Maandalizi kabambe yameanza kwa ujio wa timu ya Taifa ya Brazil itayokipiga na Taifa Stars neshno jipya jijini mnamo Dar Juni 2, 2010 kabla ya kuelekea Sauzi tayari kwa gemu lao la ufunguzi na Ureno huko Durban Juni 25, 2010.
Kwa mujibu wa tovuti ya FIFA Brazil pia itakipiga na Zimbabwe huko Harare mnamo Juni 7 kabla ya kuchupa kuelekea Durban. Mbali na timu ya Taifa yao pia Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva anatarajia kutembelea Tanzania mwezi wa saba, kwa mujibu wa balozi wa nchi hiyo Mh. Francisco Luz.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2010

    Happy April Fool!

    Vinginevyo ni Brazil 30 - Taifa Stars 0

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2010

    sasa hapa ndio mpira unatakiwa uchezwe, tutafungwa lakini chenga tutawala tu hao.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2010

    pole sana kaka yangu hata mimi nilishawahi patwa na mkasa kama wako arusha,mwizi aliniibia wallet na vitambulisho muhimu,baada ya kutoa hela akatupa vitambulisho vyangu muhimu sana,wasamaria wema wakaokota na kunipigia simu,nenda kwao na huyo kijana kaombe vitambulisho vyako bila kuwa na jazba yoyota coz najua huyo ni ibaka wala hana shida na vitambulisho,pole sana i know how u feel,na polisi hawasaidii chocho te katika hilo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2010

    KUNA "KOMENTI" IMEKOSEA NJIA HUMU NDANI.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2010

    Mechi ya Stars na Brazil itakuwa kama pambano la ndondi kati ya Tyson na mtoto mdogo wa miaka 10

    ReplyDelete
  6. itawezekanaje kucheza mechi mbili siku moja, tz na zim, au watajigawa?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 25, 2010

    sasa hapo wapenzi wa Brazil sijui tutaishangilia timu gan wallah!! TFF msianze kurafuta sifa mkaanza kuweka viingilio vya mamilioni maana usawa wenyewe mnaujua!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 25, 2010

    mdau wa pili ni kwa vipi hii ni april fool? unajuwa maana ya april fool au basi tu?

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 25, 2010

    ...Msimu wa mavuno TFF...
    Anastaafia mtu hapo!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 25, 2010

    Haya wachezaji wa kibongo nafasi ya kuuza sura hiyo, ila acheni ushamba wa kukamia mechi mkawavuja vifundo vya miguu jamaa mkawaharibia biashara yao.Fair play kama mko fit mtashinda tu, au mfanye kama timu ya morinho walipaki basi golini dk 90!

    ReplyDelete
  11. kwa nia njema tu nawaomba brazil wasije kucheza na taifa stars. stars sio kipimo cha brazil. labda ni kipimio cha kupunguza ukali wa brazil.

    pili stars imekuwa ikizipa nuksi timu zinazocheza nazo kwa maandalizi ya mashindano makubwa. walianza new zealand. walipoenda afrika kusini kwenye kombe la shirikisho wakawa urojo na kutolewa mapema.

    wakafuata ivory coast. walipenda angola kwenye AFCON wakawa asusa, wakatolewa mapemaa.

    sasa brazil ndio wanataka kuja kupata upako wa kufanya vibaya.

    kwa mashindano ya world cup mwaka huu hali ya hewa ya dar es salaam haifai kwa training. Dar ni joto, Durban ni baridi. labda brazil waende njombe.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 25, 2010

    WENZETU WANACHEZA MPIRA KISAYANSI SI WANACHEZA NA TANZANIA NA ZIMBABWE ETI NI KWA KUWA TUWAZURI NA WANAJIPIMA KIMCHEZO LA HASHA, HAPO WANACHOFANYA NI KUANGALI JINSI GANI HALI YA HEWA YA UKANDA HUU WA KUSINI MWA AFRICA INAWEZA KU-AFFECT NAMNA GANI MASHINDANONI KWENYEWE. WILL IT BE POSITIVE TO THEM OR NEGATIVE AND THEN THEY WILL SEE AND KNOW HOW TO ADJUST TO IT.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 25, 2010

    Obviously, huu ni uzushi. Naomba mdau atoe source ya habari hii, ni mtu kachukua screenshot ya habari ya ukweli mtandaoni then kaiedit kuturusha roho wabongo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 25, 2010

    NI kweli jamani, tembelea link iyo hapo chini:

    http://www.supersport.com/football/article.aspx?Id=350692

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 25, 2010

    Mechi kama hizi si za kujipima nguvu jamani, makocha hutumia game hizi kuwapa warm-up vijana wao, pia kuangalia ni wachezaji hucheza vizuri wakipangwa pamoja katika mechi, (baada ya kuwaangalia vizuri mazoezini). Lakn, mwishowe matokeo mazuri muimu, kwa kuongeza imani ya ushindi ktk timu.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 25, 2010

    masikhara!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 25, 2010

    Ebana imekaa vizuri, haya LT tupe viingilio ili mkabane kwenye migao! Tunachotaka tuone mastar!

    Mwana hiyo comment yako ya mwizi kaipost kwake! hao polis wazushi, komaa nao wanamjua, tena wakimkamata watamuulizia amepeleka wapi fito ili wakajijenge!

    ReplyDelete
  18. MkandamizajiMay 25, 2010

    Date: June 2nd, 2010

    Venue: National Stadium, DSM

    Fee: 200,000
    150,000
    120,000
    100,000
    80,000
    50,000

    Score: Brazil 12 - 1 Tanzania

    Days to count income: 14 days

    Final income count: 250,000,000 Tsh

    Aftermath: A few TFF officials quit their jobs, citing busy schedules...

