE.AKINA SILA WALITOKA KWA UWEZO WA MUNGU SEBUSE HAO.KWA NINI MNAWATESA HAO WATU JAMANI.LAKINI MALIPO LAZIMA YATAKUJA HATA KWA WAJUKUU ZAO HII NI LAZIMA.
    MDAU WASHINGTON
    DC

    ReplyDelete
  14. Nawapa pole kwa waliorudisha kifungoni na pia kwa wale walioachiwa kwa sbabu wanajua uchungu wa kuishi gerezani "kifungo cha maisha sio mchezo" God bless them ikiwa kweli hawakufanya makosa na MUNGU AWAHUKUMU wote waliosababisha hao kuwa huko hapa hapa zDUNIA na siku ya Mwisho ni kuwapiga moto tu na km wamefanya makosa basi kuna hukumu maalum ya kufanya ngono kwenye vitabu vya dini na sio kifungo cha maisha.
    Mnaosoma sheria angalieni vizuri kuna Mungu sio mnajitia ubabe... HAPA TUNAPITA TU, KAZI KWAKO UNAEJIITA JAJI BORA..........
    Osmania university
    India

    ReplyDelete
  15. Blinde side...hii movie imenifanya nisichukue upande katika kesi hii maana inawezekana tukawa fooled kwa kuwa hawa jamaa ni maarufu, wangapi wamejiuliza kilichowafanya wale watoto wawataje hawa wadau hawa mmh? Yaani kama kweli yupo kiongozi aliyewabambikia kesi basi nasema huyo ni mfuasi wa kweli wa shetani tena hukaa mkono wa kuume wa Shetani Mkuu na inshallah makazi yake yameshaandaliwa Jehannam.

    ReplyDelete
  16. To be honest, Tanzania sio nchi ya kuishi. watu wanaishi tu kwa kuwa hakuna pa kwenda. imagine, vijana hao wamesota jela miaka 6 bila kosa, serikali ilikuwa wapi. Mimi bongo sirudi, hapa Norway najua siwezi kufungwa kipuuzi puuzi kama bongo. Wabongo jela imekuwa kama kifo, huwezi tabiri lini unakufa so na jela mtu yeyote anaweza ingia hata bila hatia. Je wangapi wako jela kwa kukosa hela za kuwalipa mahakimu ili wawasaidie? umaskini huu jamani.

    ReplyDelete
  17. Wengi wetu hatujui kama kweli hawa watu walitenda hiki au walionewa kisa jamaa ana ugonvi na mtu serikalini. Roho imeniuma sana na kama wamebambikiwa Mungu wape nguvu na ufanye maajabu kwenye hii kesi (Yes hakuna linaloshindikana kwako).Na system yetu ya Tanzania SHAME ON YOU! Na kama wametenda basi ndiyo hivyo they have to face it.

    ReplyDelete
  18. Nimewachukia huyo Mihayo na Lyamuyu. Kama ni kweli hao watuhumiwa walikosea, handling ya kesi ni mbaya sana. The case took more than five years and now they are no guilty, hii kitu inahappen sana na nchi nyingi sana. Ndio maana siwapendi watu wahseria hasa malawyer na hakimu. Lakini mtalipa nyie, ni watu wangapi mpaka sasa hivi wmefungwa kwa kosa lisilo lao. kwanini uharibu maisha ya binadamu mwenzio kwasababu ya chuki na tamaa ya pesa.
    ok tangia wewe Mihayo na Lyamuya mmeshapata faida gani na maisha yenu? Mnaweza kuwa na hela lakini mna raha ya maisha. Huku marekani huwa wanawalipa watu kama , hao mdai haki zenu wawafidie haki zenu za tangia kukosa shule na maisha ya kila siku. Waende shule bure na kazi wapate haraka sana.

    ReplyDelete
  19. HUKUMU ILIYOTOA UTATA MKUBWA KAMA HII, KUWAJUMUISHA BABA NA WANAWE WATATU KWA UFEDHULI LILIKUWA SI JAMBO LINALOELEWEKA. JUSTICE, INGAWA HATUJUI HATA HAKIMU ALIYETOA HUKUMU ALIKUWA FAIR LAKINI HAKI INAPOTENDEKA KAMA HII HATA YEYE HAULIZWI ILIKUWAJE! THINK 7 YEARS IN JAIL FOR NOTHINING= WHO SHOULD PAY THEM= WHERE THEY IN WRONG PLACE AT WRONG MOMENT(HOME-WHERE ELSE SHOULD THEY BE?)

    ReplyDelete
  20. inasikitisha kwa kweli hata mimi hainiingii akilini jamani ila mimi ni mzazi lakini kwa hili kwa hili jambo nakataa kuna something hapo si bure wajameni ila mungu ni mkubwa siku zote hizo jamani wameshapoteza malengo ilikuwa wafike mbali hao wanaosoma mungu kaitika kilio chao na wakizidi kulia kwa muumba ataitika pia na baba yao atatoka tuuu!!!bongo kwa kubambikiwa kesi ndo zao hao jerry mulo alitaka kubambikiwa kesi mungu amewaumbua nabadooooo!!loh kweli bongo mdebwedo serikali ya bongo yani wanaona kama wao ni mungu wakati pia wameumbwa kama sisi tu hawajui ona sasa siku zinavozidi kwenda mabalaaaa tu wanalaana si bure na wakiendelea hivi kutatoweka amani hapo vita mojakwamoja maana tanzania nchi ya amani watu tutashindwa jamaniiii lol ndo maana hatutaki kurudi tukirudi itaja kuwa balaa maana maisha yalivyo magumu na serikali inaneemeka hatutapendelea kuona hivo mwisho tutajakuwa majambazi bure mmmmmh!!!!!

    ReplyDelete
  21. Ingekuwa wamemkosea Kiongozi Mkristo angeweza kuwasamehe. Sasa sijui huyo waliyemkosea ana dini gani. Nasikia kwenye dini za wenzetu msamaha siyo nguzo muhimu.

