Hellow kaka michuzi,
Mimi ni mdau wako wa muda na nina ishu ambayo nadhani ni vyema iongelewe kwa ufasaha, ni swala la the relationship that Tanzanian kids have with their parents.
Ni kweli kwamba ukiangalia wenzetu, wana parent-child- friend relationship yaani mzazi ni mzazi na pia rafiki kwa mtoto wake na nadhani hiyo inahitajika sana katika ulimwengu huu wa sasa kwa sababu kuna mengi yanaendelea na mtoto unashindwa kumwambia mzazi wako kwa sababu ya kuogopa atasema nini.
Mimi nina miaka 16 na kwa sababu tunaishi katika ulimwengu uliotawaliwa na American culture tume adapt mengi na mengine labda hayajazoeleka kwenye jamii yetu. Lakini labda kwa wenzetu ni kawaida ngoja niwe mkweli.
Kama swala la boyfriend girlfriend etc linapigwa vita sana hasa shuleni. Ndio, haifai kwa sababu mara nyingi inamfanya mtu adrop kwenye masomo lakini inatokea kwa sababu umri wenyewe ni wakati mgumu na mengi hutokea na nadhani kama wazazi mngekuwa wazi then sisi tungesema. Na nadhani ingekuwa vyema kwa sabau tungepata ushauri straight foward lakini unafikia situation haujui hata uanzaje watu wanafwata ushauri wa marafiki zao ambao mara nyingine haufai.
Mimi napenda tu kuomba watu walifikirie hili swala bayana kwa sababu linaweza likaonekana ni dogo lakini the situation sio nzuri kwa kweli na mimi naongea kwa sababu niko shule na mambo haya yanatokea. Watu hawajui cha kufanya,inabidi wazazi muanze kuwa wazi na watoto wenu la sivyo,tutaishia kupotoshwa.
Mdau Shuleni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

 1. AnonymousMay 25, 2010

  Hebu kelele huko!.....eti "boyfriend" na sijui "Girlfriend".....tulia usome!!

  ReplyDelete
 2. AnonymousMay 25, 2010

  Asante mdau kwa kuitoa hii,mimi ni mwalimu kitaaluma ingawa sasa sifundishi.Nimekuwa na mzigo sana wa kufundisha vijana hasa katika eneo hili,nimeendesha sana semina hizi kwa vijana mashuleni na makanisani,nimeandika mambo mengi juu ya changamoto za vijana,na niko mbioni kutoa kitabu ili kisaidie wengi( ila si leo wala kesho)Kama hutajari njoo kanisa la Tuangoma christian center (TICC)-TAG au piga simu ya mchungaji 0719964124 anaitwa mchungaji Silomba atakusaidia sana juu ya tatizo hilo.

  ReplyDelete
 3. Paul KabewaMay 25, 2010

  Mzazi si lazima akuzae hata waalimu ni wazazi wako wasikilize na nina imani wanaliongelea sana swala hili.Tafakari... chukua hatua

  ReplyDelete
 4. AnonymousMay 25, 2010

  Hebu Jaribu kuwa 'focused' na utoe kile unachotaka kufikisha katika jamii. Hao wenzetu ni nani na wanafanya nini katika lipi na linafaida gani ukilinganisha na sisi tusiofanya hilo na badala yake tunafanya lile?

