Kamanda Kova akiwatambulishwa watuhumiwa Edmunda Kapama (shoto) na Deogratius Ngassa kwa wanahabari leo sentro, akiwahusisha katika sakata la Jerry Muro
Taarifa rasmi ya kamnada kova aliyotoa leo
Watuhumiwa wawili zaidi wakamatwa kuhusika na sakata la Jerry Muro, Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inawashikiria na kuwahoji watu wawili kwa kosa la kutumia vitisho katika kudai fedha kiasi cha sh.milioni 10,000,000 kutoka kwa mlalamikaji, Michael Wage Karoli.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake leo mchana katika kituo ca Polisi Centre, Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amewataja watuhumiwa hao kuwa ni, Edmund Kapama mkazi wa Mwananyamala (52) na Deogratius Mgassa (35) mkazi wa Mbezi Beach.

Aidha Kova amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa jana katika maeneo ya Kinondoni na kabla ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao wapelelezi walifanikiwa kupata kumbukumbu za watuhumiwa hao.

Amesema kwa kutumia kifaa cha ELEKTRONIC (CCTV) chenye uwezo wa kurekodi na kutunza kumbukumbu ambapo katika tukio hilo watuhumiwa watatu walionekana wakiwa katika meza ya mazungumzo pamoja na mlalamikaji.

Kamanda Kova amesema kuwa watuhumiwa hao walifanyiwa gwaride la utambulisho na kutambuliwa na mlalamikaji, Michael Wage Karoli.

Katika taarifa yake Jeshi la Polisi imesema kuwa watuhumiwa hao wawili waliokamatwa ni matapeli sugu na hivi sasa wanakabiliwa na kesi nyingine na hivyo kukosa sifa za kupata dhamana mpaka watakapofikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
Jarida la Jerry Muro limepelekwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuona kama ana kesi ya kujibu, na kwa mujibi wa Kamanda Kova endapo mwandishi huyo bora wa mwaka 2009 akionekana ana kesi ya kujibu ataunganishwa na hao wawili kwenye mashitaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 51 mpaka sasa

  1. Haya sasa! wabongo kwa kusulubu mapema...hapa sasa mna lipi?

    ReplyDelete
  2. Sasa hao jamaa ndio waseme walikuwa na Jerry Muro au la? Hiyo CCTV inamuonyesha huyo mtu wa tatu ni nani?

    ReplyDelete
  3. kwa njia hii mnaweza kuua soo kiaina ,mtasema Muro hausiki ila hawa ndio waliofanya vitisho! na bado matatia akili polisi!

    ReplyDelete
  4. Haiiingiii akili kaka Michuzi washindwe kukamata Majambazi kwa CCTV wamakamate Muro ooh God Tanzania zaidi ujiavyo ni uongo 100% hapao City Garden kuna CCTV?Tangu lini ila kijana awe makini watamrestisha in Peace namkumbuka nae yule machachari wa ITV mkoa nimeusahau alikufa hiv hiv

    ReplyDelete
  5. hivi hii kesi ni ya takukuru au ya Polisi? mbona Kova kavalia njuga.

    ReplyDelete
  6. Ngoma inogile, patamu hapo, yetu 'mato', tupo kati kwa kati. Maana hii movie haieleweki inavyokwenda 'plot vis counter-plot' there is no sign of letting-up.

    Mdau
    Macho

    ReplyDelete
  7. Hii inachekesha sasa ndio kusema waandishi wahabari hawaruhusiwi kuzungumza na binadamu. Kama watu wametimia vitisho kosa linakuaje la rushwa hii bado haipandi. Mpokea rushwa huwa atishi mtu ana vungavunga mpaka umpe. Washitakiwe kwa kosa la unyanyanyi kwa njia ya vitisho.

    ReplyDelete
  8. kwali kwel isasa hizi habari zinaleta kihindihindi! (kizunguzungu)

    ReplyDelete
  9. when we give a press conference, do we realy stand by offenders? or we lock them up and comeout to give the press conference. Those guys do not look like they are in a tense mood. I think this is garbage

    ReplyDelete
  10. Jerry Murro kush neihe,sirudi bongo ng'o.
    manyunyu

    ReplyDelete
  11. Unajua time nyingine bwana watu wanafanyaga vitendo ambavyo vinasikitisha kama kweli wewe unakua na uwezo wa kufikiri kidogo. Ebu angalia hizi facts halafu nipe jibu:

    1- Mbona kuna data za Muirani kuibia nchi na polisi hawajamkamata na kumwekea press conference halafu wakatueleza wanapeleka faili kwa mwanasheria mkuu wa nchi kupata ushauri?