    ReplyDelete
  22. Huyo Hakimu vipi! wameshakaa jela sijui rumande kwa muda wa miaka mingapi! miaka kibao yapata hata sita! alafu leo, ndio anatoa hukumu ya kivungo cha maisha, kwa kosa la aina gani! hayo makosa, yalijificha yasio na ukweli juu yake! hii ni ukosevu wa khaki za binadamu! kwa miaka aliyokaa, ilitakiwa wawe wamesha ukumiwa na wameshatoka.sio kivungo cha maisha! hata makosa ya jinai! bado watu wanafungwa na kuachiwa huru;

    ReplyDelete
  23. Acheni umbumbumbu Watanzania. Hawa watu walitenda makosa hayo na ushahidi ulikuwa wazi pweeeee! Muulizeni Mtikila ambaye aliwatetea hadi aliooneshwa ushahidi, akasema ni heri wangenyongwa kabisa. Hawa hawakuachiwa kwa sababu ni watu safi; bali wameachiwa kwa sababu za kiufundi (kisheria), siyo kwa sababu hawakutenda kosa. Wote walishirikiana kwa imani zao za kishirikina ili kukuza muziki wao. Kwa ambao hamna taarifa, wale watoto wamaathirika na mengi, mengine wala jamii haijaambiwa. Wazazi wa watoto wale wamepoteza kila kitu ambacho mzazi hutarajia kwa mtoto wake. Kwa maoni yangu, tunapaswa kukata rufaa kwa nini hawa wameachiwa? Hii dhana ya ugomvi na mkulu fulani ni mambo ya kitaani. Kumbukeni, ushahidi ulitolewa.

    Asante Michuzi.

    ReplyDelete
  24. Mnalalamika kuwa tanzania tunakwenda wapi au tanzania tambarare, jibu ni hilo hapo mtu analeta comments ya udini hapa! hebu fikirieni sana ty, mnadhali kwa hali hii tanzania tutaendelea kweli?

    Na kwa kwa kukujibu wewe anon wa Thu Feb 11, 09:37:00 PM grow up, we don't need people like you here!!!!

    ReplyDelete
  25. Kwa kweli inasikitisha sana.Its not fair kwa swala hili.Jamani naomba kama kuna uwezekano wa kuwasidia hii familia tuungane tusaidie watendewe haki.Pia je brother Michuzi kuna uwezekano wa kuanzisha Fond iliichangishwe pesa kwa ajili ya kusaidia hawa vijana waliotoka wajiweze kimaisha na kingine kisaidia kuendelea kufuatilia haki kwa hawa baba na mwana na wengineo ambao hupata maafa ya kusingiziwa yaani kutoyendewa haki.Mimi nitachangia kama usimamizi mzuri utakuwepo.Na ningependa wengine wajitolee pia.Kwani ni lazima tukomeshe vitendo hivi vya kuonewa wanyonge.

    ReplyDelete
  26. Acha udini wewe!! kama huna ya kuongea kaa kimya!! dini zipi hazizungumzii juu ya msamaha??? hao majaji waliowahukumu sio wakristo!!Acha ujinga kabisa!! toa hoja na kama huna hoja usizungumzie udini hapa!!! una hamu yakukute ya nigeria sio!!??? usirudie tena!! omba msamaha kwa hili ulilolianika na hoja isiyo kuwa nakichwa!!!

    Mdau busara itawale mdahalo huu!!!

    Ningeongea mengi kuhusu Nguza ila huyo mshikaji hapo juu kanichefua!!!

    ReplyDelete
  27. JAMANI WATOWENI HAO WATU HAWANANA MAKOSA YOYOTE.NIMELIA SANAAAAAAAA
    MBONA SONGO SONGO NA MBOZE PAMOJA SENTANO PAKA WAMEHUA WAKO NJE YOTE HAYO FAR....KISA MKUBWA WA TANZANIA
    NCHI HII KIBOKO YAOOOOOOOOOOOO
    WATOWENI HAWANA KOSAAAAAA

    ReplyDelete
  28. Cha ajabu ni kwamba, wanaotakiwa haswa kufungwa na funguo kutupwa nje, wako huru na wanazidi kunawili na kula kuku kwa mrija.
    Stori kibao kutetewa na na mambo kufunikwa funkikwa na wenyewe.

    Akina yahe siye, tutajiju, tuki kosea kidogo tuko kizimbani, hapo ndio tunaona nguvu zote za sheria.
    Tutafika jamani??? Haki ya wananchi ya akina yahe sie tulie tu. Nchi ya wenyewe hii jamani.

    ReplyDelete
  29. "Wacheni umbumbumbu Watanzania" si lugha safi kabisa ili mtu aelewe basi tumia llugha nzuri sio matusi kuna watu wamechangia hapa wana akili timamu na elimu bora zaid yako na wengine tupo tusojua kitu lkn tunajaribu kutumia lugha safi ili kieleweke, na km wameachiwa kwa sababu nyingeni huo ni uzembe na mm naona uwongo huwezi kuachiwa ukiwa huna kosa ilhali watu hawana makosa na wanafungwa seuze hao.
    Yule mdau aliezungumzia masuala ya dini mbona anachafua hapa hakuna dini isiozungumzia MSAMAHA na hata hao majaji walikua ktk dini anayosema Msamaha ni nguzo kuu, sasa sijui anakosoa dini yke ama?
    Osmania university
    India

    ReplyDelete
  30. Zombe vipi?, vipi kuhusu Andrew Chenge?,vipi kuhusu Karamagi? vipi kuhusu Richmond na Lowassa?,vipi jamani vipi?? au ndo sheria ipo kwa ajili ya mawakili na mahakimu bali haki ipo kwa wenye fedha ushawishi mkubwa kwenye nchi hii?Maana hata kidume cha jiji mzee wa BOT anaweza kuchomoka kwenye kesi yake kwani dalili zaonesha wazi.
    Vipi stakabadhi ghalani huko kwa ndugu zetu Mtwara na Lindi mbona wakulima wanaibiwa na kudhurumiwa jasho lao na utaratibu wa mheshimiwa rais wa kuwaletea middle man arahisishe wizi wa fedha za korosho yao na hamna wa kuwatetea?
    Kwa kua blog si yangu publish ya hii comment inategemea itikadi ya blog owner!

