Hello Balozi wetu ,
Napenda kukupa taarifa kuwa mdau Ndg. ROGATIS SEBASTIAN MKENDA na Dada MARI woote wakazi wa Osaka , JAPAN, walifunga ndoa iliyopendeza wikiendi ilopita na kufuatiwa na mnuso wa nguvu katika Ukumbi wa BALI LAX Garden. Kama ilivyo kawaida yetu naomba wadau tumpe salamu za pongezi . Mzaa chema , Mzee Mkenda alikuwepo kushuhudia shughuli hii maalum .
Kidumu ! Mdau

maharusi wakiingia ukumbini huku kimasomaso cha kijepu kikirindima
Bw. harusi amvisha pete mai waifu wake
Bi. harusi naye anarivenji
pete ndiyo hizi...kuna maswali??

Bw. Harusi akianguka
Bi harusi anafuatia
maharusi wakionesha nondozzzz yao ya kumeremeta

ndugu, jamaa na marafiki wakifurahia
---------------------------------------
Kwa niaba ya Wadau wote, Globu ya Jamii
inatoa hongera kwa maharusi kwa kumeremeta
na kuwatakia maisha mema na yenye heri
-Michuzi









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. hongereni sanaaa makaratasi hayoo

    ReplyDelete
  2. Michuzi na wadau wengine, salaam.
    Hongera kwa mdau huyu kupata jiko.

    Ninaishi Japan pia na ninataka tu kutahadharisha blog yako juu ya matumizi ya neno "Ki", "Wa", "m"" Jep/Jepu. Ni neno baya sana ambalo lilikuwa linatumika wakati wa vita na waAmerika walikuwa wanatumia hilo dhidi ya waJapan (the Japs. etc). Ni sawa na kumwita mtu mweusi "nigger". Pengine hukuwa unafahamu hilo, Michuzi, na ndiyo maana umeweka kama ilivyo kwenye blog hii kama hivi: " maharusi wakiingia ukumbini huku kimasomaso cha kijepu kikirindima"

    ReplyDelete
  3. Ukioa Mjapani kumbe Michuzi anakupongezaa pia!!! Kuna ndoa nyingi tu zile za kwenye Valentine sikukusikia mzee Michuzi ukimwaga pongezi! Huu ni ubaguzi wa rangi...

    ReplyDelete
  4. Mdau mwenye fikra za ubaguzi hapo juu...kama utasoma mwanzo, mtuma habari picha alitanguliza kuomba pongezi, sasa Ankal kama mdau amepongeza kwa niaba....sioni ubaya wowote.

    Mbakiaji

    ReplyDelete
  5. Hivi siku hizi watanzania hakuna kuoana kwa mapenzi au sababu nyingine zaidi ya makaratasi? Mie mnanihudhi sana wale ambao mkisikia au kuona watu wameoana basi mnaanza kuzungumzia makaratasi. Hata Mtanzania kwa Mtanzania wakioana ughaibuni utasikia wanaulizana, "bwana harusi ana karatasi?". Au utasikia yule kafuata karatasi au kapata karatasi. Mbona wengi tu wana makaratasi yao ya hata ya kuzaliwa na bado wamedoda?
    Nachukia mno ingawa mie nimeoa Mtanzania na ndoa yetu imefanyika Tanzania na karatasi letu la Kitanzania.

    ReplyDelete
  6. japani hoyeeeeeee duh ebana sikujua kama tunaanza kukubalika japan naona nyuso za furaha za wajapani zimetawala, mazee tupo pamoja majirani zenu hapa bado ni ngumu kukubalika lakini kibishi tunatoka na watoto, tunategemea kupata wanasayansi wa ukweli ktk kizazi chenu
    maisha mema, mimi naleta mvietnam watatusaidia ktk jeshi letu

    ReplyDelete
  7. Sasa msiharibu na huko Japani kama mlivyo haribu Sweeden na Uingereza. wanawake wa ki-sweeden hawataki kabisa kusikia Mtanzania au mkenya. Yale yale ambayo dada zetu walikuwa wana lalamika kuhusu wanaume wa kibongo. tulieni funga kabisa Zip.

    ReplyDelete
  8. Mimi nina swali moja sina nia mbaya. Hivi hizi ndoa za mchanganyiko mbona huwa hazidumu au ni kwa ajili ya kuonja tu?. Mimi nimekaa ulaya sijawahi kuona Kazee ka kizungu na kazee keusi vinakokotana kwenda kuchukua pension au hata kuviona kanisani. lakini utaona kuna watoto wa mchanganyiko wengi sana tena ni watu wazima kabisa lakini huwaoni wazazi wao pamoja.

    ReplyDelete
  9. ndugu anonymous wa feb 16, 10:42:00 elewa tu kwamba ndoa za mchanganyiko ndio zinaanza kukubalikika hivi karibu. hapo zamani kuoa mtu wa rangi nyingine ilikuwa kosa la jinai kwa nchi nyingine. bado hata kwa wakati huu kuna baadhi ya jamii au wazazi hawazihafiki, kama unaoa mtu wa rangi tofauti jiandae na vikwazo vya hapa na pale kutoka kwenye familia yako na jamii kwa jumla

    ReplyDelete
  10. A'afu huyu mbongo anaonekana Jembe!