    2- Mbona akina Yona na Mramba hawakuwekewa Press Conference na kamanda wa polisi halafu wakapelekewa faili lao kwa mwanasheria mkuu kuangalia kama wana kesi ya kujibu?

    3- Mbona kuna listi ya wauza unga ambayo tulielezwa ipo tangia mwaka 2006... Kwanini polisi hawakuwakamata hao watu wakati listi ipo halafu wakawaweka hadharani kwenye press conference halafu then wakatueleza wamepeleka faili kwa mwanasheria mkuu wa serikali kuangalia kwamba kuna kesi

    4- Kuna mifano mingi ninayoweza kui-outline hapa, ila ngoja mi nikajenge nchi ya watu. Sina mda wa kupoteza kwenye "double-standards" za waheshimiwa hawa.


    Unajua mi nafikiri hawa jamaa wanazani watanzania wa sasa ni sawasawa na wale wa mwaka 47. Karne hii ni ya Sayansi na teknolojia bwana. Hachezewi mtu akili kirahisi-rahisi bwana. Hapa kuna mchezo mchafu unapikwa hapa na tumeshaushtukia.

    ReplyDelete
  12. haya sasa kumekucha,sijui da subi sijui nani msijidai kutetea wala rushwa huku,jerry ni mtuhumiwa na inaonesha wazi ameshirikiana na hao jamaa kutaka kumuingiza jamaa mjini,polisi msimuache,namuaminia sana kova,tangu apewe dar pamenyooka,jeri asilete za kuleta,za mwizi arobaini

    ReplyDelete
  13. na uhakika mwaka huu kova ndo anachukua umaarufu mazima,maana kila kitu kiko hadharani now,jerry bila wasiwasi wowote anausika,cheki sasa kwenye camera za cctv anaonekana na hawa watuhumiwa wawili,na balaaa zaidi ni watuhumiwa wanaojulikana kwa utapeli mjini,ninavyomjua kova hawezi kudandia kitu juu juu,anajua anahofanya,na hapo anasafisha njia yake mazee,kova hawezi kuropoka tuu,maana anajua yalomkuta zombe.

    ReplyDelete
  14. jerry ni kutoka kilimanjaro,haki ya mubgu sitakaa kuwapa kura yangu chadema.jamaa ni noma,kila walipo lazima waharibu.

    ReplyDelete
  15. ukisoma hiyo barua ya polisi utaona inasema,MATAPELI WAWILI WAKAMATWA JIJINI DARESALAAM,NI WALE WALOSHIRIKIANA NA JERRY MURO,hapo unaona wazi kova anaipeleka hii kesi step by step,ameshajua na kumuonaa jerry kwenye hiyo cctv,sema anatafuta heshima ndo maana anaenda mdogo mdogo,kesho jerry ataonganishwa kwenye kesi,then kesho kutwa video hadharani,alafu sasa wakina da subi ndo wanabaki haa.

    ReplyDelete
  16. DUH HII KIBOKO! MAISHANI MWANGU SIJAWAHI KUONA AU KUSIKIA WATUHUMIWA WANATAMBULISHWA "LIVE" KWENYE PRESS BRIEFING!

    ReplyDelete
  17. haya bwana Kova endelea na cctv zako.usisahau kuwaona akina mtandao wa simu ambao Jerry na hao Jamaa wanautumia.ila nakuhakikishia kesi hii haijiungi hata kidogo.ni kichekesho tupu.

    ReplyDelete
  18. Hapa sasa pameiva! Namuona Inzi akijipitisha karibu na utando wa buibui halafu ghafla akagundua kashagusa utando mmoja na alipojarubu kujichoropoa akakuta buibui yuko juu yake akizidi kushindilia utando wake kumzunguka.
    JERRY MURO; Nina ushauri wa bure kabisa kwako. Iwapo ni kweli uko mwaminifu (Faithful) basi ninachokushauri ni Mtegemee Mungu tu maana hapo uko vitani (You are in a Battle). Na hii vita si yako hata kidogo. Basi uwe mwenye busara na mwenye maombi. Usizungumze sana na iwapo utataka kujitetea vyovyote vile ambavyo ni ukweli basi muombe Mungu akupatie Roho wake akuongoze. Nilipokusikiliza kwenye mahojiano yako na waandishi wa GP jana inaonyesha unategemea sana nguvu za kibinadamu hasa uliposema eti wamekunyanganya kila kitu ulichotegemea kutumia katika kujisogeza. Huhitaji hivyo vitu ila unahitaji Kujikabidhi kwa Mungu Anayeishi na iwapo una hatia basi tubu kwake na muombe kwa dhati na Imani kuu akupiganie na kukutoa. Utashangaa hata kama wewe ni mwenye hatia utakuwa juu na utasimama kidedea. "Ila tu usije ukamuacha MUNGU baada ya ushindi maana Ibilisi atahakikisha anakutokomeza kabisa." KILA LA KHERI KIJANA.