    ReplyDelete
  31. Jamani nimelia sana utafikiri ndugu zangu wa damu,hata mm sikubaliani na hii hukumu,there is something behind the scene,basi tuu baba wa watu,i wish ningekuwa na uwezo, anyway kama hawajafanya kweli Mungu yupo na always his eyes are open!

    ReplyDelete
  32. It is very sad to think that even the investigation itself is incompetent,the case was decided on
    he said this and she said this! No DNA? Why those kids were not allowed to cross-examined?
    The whole evidence is based on third party witness, who was not present at the scene.
    Truly no parent would want/allow their child to be sexualy abused, but this one sounds a bit weird. It is possible
    people would do such a heinous crime for vodoo, but someone has to have more evidence than what has been tabled in this case.

    ReplyDelete
  33. nyinyi mnaowatetea hawa, ngojeni siku mtoto wako wa miaka minane akifanywa sambusa ya nyama kwa kupenyezwa nanihii ya saizi ya baba yake; ndiyo mtaelewa machungu yake.

    Haingi akili kwa mtu na wanawe kufanya kosa hili eeh? Kama kuna watu wenye uwezo wa kuwananihii watoto wao wa kuwazaa wenyewe, basi wapo watu wenye uwezo wa kufanya kosa hili.
    commit a crime, do the time

    ReplyDelete
  34. Mimi ndiye niliyetoa mawazo yaliyowaudhi baadhi. Nilikuwa nimesoma maoni hapo juu Anonymous wa 11 feb. 09:12:00 PM kuwa kuna uvumi kuwa walimkosea kiongozi fulani wa serikali na akashinikiza wafungwe. Hata huku mitaani watu wengi wanasema alikuwa na ugomvi na mkubwa fulani serikalini. Ndiyo nikasema kama aliyekosewa ni mkristo, tunaaswa na biblia kuwasamehe waliotukosea. Na kama ni wa dini zingine, mimi sijui zinasemaje kuhusu kusamehe waliotukosea. Mtu mmoja aliniambia dini fulani inafundisha jino kwa jino.

    Samahani kama nimekukwaza wewe uliyelalamika.

    ReplyDelete
  35. kwa kuangalia hizi picha tu unaweza ona uzuri wa huyu mzee kwa kweli. Wasipo mwachua soon anaweza jinyonga uko jela!! mimi ndo maana sikuzote naamini nibora kujamia kwenye nchi za wenzetu wazungu kuliko bongo.bongo akuna haki kabisa .aki kwa wenye pesa tu masiki ana lake!! awa jamaa kutoka adi mzee atapo toka madarakani maybe yani maybe.

    ReplyDelete
  36. UZUSHI MTUPU,HAYA WAFUNGUE KESI YA KUSOTESHWA RUMANDE BILA HATIA,HII TANZANIA NA HUYO KIONGOZI ALOKULA NAE SAHANI MOJA WOTE WALAANIWE NA MUNGU KUONEA WATU TU.
    Kuna watu wameshuka na bastola hadi gari nyengine na kuua dereva,tunaambiwa bila kukusudia,ni kosa kumuonesha mtubastola hata kama haina kitu lakini mungu amemuhukumu na yeye Tanzania ndio maana umaskini hautuondoki kwa mambo haya ya ufisadi na dhulma

    ReplyDelete
  37. Baada ya kusoma maoni ya wengi hapo juu nimegundua asilimia kubwa ya watoa maoni hawajui sheria na wameegemea katika mambo ya kusikia na kuwaonea huruma kwa kuwa ni wanamuziki maarufu. Nawaomba waende Mahakamani wakasome mwenenndo wa kesi ulivyokuwa ndio watajua undani wa mambo yenyewe. Hawa jamaa wanne wote waliwabaka watoto wale wadogo. Hao watoto wadogo wote 10 waliobakwa waliwahi kutoa maelezo bila woga wala hawakufundishwa walieleza jinsi walivyobakwa mmoja mmoja kwa nyakati tofauti, TBC TV waliwahi kuonesha mahojiano hayo mwaka 2003 kabla kesi haijapelekwa mahakamani. Washtakiwa walipewa nafasi ya kuita mashahidi wao, halikadhalika upande wa mashtaka ulitoa ushahidi wake pamoja na vipimo vya daktari. Mahakama za ngazi zote tatu ziliaangalia ushahidi wa pande zote mbili na kuridhika kuwa washtakiwa wana hatia. Hapa hakuna kuonewa bali ni ushahidi tu ndio iliowatia hatiani. Hata Mtikila bingwa wa kufuatilia kesi alikuwa na mtazamo wa kwamba hawa wameonewa lakini alipopata ukweli akadiriki kusema wanastahiri kunyongwa kabisa.Hawa watoto wawili wa Nguza washukuru kuwa wameachiwa. Ni ushirikina ndio uliomfanya babu Seya kuwaongoza watoto wake ktk kuwanajisi watoto. Wamlaumu mganga aliyewahadaa. Ni sawa na wauaji wa Albino wanavyohadaiwa na waganga

    ReplyDelete
  38. Baada ya kusoma maoni ya wengi hapo juu nimegundua asilimia kubwa ya watoa maoni hawajui sheria na wameegemea katika mambo ya kusikia na kuwaonea huruma kwa kuwa ni wanamuziki maarufu. Nawaomba waende Mahakamani wakasome mwenenndo wa kesi ulivyokuwa ndio watajua undani wa mambo yenyewe. Hawa jamaa wanne wote waliwabaka watoto wale wadogo. Hao watoto wadogo wote 10 waliobakwa waliwahi kutoa maelezo bila woga wala hawakufundishwa walieleza jinsi walivyobakwa mmoja mmoja kwa nyakati tofauti, TBC TV waliwahi kuonesha mahojiano hayo mwaka 2003 kabla kesi haijapelekwa mahakamani. Washtakiwa walipewa nafasi ya kuita mashahidi wao, halikadhalika upande wa mashtaka ulitoa ushahidi wake pamoja na vipimo vya daktari. Mahakama za ngazi zote tatu ziliaangalia ushahidi wa pande zote mbili na kuridhika kuwa washtakiwa wana hatia. Hapa hakuna kuonewa bali ni ushahidi tu ndio iliowatia hatiani. Hata Mtikila bingwa wa kufuatilia kesi alikuwa na mtazamo wa kwamba hawa wameonewa lakini alipopata ukweli akadiriki kusema wanastahiri kunyongwa kabisa.Hawa watoto wawili wa Nguza washukuru kuwa wameachiwa. Ni ushirikina ndio uliomfanya babu Seya kuwaongoza watoto wake ktk kuwanajisi watoto. Wamlaumu mganga aliyewahadaa. Ni sawa na wauaji wa Albino wanavyohadaiwa na waganga

