SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI (TUCTA) LEO LIMETANGAZA KUSITISHA MGOMO WAO ULIOPANGWA KUFANYIKA KESHO NCHI NZIMA.

VIONGOZI HAO WA TUCTA WAMETOA TAMKO HILO MUDA MFUPI ULIOPITA KATIKA OFISI ZA SHIRIKA LA KAZI LA KIMATAIFA (ILO) MTAA WA MAKTABA STREET JIJINI DAR, AMBAPO RAIS WA TUCTA BW. OMARY AYOUB JUMA, AKIWA NA NAIBU KATIBU MKUU BW. NICHOLAUS ERNEST MGAYA WALIPOKUTANA NA WANAHABARI NA KUTOA TAMKO LA KAMATI YA UTENDAJI TAIFA KUHGUSU MGOMO SHINIKIZI WA WAFANYAKAZI NCHI NZIMA (PROTEST ACTION).

"TUNAWARIFU KUWA MGOMO (PROTEST ACTION) YA KESHO IMESITISHWA KWA MUDA", INASEMA TAARIFA HIYO, NA KUONGEZEA KWAMBA "TAARIFA KAMILI KUHUSU SHUTUMA ZILIZOTOLEWA NA MHESHIMIWA RAIS KWA VIONGOZI WA TUCTA ZITATOLEA HIVI KARIBUNI..." ILIMALIZIA

HATUA HII INAKUJA SIKU MOJA BAADA YA JK KUWATAKA WASIGOMEWAKATI AKIWAHUTUBIA WAZEE WA DAR ES SALAAM UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE HALL.

KATIKA HOTUBA HIYO JK ALITANGAZA KUFUKUZA KAZI YEYOTE ATAKAYEGOMA, AKAWAITA TUCTA KUWA NI WAONGO NA WANAFIKI WAKUBWA, NA KUWATAJA KAMA WACHONGANISHI NA WATU WENYE HIANA.
PAMOJA NA KUSEMA YUKO TAYARI KUKOSA KURA KATKA UCHAGUZI MKUU UJAO KULIKO KUDANGANYA KUHUSU HALI HALISI ILIVYO, JK PIA ALIONYA KUWA ATAYEFANA FUJO ATASHUGHULIKIWA NA KUNAINISH KWAMBHA KIMA CHA MISHAHARA CHA SH. 315,000 KILICHOPENDEKEZWA NA TUCTA HAKILIPIKI NA MKUMFANANISHA BW. MGAYA NA NDEGE KONG'OTA KWA KUTAKA KUCHUUZA WENZIE.

HABARI KAMILI NA TASWIRA BAADAYE KIDOOOOGO....
ILA HABARI NDIYO HIYO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2010

    Hata ukisitishwa, TUCTA sogeeni mbele, madai yenu ni ya haki na Rais jana alitoa mawazo yake tu-He stands to be corrected!. hata hivyo kilio chenu kimesikika na ushindi ni wenu! Mgaya umeshaingia kwenye Hansard na utang'aa kama yule bwana aliyeitia serikali ya Mwalimu mfukoni enzi zile. Tunaelewa migomo Tanzania inavyozimwa, haswa kama huu wenu uliokuwa karibu na WEF hii yote ni siasa! pigeni moyo konde mjipange tena lakini be rest assured you are the winners na ingewezekana tupate debate ya Rais na Mgaya basi sisi wananchi tungejua ukweli upo wapi kwani jana tumepata upande mmoja ambao mimi siwezi kuutegemea kwa asilimia mia! wataalamu wa sheria wataniambia.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2010