  ReplyDelete
 5. AnonymousMay 25, 2010

  Mdau asante kwa mada.familia inaanzia nyumbani na sio mtaan!!.ni kweli wazazi wengi wamekuwa hawana time ya kutosha kukaa na watoto/familia zao.kuwapatia kila kitu/mahitaji haitoshi!, ila kukaa nao na kufanya urafiki na kujua shida zao na kuwapa ushauri ukiwa kama mzazi na wakati huo ukiwa kama rafiki wa karibu sana hilo ndilo jambo la msingi sana.kama wazazi wakilishupalia hili basi familia zitakuwa na misingi mizuri.Tuondoe fikra kwamba mambo fulani hayapaswi kuongea pamoja na watoto.kama ulisipomfunza nyumbani atafunzwa na jamii.. ila ukimuweka wazi na mkikubaliana kwa pamoja hata akienda kwa jamii atakumbuka kuwa hata mzazi alisemaga hili na yeye atakuwa muwazi tena kuja na kusema aliyokumbana nayo huko nje..ila watoto wanatofautiana.. kuna wengine hata uwashauri vipi wanakwenda njia potofu.. ila tukiwa kama wazazi kila mtu na afanye upande wake.Nasisitiza tena malezi bora huanzia nyumbani.swali!! Je umewasalimia wanao leo kwabla ya kuondoka nyumbani na kwenda kazini! Je huwa tuna ratiba ya kuongea na watoto wetu kila mara!

  ReplyDelete
 6. AnonymousMay 25, 2010

  Michuzi naomba email yako uipost nina jambo nataka kutuma.

  ReplyDelete
 7. AnonymousMay 25, 2010

  Mtoto soma, mambo hayo yatakuja tu.

  Hilo la ulaya unalolisikia kuhusu urafiki wa mtoto na mzazi ni wa kwenye mdomo tu.

  Ndiyo maana Ulaya kwa mfano Uingereza kuna old people's home. Yaani mzazi wako akizeeka kijana/binti wako anampeleka mzee/mama akaishi nyumba ya wazee.

  Kijana (mtoto) anaona taaabu kuishi na wazazi wake wazee, hivyo anampeleka huko nyumba ya wazee, halafu anamtumia kadi' mum/dad I love/I miss you so much'. Hii yote kwa kuwa kijana/binti hataki 'bugudha' ya kuwalea wazazi wake wazee.

  Hivyo ya wazungu waachie wazungu. Ila kama ulivyosema itabidi vijana wa miaka 16 Tanzania wawe wanapelekwa kambi jandoni, kurudisha elimu ya kijamii ikiwemo wazazi wako wakizeeka uwalee nyumbani mwako pamoja na familia yako.

  Huko kambini jandoni mtafundishwa maadili yetu ya kiafrika kama kuwa na subra uchaguliwe mchumba, nini maana ya kuitunza na kuilinda familia yako, kuwaheshimu wazazi, kumpenda mkeo na ndugu zote.

  Mdau
  Ughaibuni

  ReplyDelete
 8. AnonymousMay 25, 2010

  hey we dogo mwambie kakamichuzi shikamoo basi. Hata hilo mnataka watoto wadogo kulipinga nalo?

  Kama una miaka 16 basi hingera umeweza kujieleza vizuri sana. kama vijana wote wangekua na akili kama zako nadhani wazazi wangeweza kuwaamini.

  Back to ur issue. Ni relationship gani u're talking here. Kwasababu wazazi wetu hawawzi kubadilika kabisa. Miye mwenzio mkubwa wako lakini bado wako nyuma.

  Ila ninachokuambia tafuta mentor. Mtu mkubwa kuliko wewe uncle, aunt au walio mbele ya shule kabisa kwa vile huyo atakusaidia kimawazo. Mliolingana hamtaweza kuelezana chochote wakati testosterone zikiwa zimepanda. Na jaribu tu kuongea na mama na baba polepole kumtambulisha rafiki yao kwanza huwezi kujua wao wala sio wakali kama unavyofikiria.

  Good luck

  ReplyDelete
 9. AnonymousMay 25, 2010

  Wewe nenda kasome shuleni, achana na mambo ya Amerika. Wamerikani wenyewe wanatamani wangekuwa na tabia kama za Afrika halafu wewe unataka kuiga za kwao.

  Swala hili ni mmoja ya mambo ya culture and ethic za kila jamii, haya ni mambo ambao labda wewe mtoto wa shule ya sekondari au msingi bado hujui.

  Kwa kifupi wewe fuata jamii na watu wako wa karibu wanafanya nini, mambo ya wamerikani aachana nao. Wahenga walisema ukiiga tembo kunya utapasuka msamba.