    ReplyDelete
  39. KAKA MICHUZI, KESI ZA NYUMBA NDOGO HUWEZI KUTEKETEZA MAISHA YA MTU. ILA KESI KAMA YA ZOMBE ALIHITAJIKA KUNYONGWA KWAKUA ALIKUA KTK SYSTEM YUKO KITAA, HAKUNA MUHIMU WA MAHAKAMA HAPO BONGO, WAPI HUMAN RIGHT???????
    WE JOSEPH KABILA TETEA WATU WAKO,

    ReplyDelete
  40. Hivi nyie mnaosema kuwa waachiliwe mlikuwa nao wakati hao watoto wakifanyiwa hivyo vitendo vya kinyama? I am not going to side with and site. It is well know that the prosecution must prove beyond reasonable doubt that they committed the offences. Once they have done that it is upon the judge make his decision basing on the evidence provided and also follow the law.

    Of cource judges are human beings, they make mistakes. Thats why there is a right to appeal.

    Some people here are saying that the governmnet iingilie hili swala. Well, we have been crying for the independent of judiciary for so long time now you want to take that away?

    Someone even say this decsion is a prove of why s/he lawyers. Well, we all know that you are faced with a legal problem you will be running all they to a lawyer for help. Respect other professioanals and they will respect yours.

    The court of appeal may have reached a right or wrong decision. But before making your own judgment, have you read the court's judgment itself? Waandishi wa habari wanaripoti kesi tuu, they dont go into details on the law and basis of the decisions.

    Another thing, we need kutofautisha between law and morality. Some people seem to argue basing on morality. Until we read the full judgment of the court of appeal, we will not know why the court reached that decision.

    May be Michuzi Blog could help us to get the full judgment of the court and post it here so that people can make an informed argument instead ya kupayukapayuka ovyo.

    ReplyDelete
  41. BADO WANAWEZA KUKATA RUFAA HAIKATALIWI NA HAO WATOTO WAFUNGUWE KESI YA MADAI KUDAI FIDIA YA KUFNGWA MIAKA YOTE HIYO TENA WAFANYE HARAKA SANA TENA SANA

    ReplyDelete
  42. kina babu seya wangekuwa katika nchi za kiarabu wangenyongwa wote washukuru Tanzania haina dini huko kwa waarabu ni sharia tu nyonga kabisa watu kama hawa

    ReplyDelete
  43. Ila wandugu wajameni...hii kitu imeniuma sana mwenzenu.nimelia sana.tena sana.nimejisika uchungu sana.naumia sana.anyway JK namuamini sana na naaamini ana mtazamo mkubwa na anajua nini cha kufanya kama amiri jeshi mkuuu. I believe JK is able to save any man in jail.naaamini atamsaidia si babu seya tu..na vijana wengine wenye matatizo kama.jamani tuwaombeee,,,,si hawa tu na wengineo.ikiwa mandela aliwasamehe wangapi?

    ReplyDelete
  44. Raisi Jakaya Kikwete, naomba msamaha kwa ajilli ya watu wote ambao wanajutia makosa yao.waasamehe tafadhali.hata kama wameua!!!waaache jela kwa miaka kadhaaa alafu wasamehe ikiwa wameomba msamaha.nakuomba sana.JK nimelia sana.saidia hawa watu.simaanishi babu seya na ufiraji wake.namaanisha samehe wafungwa..inapobidi.

    ReplyDelete
  45. pedejeee fulani kazi kwako mwenye mali karudi uraiani te te te

    ReplyDelete
  46. Jamani inasikitisha, yaani inauma sana, hii kesi imetugusa wengi, watu tumeomba na kuomba haki itendeke, tunamshukuru Mungu kwa angalau ya majibu ya maombi yetu kwa hao wawili kuachiwa huru, naamini Mwenyezi Mungu atatenda muujiza tu kwa waliobakia (kama kweli hawakutenda) hakuna lisilowezekana kwa Mungu, yote yanawezekana! Sasa inakuaje kwa hao vijana wawili waliotoka? Wataishi vipi? Tunataka kujua serikali itafanya nini kwa hawa vijana waliotoka katika kujikimu kimaisha, serikali mtawalipa fidia gani? manake fyucha yao ndo ishaharibika. Anko Michuzi tunaomba ufanyike utaratibu wa kuweza kuwachangia chochote hao vijana waliotoka kama pole kwa yaliyowakuta. Ikiwezekana tupate hata namba zao za simu, tuweze kuwachangia. Angalia afya zao kwa kweli inasikitisha, wanaanza moja kimaisha, pliz anko Michuzi do something ili tuweze kuwachangia.

    ReplyDelete
  47. Siku ya mwisho yote yatakuwa wazi... mkweli na muongo. Hapa duniani tunapita tu. (Kuna watu wanafungwa bila makosa na kuna wengine huwa hawafungwi na wanamakosa). Si wote wanaotembea ni innocent na si wote waliofungwa wametenda makosa walioshitakiwa. Si vema kusema vitu vya kufikirika tu utadhani mtu ana huo ushahidi au aliona, au alijua lengo la hao watu kubaka ni ushirikina n.k. Kama kuna mtu anafahamu tukio hilo kiuhakika kwa nini hadithi nyingi?

    ReplyDelete
  48. MICHUZI COMMENT ZA UDINI MAHALI PASIPOHUSIKA USIZIWEKE, HATA HIVYO KILA MARA WAISILAMU WANAWALAUMU WAKIRISITU NAWE PIA UNAHUSIKA? KAMA HUHUSIKI BASI USIWE UNAZIWEKA. SIJUI HAO WANA USHAHIDI KUWA BABU SEYA NA WANAE NI WAISILAMU.