    Pamoja na TUCTA kusitisha mgomo, naomba kumkumbusha Mh Rais yafuatayo:
    1. Naamini alikuwa na nia njema lakini ujumbe alivyoufikisha haikuwa njia sahihi kwa kiongozi wa nchi inayothamini demokrasia na utawala bora
    2. Nchi haiendeshwi kwa vitisho na sisi tuliomchagua hatujamtuma kutumia kodi zetu kutishia wafanyakazi kwa mabomu ya machozi, maji washa wala risasi.
    3. Watanzania tuna utamaduni wa kutatua migogoro kwa njia ya majadiliano na si ubabe wa kijeshi- au amri moja.
    4. Keki ya taifa igawanywe sawa kwa wote na si posho za wabunge, vigogo na wawekezaji peke yao. Gap ya walionacho na wasionacho ni kubwa mno!
    5. Mjadala wa haki na mafao ya wafanyakazi uende kwa kasi kama ilivyokuwa ktk maslahi ya wabunge.
    6. Mabilioni ya JK, Kagoda, Richmond, Meremeta na EPA yarejeshwe
    7. Kilimo Kwanza- Siasa ni kilimo??!!muda wa kazi upunguzwe ili wafanyakazi waanzishe bustani mitaani na majumbani mwao kujiongezea kipato.
    8.Najitolea kumpa Prof Kapuya Tsh 315,000/- kwa mwezi mzima, aishi yeye na familia yake kama sehemu ya majaribio- bila mafao yoyote mengine!

    TANZANIA BILA VITISHO-INAWEZEKANA

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 04, 2010

    A coward gets scared and quits. A hero gets scared, but still goes on.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 04, 2010

    mbona jk hakuainisha mshahara wake, wa mawaziri wake, manaibu mawaziri wake, makatibu wakuu wa wizara, manaibu katibu wakuu wa wizara, na wabunge pamoja na marupurupu wanayopata.
    katika hao wafanyakazi????

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2010

    Wametishwatishwa hawa, wakaambiwa toeni tamko la kufuta mgomo, tuendelee na mazungumzo tuone tutawaongezea ngapi. Ila mkiendelea na mgomo wenu tutawahaulisha/tutawafuta kwenye sura za wananchi na wafanyakazi hasa ninyi kina Mgaya. Unajua tukitekeleza maombi yenu kwa shinikizo la mgomo basi tutashindwa kutawala maana kila mtu atajua kuwa hii ndiyo njia muafaka.

    Hivi vipi na ule mgomo wa Wahadhiri wa vyuo vikuu unakuwaje?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 04, 2010

    jaman watanzania tubadilike! Tusiwe bendera fuata upepo especially kwa baadhi ya watu amabao wanajidai wana uchungu na wanakipenda sana chama utafkiri wamenyweshwa maji ya bendera...nadhani wanajijua, hawa si wengine bali ni UVCCM amabao kuna baadhi wametoa comments kupitia blog moja maarufu bila kufkiri kwamba wao ni wasomi na ni vijana hivyo suala la mh.Raisi mimi sijaliafiki na kwa position yake hajatenda haki n i didnt expect such thing from mr.president! Inabid akae tena upya pamoja na timu yake nzima kufkiria upya juu ya speech yake ya jana akiwa kama raisi!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 04, 2010

    Kilichonishangaza kuliko vyote ni aina ya wazee waliokuwemo ukumbini maana jinsi walivyokuwa wakivinogesha vijembe vya mheshimiwa, nilipata wasiwasi kama kweli wazee wa siku hizi bado wana busara. Au hawakuwa wazee? Mheshimiwa alitumia mkwara kusitisha maandamano, bila shaka mkwara huo umeendelea hata baada ya pale. Nawapongeza TUCTA kusimamisha mgomo maana baada ya ule mkwara hata wafanyakazi wenyewe wasingediriki kuitikia, isipokuwa wachache. Tulizeni boli, ngoma hii iendelee baada ya mkwara kupoa. Nilifurahi mheshimiwa alipombatiza waziri Kapuya jina analostahili... "Gramaphone"!! VIVA TUCTA!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 04, 2010

    jamani tubadilike

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 04, 2010

    msije mkabambikiwa mikesi ya uongo au wakakolimba hilo linchi wakiona umewazidi kete wanatumia ubabe hivi huyu osama kwa nini hatupi bomu maeneo flani hapo bongo??