  ReplyDelete
 10. USIWAZE NGONO DOGO,,,,NA WALA HILO SIYO WAZO LA KUJADILI HAPA TUNA MAMBO MAZITO YA KUJADILI SIYO LA NGONO KATIKA UMRI WAKO HUO,,,BORA UNGEZUNGUMZIA MAMBO YA MASOMO SIYO BOYFRIEND NA GIRLFRIEND,,,,NADHANI NI JINI MAHABA LINAKUNYEMELEA,,,,WAZAZI WAKO WAKUWAHI....AND STOP IT.OK

  ReplyDelete
 11. AnonymousMay 25, 2010

  DA KIJANA POLE SANA. HATA HUYO BABA YAKO HAYAJUI HAYO KWANI BABU YAKO HAKUMFUNDISHA. MAMA YAKO ANA AFADHARI KIDOGO KWANI NYANYA YAKO ALIMPELEKA KUCHEZEWA UNYAGO. HIVYO NDIO MAANA UKIMUULIZA BABA YAKO ATAKUA MKALI KWANI HANA JIBU....

  ReplyDelete
 12. AnonymousMay 25, 2010

  Mdau wa Miaka 16 binafsi nadhani uhusiano kati ya Mzazi na Mtoto ni swala la watu wawili. Hivyo mzazi ananafasi yake kama mzazi na mtoto pia ananafasi yake kama mtoto. Katika mila za kiafrika wazazi walio wengi ikifika katika maswala ya mahusiano (wenyewe mnaita mapenzi) walifunzwa na mashangazi, bibi, babu au katika unyago na siyo na wazazi kama ilivyo sasa. Hivyo ni muhimu ukawaelewa. Mapenzi inanafasi yake na ni mazuri lakini katika umri mdogo athari ni nyingi pengine kuliko mazuri. Kuna hatari ya kupata mimba kama wewe ni msichana na kwa kijana unahatari ya kuwa mzazi ukiwa na umri mdogo ambayo pia inaweza kukuathiri katika maisha ya baadaye. Kama wazazi hawapo "free" nawe usiwalaumu ila naomba uchukue nafasi yako kama mtoto na uweze kuwasiliana na mjomba au shangazi au ambaye unauhuru naye wa kujielezea ili akushauri. Pia naamini kati ya baba au mama kuna mmoja ambaye utakuwa naye huru zaidi hivyo unaweza kumuuliza maswali fulani. Kumbuka kwamba ujana ni nafasi nzuri ya kujenga mipango ya baadaye ili kwa baadaye uweze kuwa mtu mwenye kuheshimika na kutegemewa katika jamii. Kwa umri wako pengine ni bora ukaendekeza nguvu zako katika masomo maana ukianza maswala ya mapenzi (miaka 16) huenda usiweze kutimiza malengo yako mengi kama kumaliza elimu na kuingia kwenye taaluma unayopenda. Asante. Mdau Suleiman

  ReplyDelete
 13. Kijana mada yako ni nzuri na inaguvu kabisa.lakini mimi nataka kuungana na wadau wachache hapo juu kua,

  mambo ya ulaya waachie wenyewe.Uwazi ukizidi sana kati ya wazazi na mtoto heshima inapungua.wewe soma na sahau mambo ya marecani.kwanza nataka kukwambia jivunie kua mtanzania.

  Kwasi hakika sijui taifa lolote lenye tabia nzuri kama sisi.
  mme wangu mimi haogei na baba yake kwa miaka kadhaa sasa,nikuiliza sababu.Eti baba yangu hakuja mahakamani kuniona.

  sasa kweli watanzania wenzangu je hi ni sababu kutoongea na baba yako kisa hakuja katika kesi yako?
  tangu nimeolewa na huyu baba sijawahi kumwona baba mkwe wangu,sasa kweli mdogo wangu wewe unataka kuiga haya ya ulaya.

  tafadhali sahau kabisa ya ulaya.