    ReplyDelete
  49. Anon wa tatu, hapo juu kweli ameguswa mpaka ameshindwa kuandika neno kesi (case) na kuandika kassy sasa sijui alikuwa anamaanisha shitaka au kessy wa pale marangu mtoni!!! kazi ipo...

    ReplyDelete
  50. HAKUNA ANAYEJUA UKWELI ZAIDI YA

    MUNGU NA KINA NGUZA. NA MUNGU

    MWENYEWE NDIO ATAKAYE WATETEA.

    WAKATI UKIFIKA,HAKI ITATENDEKA,

    WAVUTE SUBIRA NA KUMUOMBA MUNGU

    TU. HAKI ITENDEKE.

    ReplyDelete
  51. huyo aliyeleta udini huwendan hata si mkristo na ni mmoja ya wahusika wa upande wa pili,kuweni macho na hawa watu wengine lengo lao ni kupindisha mada ili wachangiaji waache kujadili mada iliyopo nakuanza kujadili yasiyohusiana na mada
    msiwajibu chochote na hata hapa naona kuna watu tayari wameshatoka nje ya mada

    ReplyDelete
  52. kama case hii niyakupikwa wote wahusika walaniwe kwa jina la Yesu

    ReplyDelete
  53. nimelia machozi awa vijana jamani,siamini siamini siamini,,,heee kweli izi sheria ovyo kabisa!!!

    sasa ukikata rufaa ivi afu ukaonekana ULIONEWA/KUFUNGWA KIMAKOSA yaweje tena?

    ReplyDelete
  54. Tunatenda dhambi ya kuhisi kuonewa kwa hawa jamaa ila kubwa tumwachie mungu amuhukumu kila mmoja kwa haki.

    May be walifanya acheni ushabiki
    Na wako wazazi na watoto walilia kwa waliyofanyiwa watoto wao.

    Na kama wamesingiziwa ungu awalipize waliosingizia

    Wewe namimi ni mambumbu hatujui kitu

    Usihukumu kwakuwa akili yako haiwezi kuona kila jambo kama yalivyo macho ya mungu

    Tumwachie mungu
    Tusihukumu wala kuita wameonewa
    Tusimhisi kigogo yeyote kwakuwa kuhisi ni dhambi
    Tusali kuomba mungu awatendee haki kama wamesingiziwa

    Na kama wamefanya pia mungu awajalie msamaha na awapunguzie maumivu

    ReplyDelete
  55. wewe anon wa Thu Feb 11, 09:37:00 PM Acha udini hapa stick kwenye point.

    MDAU. ABDALAH YAHYA

    ReplyDelete
  56. Nyie wanawake mnaowatetea malawiti wa watoto kumbukeni mnapalilia kitu ambacho ipo siku kitawarudia watoto wenu kiaina. Tunaokaa uswahilini tunajua kuwa hata sasa kuna wazazi wanakaa vijiweni na watoto wao wakipokezana bangi, je hili la kushauriana kutembea na vitoto vidodo ili kupalilia nyota haliwezekani? Acheni ujinga, kama wamefanya makosa halali yao ndo hiyo. Michuzi tumwagie hiyo hukumu hapa mtandaoni...najua hawatasoma bali wataendelea kusikiliza maneno ambayo wanapenda kuyasikia.

    ReplyDelete
  57. JK hawa watu wameshakoma na adhabu waliyopata imetosha. Uchaguzi unakuja na njia pekee ni kuwafurahisha watu katika kipindi hiki. Nina imani kwamba kama muumini unajua kusamehe. basi msamehe kwa alilolitenda maana inajulikana sababu ya wao kusota ndani. Hawatarudia tena kwa shuruba walizozipata huko lupango.

    ReplyDelete
  58. we michuzi bwana sio ishu....mambo yakurusha hadharani ishu zaudini haujengi unabomoa we unapenda kuona watu wanatoka nje yamada...unachekelea sjui kwanini.hujui kama inaboa au?chokochoko utakuja kuskia siku varangati kisa kimeanzia kwenye blog yamichuzi mdau alikomment kidini....ohoooo mi nakumaindi nanajua unaweza kunibania comment yangu...utajua mwenyewe kuiweka kapuni au kuirusha but unaniboa....NIKIRUDI KWENYE MADA KWAKWELI MI NIMELIA HADI BASI...HAKUNA USAWA NA NIMEONA KULIA NDIO NJIA YAKUONDOA KINYONGO CHANGU JUU YAUAMUZI HUU KWANI SINA LAKUFANYA.JAMANII IIIII IIIII IIIIII BADO NALIA MIMI

    ReplyDelete
  59. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  60. UKIONA M2 MZIMA MAMAAAAAA TILITITIIII ANALIA MBELE ZA WATU UJUE KUNAJAMBOOOO!!!!SI BURE HAKI HAIKUTENDEKA!!!

    ReplyDelete
  61. SIKU ZOTE UBAYA HURUDI KWAO, KWA ALIYE WAPIKIA KESI HII KINA BABU SEYA NAYE KAMA SI YEYE BASI WATOTO WAKE WAJIANDAE KUKUMBWA NA DHAHAMA KUBWA WASIOTEGEMEA, MUNGU NI MKUBWA BABU SEYA NA MWANAO ZIDINI KUMWOMBA MUNGU NA IPO SIKU MTATOKA KWANI YEYE HATAMWACHA MWENYE HAKI AANGAMIE MILELE.

    ReplyDelete
  62. JAMANI NISAIDIENI SHERIA IMEKAAJE KWA HAO WALOACHIWA,,,,,,,,,??????????huyu wakili wao asimame kidete haki itendeke kwa hao walio nje..but babusea jamani jita lol linatabasam kumbe kidonda alokuwanacho rohoni kimeshakuwa donda ndugu.......pole babu seya na mwanao naelewa jinsgani unaumia...