    ReplyDelete
  19. Bwahaaaaaaaa Police wa Tz, eti CCTV, Kweli wabongo mmeendelea kwa uongo?
    Wapeni watanzania wenu umeme wakutosha wataonana hata usiku nakupunguza ujambazi lakini CCTV umeme wa msimu?
    Kenya Oyeeeeee bwahaaaaaaa nimecheka mpaka najamba puuuuuuuu.

    ReplyDelete
  20. Niliwaambia, polisi wan kesi zao bwana hazina watuhumiwa, wanachohitaji ujitokeze tu wakugaie. Na ni mabingwa wa kutengeneza ishu si mchezo.

    Sasa hapo, hao jamaa wamekamatwa na ishu zingine kabisa, mchezo ukatengenezwa wakubali kuhusika na Jerry Muro, halafu virungu havitatumika, vinginevyo watakula kibano mpaka wafie jela.

    Kwa ufupi ni kuwa, polisi watamlazimisha mtu mwenye kosa jingine kabisa akubali kuwa wewe Muro unahusiana naye, halafu ngoma inakwenda mahakamani, wao vibaka wao ndo mashahidi kusema kuwa wewe unahusika, basi, hicho tu. Wanakutia hatiani.

    Kumbuka, mahakimu nao wapo kwenye mtandao wa rushwa wa polisi. Mwanangu hufurukuti.

    Hii ni fundisho jingine kwa wale mnaojifanya wazalendo na nchi ni yenu, yaani hadi leo mnaishi kwenye denial kwa kuamini kuwa eti nchii hii ni yetu. Hii nchi si yetu wale yenu ni YAO jamani msijidanganye, hamuwezi leta mabadiliko yeyote. La msingi ni kutafuta njia ya kutoka tu Bongo.

    Twendeni tu kubeba box, kuchambisha vibibi na vibabu, si mbaya wala nini, mshiko wako unapata, unatumia pesa ndugu zako walioko huku jela (Tanzania) nasi, wanazitumia kujitibu na kununua chakula pamoja na kutoa hongo kwa wenye nchi.

    Nchi za wenzetu sistem imeshawekwa, ingawa unaweza nyanyaswa lakini ukilalamika unasikilizwa na ukweli unatafutwa ukafanyiwa haki, au ukiwa ni mtu wa kufuata sheria maisha yako hatavurugwa na mtu yeyote.

    Pole Muro, hukujua hilo. Michuzi, please tuanzishe harambee ya kumchangia huyu jamaa yetu, kama nilivyosema awali, jeneza na at least pesa ya kuendeshea kesi na kununulia sabuni akiwa jela hiyo miaka thelathini atakayofungwa. Si unajua hukumu ya ujambazi ni si chini ya miaka 30?

    Hawezi kushindana na hawa watu hata kidogo, kajiingiza mwenyewe na wa kumsaidia hana.

    Please Michuzi, kabala mambo hayajaharibika zaidi, TUMCHANGIE.

    ReplyDelete
  21. MASHAHIDI WA UONGO WANAENDELEA KULA SEMINA YA KUJA KUMMALIZA JERRY.

    WATUHUMIWA GANI HAO WAMETULIA, HAWANA WASIWASI. INAONEKANA WAZI WAMEHAKIKISHIWA AMANI! MASHAHIDI WA UONGO BONGO NDIO KWAO!!!!