  mdau
  Usa

  ReplyDelete
 14. AnonymousMay 25, 2010

  kijana kwanza hongera sana kwa maelezo yako yote ni mazuri sana .sikuzote unaambiwa usiige jambo kabla hujalifanyia kazi.
  ukweli wenzetu wa ulaya yote mwisho wao unakuwa mbaya kimaadili.
  kwanz hakuna heshima pili ikifika miaka 18 anamaamuzi yake lakini bado anaishi na wazazi wake. kazi hana na anawategea kimasomo huoni makosa hayo.
  kama msichana hana time ya kusaidia wazazi na ataingia na mmvulana chumbani nahuku anamuimiza mama apike haraka.
  mvulana halikadhalika ni sawa tu.
  na hakuna masomo hapo hasara.
  na atawadhamini wazaziwake wakiwa na kitu anajua wakizeeka atachukua mali yeye na tawapeleka sehemu yakulelewa ili atumie pesa vizuri je kuna mapenzi na heshima na imani hapo?
  tukirudi swala lako nikweli wazazi lazima wawe karibu na watoto wao ili kuwapa elimu ya maisha lakini sio kukubali kama wazungu wafanyavyo asilimia nyingi wanapotea tunawona huku. ahsante mdau

  ReplyDelete
 15. AnonymousMay 25, 2010

  We dogo unataka kupinda! unataka baba yako awe rafiki yako akufundishe kutongoza au? halafu ukishajua ukapata demu uwe unamsimulia jinsi unavyomfaidi huyo demu! marafiki wa umri wako ndo wanasimuliana vitu kama hivyo. Fuata maadili ya kiafrika dogo na utaifaidi dunia vinginevyo utajuta kujua malezi ya wazungu.

  ReplyDelete
 16. AnonymousMay 25, 2010

  Kijana tulia, mie mwenzio nimefanya madudu hayo baada ya kumaliza university, kile kipindi cha kusubiria majibu ya mwisho kabla ya kwenda mtaani,na nweza kusema kuwa ilinisaidia sana kuwa 'focused' kwenye masomo yangu nafikiri usipende kuendekeza masuala hayo hata kidogo.


  Nkabo

  ReplyDelete
 17. Shukrani kwa barua yako mdogo wangu, bila shaka wewe ni mtu mwenye kutafakari mambo. Mada yako ni nzuri na ni ukweli mtupu!

  Now, to all of those who say you should just drop all those "American cultural influence" au Western culture as a whole...I say BE REAL. Hii ni sawa na wale wanaopinga wanafunzi kufundishwa kinga ya ukimwi kwa condoms. Most of these kids ARE sexually active already!!.

  Back to the subject. Wazazi naona wanakeep distance kubwa baina yao na watoto zao. Triple F are the magic words when it comes to parenting: be FIRM, FAIR, and FRIENDLY!. Mtoto hapaswi kuogopa mzazi....anatakiwa kuheshimu wazazi. In true respect there is love and trust. Mtoto anatakiwa aweze kuwa wazi kueleza mmzazi waki jambo LOLOTE linalomsumbua roho au akili bila kuhofu kuwa judged au kuadhibiwa. Mzazi anatakiwa awe ni guide wa mtoto. Suala la 16 year olds kufikiria kuwa na lovers ni absolutely natural. Wengine wana supress feelings zao cold turkey, wengine wanaoa/ kuolewa at that age, wengine wana act on it in secret...wanapata viji wapenzi in the dark. Matokeo yake kwa kuwa hawana mwongozo wanafanya kila kitu rafiki zao wanachofanya....and sometimes wanalaghaiwa hata na watu wazima!. And that's a sad story!.

  Nasema hivi....wazazi wanatakiwa kuwasikiliza watoto wao, na sometimes wao ku-initiate maongezi juu ya mapenzi. Kama mzazi anakuwa makini juu ya mwenemdo wa mwanae ataona dalili kuwa mwanae anaweza kuwa na mpenzi. Earn their trust, it will go a long way in your children's life.

  American/western culture is a real influence not only to kids...but adults as well. Mnakuwa in denial mnapo underestimate its power....kusema tu eti acha kufuata tamaduni nyingine hakusaidii kitu.

