Profesa Justinian Rweyemamu

Ninakumbuka vizuri sana jinsi wanazuoni tulivyostuliwa na kifo cha ghafla cha mmoja ya wachumi wakwanza Tanzania, Prof. Justinian Rweyemamu mnamo mwaka 1982, akiwa na umri wa miaka 40.
Katika umri wake mdogo aliweza kufanya mengi kwa kutumia kipaji chake kwa ajili ya nchi yake na nchi maskini duniani. Katika kipindi hicho marehemu alifanikiwa:
1) kupata PhD ya Uchumi (Harvard),
2) kuandika vitabu kadhaa mashuhuri kuhusu historia na muelekeo wa uchumi wa Tanzania,
3) kuwa mhadhiri na mkuu wa idara ya Uchumi wa kwanza mzawa hapa UDSM, 4) kuwa katibu mkuu Wizara ya Mipango,
5) kuwa Mshauri mkuu wa Rais katika masuala ya Uchumi,
6) Mjumbe wa sekretarieti ya "Committe for Development Planning", Umoja wa Mataifa, n.k.
Alikuwa mcheshi, msikivu, na mwenye upeo wa hali ya juu katika kuchanganua masuala ya Uchumi na Falsafa. Je watanzania, mnamkumbuka msomi huyu?
Nipo katika mchakato wa kuandika biography ya Prof. Rweyemamu, na ningeomba yeyote mwenye kumbukumbu muhimu tuwasiliane kupitia anuani: mfaume.abdalla@gmail.com

kwa wasifu tembelea:
http://en.wikipedia.org/wiki/Justinian_Rweyemamu

asante

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Huyu bwana alijaaliwa intellect ya hali ya juu sana.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  2. Kama umewahi kutazama filamu ya "A Beautiful Mind" (ya mwaka 2001) inayoeleza maisha ya mchumi John Nash, nadhani utakubaliana na mimi kuwa maisha ya gwiji Rweyemamu yanashahabiana sana na ya John Nash; details aside. Shemeji yangu amefundishwa nae na amenipa feedback kuhusu Rweyemamu na ni kwamba kiufupi, the man was a genious.

    ReplyDelete
  3. Just a slight addition ya mapokeo

    Ni kwamba yasemekana shule ya Sekondari Ihungo iliyopo Bukoba Mjini ilipewa hadhi ya kuwa na Vidato vya Tano na Sita kama tuzo ya Rweyemamu kuwa wa Kwanza katika mtihani wa Cambridge Jumuia ya Madola.

    kwa mantiki hiyo no doubt he stands as one of Tanzania's Geneouses.

    Labda cha kujiuliza mbona vipaji hivi vimeyeyuka? Kulikoni?

    ReplyDelete
  4. Its very hard to find history of Tanzania. Reading his thesis and some of his work, you get an idea of what happened before independence to 1980. It is very sad, that no one else has really written the history of Tanzania. So when people talk about TZ. THere is nothing to say between 1980 and 1990, but rather lots of speculation rarely supported by facts.

    I only know him through reading his work. I salute you.

    Mfaume thanks for bringing this up.

    ReplyDelete
  5. Sio mnaenda andika kitabu cha ndugu yetu tu..najua intention yenu sio mbaya lakini ...omba permission kwa family yake wanaishi New York......anza na UN office kuuliza - google last name utapata info. To be on the safe side...GOOD LUCK!!

    ReplyDelete
  6. ADILI NA NDUGUZEFebruary 05, 2010

    Wasiliana na mkewe Anna Rweyemamu. She used to run Ethiopian restaurant pale Arusha mjini.She is equally and enlightened woman. Ni mtu mzima but looking fortyish. She might be able to tell you relevant things about her late husband

    ReplyDelete
  7. Kulikuwa na tofauti ya maelewano kati ya Nyerere na Prof. ndio maana akahama na kwenda kufanya kazi UNO. Si unajua Nyerere alikuwa mbishi.

    ReplyDelete
  8. ''...Conflicting direction of thoughts between President Nyerere and Rweyemamu forced him to leave his job as adviser and left the country for a high profile appointment in the UN first in Switzerland and then later New York, USA. During his time in the UN he was a member of the UN Committee for Development Planning, worked for the Brandt Commission and worked for the UN Director General for Development and International Cooperation till his untimely death caused by Cancer in March 30, 1982. He is survived with his wife Anna, and three children, Kemilembe, and Rushuma, who live in New York to this day''..source-google.
    Now i am thinking, how many rweyemamus are out there? not fully utilized to boost this country economy. i think its about time now the high profile jobs like permanently secretary of any ministry,directors of public companies such as Tanesco,TRA,TPA,AIR TANZANIA,TANAPA,TANROADS should apply for those jobs and the parliament approves their qualifications/selection.this way we will be able to get suitable guys not president or ministers' buddies who ruin our economy.

    ReplyDelete
  9. ni muhimu kumbukumbu ya watanzania mashuhuri iwekwe "alive". asante mdau kwa kutukumbusha

    ReplyDelete
  10. Jamaa ni kichwa, hajatokea mchumi anayetisha kama yeye kwa Tanzania and may be the whole of East Africa tangu afariki. Alifanya mabo makubwa san at a very tender age. Aliwafundisha akina JK na wachumi wengine mahiri kama Ndullu, Lipumba na Delphin Rwegasira. Kun jamaa alinipa story zake, sikumuelewa nikaenda kuchungulia Wikipedia, he was simply brilliant!!