    ReplyDelete
  22. Mara nyingi mambo ya kitaalamu hayahitaji longolongo kama hivi . Bingwa anony Feb 2: 06:12PM umenifurahisha na ndo maana Muro akaambiwa aache sound (taarabu) na hili suala kulipeleka kwa DPP, Kova ana nia nzuri ya kutaka asihusishwe na ripoti za Muro(za kuwaumbua polisi wala rushwa huko Iringa). Rejea pia maneno yake...Muro ni rafiki yetu.Sisemi Muro ana kosa, bali tumwachie DPP na ikibidi mahakama itafsiri (ma)kosa kama (yapo)lipo. Kuna maswali ya kujiuliza, Muro kweli news conf. City Garden!!, je, TBC (nao)kama walipewa taarifa rasmi wakatuma mwanahabari, ya nani ingerushwamaana wewe umeidaka juu kwa ju(wanahabari nifahamisheni huenda sijui) na je alimtaarifu mwajiri kuhusu hilo (je huo ni utaratibu? taratibu zinasemaje?),mlalamikaji alisema aliacha miwani, aliona bastola na pingu na Muro akakiri kuwa nazo (kama ni kweli). Polisi wanasema bastola anamiliki kihalali lakini pingu, itakuwa kazi kuthibitisha imekaaje!! na kuna nia ovu ya Kova, CCTV(camera kurekodi nyendo zao vipi?), hao mabingwa wengine waliokamatwa ni vipi na kama alikwenda Moro wakitambuliwa na mashahidi wa mji kasoro bahari, hii imekaaje!!!na kuna mtaalamu aliniuliza kesi ya rushwa ni Takukuru au Polisi?, kwa upeo wangu mdogo polisi ni zoazoa hata rushwa kwao ni ndani na ukicheza hata madai atakamata na akishapeleleza na kukuta ni madai ndo pona yako, anakamata TAKUKURU, JWTZ, nk. kama ambavyo polisi akiingia anga za TAKUKURU atakavyokula za usoni. Nashauri tuiachie ofisi ya DPP, Muro ni binadamu na kama kaonewa itajulikana na pia tusihukumu eti polisi wanalipiza kisasi hiyo haijatulia. Kwani mwanahabari akila rushwa ndo tuseme wote na hivyo wakiandika habari basi wanalipiza kisasi!!!, NO, traffic police akilamba ndo tuseme wote, hapana!!, No.

    ReplyDelete
  23. Huu ni ubabaishaji katika kazi katika polisi na hawana kesi yeyote ya maana hapo,najua sasa hapo lawyers wanatamani sana hii kesi maana nina uhakika kina Kova wataaibika sana...hakuna haja ya kuendelea na hizi porojo zao za press conference kama wana kesi kweli wakutane kwa judge

    ReplyDelete
  24. Ok matapeli wawili,SASA jeryy ni Tapeli au MlaRushwa?Sasa KAMA kweli walishirikiana na hawa watu,Mbona alimwachia Jerry?na mbona walikamatwa haraka sana watu wawili tofauti kwa muda wa siku 1 tu?Huu ni mchezo tosha,BABU KOVA anataka kujikosha lakini unga umezidi maji hapa haukandiki,Hiyo CCTV je iliwaonesha wote pamoja?Mbona alikamatwa Jerry Juzi hatujaambiwa kuwa alikamatwa na wahusika wengine,Mchezo tosha KIKWETE AIBU YETU AIBU YAKO!!!!(Nuramo)

    ReplyDelete
  25. Hao ni WATUHUMIWA sio WASHITAKIWA they are still innocent till they have been approved by Court of Law!! Sasa iweje uwatangaze hadharani? Je unavisibitisho vya kutosha KUWASHITAKI? Je kama Mahakama ikikuta visibiti havitoshi na kuwaachia huru Jeshi la Polisi litawalipa fidia ya kuwachafulia maijina yao??
    Hivi Wanasheria wa Tanzania wapo?? Mbona kesi za Madai ya Haki za Binadamu ziko nyingi?? Au ndio kwa wale wanaojua tu?? Mbona hamuzifuatilii?? Haya ngoja mi nikabebe boksi labda nitaangukiwa na boksi nami tajiri maana hizi nchi za watu Sheria inashika mkondo wake na sio mchezo!!

    ReplyDelete
  26. HII INCHI IS FUCKED UP...na usibane, huyo MURO atauwawa karibuni..na mtakuja sema eeeh HOW LONG WILL THEY KILL OUR MESSENGERS WHILE WE STAND ASIDE AND WATCH....

    ReplyDelete
  27. YANI serekali yetu imeoza....nchi yetu inaoza kabisa, alafu mwisho wa mwaka narudi huko duuh!

    eti jirani akiripoti kwa polisi ya kwamba ulitaka kuiba gari lake alafu ikienda garage kwake mnakuta gare lake liko poa tu kuna mtu atakamatwa??? sasa tofauti ya hiyo na jerry kukamatwa bila millioni 10 ni nini?

    hauwezi kumkamata mtu bila kitu cha kuunganisha huyo mtu mwenyewe na makosa au kosa. hata kama jerry alikuwa na makosa, polisi haina kesi yoyote maana wamshindwa kumkamata mwizi wa supu jikoni akila.

    washenzi kweli polisi....na hii ni kama kioo cha jinsi serakali yetu inafanya kazi. Watanzania napenda upole wetu lakini kwenye mambo ya kudai chako, (basic human rights) tusiwe wa pole ili serekali yetu ianze kututumikia sis wananchi!

    mdau wa scotland

    pooza hasira hapa http://www.youtube.com/watch?v=HZKAn2pn95M

    ReplyDelete
  28. Michuzi umewaumbua watu kwa kutoa maoni yao. Sasa angalia wanavyoadhirika. Muro yuko wapi?