  Parents...LOVE your children, SUPPORT them, LISTEN to them, ADVICE them. LET THEM COME TO YOU FIRST for advice. Because if you don't....some bigger kids around the block will be their role models.

  To ALL kids whose parents don't listen to them, or who are afraid to go to their parents for counseling....TALK to GOD. Just be sincere, and say all your true feelings to GOD and ask his guidance.....you will never go wrong!

  Thank you brave, smart 16 year old. Boy/girl love relationship is a wonderful thing if you learn its rules and boundaries. It can be a sacred thing....but don't act like you're married. Some things are to be saved until marriage.

  Good luck to you, and God bless you!

  ReplyDelete
 18. AnonymousMay 25, 2010

  Sikiza Dogo, mimi nimeisha USA na Europe. Believe or not, hiyo liberalism unayoisema imanza miaka 30 tu iliyopita!!!! YAANI, NCHI HIZO ZILIANZA NA NIDHAMU, MAADILI, UCHAPAKAZI, ETC, NDIPO BAADAYE - YES AFTER CENTURIES!!! - BAADA YA KUENDELEA KIUCHUMI, KITEKNOLOJIA, NA KI-INSTITUTION NDIPO SASA UHURU WA KUFANYA NGONO OVYO NA USHOGA NA USENGE NA KUTUKANANA NA WAZAZI UKAKUBALIKA. So, my dear child, before talking about America culture, plase learn about how they asvanced so far before relaxing moral norms. Yaani, don't put the cart before the horse, sawa???

  ReplyDelete
 19. AnonymousMay 25, 2010

  Asante kijana nadhani Tanzania tuna mila na Desturi nzuri sana, naomba ukizifuata hizo utafanikiwa katika kila kona ya maisha yako. Bado mamilioni ya watu tunahangaika kutafuta mlo na kupeleka mtoto shule, jitahidi umalize shule upate kazi na uanze familia yako. No short cut, ukimwi upo kila kona hakuna aliyekwenda shule au ambae hajakwenda,TV imekuja watu wanaiga kila kitu hakuna naetaka kuwa na limit au kujielimisha kujuwa kwamba siwezi kuvuka huu mpaka, hilo ni tatizo tosha la kukuambia kwamba bado hatujafikia kiwanga cha kuiga Culture za watu wengine.Jiulize kwa nini wao hawataki kuiga culture zetu sisi tu ndiyo tunaiga za kwao.Mila zetu na desturi ni nzuri sana na napenda utafute wazee uwaulize maswali mengi na watakusaidia, tatizo ni kwamba kama unatarajia majibu utayapata kwenye Tv na watu wenye age 16 hutapata jibu. Mdau tafuta wazee uwaulize maswali na watakujibu vyema kabisa.

  ReplyDelete
 20. AnonymousMay 26, 2010

  I second you at Tue May 25, 05:46:00 PM. Hii ni issue nzuri sana na watu wanajidai kumwambia kijana kasome wakati wao ndio wanaoegesha magari nje ya masecondary kuvizia wanafunzi wakike wakitoka shule bila kujali kuwa huyo ni mtotowa watu pia. Unatake advanage ya mtu asiyekua na ubongo uliokomaa. Lets be real...Tanzania tunatakiwa tuchange sana. Hizi nchi mnazosema hazina heshima mbona ukimwi sio mwingi kama nchi zetu zenye heshima?

  Tunatakiwa tufundishe watoto wetu socialization katika gender tofauti na ni vizuri wazazi wakijua rafiki zako ni wapi wakike na wakiume ili wakushauri. Na pia ujue watu wanasema mtoto wangu anatabia nzuri lakini kwa vile hujui hata rafiki yake mmoja.. You are who you spend time with....

  Ukali hausaidi kitu na wote mnaopinga mujiulize mlivyokua na miaka 16 ilikuaje? Mtoto akielewa vitu mapema na wala temptation hazita kuwa kubwa au curiosity. Freedom and trust should begin at early age..