    ReplyDelete
  11. Kwa wanaotaka kupata uelewa chimbuko la umaskini wetu, soma kitabu chake "Underdevelopment and industrialization in Tanzania : a study of perverse capitalist industrial development"

    http://www.amazon.com/Underdevelopment-industrialization-Tanzania-capitalist-development/dp/019572321X/ref=sr_1_1?ie=UTF8&s=books&qid=1265359483&sr=8-1

    ReplyDelete
  12. WATU WENYE AKILI NYINGI TANZANIA WAKO WENGI TU ILA TATIZO HAWAFANYE BIDII KATIKA NYANJA YA ELIMU. WENGI WANAFIKIRIA ZAIDI HALI NGUMU YA MAISHA NA JINSI YA KUPATA HELA ZA HARAKA HARAKA.

    ILI MTU AWEZE KUANDIKA ANATAKIWA AWE MFUATILIAJI NA MWELEWA WA MAMBO MBALI MBALI YANAYOINGILIANA NA NYANJA YAKE.

    SIKU HIZI WATU KAMA NI WAELEWA BASI WANAKUWA SIO WAFUATILIAJI.

    KAMA MTU ANASOMA PhD USA au ULAYA na kufanya kazi za mabox hawezi kuwa makini sana kwenye academic.

    ReplyDelete
  13. Tanzania wasomi wengi sana na wenye uwezo wa kuinua nchi yetu, lakini tangia "Rushwa" iwe kipaumbele ndo pande kazi inakuwa ngumu sana kwa wasomi wetu kupata hizo kazi. Na ndo maana tutaendelea kuwa masikini.

    Naamini Tanzania kuna watu wana uwezo mkubwa wa kuinua nchi yetu.

    ReplyDelete
  14. Kila nikisoma post kama hizi kwakweli nalia moyoni....
    Imagine someone at the time managed to make to Harvard and hailed as the genious. Then leo the whole nation has completely lost direction.
    Hata sisi tunaopenda kusoma bahati mbaya kama mtu alivyoandika hapo juu tumepotelea kwenye box kwasababu our country background has made the road ahead completely impassable..
    Sio kwamba hatuna kina Rweyemamu wengine, ni kwamba mfumo wetu wa elimu umekata miguu

    ReplyDelete
  15. WATU WA SASA PIA TUNAPENDA KUSOMA NA KUANDIKA VITU KAMA WA ENZI HIZO TATIZO TULILONALO NI UWEZESHAJI KWANI KUSOMA NA KUANDIKA VITABU KUNAHITAJI UWEZO MKUBWA WA KUJIKIMU KWANI HUWEZI KUSOMA WAKATI HUNAUWEZO WA KULIPIA MASOMO HAYO, PIA HUWEZI KUCHUKUWA MUDA WAKO KUANDIKA KITU WAKATI MUDA HUO PIA UNAUHITAJI KUTAFUTA LISHE YA FAMILIA NI VIGUMU SANA KUWA MAKINI KATIKA KITU FULANI WAKATI HUNA SOURCE YA KUAMINIKA JUU YA KUJIKIMU NA FAMILA YAKO, UKIANGALIA SANA WATU WENGI WALIKUWA NA UWEZO WA KUSOMA VIZIRI KWA KUELEWA WAKATI ELIMU ILIPOKUWA BURE SIS WA SASA HATUPENDI ELIMU KAMA KITU CHA KUTUELIMISHA MASWALA YA DUNIA TUNAPENDA ELIMU ILI TUPATA KAZI NDO MAANA TUNASOMA KWA KUKARIRI ILI TU-PASS MTIHANI ILI TUPATE CHETI CHA KUTUPATIA AJIRA TU AFTER THAT WE DONT LOOK BACK AT BOOKS. IN SHORT MUDA NA UHAKIKA WA KUJIKIMU UNAHITAJIKA SANA MTU KUWA CREATIVE NA MSOMI MWELEDI. MWISHO NINA OMBI KWA IDARA YA LUGHA CHUO KIKUU CHA DAR-ES SALLAM SEHEMU YA KISWAHILI NA NI JUU YA SHABAN ROBERT, JUZI TU NILISOMA JUU YA HUYU GWIJI WA LUGHA NA MAANDIKO KUWA ALIKUWA NI MTU MAKINI KATIKA HII LUGHA YA KISWAHILI NA WALA HAKUWA MSOMI SANA KUTOKANA NA HABARO HIZO NAHISI ANALIMALIZA SI ZAIDI YA DARASA LA NANE NA MTU WA DARASA LA NANE LA WAKATI HUO KUANDIKA VITABU 22 SI KITU CHA MCHEZO KWANI SASA MTU NA PhD HAJAANDIKA HATA KITABU KIMOJA. OMBI LANGU NI HILI KWANZA CHUO KIENDE KUSAFUSHA KABURI LAKE NA PILI NAOMBA SANA TENA SANA HUYU MTU APEWE PhD YA MASWALA YA LUGHA. HII KITU INAITWA POST HUMOUR NI DEGREE ZA HESHIMA HUPEWA WATU WALIOFARIKI LAKINI WAKATI WA UHAI WAO WALIFANYA MAMBO MAKUBWA AMBAYO YALITOWA MCHANGO MKUBWA KWA JAMBO FULANI NA SHABAN ROBERT NI MMOJA WAO ANASTAHILI PhD ANASTAHILI PhD KWA MCHANGO WAKE KATIKA FASIHI ANDISHI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI JAMAA ALIKUWA GWIJI NA MSOMI KWELI KWELI ANGEKUWEPO HADI SASA NINA HAKIKA ANGEKUWA PhD HOLDER NA PROFESSOR OF LINGUISTIC JAMANI TUMUENZI NI MTU MASHUHURI SANA FIKIRIA KUPEWA MBE NA QUEEN ENZI HIZO SI MCHEZO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...