    ReplyDelete
  63. huyo anayejiita Bush Lawyer sijui, naomba nikuulize, Tanzania imeanza lini kufuata sheria katika hukumu? au ndio wameanza kwenye kesi ya nguza. nijuavyo mimi asilimia kubwa ya wafungwa hawana hatia, na yote ni kukosa kidogo dogo cha kuwapa polisi, au hakimu au hata kuweka wakili mzuri. sasa hapa unatuambia nini? unakua kama mgeni wa hii nchi. wewe mwenyewe kama ni lawyer kweli, nina hakika ushashinda kesi nyingi za uonevu. hiyo report inayosema wewe mimi pia nimeisoma, yote in ya kupikwa haina ukweli wowote. wale watoto walishindwa kuongea tena baada ya hii miaka kupita. mtoto wa miaka 11 akibakwa kikweli hawezi kusahau maisha yake yote, iweje hawa walisahau issue karibu yote baada ya miaka mitano tu? acha kudanganya watu hapa wakati wewe pia ni Mtanzania na unajua sana mahakama zinavyoishi kwa rushwa.

    ReplyDelete
  64. wether walilawiti au hawakulawiti ila wengine tuliomba Mungu aingilie kati hii kesi kwa vyovyote vile

    watoto waliolawitiwa nao its only God who can judge kwakweli

    im shocked!!!!!!

    ReplyDelete
  65. kwanza naanza kwa kuwapa pole familia ya babu sea kwa kilichojiri huko mahakamani

    Pili kwa mtazamo wangu na upeo wangu haki haikutendeka something is wrong somewhere, kiukweli kuna procedure irregularity. Hivi inakuingia akilini familia ya watu wanne wakatende hayo makosa at the same time pamoja na baba yao?

    Halafu baada ya hukumu washtakiwa wakaappeal mahakama kuu jaji akafutilia mbali appeal na ku-upheld decision ya kisutu, sasa hivi mahakama ya rufaa imewafutia mashtaka wawili na wengine kuendelea na hukumu, hivi wadau kimsingi jaji wa mahakama kuu hakuliona hili au ndo tuite ubabe?

    Hivi inaingia akilini mtu kafutiwa mashtaka kumi na, na kakutwa na matano tu? walikuwa wapi kufanya upelelezi wa kina toka mwanzo? na hawaoni wamewaharibia muelekeo wa maisha hao walioachiwa manake walikuwa wanasoma ati walivyowaweka behind bars siku zote hizo leo ndo wanakuja kuujua kweli! Kiukweli hata Mungu hapendi

    kwa kumalizia nasema hivi court system yetu ijirekebishe na naanza kuamini yanayosemwa mtaani kuwa kuna cha kigogo kimeliwa hiyo ni revenge.

    Too bad

    ReplyDelete
  66. Kwanini mnadhani hawawezi kutenda makosa hayo wakati kila siku mnasikia fulani kammuua baba au mama yake, kambaka mama, kikongwe n.k na hampingi? Mimi nadhani hata hao walioachiwa walitenda makosa na wanajua kila kitu ingawa wakati mwingine ilitokea wakawa hawapo na ndio salama yao. Hakuna kiongozi anaweza kuingilia mahakama katika ngazi zote hizo.

    ReplyDelete
  67. Ninakwambia hivi karibuni huyu mungu atawahadhibu hao waliowafanyia hii familia huo ukatili na wale wote waliotoa ushaidi wa uongo watapata adhabu kali kutoka kwa mungu ,hivi huu ni unyama gani kumfanyia binadamu mwenzako alafu eti unaenda kanisani au msikitini,mnafikiri hakuna mungu? haitapita miaka miwili mkono wa mungu utawaangukia,pole babu seya na mwanao mungu yuko na nyinyi.

    ReplyDelete
  68. Mimi nasemaje.......tufanye kweli 2010,uchaguzi wetu ndio mbaya,tunachagua viongozi wanokuja kupindisha haki za watu
    naamini kabisa babu seya na watoto wake hawajafanya ilo kosa bali ni ufisadi wa huyo member wa ikulu.........rafiki zake wanatuibia kodi zetu na mikataba feki lakini wako nje.....chenge ameua,yuko nje.......watanzania tuamke na macho tuyafungue,serikali hii siyoooooooooooo kabisaaaaaaaa. ufisadi upo kila mahali.........mahakamani,ikulu,wizarani na sasa mpaka kwa wananchi(kumbukeni askari wa ultimate aliyefukuzwa kazi kisa kasema mbovu kwa waziri) kwani kwenye atm ni sehemu ya kuongea na simu au kuchukua pesa??????tatizo wana maovu mengi kiasi ata madereva wao hawawaamini wanaamua kuongelea simu sehemu za kujificha.

    JK badilika na badili muundo wa selikali yako maana inakutia aibu


    ALL FOR NOW

    ReplyDelete
  69. Watanzania tuungane tugome tutafute international lawyers twende hadi mahakama ya united nation au the Hague Uholanzi.Huu ni ukatili kuzidi hata kuua,yaani hata walio nje watoe taarifa kwenye taasisi za haki za binadamu
    Hatujawahi kuona unyama kama huo.jamani tufanye kitu kuwanusurisha hao binadamu hawana hatia wanasingiziwa tuuuuuuuuu.inasikitisha machozi yananitoka,jamaa wa washington organize tupate, mtu kutoka nje afutilie haki za hawa watu, ni kilio haki za binadamu zinavunjwa hapa hapa nchini kwetu,yoyote anae mlipiza bado amjatosheka tu na mateso aliopata huyu bwana na wanae jamaniiiii doh

    ReplyDelete
  70. So sad. nini wamefanya?
    President have a look on this.
    Machozi ya watu hayadondoki BURE.

    Je wangekuwa na makosa kama waliowauwa wale wafanyabiashara pale Sinza ingekuwaje?

    Anyway, lenye mwanzo lazima liwe na mwisho.

    ReplyDelete
  71. mh sasa yupi ni papii kocha alovaa tsheti nyeupe au ya blue?

    maana maelezo ya picha #3 na #8 mh!

    aya vijana nendeni mkaoe sasa maana uo ukame mweee!!mkasome na mkale vizuri mrudishe afya

    MUOKOKE PIA

    ReplyDelete
  72. anony feb 11 10:40
    Acha ujinga ugomvi na mukulu upooo.
    Kama ushahidi ni picha mbona the utamu walionyesha picha za mukulu lakini ikasemekana zimepikwa iweje hawa picha zao museme ni za kweli?