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 04, 2010

    msiwe na wasi wala huzuni TUCTA wanainchi walio wengi tuko nyuma ya hili sana tu,,,na mimi binafsi hii naiona ndio HEKIMA NA BUSARA ya nyie viongozi Mr Mgaya na president maana kujibu kwa jazba za kibabe kama JK mngeonekana na nyie wa ovyo tu
    mmetumia ushujaa na akili ya hali ya juu sana katika kutatua hili...ushindi ni wa wafanyakazi wa nchi ya tanzania na aluta kontinua....

    kama usoshalisti ulikufa urusi nani atayezuia mabadiliko sehemu yoyote duniani???ata kunataka kutokea utawala wa kidikteta wa JK...yana mwisho haya na watalipa hili kosa kubwa sana la kutusi wafanyakazi namna ile na kiongozi aliyechaguliwa kisheria namna ile

    yani leo wafanyakazi wanafanyanishwa na mbayuwayu?wanaitwa wanajifanya wanafiki na kula mali za wengine?kwamba muajiri mkuu anaweza kufuta kazi wote?na kuitwa wezi?na kutishiwa nguvu ya jeshi?NA KURA ZA WAFANYAKAZI 350,000 haziitaji na hawamuwezi ng'oo?

    TUCTA kweli tunasubiri tamko lenu hilo baadae ili tujue wapi tunaanzia katika nchi hii

    kweli akili ni nywele

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 04, 2010

    Hili ni Jambo lakawaida tu.
    Sio la kushangaza uma hata kidogo.
    Uongozi najua umesitisha mgomo kwa maslahi ya Serikali and sio Taifa.
    Tufike mahali tuache kuficha jipu wakati likitumbuka harufu Itatuumbua tu.
    Kama munasubiri Hao waliokaa Mlimani City kujadili uchumi , then ndo mahala pake hapo wajue nchi waliokuja inahali mbaya. Mimi huwa nashindwa sana kuelewa tunakuwa wepesi kuiga Vitu kutoka nje hadi tabia Za Watu wa jinsia moja kurithishana kimapenzi lakini tunashindwa kuiga misimamo yakudai haki zetu kimaendelea.
    jamani waTanzania wenzangu tubadilike kiakili na kimwelekeo hasa katika kudai uhuru wa Maisha salama na bora kwa kila moja wetu.
    Huku Tunapoiga mengine huwa wanafanyaga hapo kwenye mkutano ndo mahali pakuonyesha uozo wa hao watu wao waliovaa suti kuwakaribisha hao wageni.
    Things won't work anymore kwa style hiiii.
    Regards,
    Mwanaharakati.

    ReplyDelete
  12. Kudadadek!
    Tehe teh tee te!
    JK Hongera. Umechimba BITI mpaka jamaa wamenywea. Tehe tehe tee!
    Walikuwa wanakuona ukitabasamu kila saa walidhani huwezi kuchimba Mkwara. Tehe teh tee! Kudadadek!

    Big Up Kikwete. Huo ndio urais bwana. Sio kila mtu anakuchezeachezea na kukutunishia msuli tu.

    Kudadadek! Safi sana JK. Kura yangu Oktoba umeipata Mwanangu.

    Nipe TANO mwanangu!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 04, 2010

    MIMI NINAUNGANA NA MGAYA KWANI SERIKALI HAIWAJALI WATUMISHI WAKE INAJIJALI YENYEWE KWA SAFARI ZISIZO NA TIJA KWA KURAMBA KODI ZA WALALA HOI. HUYU MHESHIMIWA WETU USANII HAJAANZIA HAPA KWENYE MGOMO WA WAFANYA KAZI YEYE NI MSANII HASA HANA SURA YA UTENDAJI. NASHAURI BW. MGAYA HUU MGOMO UAHIRISHWE LAKINI PASIPOTIMIZWA MADAI YETU TUUENDELEZE.
    KODI SISI TUNAKATWA KILA MWEZI HATA MSHAHARA WA 80,000/= LAKINI WENYEWE KAMA WAFANYA BIASHARA WENYE MTAJI WA MILIONI 19 NA WANASIASA HAWAKATWI KODI, SI USANII HUO??
    NCHI IMETAWALIWA NA SIASA ZAIDI KULIKO UTENDAJI. MUNGU IBARIKI TANZANIA, IBARIKI TUCTA NA MBARIKI BW. MGAYA.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 04, 2010

    Hivi kama kila mfanyakazi (350,000) wana tegemezi wastani wa 10 wenye umri wa miaka zaidi ya 18, kwa hotuba hii ya JK, ikiwa wafanyakazi watawashauri tegemezi wao kutompigia kura JK (kama yeye alivyotaka) maana yake JK atakosa kura zaidi ya 3,500,000 octoba au?