  Mnaosema marekani hawana heshima hamjui mnalosema..Heshima za kitumwa na uoga ndio mnazocount? Heshima ni kutoka rohoni. Heshima ya kijeshi sio heshima. Unawezxa ukaona watoto wako wanajump all over the places wakikuona unafikiri wanakueshimu kumbe wanakuogopa. Mtoto haweza hata kuja kukwambia kitu chochote kwa ajili ya uoga basi wewe unaona umzazi mzuri. We need to change kabia.

  Na ungekua unaishi na mwanao mpaka kufa basi ungemconrol unavyotaka. Lakini ukimfundisha independent na kutrust toka mwanzoni na kumuachia mwanao ajue limitation zake itamsaidia kubuild future yake. Nilivyokuja huku mara ya kwanza nilikua nipo na wanafuzni wakike ambao wao baba yao aliwafungia ndani sana ulizia huku huo uhuru walivyoupata waliutumiaje? Dada mtu alianza hakumaliza hata mwaka wa kwanza alikua ana mimba. Mdogo mtu kuja huku naye miezi mitatu tu akawa knocked out. Na sasa hivi mmoja ana watoto watatu baba tofauti..I don't pass judgment to people lakini mimi ninamlaumu mzazi wao...Thanks to God baba yangu alikua social toka tu wadogo . Na tulijua right from wrong toka tunakua...

  Na kwa taarifa yenu watowo wa siku hizi wanajua mengi kuliko mnavyofikiri. Na usipomsaidia kuyachanganyua hayo mambo usije kujilaumu baadaye na kukali kumsema mtoito hukusikia nilichokufundisha wakati you never took time to talk to your kids before.

  Mnasema mtoto akikuzoea heshima itapungua looo??? Heshima sio kuogopwa tulivyokuja huku kusoma tulikua tunaogopa hata maprofessor. kwa vile tumeshafundwa tabia za kuogopa ogopa tu.

  Acheni kumsema huyu kijana na wala kuwa na girlfriend/boyfriend sio kufanya mambo ya ajabu kama manavyofikiri au kama mlivyofanya nyie. Ni kuna mambo mengi ya kulearn na kujua jinsi ya kutreat a different person.

  ReplyDelete
 21. AnonymousMay 26, 2010

  michuzi hizi habari anazitunga mwenyewe ili apate wasomaji n waandikaji maoni, anajua vzuri topic gani itapendwa na wa2. eti ana miaka 16 ndo kaamua kuandika hii habari, kweli jamani inakuingieni akilini hii. big up michuzi.

  ReplyDelete
 22. AnonymousMay 26, 2010

  Ama kweli upeo wako mdogo sana!!! Si lazima tuige kila kitu kutoka kwa wazungu. TUYAIGE yale mazuri tu kama vile UCHAPAJI KAZI, UBUNIFU, PUNCTUALITY, NIDHAMU, USAFI WA MAZINGIRA, N.K. Lakini TUSIYAIGE MABAYA YAO, KAMA VILE KUTOHESHIMU WAZAZI, KUPIGANA KISSES HADHARANI, NDOA ZA WASENGE NA WASAGAJI, MADAWA YA KULEVYA, N.K. Mimi nimesoma na kufanya kazi miaka mingi sana Ulaya na USA: nakuhakikishia kuwa uhusiano kati ya wazazi na watoto si 'idyllic' kama unavyofikiri. Watoto kujibishana na kutukanana na wazazi wao ni jambo la kawaida (jambo ambalo halikubaliki katika jamii zote za kiafrika, kikristo na kiislamu). Aidha, 97% ya wazazi wakishastaafu wanakwenda kuishi katika nyumba za wazee ambapo Afrika tunaishi na mababu na mabibi zetu nyumbani mwetu. Kitu ninachokubali ni kuwa ni muhimu wazazi waongee kwa uelewa na watoto wao ili wawaeleze ukweli wa wa maisha na ubaya wa madawa ya kulevya, ulevi sugu, wizi, ngono utotoni, n.k.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...