    ReplyDelete
  29. KAMA ANACHOSEMA KOVA NI SAHIHI NI KWAMBA WALIPANGA NA HAO MATAPELI ILI WAMNASE JERRY MURO, HAO MATAPELI THEY HAVE NOTHING TO LOSE, TAYARI WANA KESI NYINGINE NA HIYO NIDILI HUJUWI WAMEAMBIWA NINI ILI WAFANYE HICHO KITU, WANAMJUWA JERRY MURO KWA NINI WAMUHUSISHE KWENYE MAMBO YA RUSHWA, LABDA UNIAMBIE JERRY NA HAWA JAMAA WANAFAHAMIANA MUDA MREFU NA HIZO NDO ZAO LAKINI KAMA NI FIRST TIME IKO KITU SI CHA KWELI, NA HII CCTV IKO WAPI KWENYE GARI ZA POLISI,KWENYE PIKIPIKI ZA POLISI AU KWENYE MGAHAWA HUO? NA KWA NINI FAILI LA JERRY LIPELEKWE KWA MWANASHERIA MKUU, MLA RUSHWA FAILI HUPELEKWA KWA MWEANASHERIA MKUU, HIYO SI KESI YA KUPELEKA KWA MWANASHERIA MKUU, HUO NI UTAPELI MTUPU MNATAKA KUMFUNGA MTOTO WA WATU BUREEEEE!!!! KISHA KUFICHUWA VITENDO VYENU VYA RUSHWA. WANASHERIA VIJANA MSAIDIENI JERRY JAMANI HUO NI UONEZI WA BURE KABISA. HAO AKINA KAPAMA MMEWATUMIA KUHALALISHA KESI YENU, MBONA SIKU YA KWANZA HAMKUWATAJA, YAANI KESI YENYEWE NI YA VIPANDE YA KUUNGAUNGA TU, CCTV NI VIDEO RECORDER HUNA HAJA YA KUCHUKUWA MASAA KUANGALIA KILICHORECORDIWA, UNAWEZA KURUDISHA NYUMA INSTANTLY NA KUONA TUKIO LILILOPITA SASA IWEJE ICHUKUWA SIKU INZIMAAAA KUTAMBUWA WATU, NI UONGO WA KIKUBWA, POLISI HIYO NI AIBU

    ReplyDelete
  30. Kova hana mamlaka ya kuwa convict watu. Mamlaka hayo ni ya mahakama tu, kitendo cha kuwasimamisha hapo hao watu na kusema ni matapeli, je mahakama ikiwakuta si matapeli Kova atarudi tena na kuwasimamisha na kusema kuwa mwanzo alikosea hao si matapeli?.

    Je wakimfungulia kesi ya madai kuwa kawafanya jamii iwaogope na hivyo kuathiri maisha yao so jeshi liwalipe bilioni moja Kova atakuwa na cha kujitetea?.

    Kwa kusema kuwa kulikuwa na gwaride la utambulisho na mlalamikaji akawatambua Kova haoni kuwa bado haaminiki kwani yeye na Mlalamikaji wanaonekana kuwa upande mmoja wa kummaliza Jerry na hivyo alioneshwa picha za hawa watu in advance ili akawapoint atakataa?.

    ReplyDelete
  31. Kwa jinsi ngoma inavyosonga hii inabidi watu ka hao kina sijui Da Subi na wengineo wajifunze kuwa makini na ushauri wao wa "Dr Phil" manake wanaweza kujishushia heshima pale ngoma ikiwa ndivyo sivyo.Hapa ni kucheki mchezo umekaa vipi then "udokta Phil" uje mwisho wa mchezo.Kuna wajanja wengi hapa wanacheki tu movie linavyoenda ndo kwanza liko nusu.

    ReplyDelete
  32. Hawa watuhumiwa wanatambulishwa kwenye press conference kama wameshinda bahati na sibu, mbona hatukuona huyo jamaa anaewatuhumu kuwekwa kwenye press conference baada ya kufukuzwa kazi kwa kuhujumu na kutumia vibaya pesa za wananchi? kweli bongo tambarare!