    After the Aftermath: An election called for the TFF and a whole lotta other internal rumblings...

    SUBIRINI MUONE!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 25, 2010

    mdau wa Tue May 25, 02:03:00 PM kujifanya kwako kama unajuwa kiingilishi kumekufanya sisi wenzako tukucheke, sio tabia nzuri kukaa na kujifanya unajuwa ilhali hujui, ni vizuri wakati mwengine uwe mstaarabu. Soma vizuri hiyo post na gonga kwenye hiyo taarifa yenyewe upate maelezo zaidi kabla ya kuja hapa na vikomenti vya kitoto. When will you grow up?

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 25, 2010

    Brother michuzi mbona unatutatanisha sasa? hii ratiba mpya imetoka lini? maana kwa ninavyokumbuka Brazil fungua dimba yao ni tarehe 15/06 tena wanaanza na korea, sasa wewe unasema wanafungua dimba tarehe 25/06 na ureno, hii haiko sawa. Brazil vs portugal ni mechi ya tano katika kundi G. unless kama ratiba imepanguliwa.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 25, 2010

    mdau Tue May 25, 04:47:00 PM na Tue May 25, 04:30:00 PM what kind of comments are these? naona mnajichanganya wenyewe tu. Kwani kusema kujipima nguvu sio sawa na kusema mechi ya kirafiki? au utasema hii sio mechi ya kirafiki? sasa ulitaka tuiite mechi gani?

    Kwa taarifa yako tu wewe Tue May 25, 04:30:00 PM kwa wakati huo watakapokuwa wanacheza na taifa stars itakuwa muda wa kuwasilisha majina ya wachezaji watakaocheza world cup ushapita kila atakaekuwepo katika timu itakayokuja tanzania atakuwa yumo katika final list ya brazil.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 25, 2010

    Asante Mkapa kwa kutujengea stadium la ukweli...ingawa shukrani yetu ni kulipaka choo ukutani.

    Asante JK kwa kumleta Maximo.

    Asante Maximo kwa kutupigia debe mpaka Dunga akaleta timu.
    Nasubiri kwa hamu siku Robinho atakapokabwa na Nsajigwa, Luis Fabiano na Cannavaro. Kwa upande wa ushambuliaji Mrisho Ngassa ataonyeshana kazi na Michel Bastos huku Mgosi akimwonyesha kazi Lucio. Kati Humoud atakuwa akionyeshana kazi na Felipe Melo na Gilberto Silva. Lazima Julio Cesar akaokote mpira wavuni. Pia Maximo lazima azomewe tena manake hata afanye nini watu wanaona hakuna jema.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 25, 2010

    TFF wapi mpo? david mwakalebela tupe confirmation iyo....muhimu ni kujua brazil waja, kuhusu matokeo juu ya game kati yao na sisi ni mbele na mbele...

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 25, 2010

    HAPO KAMA NI KWELI BASI UJUE IKULU ITAFUNGWA WIKI MBILI ......MOJA KUZUNGUMZIA HUO UJIO NA YA PILI KUJADILI MECHI ILIVYOKWENDA HUKU DAFU HILOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO LINAKUWA CHACHU...SASA 1500 UPATE DOLA MOJA. SASA WESE SHUGHULI YAKE MBONA TUTAPAKIIIIIIIIIIIIIIIII.
    IKIJA UCHAGUZI AAH TULIWALETA BRAZILI, IVORY COAST,,.....VIKAANGA JUA VIMEONGEZEKA WEWEEEE CCM JUU, JUU JUU JUU ZAIDI.
    NA KIBANO KINACHOENDELEA HUKU ULAYA UJUE OMBAOMBA WOTE HAWATAKIWI, WATALII MMMMMMMMMMMMMHH SIJUI KWA HIKI KIBANO SIWAONI WENGI. SASA HIVI TAYARI WASHATUPIGA PANGA DOLARI MIL 200 ZA BAJETI YA MWAKA HUU. WAKIANGUSHA LINGINE DU TUTATAFUTANA............LAKINI SI TUNATEMBELEA X5 BWANA.....WHO CARES TWENDE TUKAMCHEKI KAKAAAAAAAAAA!!
    TUBARIKIWE!!!!
    MZAWA

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 25, 2010

    Kwa upande mwingine, vipi kuhusu utalii. Tafadhali, wahusika (nawanyooshea vidole watu wa Wizara ya Utalii) mtumie hii fursa ipasavyo. Brazil itakuja na wanahabari kutoka kila kona ya dunia.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 25, 2010

    WATZ NI TU BUMBAFU KWELI BADALA YA KUFAGILIA TIMU YETU TUNAFAGILIA ZA WATU, NDIYO MAANA MAENDELEO HAKUNA. LAZINA TUTAMBE NA TIMU YETU ILI HATA KIWAPA MOYO KULIKO KUWAKANDA, THIS IS NOT NORMAL!

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 25, 2010

    Japo kuwa si mganga wa kienyeji na pia si mnajimu kama sheikh Yahaya, naweza tabiri kuwa kama Brazil itatua Dar na kucheza na Taifa stars, basi wajue kitawakuta kama kilichowakuta Ivory cost kwenye mashindano ya kombe la club bingwa Africa walitoka mikono mitupu.Na Brazil nao wategee hayo kwenye mashindano yajayo huko South. Waswahili husema Ukitembea na mwizi nawe utakuwa mwizi, Na UKICHEZA NA WALOZOEA KUFUNGWA NAWE UTAFUNGWA!!! Tusubiri tutajionea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...