    ReplyDelete
  11. The bride was beautiful.I want a wedding like that.

    ReplyDelete
  12. Nawapongeza maharusi kwa kukamilisha ndowa zao Binafsi nilikuwa na mchumba wangu kule japani nilipokwenda kwa kusomea mambo ya Uvuvi tukapendana sana akawa tayari tuowane na tuje kuishi hapa kwetu zenj lakini wazazi na jamii ya kijapani kwa miaka ile ya 80 alinikatalia kata kata sasa leo kumuona mwenzangu amebahatika kukubalika nawaombea maisha mema huku namie nikihisi ningekuwa kama yeye wakati huu Mungu ailinde ndowa yenu .
    Mlekwa uledi

    ReplyDelete
  13. ndege wa majira ya kiangazi.February 17, 2010

    Mimi ni mmoja wao,niko kibabu sasa na bado niko na mke wangu wa kiswede na watoto wetu,na familia yetu imejaa furaha sana.Kila ndoa inategemea na kama kitu hujakiona haimaanishi hakipo!

    ReplyDelete
  14. This is not fair,Mjapani na mbongo jamani? sasa nani ataowa dada zetu? hapa tanzania kwa sasa kuna idadi kubwa sana ya wanawake kuliko wanaume. Ratio ni kila mwanaume mmoja kwa wanawake watatu. 1:3 hii ni mbaya sana. Hivi sasa Mzee wa kiume wa miaka 70 anaweza kuowa msichana wa miaka 25 bila hata taabu ya kuhonga sana. Huu ni ukweli ndio maana nyumba ndogo zina ongezeka sana Tanzania. kama Ratio hii ingekuwa 1:2 kama nchi zingine nyingi,si zote, hata nyumba ndogo zingepungua kiasi.

    kuna dada zetu wamesoma na hawana wanaume wa kuwaowa. Ndio maana wengi wanaishia kuwa machangu, si kwa sababu wanapenda,la hasha, ni kwa sababu ya kukosa wanaume.
    Michuzi, washauri vijana wa kiume hii ni hatari sana kwa jamii yetu. Wanawake wakizidi katika jamii ni ni baraa kubwa.

    ReplyDelete
  15. kabla hujaoa mjapani lazima wajue astrology yako kama ni compatible ama vipi. ni shughuli ndefu

    ReplyDelete
  16. Hongereni maharusi. Ishu ya karatasi ningeweza kusema kuwa kwa nchi nyingine inaweza ikawa ni sawa inaipa, yaani ukioa baada ya muda fulani unapata karatasi zako na unakuwa huru (kama hutaki kuendelea na mke/mume wako) na kuendelea kubaki kwenye nchi husika. ILa kwa Japan ni tofauti, utakuwa na karatasi zako pale tu, i repeat pale tu utakapokuwa kwenye hiyo ndoa(una renew viza kila baada ya muda fulani), pindi mkifarakana tu, then unarudisha karatasi zako (au wakati wa ku renew viza ukifika unakuwa huna supporter) na wewe inabidi utafute viza ya aina nyingine ikishindikana ndio kwaheri ya kurudi kwenu. Kwahiyo sidhani kama jamaa kaolea karatasi itakuwa ni kweli maana najua anajua fika akiharibu hana hizo karatasi.

    ReplyDelete
  17. Bibi harusi mwembamba kapendeza, bi harusi akiwa na umbo hilo anapendeza sana kwenye gauni lake, kiuno kwake kwa mpango unaoeleweka, hongera kaka natumai atendelea kuwa MODEL hata akishazaa, umeopoa CHUMA mzee mzima!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  18. hakika walipendeza sana hongreni saaana kwa kumeremeta mishi kwa amani daima

    ReplyDelete
  19. Hongera sana Mdau kwa KUWOWA. Nakukumbuka sana kuna wakati nilifika OSAKA mlitukarimu sana wewe na mama Albina Chuwa. Nakumbuka pia iliandaliwa Maulidi ( kwa wasiojua kule Osaka watanzania wakiwa na sherehe ya pamoja wanaita Maulidi, na hii haijalishi ni dini gani)

    Kila la kheri Rogati

    ReplyDelete
  20. Kwa kuwa naishi Japani napenda kuwapa darasa kukusu maisha kiujumla hapa.

    1. Japan sio Sweden. Kupata viza hapa ni kasheshe, hata ya kutembea. lazima mtu akupe barua ya kukualika.

    2. Japan inajulikana duniani kote kwa kuwabana wakimbizi, wa halali na feki. Inatoa viza kama 20 tu za ukimbizi.

    3. Japani hamna haki kwa wageni. Ukimwacha mkeo, mke anachukua watoto. Wajapani wanaoishi nje, wakiwaacha mabwana zao, wanakimbia ahpa kwa kuwa serikali yao hairuhusu wageni kuwachukua watoto, hata kama ni kosa la mke.