    ReplyDelete
  73. Hii nchi kweli haki iko kwa aliye kwenye system, kwa sababu haiwezekani mwanzo wakutwe wana hatia na Mahakama hiyo hiyo inayojua sheria na leo wakutwe hawana hatia, sasa Serikali itawasaidiaje hao vijana kimaisha? Lakini MUNGU ANALIPIA HAPA HAPA DUNIANI kama kweli hawakutenda MUNGU ATAWALIPIA, na kama ni kesi ya kupikwa, huyo aliyepika ajifikirie kama ni yeye angeharibiwa future yeye na familia yake ingekuwaje?

    ReplyDelete
  74. Mimi sielewi kama tatizo ni waandishi wa habari au ni wahukumu wetu.
    Nimesoma tena leo gazeti la guardian wananukuu Hakimu akisema kuwa:
    "Mtoto alisema kabakwa na Dr alithibitisha".

    Na mlolongo huu ni kwa kila kosa sasa najiuliza ushahidi hapa uko wapi?! Tokea kuanza kwa kesi hii kila nikisoma sijawahi kuona wanasema ushahidi kuwa Nguza au Papii alimbaka mtoto X ni huu. Ikumbukwe haihitaji mtu awe mwanasheria ili uweze kuona ushahidi. Ndio maana wenzetu wanatumia watu wa baraza kuamua na sio wanasheria (Jury).

    Sasa waandishi wetu wanaowajibu wa kuhoji haya maswali na sio kushabikia mara nyingi habari tunazoandikiwa ni za kiushabiki tu hata siku moja sioni uandishi makini wenye kuuliza kulikoni.

    Kwa misingi hiyo waandishi wana kosa kubwa katika nchi yetu.

    Kama tunavyojua maisha yetu ya uswahilini inawezekana kabisa Nguza alifanya hayo ila kwa kesi hii ushahidi sijauona naona maneno tu ya daktari na ya mtoto. Kwa misingi hii ni rahisi sana mtu yeyote ukapigwa ndani maisha sababu tu ya ugomvi na mkubwa au mwenye hela zake...HATARI SANA!!
    Mzawa

    ReplyDelete
  75. We Michuzi una unazi sana comment za matusi unaziacha ila za kuisema serikali ya CCM unazitupa kapuni. Unataka ubunge wa kuteuliwa nini?
    We annoni wa Frid Feb 12 10:25:00 mbona umeiacha? Ile ya Udini hujaitoa mi kwa kuponda serikali ya CCM unatoa.Sasa unajua kuhusu viongozi wa serikali waliofoji vyeti? Sio ajabu hata utendaji wao kua mbovu sababu wapo waliofoji vyeti na kujitwika vyeti wasivyosomea.Futa na hii

    ReplyDelete
  76. Nimesoma maoni ya wengi ni hisia tu za kuwaonea huruma Babu Seya Na Watoto wake lakini hawana ushahidi kuwa Babu Seya na Watoto wake ni wasafi, hawakufanya unyama kwa watoto wetu.

    Mahakama zetu kweli zina matatizo ktk kesi za ufisadi wa pesa, lakini kwa hili la kuwahujumu watoto ni lazima tuwe waangalifu kuwalaumu kwa kulinda jamii yetu kutokana mashetani yanayotaka kuharibu watoto wetu kwa imani zao giza na ushirikina au "perversion" .
    Tusiwe washabiki tu wa kuhukumu, wala tusiwe wavivu wa kufuatilia ukweli toka pande zote bila ya kuwa na akili ambazo tayari zishasema fulani kaonewa kabla ya kujua undani wa jambo.

    Wengi watoa maoni walio nje ya nchi wanakumbukumbu nzuri za Nguza Viking akiwaburidisha miaka mingi akiwa na Marquiz Du Zaire Band. Hiyo isiwe sababu ya hisia za kumtetea kwa sababu ya "u-celebrity" wake. Kama ilivyoamuliwa na mahakama kuwa yeye na mtoto wake wanahatia basi tukubali na kama kuna asiyekubaliana na hukumu afuate mkondo wa sheria kukata rufaa. Lakini kusema tuu hawana hatia na mahakama zimekosea ni kuzihukumu mahakama kabla ya kuwa na ushahidi.

    Kuhusu kesi za kubaka, msifikirie ni kesi za mchezo kwa kuendelea kuwatetea waharibifu, kwani madhara yake kwa waathirika ni makubwa sana. Kama Msomi wowote wa jamii akaamua kufuatilia maisha ya watoto hao mpaka watakapokuwa wakubwa na kuandika mlolongo wa maisha yao na maamuzi watakayofanya ndipo mtajua hathari zake. Kwenye nchi zilizoendelea madhara ya watoto kuhujumiwa wakiwa wadogo yanaoneka katika wasichana kuwa malaya wa kutupwa, "porno actress" wahigizaji wa sinema za matusi, watumiaji wa madawa ya kulevya, na kujiona hawana thamani yoyote. Sasa utakubali binti zetu wawe hivyo.

    Vile vile mbakaji wa watoto au muuaji wa watoto hasa Marekani akienda jela mara nyingi anauliwa huko jela na wafungwa wengine. Sababu wafungwa katika kosa ambalo wanalolichukiwa na mtu aliofanya hana heshima kabisa ni mbakaji. Wao hawana tatizo na ujambazi mwingine wowote lakini sio kuhujumu watoto wasio na hatia, malaika.

    Mdau

    ReplyDelete
  77. Kifuatacho ITV: Jerry Muro.