    ReplyDelete
  33. kwa nini hili limetokea baada ya jerry kutoa picha za wale mapolisi iringa?
    hapa kuna kitu

    mlioko ughaibuni msirudi kwa kweli huku ni kulindana kwa kwenda mbele mi nisingekua na familia ya kuiangalia mbona ningeshasepa siku nyingiiiiiiii ,huku noma, no piece at all,no human rights

    ReplyDelete
  34. Wanasheria wa bongo tusaidieni, Je ni haki kuwaonyesha watuhumiwa hadharani?

    Eti Elektrinik, si useme camera tu.

    ReplyDelete
  35. Huyo Jerry hana kesi yoyote ya kujibu. Hivi kuwa na kisu ni kosa?

    ReplyDelete
  36. NAPATA TABU SANA NA KOVA KWA HII STAILI YAKE YA KUTAKA KUJISAFISHA WAKATI ANA HARIBU KESI. KAMA UNASEMA HAWA WATU NI WATUHUMIWA KWA NINI UANIKE KWA JAMII KUPITIA VYOMBO VYA HABARI KUWA NI "MATAPELI SUGU"??? KATIBA YETU IPO WAZI KUWA MTU ANAETUHUMIA BADO NI MTUHUMIWA MPAKA MAHAKAMA YENYE MAMLAKA ITAKAPOTHIBITISHA KUWA AMEHUSIKA KATIKA KOSA ANALOTUHUMIWA!. KAMA KUNA TUHUMA YA NINI KUANIKA KWENYE VYOMBO VYA HABARI HIVI? NA NI WAHARIFU WANGAPI WAMEWAHI KUANIKWA HIVI?..KAMA JALADA LIMEKWENDA KWA MWANASHERIA MKUU AU SIJUI DPP, KWA NINI YEYE AKURUPUKE KUJIHAMI KAMA SIO ANA VITA BINAFSI NA MURO?...HIVI KAMA POLISI WANA MTAMBO YA KISASA YA CCTV, KWA NINI WAIITUMIE KWENYE MATUKIO YANAYOMALIZA MALI NA MAISHA YA WATANZANIA WENGI KAMA AJALI, UJAMBAZI NK WAENDE WAKAITUMIE KWENYE TUHUMA ZA RUSHWA ZA MURO KIJANA MDOGO TU ANAYEPIGANIA MAISHA KAMA SIO VISASI?....

    ReplyDelete
  37. Mh. KIKWETE UNAKULA VACATION WATU WANAUANA HUKO! NCHI ISHAUZWA HUKO WATU WANAFANYA MADUDU KAMA SI UTUMBO!! UWWWWWWIIIIIII!!

    ReplyDelete
  38. Kuna ulazima wa kumwagiwa maji baridi-literally, ili jamii izunduke. Watumishi wa Umma inabidi muwe makini na kupunguza lipua lipua. Nilivyosoma hiyo Press release, nimeona makosa yafuatayo, kitaaluma na kinasaha:

    1. Typo: Soma wasifu wa mtuhumiwa kwa kwanza, "h" imepungua kwenye neno "hana".
    2. Badala ya kuandika "hana kazi", kiripoti ingeliandikwa "hana ajira" (i.e. unemployed)
    3. Para ya tatu mstari wa pili, ilitakiwa uwekwe mkato (comma) kabla ya neno Polisi.
    4 Mstari wa mwisho para ya pili. Kitaaluma Press Release haikuwa na ulazima wa kutumia kuvumisho cha sifa "maarufu" (wakati wa kiutaja PR Camp. Kitaaluma, wangeandila "...mgahawa wa PR Camp.."
    5.Para ya tatu, palitakiwa mkato (comma) kabla ya neno Polisi)
    6. Lugha sahihi ni Wapelelezi wa Polisi na sio Polisi wapelelezi. Fikiri kidogo.
    7. Ni aibu kuandika (tena kwa herufi kubwa ELEKTRONIKI (CCTV). CCTV ni fupisho la Closed Circuit Television...ni kweli inatumia nguvu umeme, lakini tuwe makini, hatusemi ELEKTONIKI Computer, ELEKTONIKI Microphone...
    8. Consistence: Kama wale wawili wametambulishwa kama "watuhumiwa" na mtangazaji kama "Jerry Muro", na sentensi ya tatu para ya tatu ilitakiwa ifafanue hali (status)ya mtuhumiwa na tatu aliyetajwa hapo, i.e.Je ni Jerry? Je ni mtuhumiwa mwingine ambaye bado anatafutwa, au Je ni Bwana Michael Karoli?, Je ni Askari kanzu?
    9. "Innocent until proven guilty": Chombo cha sheria, tena via Press Release, kitaaluma kilitakiwa kuendelea kuwaita wawili wale "watuhumumiwa" mpaka hakimu atakapotoa hukumu (nimesoma wapo nje kwa dhamana ya kesi nyingine). Neno la kitaaluma na kifasihi ambalo lingetumika hapa ni lenye kuelezea "tuhuma za ulaghai". Unapomuita mtu "tapeli", umemuhukumu tayari. Wakishinda kesi wanahaki kikatiba ya kufungua kesi ya kuchafuliwa majina na chombo cha dola--na kabla ya hukumu wanaweza kufungua kesi ya kulishtaki Jeshi la Polisi kwa kuchangia kuongoza jamii iwaone wana hatia kabla kesi haijasikilizwa na kuisha.Maandiko kama haya yatatutia hasara walipa kodi-maana faini hiyo itatoka Hazina (if you trace the money)
    10. "Upelelezi wa shauri hili unaendelea kwa kasi na kwa umakini kwa kuzingatia sheria na taratibu". Kama mwandishi wa hii release aliona umuhimu wa kuichapa, je msomaji atakuwa amekosea kuwaza kama kuna kesi nyingine ambazo upelelezi wake sio wa kasi? sio makini? haufuatilii sheria na utaratibu?