    4. Hapa hamna mambo ya astrology, hayo ni mambo ya wachina. Hapa ni maelewano tu.

    5. Rangi njeusi hapa bado haikubaliki, usione picha tu. Mara nyingi utakuta wqazazi wanakataa kuibariki ndoa.

    6. Uzuri mmoja tu wa Japani kama utaingia ni kuwa kuna wasichana wengi mbo hawajaolewa. Walifanya kazi sana na kupenda kuishi kistarehe. Sasa wanaelekea miaka 40 bila mume. Kwa hivyo, kama una ubavu, na viza mkononi, karibu, hapa wanatafuta sana kuolewa, kila sikuw anajitangaza kwenye magazeti.

    7. Maisha ya Japani ni mazuri kuliko ulaya au Marekani. Kuanzia shule mpaka kwenye mahospitali yao, ni bora mno. Serikali inawapa fedha watoto kila mwezi ili wazazi wazidi kuzalisha kwa kuwa watoto ni kidogo Japani, wanawake wengi aidha wameshindwa kupata bwana au hawataki kuolewa, wanataka kazi na maisha yao bora binafsi kuliko kulea watoto.

    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  21. we kichura acha hizo kila mtu anakula kitu roho inapenda isitake kulazimisha mabo mbona mademu kibao wanaolewa na wazungu? kila mtu na pendekezo lake

    ReplyDelete
  22. We anon wa Feb 17 10:33AM. Usiwe na mawazo finyu. Fanya utafiti kabla hujaanza kubwabwaja. Dunia nzima sio Japan tu kuna wanawake wengi sana tena sana hawajaolewa, wanawake karibuni wote ni ndoto yao kuolewa. Hata hapa nyumbani wanawake wasomi au walioendelea wanataka kazi na maisha yao bora binafsi kuliko kulea watoto sio Japan tu! Fanya utafiti, japo umasikini unapelekwa waolewe lakini majority walio wasomi na kazi nzuri wanatabia kama za hao wajapan na nchi zilizoendelea.

    Rangi nyusi hubaguliwa popote ambako wako watu weupe wapo, hata hapa nchini ubaguzi wa rangi upo. Katika maofisi au jamii ikiwa na wahindi, wazungu, wachina au makaburu weupe, basi mtu mweusi hubaguliwa atake asitake. Na sio Japan peke yake.

    ReplyDelete
  23. Hongera manake ni makaratasi hayo

    ReplyDelete
  24. DUAL CITIZENSHIP....

    tehe, tehe, tehe, tehe......

    ReplyDelete
  25. Mkenda San Kekon Omedeto Guzaimasu

    ReplyDelete
  26. Anony 11:44 AM, najibu.

    Sina mawazo finyu ila nilikuwa natoa maoni kuhusu JAPAN. Sijaongelea mambo ya wasichana duniani kote wala mambo ya ubaguzi duniani kote, so tuliza boli. Soma maoni yangu kwa makini kabla hujaanza kubwata. Labda umesoma kabla ya kula maandazi ya mama ntilie.

    Kama unafikiri sina elimu ya kutosha unafikiri nafanya nini Japani? hapa hamna kubeba maboxi kama ulaya bila eimu, hata maboxi lazima uwe na elimu ya kutumia robot akusaidie kupeleka katika lori na kompyuta. Wewe ndio ufanye utafiti katika ubalozi wa Japan Bongo, kaulize je, vipi Mtanzania anaweza kupata viza vipi kuishi Japan? Halafu rudi hapa utupe elimu.

    Nilisahau kutoa hongera kwa Bwana na Bibi Harusi. Bali kuzuri sana, ni kisiwa cha Indonesia kwa wwadau walalahoi ambao Geography haipandi. Wajapani wengi wanapenda kwenda kuowa/kuolewa Bali au Hawaii.

    ReplyDelete
  27. jamani ehh ni kweli kampenda kutoka moyoni au ni missing in action hiiiii lol !
    any wayz hongeraa

    ReplyDelete
  28. Kazee kakizungu na keusi vinakokotana hata kuviona kanisani n.k.
    Anony Feb 16 10:37 yaani umenichekesha karibu haja ndogo initoke.Kweli kiswahili kitamu mno
    Sidhani kama kuna mtu anaweza kui translate kwa kiinglish ikaleta raha kama ulivyoandika.

    ReplyDelete
  29. waoooo kaka bingo ilo..safi sana

    annon unaeshangaa vibabu kizungu na mbantu:haiwezekani kwakweli maana mbantu LAZIMA ataonyesha tabia yake ya asili mf kupiga mke,kunogewa na penzi la mbantu mwezio (kuiba nje kwa mweusi mwezio) na extended family zetu asili haimtupi mtu katu ata km umezaliwa mamtoni.zile cromosomes za kibantu unazaliwa nazo

    hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...