    Babu seya Kaenda jumla, Jerry Muro jiandae.
    Too Sad

    ReplyDelete
  78. Naunga mkono hoja aliyotoa blogger anayayejiita Bush Lawyer hapo juu. Watu wengine tunatoa maoni kwa kuwaonea huruma bila ya kujua sheria. Story za mitaani za kwamba nguza alitembea kiwanja kimoja na mkuu wa Serikali ndio chanzo cha kufungwa huo ni upuuzi mtupu. Playboy yeyote duniani hawezi akaweka kisasi wala kujinyonga kwa kwa sababu ya demu. Demu akizingua anahamia kwa mwingine fasta. Pili watu wafikirie ingekuwaje kama ni mwanao au mdogo wako ndiye aliyebakwa. Tatu, nguza na wanae kubaka watoto akiwashirikisha wanae ni jambo linalowezekana kabisa kwa imani za wanamuziki wa kizaire.
    Nilikuwepo Zaire (Congo) mwaka 2000 wakati huo J.Mpiana na wanamziki wenzake walikuwa hawelewani kabisa na Mpiana alikuwa anavuma sana, story iliyokuwa inaelezwa mitaa yote ya Kinshasa, Lubumbashi na Mbujimayi ni kuwa alimeza chura mzima ili awazidi zauti wenzake na umaarufu.
    Tanzania ni Nchi bomba sana ya kuishi, ni mambo madogomadogo tu ya kurekebisha na tutakuwa kwenye mstari. Ukiishi nje ya Tanzania kwa muda fulani ndio utagundua ni jinsi gani nchi yetu ni sehemu nzuri ya kuishi. wacheni sheria ilichukue mkondo wake tuache ushabiki.

    ReplyDelete
  79. kwakweli tanzania hakuna right hata kidogo, wakubwa wangapi wamefanya makosa makubwa kuliko hayo na wameachiliwa? wengine ni wezi wengine wameua hata watu.tunaomba waachiliwe huru jamani.

    ReplyDelete
  80. According to the U.S. Bureau of Justice Statistics (BJS): "In 2008, over 7.3 million people were on probation, in jail or prison, or on parole at yearend — 3.2% of all U.S. adult residents or 1 in every 31 adults."
    ...Hapo vipi ni sheraia ianfanya kazi au wnafungwa bila makosa???

    ReplyDelete
  81. dah mi nimechoka niko hoi sijiwezi...nikakae wapi...kwa wabeba mabox?maganda sina na channel sina...ninamachungu tanzania yangu sina hamu nayo..ndotozangu zinaniambia niwe mwanasiasa...but kwahapa tz itaniua na umriwangu bado mdogo sana...uwanasiasawangu nikijitazama niko tofauti na siasa mbovu ya nchi yangu ilojaa uozo..ninawahka wakutaka kufichua waovu namaovu nakutetea haki zawanyonge...but now adays niko more than discouraged!!!niko hoi...

    ReplyDelete
  82. WEWE MWENYEMOYO WA KUTU USIYENAHURUMA LOL EM ONA AIBU.ASSUME BABUSEYA NI BABAYAKO MZAZI LEO YANAMKUTA MASAHIBU KAMA YALE WE UTAAMINI MARAMOJA?BASI NDIVYO INAVYONIUMA MIMI NAONA KAMA BABANGU NDIO ANAPATA MIKASA HIYO ALAFU NAUMIA KUDADADEKI.DAH KUDADADEKI WALAI.

    ReplyDelete
  83. NI KWELI MUNGU NDIYE ANAYEJUA NA NDIYE ATAKAYETOA HUKUMU STAHILI. HII YA KIFUNGO CHA MAISHA HAITOSHI KAMA KWELI WALIFANYA HAYO TUNAYOSIKIA. JIULIZE; HIVI MAMBO HAYO ANGEFANYIWA BINTI YAKO AU DADA YAKO UNGEJISIKIAJE???

    ReplyDelete
  84. awa jamaa wamefanya na watoto waliowafanyia wanafaamika na jamaa aliyeachiwa alikuwa anamichongo kweli kwenda nyumba ya dogo aliyefanyiw madhambii sema waliochiwa walichukuliwa kwa sababu zaidi kiusalama maana wazazi wengine walitaka kuuwa wao wilishiriki kuleta watoto kwa hiyo usitete tuu mambo usiyojua kuna watoto wameharibiwa boi hacha ww usiseme watz wengi niwashabiki pili hakuna haki duniani hata uwe marekani tena huko ndio usiseme ukicheza dili kafiri utakuwa unanielewa sababu kubwa nature ya human being ni corupt msisitizo

    ReplyDelete
  85. MBONA HII ISSUE NI NDOGO SANA.LAZIMA TU ADAPTI SKILL YA WABRAZIL,COLOMBIA ,AU NISEME AMERIKA YA KUSINI.KUNA MBINU NYINGI SANA.MSIWE NA SHIDA TUNAKUJA.LABDA WATOTO ZAO BINAMU,KAKA ZAO,MAMA ZAO,BABA ZAO.NASEMA UKOO WAO WATEMBEE NA JESHI NA SIO POLISI.HATA HIYO SHUGHULI ITAFANYIKA TU.HUKU AMERIKA YA KUSINI WATU WANAHESHIMA HATA UKIMPA MTU PESA INAFIKA.HUSIFANYA HIVYO.WANAUA FAMILIA YAKO YOTE .SIO MBOGO YAANI WANAUA MMOJA HAPANA HUKU WOTE UKOO MZIMA.SASA HUYO KIONGOZI SI ANAJULIKANA BASI NGOJA.NDUGU ZAKE SI WANATEMBEE MITAANI,WNAKWENDA MADUKANI ,KUNUNUA MITUMBA AU DISCO .AU SIWANASAFIRI KUJANJE YA NCHI.ASANTE.

    ReplyDelete
  86. KESI HII INACHAFUA MNO UTU WA MWANADAMU HAKUNA SABABU YA KUONEANA WAKATI WOTE NI WATANZANIA NA RAIS WETU UNA JUKUMU LA KUINGILIA KATI UNAPOONA KARIBU WATANZANIA WOTE TUNASIKITISHWA NA HUKUMU HII KWANI SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU. HAIWEZEKANI MAHAKAMA ZETU ZIKASHINDWA KUTUMIA VIPIMO VYA DNA KUMBAINI MBAKAJI BADALA YAKE KUTUMIA MAONI TU. WAACHIENI HURU WATANZANIA WENZETU JAMANI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...