    Mwisho, pamoja na kuhisi kiprotokali yeye sio mwandishi, ila naona aibu chapisho hilo (Press Release) kuwa na jina la Kamanda wa Polisi, tena Kanda Maalum ya jiji mashuhuri. Logically, pamoja na kutingwa na kazi, Kamanda nilitegemea kwamba angeipitia neno kwa neno na kuruhusu itolewe kwa umma kitu ambacho kimenyooka kitaaluma na kifasihi. If anything, one should know, when announcing an arrest of a popular individual such as as this journalist, is likely the public will pay a little more attention to details, and handle outs such as these.

    Tuamke!!

    Kaka Yenu

    ReplyDelete
  39. Bongo Kweli Tambarare hii sijawahi kuona,watuhumiwa utafikiri ni Mabodigadi wa Kova,hata handcuff,haya Mkuu wa Polisi anajibishana na Muro kumbe bongo Polisi si wa kuwaogopa ukijitoa tu kwenye Michuzi wanakuacha mwenyewe,Na huyu Muro Pingu kapata wapi?inaonekana kweli kuna mchezo ila Kova kashindwa kuupanga uzuri tu,Haya hawa majamaa wameshikwa siku moja tu,OK KAMA Jerry alitaka kuchukua Rushwa na yeye abadilishe aseme amemkamata mtu alitaka kutoa rushwa kamtega,sasa Kova anasema kesi pengine itaenda mahakamani file kwa mwanasheria mkuu,HE! UTAFIKIRI KESI YA KUPIGWA KIBAO MWINYI!KIKWETE HEBU NJOO MSAIDIE HUYU MZEE.

    ReplyDelete
  40. NAIPENDA BLOG YA MZEE WETU MICHUZI NIKISOMA NACHEKA HADI NAKUMBUKA NYUMBANI NA MBAVU ZINAUMA KARIBU NIFE ANNOY WA FEB 2 9:38PM AMENIFURAHISHA SANA HADI UCHOVU NA BARIDI IMETOKA ANATUAMBIA TUSIRUDI NYUMBANI HAKUNA KAKI KABISA YEYE NI FAMILIA TU ANAYOINGALIA TU NDO INAMZUIA LA SIVYO "ANGESEPA" KITAMBO

    ReplyDelete
  41. we michuzi faalaaaaaaaaaa kweli kweli tukisema ukweli hutoi NCHI INAONGOZWA KIJESHI nimetoa ktk kesi ya FUNDIKIRA hukutoa unatoa coment za wajanja wako poa!!!!!!!!!!!!!!! muro aaaahhhhhhhhh

    ReplyDelete
  42. kaka Michuzi tunaomba background check and public records services za hayo watu wawili ya J muro na kamanda Kovu. walisoma wapi? na lini? kama utaweza mimi naona wamechukulia mwanamke/mrupu

    ReplyDelete
  43. jamani haya ndio mambo ya bongo muamini mtu kwa atakayosema lakini usimuamini kwa alichokifanya. Hapa naona story inakuwa juu ya story.
    Uzuri wa bongo kila mtu anahitaji maisha mazuri tatizo kipato ni kidogo Matokeo yake kila mtu anataka apate pesa kwa njia za mkato.

