Mnadhimu mkuu wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo (mbele) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Eng. Omar Chambo eneo la Kidibo Mpwa leo wakikagua eneo lililokamilika kukarabatiwa na jeshi hilo shupavu ambalo leo limekabidhi kwa Wizara ya Miundombinu sehemu ya reli ya kati iliyoharibiwa na mvua mwishoni mwa mwaka jana (dec 2009) kati ya maeneo ya Gulwe hadi Kilosa mkoani Morogoro. Ukarabati huo wa 68 km umegharimu shilingi 15.6 bilioni (tz), Jeshi la wananchi limekamilisha agizo la RaisJakaya Kikwete kulitaka kukamilisha ukarabati huo kwa haraka ili wananchi kuondokana na kero ya usafiri pamoja na kuiletea taifa mapato ya uchumi. Kwa wakati huu itaanza kutumika kwa treni za mizigo hadi itakapotangazwa rsami kuanza safari za abiria.Picha zote na Mwanakombo Jumaa -MAELEZO
Mnadhimu mkuu wa JWTZ Luteni Jenarali Abdulrahman Shimbo (mbele) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Eng. Omar Chambo ktk eneo la Kidibo Mpwa

shanta akiwahi eneo lake
sehemu iliyokarabatiwa na JWTZ kwa muda mfupi sana
Afande Shimo na Injinia Chambo wakiendelea na ukaguzi





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2010

    Hongera kwa kukarabati uharibifu wa mafuriko ya Mvua. Lakini mafuriko ya TRL yataendelea kuwepo?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2010

    Safi sana jeshi letu ndio maana wananchi tunalipenda na kuliheshimu jeshi letu ni vizuri kuendelea na kazi kama hizi wakati wa amani maana kuna walioingia jeshini baada ya vita ya kagera hadi sasa wanakaribia kustaafu hawajafanya job discription yao ya kupigana bora wawe wanafanya kazi kama hizi zitasaidia kupunguza vitambi kwa maafande wetu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2010

    Hongera jeshi letu shupavu kwa kukamilisha kazi mliyotumwa na Amiri jeshi mkuu kwa haraka sana. Kwa kweli ingekuwa amri yangu hata barabara zinazosua sua wangepewa wao wakamlishe, kuliko kulipa makampuni ya wahindi wanaojizungusha wee huku vibarua wao wakijigalagaza michangani kutwa nzima wanasubiri Nyapara akifika ndio wafanye kazi.

    Kuna mradi mdogo tu wa ujenzi wa majengo kwa ajili ya umeme huko Somanga kampuni ya wahindi ya kitanzania imechukua zaidi ya miaka mitano kukamilisha na bado ujenzi haujesha, ilikuwa uishe 2007!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2010

    Mimi napendekeza JWTZ wapewe tenda ya kumiliki na kukarabati miuondo mbinu ya reli ya kati Tanzania.

    Sababu reli ni kiunganishi kikuu cha uchumi na ulinzi wa Tanzania. Nchi nyingi zilipokabiliwa na changamoto kubwa kama vita n.k kama ilivyokuwa Vita Kuu ya Kwanza na Ya Pili ya Dunia, nchi nyingi za ulaya majeshi yao yalichukua uendeshaji wa reli zao ili kufanikiwa malengo yao.

    Kwa hapa Tanzania Vita yetu kuu ni ya Kiuchumi na wahujumu wa miundo mbinu ya reli, hivyo ni wakati muafaka JWTZ kumiliki miundo mbinu ya reli ya kati, huku makampuni yanayokodisha au kumiliki mabehewa na vichwa vya treni kulipia gharama za kutumia miundo mbinu hiyo.

    Naamini mkakati huu niliosema ukitekelezwa, basi reli ya kati itakuwa miongoni mwa reli bora ktk Afrika.

    Pia serikali ipatiwe JWTZ ruzuku maalumu ya kuboresha, kukarabati reli hii ya kati, kama vile ifanyavyo kwa TANROADS na Viwanja Vya Ndege. Hapa duniani reli zote bora za USA, India, UK , China n.k serikali huchukulia reli kwa uzito unaofanana na invyotoa ruzuku kwa barabara, viwanja vya ndege na bandari.

    Mdau
    Shimoni Kariakoo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2010

    Wanakaghua huku wakitembea kwa miguu kwa sababu si umbali mrefu au ndio protokali regardless of the distance???? Maana duh!

    Yote na yote, hongereni sana JWTZ kwa kazi nzuri.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 22, 2010

    HONGERA SAANA GEN MWAMUNYANGE NA GEN SHIMBO
    JWTZ NI MOJA YA TAASISI ZA SERIKALI YETU AMBAZO WATANZANIA TUKO PROUD KUWA BADO ZINAWEKA UTAIFA MBELE.
    NATAMANI NINGEKUWA KIJANA NA KUJIUNGA NA JWTZ.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 22, 2010

    kusafiri na treni ni raha sana ila kama ni ajali mtindo mmoja heri nibakie na mabasi au ndege. Hizi reli wangeweza kuzifanyia urekebisho wa nguvu na watu wote wangekimbilia treni, lakini ndio hivyo tena. Mpaka wakiona mzungu fulani kaja labda toka sauzi africa anataka kushugulikia hili swala ndio watashtuka... vitu vingine tufanye wenyewe kabla wenzetu hawajachukua vilivyo vyetu.


    NB: kamichu vipi ile blog ya imichuzi.com mbona huweki news tena mambo tunasubiria kwa hamu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 22, 2010

    kwa kuwa ni mwaka wa uchaguzi hakuna cha ajabu, ingawa ni ukombozi wa wanaotegemea reli hii.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 22, 2010

    INGEKUWA VEMA KAMA JESHI LINGEPEWA MIAKA 5 IJAYO. NA WANA"SIHASA" WOTE TUWASUBIRI 2015.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2010

    Army Engineering Corps ya US ndiyo wamepewa kazi ya kukarabati kuta zilizosombwa na mafuriko ya New Orleans.

    Tanzania tunapaswa tuboreshe kikosi cha Ujenzi cha JWTZ wameze kushiriki ktk ujenzi wa miundombinu nchini.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 23, 2010

    Anonymous wa May 22, 12:31,

    Ni kweli kabisa, watu twasubiria kwa hamu!

    Pia mdau wa kariakoo shimoni naona naye ana viji point.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...