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 04, 2010

    Watanzania wenzangu, nadhani sasa ni muda wa sisi kuungana na kuwa kitu kimoja katika jitihada zinazofanywa na viongozi wetu za kukuza uchumi wetu. Uchumi ukikua, hayo mengine yote yatafuata! Migawanyiko haitosaidia chochote!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 04, 2010

    COWARDS!!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 04, 2010

    Mbona Maoni yangu yote mmeyakataa kuyatoa.

    Hii globu imeshakuwa ni sehemu ya propaganda za serikali.

    Mimi nilikuwa nashangaa iweje JK amshambulie Mgaya kibinafsi? Kwanza Raisi wa TUCTA ni mtu mwingine Kabisa. Jamani mambo ya ubaguzi wa Itikadi za kidini awamu ya nne vipi??

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 04, 2010

    Jamani nafikiri kwa watu waliongelea hili swala na pia kuonyesha hali ya kusikitishwa naona wana haki. Kwa wale ambao wanaona Mkuu wa nchi ana haki ya kusema hivyo nafikiri nao wana haki ya kufanya hivyo kwani hawa watu wanajulikana wana toka wapi na wana kwenda wapi. Kwa wale wote ambao wamesikitishwa na majibu ya mkuu wa nchi basi nawashauri kufanya jambo moja muhimu nalo ni kuhakikisha katika uchaguzi mkuu ujao CMM haipati kura yao. Na hii ni pamoja na familia zao wasitoe kura yoyote kwa CCM. Hii ndiyo siraha iliyobakia!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 05, 2010

    Tutaendelea kukanyagwa na viongozi hawa mamluki kwa kuwa ujamaa ulishatulemaza kiakili kiasi kwamba tukichimbwa mkwara kidogo tu tunanywea. Eti JK kaongea na "wazee" wa Dar. Hawa ni wazee nuksi wasiochambua hoja wao kazi yao ni kuuunga mkono kila kisemwacho na JK. Kilichofanyika ni kuhairisha tatizo. Dawa yenu ilishachemka bado kunyweshwa tu!

    Michuzi bania komenti kama kawaida yako!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 05, 2010

    Watanzania wenzangu, nilisikiliza sana hotuba ya Rais, lakini sikuona kitu cha maana alichokuwa anaongea kwani alishupalia point moja na vitisho vingi na kejeli za kila aina kwa wafanyakazi.

    Nilimshangaa sana JK kufikiri kwamba suluhisho la mishahara ni kukopa hivi hawezi kufikiria njia mbadala ya kuboresha uchumi na kuongeza kipato kwa watanzania zaidi na kuombaomba!

    Rais muda mwingi wa hotuba utafikiri alikuwa akiwasuta viongozi wa TUKTA kama vile watu uswahili wanasutana, alichefua sana sikuamini kuwa kumbe mtu anayetuongoza nchini ni wa namna hiyo.

    Viongozi wa TUKTA mmetumia busara sana kusitisha mgomo kwani kama alitangaza kutumia jeshi lake akishahau kuwa hata polisi wake hawalipwi vizuri, madhara kwa wafanyakazi yangekuwa makubwa sana na mngebeba lawama.

    Watanzania wenzangu tuonyeshe kutokubaliana na hali hii kwa kupiga kura tu.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 05, 2010

    Hivi ni wazee gani wasio na busara ya kupima hoja? maana kazi kubwa kwao ilikuwa kuchekacheka na kuunga mkono kila linalosemwa!!
    kwa kawaida wazee umwonya hata msemaji mkuu ili aendane na wenzake na kutumia busara ili kumaliza tatizo. kama ndio wazee wenyewe ni wa namna hii, Tanzania ina kazi kubwa kufikia maendeleo.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 05, 2010