    Sasa hivi uaminifu umekwisha mtu anatangaza neno la mungu mchana usiku kibaka.Unamuona dada wa heshima mchana usiku kichaka nk

    Sasa haya yote yanawezekana kwa yanayomkuta Bw Muro kuwa na chembe chembe za hisia za kweli, maisha ni magumu kamshahara ka TBC kiduchu sasa afanye nini aongeze kipato? jibu chukua njia ya mkato shirikiana na kinatapeli 1&2 tisha toto na bastola na pingu.Sasa jamani muandishi wa habari na pingu wapi na wapi.

    TUsubiri mwisho wa ngoma itakuwa vipi

    ReplyDelete
  44. Wandugus.... I think will all know that our country is infested with fraud and curruption. I agree with most of your comments regarding Kovas press breifing. Probably Jerry is not involved what so ever...Hey,innocent till proven guilty..right!. But the action that Jerry took after the fact....talking to the media, talking about issues that happened yrs ago,demeaning Kova, will make things difficult for him. And also there could be something about Jerry too..... This will turn out to be like a cat and mouse game.Too bad Jerry is the mouse here

    ReplyDelete
  45. Muro anaweza kuwa mdhambi like anybody.
    He is not ma messenger wala nn
    You go Muro-Kama kweli kura mvua.
    Subi unayaona haya? Uliyajua ama unamsaidia mungu kuhukumu?
    Mwachieni DPP

    ReplyDelete
  46. Watanzania,

    Kamanda Kova anakiuka misingi ya kazi yake kwa kuogopa Wahandishi wa Habari??!!

    1. Tangu lini ukamuita MTUHUMIWA "TAPELI SUGU" kabla hajafikishwa mahakamani na kuthibitika ni kisheria?

    2. Sasa utawezeaje kwenda Mahakamani kumshitaki kwa UTAPELI tena?

    3. Tangu lini ukawatoa WATUHUMIWA hadharani kabla upelelezi haujakamilika au HAWAJASOMEWA mashitaka?

    4. Iwapo hao WATUHUMIWA wakishinda kesi Mahakamani, si wataidai Polisi fidia kubwa sana kwa Udhalilishaji?

    Kamanda Kova, vitendo hivi kwa wanaojua sheria na maadili ya kazi za polisi vinakupunguzia heshima kabisa. Jirekebishe.!!

    Mzee K.

    ReplyDelete
  47. YALE YALE YAKINA DITOPILE NA ZOMBE KWANI HAKI NI NDOTO AU MLIDHANI TANZANIA WANAWAUA KAMA ALIVYOFANYIWA KEN SAROWIWA HAPA NI KIMTINDO ALAFU UNAZIMISHWA HIYO NDIO NGUVU MPYA, ARI MPYA NA KASI MPYA MANAKE KASI HIYO INGEKUA INAFANYIKA NA KWA KINA LOWASA AAH INGEKUA FAIR ILA WAANDISHI WENGINE MJIFUNZE - KAPU LA MJANJA MJINGA HATII MKONO. SASA JERY ALIINGILIA KAPU LA WAJANJA UNAONA....

    ReplyDelete
  48. Hop! tooooo! much of srap! give a break.... by the way nyie wandugu mliopo ughaibuini hasa pande za OBAMA nawaomba mtafuteni mtunzi mzuri wa filamu toka pande za HOLLYWOOD akutane na afande KOVA wanaweza tengeneza movie kali wakalikwamua Geshi la wababaishaji kwenye dimbwi la ukata!Nimtizamo tu afikishiwe kova.
    MDAU
    UG

    ReplyDelete
  49. Hao watuhumiwa wamepandikizwa kabisa wanajua nini kinaendelea wamewekwa kumuua Jerry sura za watuhumiwa zinajulikana na dhamira zao pia ila hao ni uwoungo mtupu, mambo yamesukwa haya na yatazidi kusukwa tu.

    ReplyDelete
  50. Polisi wetu wamezoea mno kubambikia watu kesi kwa maslai yao...sasa kwa issue ii ya muro wanaumbuka.Hili crisis inayotokana na uongozi legeleg.Mengi yatafuata.

    ReplyDelete
  51. jerry amekili kuwa na pingu sababu nihao polisi waliompa inaelekea walisha fanya nae kazi miaka ya nyuma. na inawezekana kweli walikuwa hotelini na huyo gawe siku za nyuma kwa kuwa kama jerry ni investigative journalist huenda kahusika na kufukuzwa kazi huyo gawe, sasa gawe kufukuzwa+polisi kuumbuliwa= jerry kaomba rushwa na pingu na tissue

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...