    Dah! Ama kweli Wazee wa Tz ni noma,yaan wanshangilia tuuu.Hivi hawajui hizi kazi tunazo fanya na kamshahara kiduchu ndo tunawatunza wao.Hivi tukiamua kuwachenjia tusiwatunze tuwaambie mshahara hautoshi,wataenda serikalini wakaombe watunze eboh.Wazee fikirienini kwanza.Ila nahisi wale walikuwa washabiki tu kama mpirani au wengi wao ni unshuled(hawajaelimika) na hawajui inji inakwendaje maadam wamekula nakulala basi.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 05, 2010

    kweli hii inji ni ngumu!

    nilikuwa nazunguka zunguka kwenye pub wakati mheshimiwa anahutubia na nikagunduia waTZ wengi tunalemazwa na statu quo! yaani madaraka. si raisi, si wananchi...kwanini....wakati raisi anahutubia with full mamlaka watu wanashabikia kama wanavyoshabikia mshindi kwenye WWF!! raisi mwenyewe amelemazwa na status quo pia kwani hajui kuwa magwanda yaliyomzunguka si kitu bali busara kuu toka kwa Mungu ndio jambo la msingi....ni kwa mara ya kwanza kusikia mwanasiasa akizikataa kura...au kwa sababu anajua ni mtindo gani utatumika?.Huyu mgaya amemkosea nini hadi amtukane kiasi hiko mnafiki? hana akili? je akiamua kumfungulia kesi ataruka kweli? yeye nani alimpa akili zaidi? je baba ukaona watoto wako wakaja na hoja utukane tu?

    wafanayakazi madai yao yalioainishwa ni ya msingi. kitu kinachowafedhehesha WAFANYAKAZI ni kwamba serekali imekuwa ikidharau mazungumzo na mara zote kuja na rules badala ya negotiations..

    Mh Jk umesahau katika chata yako katika yale mashati ya kijani kuna jembe na shoka? shoka linawakilisha nini? kweli chama kimepoteza dira sasa!

    Mh.raisi kaa chini na kina mgaya, sie tunawaheshimu, pia tunakuheshimu,kama hutegemei wakulima na wafanyakazi wako tuijenge inji, basi jaribu wawekezaji!

    KIITIKIO

    ukienda kwa wanyama anaitwa Simba wa Yuda!!!...ukienda kwa mimea yeye ni mti wa uzima....kweli yu hai!!! mtetezi wangu Yesu anaishi leo..kweli yu hai!!!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 05, 2010

    AAH WATANZANIA BWANA!! KILA KITU MNAJUA!! MARA OHH RAISI MPOLE, OHH SIO MKALI. SASA MNATAKA NINI??

    MIMI NAMPONGEZA RAISI NA NIMEMPENDA ZAIDI BAADA YA ILE SPEECH, MAANA HUWEZI KUTATUA MATATIZO YA KITAIFA KWA MGOMO, NA KILA KITU TUMEAMBIWA. TATIZO WATANZANIA TUNAPENDA KUONGOPEWA, MH RAIS KATUAMBIA UKWELI KUWA KIWANGO CHA LAKI 3 HAKILIPIKI! SASA MNAPIGA KELELE YA NINI?? SI NDIO UKWELI?? WEWE UNAYEONA NI SIASA, UNGEGOMA UONE!! AHAH

    BIG UP MH RAISI. MIMI, FAMILIA YANGU, NDUGU ZANGU NA RAFIKI ZANGU WOOTE TUTAKUPIGIA KURA. ENDELEZA MAPAMBANO MKUU. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MBARIKI MH KIKWETE.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 05, 2010

    Duuuh.wadau wenye akili woote mtakubaliana na mimi kuwa Mh Kikwete kaleta Democrasia Tanzania. maana wadau mpo huru kuongea na wengine naona kama mmeanaza kumtukana Rais vile!! SASA MJUE KUWA MH RAISI HANA MATATIZO NA NI BABA WA DEMOKRASIA. MAANA ENZI ZA MKAPA SIJUI NANI ANGETHUBUTU KUTOA KAULI CHAFU KAMA HIZI. Hata Ankal asingethubutu kuzichapa hewani!!! ahahaha Mh Rais Big Up, Tutakupigia Kura tena zaidi ya zile za 2005.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...